John Heche moments special thead

Katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu shahidi wa tano wa upande wa utetezi na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche ameieleza Mahakama kuwa madhila mbalimbali ambayo CHADEMA ilipitia katika chaguzi zilizopita ndiyo yaliyochochea kamati kuu kupitisha msimamo wa “No Reforms, No Election”… yaani, bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Heche ameyasema hayo mbele ya Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, wakati akitoa ushahidi katika kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Jaji Dustan Ndunguru.
 
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema bara John Heche, ameeleza Mahakama Kuu matukio aliyodai kuyashuhudia katika chaguzi zilizopita, akitaja mauaji, kukamatwa kwa viongozi na wafuasi, kuenguliwa kwa wagombea na malalamiko kuhusu taratibu za uchaguzi.

Heche ametoa maelezo hayo Septemba 9, akiendelea kuhojiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akitoa ushahidi wa kumtetea Tundu Lissu katika kesi ya uhaini inayomkabili.

Akijibu swali la Lissu kuhusu mabadiliko yaliyohitajika kabla ya uchaguzi, Heche amesema Kamati Kuu ya CHADEMA ilitaka mabadiliko ya kikatiba na kisheria, ikiwemo kuondoa mamlaka makubwa ya Rais katika kuunda Tume ya Uchaguzi na uteuzi wa Wakurugenzi wa Uchaguzi.

Amesema chaguzi hizo ziliambatana na mauaji, kuenguliwa kwa wagombea, kunyimwa fomu za mawakala na matokeo, pamoja na mikutano kuvurugwa.

Akieleza tukio la Arumeru Mashariki, amesema Katibu wa CHADEMA Usa River, Msafiri Mowambo, aliuawa kwa kuchinjwa kwa chainsaw mwaka 2012/2013, akidai hakuna aliyekamatwa.

Kuhusu Kinondoni, amesema Februari 2018 walinyimwa fomu za viapo vya mawakala na Mkurugenzi Kagurumjuli. Wakati wakifuatilia, walishambuliwa kwa risasi na Polisi na mwanachama Akwilina Akwilini akauawa. Amesema Kamanda wa polisi wa wakati huo Mambosasa alithibitisha mauaji hayo, lakini hakuna askari aliyekamatwa.

Heche amesema yeye na viongozi wengine wa CHADEMA walishitakiwa Kisutu kwa uchochezi na mkusanyiko usio na kibali. Walihukumiwa miezi sita au faini; yeye alilipa Sh milioni 40, huku jumla pamoja na washtakiwa wengine faini ikizidi Sh milioni 310.

Heche amesema walikata rufaa Mahakama Kuu na kuamriwa kurejeshewa fedha, lakini bado hajarejeshewa Sh milioni 40.

Katika tukio la mwaka 2015 Nyanyungu, Tarime Vijijini, Heche amesema Bhoke Mwita Waitei aliuawa kwa risasi na watu waliokamatwa wakaachiwa baadaye. Pia amesema katika uchaguzi huo huo wa Busanda, mgombea wa CHADEMA Alphonce aliuawa.
 
DUDE linaendelea kuuchapa mwendo! Chini ya dereva wa zam kamanda John Heche
 
Taarifa ya Msiba wa mwanachadema Marehemu Mzee Kamanga.

Leo tarehe 18.09.2026 Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe John Heche. ameongoza Viongozi na wanachama wa Mkoa wa Mwanza Katika zoezi la kutoa salamu za mwisho Kwa Marehemu Mzee Kamanga.
Makamu Mwenyekiti ameambatana na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Victoria Mwl. Zacharia Obad pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa, Wilaya za Nyamagana na Ilemela pamoja na wanachama..

Pumzika Kwa amani Mzee Kamanga.

AMED SOMBI
Afisa wa Kanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…