John Mnyika: Rais Samia "aidha amepotoshwa au ameamua kusema uongo”

Mnyika huyu huyu ndiye aliye kuwa namtukana kiongozi ktk awamu ya 4, akatumia kinga ya bunge.

huyu jamaa amekosa adabu sana kwa viongozi wetu.

sasa sijui inawezekana kufundishwa adabu ukubwani?

kama inawezekana basi afundishwe angalu siku nyingine asiwe anaharisha.
 
Kauli alizo zitumia Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika dhidi ya Rais zina ukakasi sana, zimekosa adabu na nidhamu kwa kiongozi wa nchi.
nadhani kwa utovu huu alio uonyesha Mnyika nimeshangaa kwa nn alipewe nafasi ya ukatibu mkuu...
niidhamu za kijinga unaongelea bila shaka
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Rais kapotoshwa na nani?

Huyu ni Rais gani anayepotoshwa kila mara namna hii??...
Wewe ukisema watakusikiliza ndugu yangu... Hii interview ya BBC imeacha maswali mengi:
1. Ni kwa nini polisi walimuacha mtuhumiwa wa Ugaidi toka September kabla ya uchaguzi analandalanda bila kumfikisha kwa Pilato?

2. Huyu mtuhumiwa wa ugaidi, amewezaje kusafiri nchi mbalimbali akipitia mipaka ya Tanzania na passport ya Tanzania?

3. Huko alikokuwa anatembelea, alikuwa anafanmya nini au kuratibu nini? Je Ziara hizo zina athari gani kwa taifa kwa kuwa huyu mtuhumiwa labda alikuwa anawatembelea magaidi wenzake

4. Tuko salama kiasi gani kwa sasa kama nchi ikizingatiwa tuna watuhumiwa wa ugaidi kuanzia wale wa Uamsho na sasa Mbowe?

5. Ni kwa nini Polisi hawakumhifadhi hiyo September 2020? Kwa nini sasa? kuna ulazima gani sasa kumukweka rumande ilihali aliku free tu huko nje bila madhara? Kwa nini sasa na kwa nini sio September 2020.

Maswali ni mengi, Labda Nyani Ukiwauliza watakusikia
 
Rais HAPOTOSHWI kwa mambo yasiyo ya kitalaamu bali anaamua kwa makusudi kuchukua ushauri ule unaodhani amepotoshwa!!!

Hata kama ingekuwa kweli amepotoshwa, bado angesema "Hapana... nimeshatangaza hadharani kwamba tunaanza upya, kwahiyo hizi kesi sijui za ugaidi sitaki kuzisikia hadi mniletee hard evidence isiyo na shaka yoyote ile inayohalalisha kumpeleka Mbowe Mahakamani"!

Ikiwa alitamka hadharani kwamba kesi za uhujumu zipitiwe upya na kuzifuta zile zote zisizo na ushahidi, je alifanya hivyo kwa kesi ya Mbowe iliyoibuka from nowhere?!

Leo anadai hawezi kuongea sana kwa sababu kesi ipo mahakamani, je alijaribu kutaka kuiongelea kabla haijapelekwa mahakamani?!

Au amesahau kwamba Mbowe amepelekwa mahakamani wakati wa utawala wake? Kwanini basi hakuingilia kati wakati huo?
 
'" Askari wetu huwa awakosei shabaha"
"Lisu alijipiga mwenyewe risasi"
Hapa alidanganywa
 
Rais kapotoshwa na nani?

Huyu ni Rais gani anayepotoshwa kila mara namna hii?

Kila akiboronga, ni kapotoshwa!

WTF 😳.

Ina maana ni mweupe kiasi hicho cha kuweza kupotoshwa kila mara?
Ok tufanye hajapotoshwa he, Kwa kesi ya mbowe Nani ambae ameshafungwa?
 
Chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema, kimesema rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan “aidha amepotoshwa au ameamua kusema uongo” katika baadhi ya mambo ambayo ameyatolea ufafanuzi katika mahojiano yake maalumu aliyofanya na BBC.

Kauli hiyo, imetolewa hii leo na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika pindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mnyika, amepinga baadhi ya hoja zilizotolewa a rais Samia ikiwemo zile zinazodai kwamba, Mbowe kwa muda mrefu alikuwa nje ya nchi baada ya kujua ana kesi inayomkabili, hivyo kusema, “hakuna wakati ambao kiongozi huyo ametoroka nchi au amekuwa nje ya nchi kinyume cha sheria.”

Mnyika ameongeza kusema kuwa, wakati ukifika, “chama kitatoa vielelezo vitakavyoonyesha uhalali wa safari hizo.”

Hata hivyo, rais Samia alipoulizwa iwapo kesi hiyo ya Mbowe ni ya kisiasa, alikataa kulitolea ufafanuzi wa kina kwa kusema kuwa, tayari kesi hiyo iko mahakamani, hivyo ni vyema kuachia mahakama kufanya kazi yake.

Lakini tayari Chadema inamlaumu rais Samia kwa madai kwamba ameingilia uhuru wa mahakama, na kusema, wameongeza na jopo la mawakili wao ili kuona ni hatua gani wanaweza kuchukua.

Aidha miongoni mwa mambo mengine ambayo Chama hicho kimeyajibu ni pamoja na kauli ya rais aliposema kuna tofauti kati ya demokrasia ya kisiasa na fujo za kisiasa, hivyo kuashiria kwamba, baadhi ya maandamano yanayoitishwa na vyama vya kisiasa kama fujo za kiasa.

Hata hivyo, kauli hii inaonekana kuwa mwiba kwa chama hicho cha upinzani ambapo Mnyika amesema kupiga marufuku mikutano hiyo ya hadhara ni kinyume cha katiba ya nchi na sheria za vyama vya kisiasa.

Chadema pia imedai kwamba rais Samia amepotosha umma pale aliposema kwamba, wananchi wamekubali tozo za simu, ila kiwango cha tozo ndio hawajakikubali.

Nchini Tanzania kumekuwa na maoni tofauti baada ya BBC kufanya mahojiano na rais Samia ambayo yamegusia nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari pamoja na masuala mengine kadhaa.

Sorce: BBC Swahili
Tozo ilipitishwa Bungeni. Bungeni wanawakilishwa na wabunge tafsiri yake " wananchi wameikubali tozo "
Wamekubali kwa kiwango gani huo ndio mjadala.
 
Mnyika huyu huyu ndiye aliye kuwa namtukana kiongozi ktk awamu ya 4, akatumia kinga ya bunge.

huyu jamaa amekosa adabu sana kwa viongozi wetu.

sasa sijui inawezekana kufundishwa adabu ukubwani?

kama inawezekana basi afundishwe angalu siku nyingine asiwe anaharisha.

Labda atakuwa kamwelewa huyu hapa:

IMG_20210707_084839_278.jpg


Kukemewa kwa viongozi wa aina hii wenyewe na washirika wao huita ni kutukanwa.
 
SSH anadhani kujipanga na Sukuma Gang kutampa urais 2025:


Kama Neema hata kazini kwake hataki aguswe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom