John Heche: Tunaomba pesa zetu tuwapelekee waathirika wa tetemeko

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Mbunge wa Tarime Vijini Mhe. John Heche Leo Bungeni ameomba Muongozo Kwa kusimamia Kanuni ya 68:7 juu wa wahanga wa tetemeko la Kagera.

Akieleza jinsi watu wa wanavyopata madhira kama vile kunyeshewa mvua kwa sababu wanalala nje kwa sababu nyumba zao kubomolewa na tetemeko kwa hali hiyo ambayo itapelekea milipuko ya Magonjwa.

Bw. Anaendelea kueleza " utakumbuka tarehe 12 mwezi wa 10 nilisimama kuomba Bunge liharishwe kwa kanuni ya 47 ili kupisha tujadili jambo halisi na Dharula kwa wakati huo

Anaendelea kueleza "ambapo ndugu zetu Kule Kagera walikuwa wamepata tatizo la Tetemeko Nyumba zao zilibomoka..".

Mbunge huyo jasiri ameomba pesa ambazo walichanga zirudishwe ili wenyewe wazipeleke kwa waathirika wa tetemeko.

Kwa sababu Rais alipokuwa kagera alisema kwamba serikali haitatoa chochote kwa waathirika wa Tetemeko badala yake pesa zitatengeneza miundombinu ya serikali.

Ni Mimi Mhere Mwita
 
Hongera sana John Heche ni kweli kabisa bora warudishe pesa zetu ambazo tulichanga kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi Kagera tuzipeleka wenyewe wahusika wameshindwa kuzipelekea na kuzipangia matumizi ambayo hayana faida kwa wananchi wa Kagera.
Kama pesa hizo kutumika kujenga maghorofa huko kwao
 
Mbunge wa Tarime Vijini Mhe. John Heche Leo Bungeni ameomba Muongozo Kwa kusimamia Kanuni ya 68:7 juu wa wahanga wa tetemeko la Kagera.

Akieleza jinsi watu wa wanavyopata madhira kama vile kunyeshewa mvua kwa sababu wanalala nje kwa sababu nyumba zao kubomolewa na tetemeko kwa hali hiyo ambayo itapelekea milipuko ya Magonjwa.

Bw. Anaendelea kueleza " utakumbuka tarehe 12 mwezi wa 10 nilisimama kuomba Bunge liharishwe kwa kanuni ya 47 ili kupisha tujadili jambo halisi na Dharula kwa wakati huo

Anaendelea kueleza "ambapo ndugu zetu Kule Kagera walikuwa wamepata tatizo la Tetemeko Nyumba zao zilibomoka..".

Mbunge huyo jasiri ameomba pesa ambazo walichanga zirudishwe ili wenyewe wazipeleke kwa waathirika wa tetemeko.

Kwa sababu Rais alipokuwa kagera alisema kwamba serikali haitatoa chochote kwa waathirika wa Tetemeko badala yake pesa zitatengeneza miundombinu ya serikali.

Ni Mimi Mhere Mwita
Kwani CHADEMA walichanga shs ngapi? Maana hata chakula cha msaada walichoahidi ni magumashi
 
Hajasema anazihitaji akanunulie pombe bali ameziomba kwa kuwa zilirekodiwa wazirudishe vivyo hivyo wao ndio wawapelekee wahanga wale. Nadhani hii ni nzuri ili mtu amshukuru tu aliye mchangia. Kwetu wanaleta Dengelua ka kichips na unaandikwa na wamama wanaleta mahindi yalio kobolewa na maharagwe kwa ajili ya Pure. Nao pia huandikwa, iweje mseme mnazipeleka na mtawaambia walio toa halaf mkawape wachimba barabara. Watatushukuru lini?? Watu wanafia nje kwenye mvua na baridi. Hizo barabara atapita nani hawa wakishakufa??
 
Kwani CHADEMA walichanga shs ngapi? Maana hata chakula cha msaada walichoahidi ni magumashi
Shirikisha ubongo wako unapojadili mambo!! Heche bungeni anasimama kwa niaba ya CHADEMA au kwa niaba ya wananchi wa Jimbo lake waliomchagua kutia ndani wana CCM na wasio na vyama. Na hiyo misaada ya chakula itakwendaje kama tu kusalimia walikatazwa?
 
Bwn. Nyenyere, hoja ya msingi sio uchama, kwamba chama fulani kilichanga kiasi kadhaa kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi kule Kagera. Hoja ni kuwa kiasi chote cha fedha zilizochangwa na watu, taasisi mbali mbali za kitaifa na kimataifa na mataifa kwa ujumla wake zinapaswa ziwafikie waathirika wa tetemeko ili kuwapa ahueni ya maisha badala ya kujengea miundombinu.
 
Ndio maana bunge live linaogopwa. Sipati picha body language ya Heche ilikuwaje wakati anawasilisha hoja hiyo muhimu
 
Back
Top Bottom