Nahisi unaumia na kushikwa katika mtanziko kutokana na kinachoendelea katika chama chenu. Hali yako inakuwa mbaya sana pale unapohisi katika baadhi ya mambo nafsi haikubaliani na hukumu wala mikakati inayofanywa na waliokujengea mazingira wewe kuwa upande wao dhidi ya pande hasimu. Unatamani uwe impartial lakini katika vita hivi hakuna nafasi hiyo. Wakati mwingine unatamani uvuke zuria ujiunge na upande wa pili lakini nalo hili linakuwea gumu. Umefungwa katika kifungo cha kulipa fadhila kiasi kwamba kuna mahali unadhulumika kuafikiana na unaopingana nao kimawazo na kimkakati. Katika mtanziko huu naamini unaweza kuwa unapita katika wakati mgumu zaidi hata kuliko MM, M1, M2 na M3.
Naweza kukutabiria kwa hakika kuwa uamuzi mgumu na wa busara utakaoufanya katika sakata hili utakuwa na ubashiri wa mafanikio yako ya kisiasa kuanzia ubunge 2015 na vyeo vikubwa katika chama na nchi katika kipindi cha 2015-2025 Mungu akikupa uzima. Lakini iwapo utashindwa kupiga hesabu vizuri matokeo yatakuwa kinyume chake. siombei, ila utapotea katika siasa za uwakilishi na za vyama. Katika kadhia hii, kulingana na hitimisho la saga zima wako wanasiasa wengi e.g Mch Msigwa, Mh. Halima, etc watapotea na wengine watapotezwa katika ulingo wa siasa. Wewe Mnyika siombei na sitopenda upotee wala nyota yako izamishwe. Napenda niendelee kukuona ukishiriki kutoa mchango katika uwakilishi na siasa za vyama vya nchi ijayo baada ya 2015.
Katika suala hili kujiweka kwako sawa siyo lazima uhame kambi. Unaweza ku-play determined role ya ku-initiate upatanishi wa kambi hasimu na record itakupa heshima ya pekee. Na utabaki salama ukikwea juu katika siasa za nchi hii.
Ninakuombea tafakuri yakinifu itakayofuatiwa na maamuzi makini.
Lakini katika yote kumbuka kuwa mpole kama ua maana MM ni mjanja kama nyoka!