John Mnyika: Sihusiki na mauaji ya Ali Kibao

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amekanusha vikali tuhuma zinazomhusisha na mauaji ya aliyekuwa mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho, Ali Mohamed Kibao, akitaja majaribio hayo kama mkakati wa kisiasa wa "kubambika kesi" na kuhamisha lawama kutoka kwa wahusika halisi.

Akizungumza leo, Januari 17, 2026 mbele ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), Mnyika amehoji uwezekano wa yeye kusimamisha basi mchana kweupe maeneo ya Kibo na kumteka kiongozi huyo bila vyombo vya dola kuchukua hatua.

Katibu Mkuu huyo ameibua upya maswali kwa Jeshi la Polisi kuhusu hatua zilizochukuliwa tangu mwaka 2024. Amehoji kama polisi waliwahoji mashuhuda muhimu waliokuwemo ndani ya basi wakati Kibao anatekwa, akiwemo dereva wa basi lililokuwa limembeba marehemu, kondakta wa basi husika na askari mstaafu aliyekuwa abiria na ambaye alishuhudia watekaji wakiwa na bunduki na kuwaonya abiria wasiingilie kati.

Ali Mohamed Kibao alitekwa Septemba 6, 2024, na mwili wake kupatikana Ununio siku iliyofuata ukiwa umeharibiwa vibaya, tukio ambalo lilizua mshtuko mkubwa nchini na kimataifa.

policccm wanatapatapa sana watuona kama makalio yao....na hizi media uchwara ,,,MC pilipili hadi leo tu uchunguzi haueleweki au wanadhani tumesahau
 
Akili itakurudia siku ukimwona Mnyika yupo CCM tena!! Chezea wanasiasa wewe!! Wakina Esther Matiku na Bulaya wako wapi vile??!!
Mkuu tulijenge Taifa, washaondoka wengi, Mbowe mwenyewe tia maji tia maji ila CHADEMA iko pale pale.
 
Siyo CDM pekee kulikuwa na vyama imara zaidi kama NCCR, CUF lakini leo viko hoi bin taabani kwa hiyo usishangae miaka ijayo CDM ikawa kama vyama hivyo!!
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amekanusha vikali tuhuma zinazomhusisha na mauaji ya aliyekuwa mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho, Ali Mohamed Kibao, akitaja majaribio hayo kama mkakati wa kisiasa wa "kubambika kesi" na kuhamisha lawama kutoka kwa wahusika halisi.

Akizungumza leo, Januari 17, 2026 mbele ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), Mnyika amehoji uwezekano wa yeye kusimamisha basi mchana kweupe maeneo ya Kibo na kumteka kiongozi huyo bila vyombo vya dola kuchukua hatua.

Katibu Mkuu huyo ameibua upya maswali kwa Jeshi la Polisi kuhusu hatua zilizochukuliwa tangu mwaka 2024. Amehoji kama polisi waliwahoji mashuhuda muhimu waliokuwemo ndani ya basi wakati Kibao anatekwa, akiwemo dereva wa basi lililokuwa limembeba marehemu, kondakta wa basi husika na askari mstaafu aliyekuwa abiria na ambaye alishuhudia watekaji wakiwa na bunduki na kuwaonya abiria wasiingilie kati.

Ali Mohamed Kibao alitekwa Septemba 6, 2024, na mwili wake kupatikana Ununio siku iliyofuata ukiwa umeharibiwa vibaya, tukio ambalo lilizua mshtuko mkubwa nchini na kimataifa.

huenda mnyika alikua mastermind na jacob ndie alikua mpiga picha wa tukio zima :HAhaa:
 
CDM hawajaishika nnchi ,usiwaamini kwa lipi?
Yaani mpaka washike nchi ndio uwaamini!!? Lazima mfumo wa chama uwe imara, maridadi na uaminike kwa watz kabla ya kuchukua nchi. Sasa Mfumo wa CDM ni mbovu sana ndio maana umejaa maburuki tupu yanahama chama kila mara wakati wa uchaguzi mkuu.
 
Pumzika tu ignore, mimi na watu aina ya chawa hapana.
 
Akili itakurudia siku ukimwona Mnyika yupo CCM tena!! Chezea wanasiasa wewe!! Wakina Esther Matiku na Bulaya wako wapi vile??!!
Uwezekano wa Mnyika kwenda CCM kama ulowataja ndo uuthibitisho wa uhusika wake kwenye mauaji ya Kibao?
Akili yako haijabarehe hivyo huwezi tambua!
Ndugu mwenye akili nzee, ninaheshimu uhai kuliko jambo lolote.
 
Siyo CDM pekee kulikuwa na vyama imara zaidi kama NCCR, CUF lakini leo viko hoi bin taabani kwa hiyo usishangae miaka ijayo CDM ikawa kama vyama hivyo!!
Kabisa. Pia usishangae miaka michache tu ijayo CCM kupoteana na kufa kama KANU ya Kenya.
 
Siyo CDM pekee kulikuwa na vyama imara zaidi kama NCCR, CUF lakini leo viko hoi bin taabani kwa hiyo usishangae miaka ijayo CDM ikawa kama vyama hivyo!!
Mambo ya kutarajia tarajia siyapendi sana. Kafatilie sababu za hivyo vyama kufa utaelewa kwanini CDM ipo na Mwenyekiti wao yupo jela. Inakijua chama cha ukombozi Kenya?! Cha Jomo Kenyata? Kinaitwa KANU, unakisikia leo, basi usishangae miaka ijayo CCM kupotea, na mali zote wana,odai zao zikarudishwa kwenye halmashauri husika.
 
Back
Top Bottom