TANZIA John Livingston Mwakipesile, Mbunge wa zamani wa Kyela afariki dunia

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,875
Aliyekuwa mbunge wa Kyela na baadae mkuu wa mkoa wa Mbeya mzee Mwakipesile amefariki dunia

IMG_20210817_113211_921.png
Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya, John Mwakipesile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 17, 2021. Marehemu Mwakipesile aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kyela (1995 hadi 2005) na kisha kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuanzia mwaka 2006 hadi alipostaafu mwaka 2011.

RIP

====

Mbeya. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye Serikali ya awamu ya nne, John Mwakipesile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Agosti 17, 2021.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya Simu, Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Ismail Mlawa amesema wamepokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa.

"Tumepata taarifa na sasa naelekea nyumbani kwa marehemu kujua taarifa zaidi na nitaweza kukuunganisha na familia ya marehemu kwani mimi sio mzungumzaji wa familia," amesema Mlawa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jacob Mwakasole naye amethibitisha kupokea taarifa za msiba wa Mwakipesile na kwamba ni pigo kubwa kwao. Ameongeza kuwa hakuwa na taarifa za kuugua kwa Mwakipesile.

"Ni kweli nimepokea taarifa za msiba huo mkubwa wa baba yetu na kada wa chama. Chama tunataratibu zetu, tutashirikiana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kumsitili marehemu Mwakipesile,” amesema mwenyekiti huyo.

Princes Mwaihojo, mdau wa maendeleo Mkoa wa Mbeya amesema watamkumbuka marehemu kwa namna alivyoupigania mkoa huo kuvutia na kupata wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi.

Chanzo: Gazeti Mwananchi
 
Born: 15th May, 1940. Departed: 17th August, 2021. With great sadness, the Mramba’s Family hereby announce the passage of our beloved father, Basil Pesambili Mramba; A life so beautifully lived deserves to be beautifully remembered. Mzee succumbed to illness at the Regency Medical Center earlier this morning, 17th August; 2021. Given the pandemic situation, the family accepts your sympathies and prayers and asks for privacy. We will receive visits from Family Members ONLY at his residence on Mawenzi Road, Oysterbay. Further information and program will be shared at a later stage. The Lord has given, and the Lord has taken away; May God rest his soul in eternal peace. Amen. Godfrey B. Mramba.
 
Chanjo ni muhimu sana
 
Mbeya. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye Serikali ya awamu ya nne, John Mwakipesile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Agosti 17, 2021.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya Simu, Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Ismail Mlawa amesema wamepokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa.

"Tumepata taarifa na sasa naelekea nyumbani kwa marehemu kujua taarifa zaidi na nitaweza kukuunganisha na familia ya marehemu kwani mimi sio mzungumzaji wa familia," amesema Mlawa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jacob Mwakasole naye amethibitisha kupokea taarifa za msiba wa Mwakipesile na kwamba ni pigo kubwa kwao. Ameongeza kuwa hakuwa na taarifa za kuugua kwa Mwakipesile.

"Ni kweli nimepokea taarifa za msiba huo mkubwa wa baba yetu na kada wa chama. Chama tunataratibu zetu, tutashirikiana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kumsitili marehemu Mwakipesile,” amesema mwenyekiti huyo.

Princes Mwaihojo, mdau wa maendeleo Mkoa wa Mbeya amesema watamkumbuka marehemu kwa namna alivyoupigania mkoa huo kuvutia na kupata wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi.

Screenshot_20210817-112817_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom