John Mnyika: Rais Samia "aidha amepotoshwa au ameamua kusema uongo”

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema, kimesema rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan “aidha amepotoshwa au ameamua kusema uongo” katika baadhi ya mambo ambayo ameyatolea ufafanuzi katika mahojiano yake maalumu aliyofanya na BBC.

Kauli hiyo, imetolewa hii leo na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika pindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mnyika, amepinga baadhi ya hoja zilizotolewa a rais Samia ikiwemo zile zinazodai kwamba, Mbowe kwa muda mrefu alikuwa nje ya nchi baada ya kujua ana kesi inayomkabili, hivyo kusema, “hakuna wakati ambao kiongozi huyo ametoroka nchi au amekuwa nje ya nchi kinyume cha sheria.”

Mnyika ameongeza kusema kuwa, wakati ukifika, “chama kitatoa vielelezo vitakavyoonyesha uhalali wa safari hizo.”

Hata hivyo, rais Samia alipoulizwa iwapo kesi hiyo ya Mbowe ni ya kisiasa, alikataa kulitolea ufafanuzi wa kina kwa kusema kuwa, tayari kesi hiyo iko mahakamani, hivyo ni vyema kuachia mahakama kufanya kazi yake.

Lakini tayari Chadema inamlaumu rais Samia kwa madai kwamba ameingilia uhuru wa mahakama, na kusema, wameongeza na jopo la mawakili wao ili kuona ni hatua gani wanaweza kuchukua.

Aidha miongoni mwa mambo mengine ambayo Chama hicho kimeyajibu ni pamoja na kauli ya rais aliposema kuna tofauti kati ya demokrasia ya kisiasa na fujo za kisiasa, hivyo kuashiria kwamba, baadhi ya maandamano yanayoitishwa na vyama vya kisiasa kama fujo za kiasa.

Hata hivyo, kauli hii inaonekana kuwa mwiba kwa chama hicho cha upinzani ambapo Mnyika amesema kupiga marufuku mikutano hiyo ya hadhara ni kinyume cha katiba ya nchi na sheria za vyama vya kisiasa.

Chadema pia imedai kwamba rais Samia amepotosha umma pale aliposema kwamba, wananchi wamekubali tozo za simu, ila kiwango cha tozo ndio hawajakikubali.

Nchini Tanzania kumekuwa na maoni tofauti baada ya BBC kufanya mahojiano na rais Samia ambayo yamegusia nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari pamoja na masuala mengine kadhaa.

Sorce: BBC Swahili
 
Kesi iko mahakamani sasa Mnyika ana shida gani tena kumfokea raisi wetu!! Au CDM wanamtest mama!

Mama ukicheka na nyani utavuna mabua ndo maana mtangulizi ilifika mahali akaamua kwenda nao sawa.

Wanamwambia atii utawala wa sheria huku wanamuambia aingilie mahakama kwa kuifuta kesi!

Kama Mbowe Hana hatia mbona CDM hawataki trial mahakamani badala yake wanataka ifutwe kinyemela?
 
Unaweza kutoroka nchi kwa kutumia nyaraka halali. Kwani lazima useme mimi mwenzenu nasepa?
japo inaweza kuudhi kuwepo mahabusu, lakini kuiachie mahakama ifanye kazi kwa uhuru
 
Kauli alizo zitumia Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika dhidi ya Rais zina ukakasi sana, zimekosa adabu na nidhamu kwa kiongozi wa nchi.

nadhani kwa utovu huu alio uonyesha Mnyika nimeshangaa kwa nn alipewe nafasi ya ukatibu mkuu lkn pia nitashangaa sana kama Mnyika hakuchukuliwa hatua kali kwa kauli za kifedhuli na dharau alizo zitoa.

hata kama hato chukuliwa hatua za kisheria lkn namshauri Mnyika ajivunze adabu na nidhamu ya uongozi, kwa nafasi yake hapaswi kuwa mlopokaji kama wapiga debe.
 
Huyo UVCCM, wao nikuwapima watu wasiowapenda ili mkubwa awaone kiuteuzi
 
CDM ya sikuhizi ni matusi tu baada ya kushawishi watu kwa hoja wanatumia lugha chafu, wamenisikitisha sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom