John Heche: CHADEMA waahidi kujenga chuo kumuenzi hayati Edwin Mtei

John Heche: CHADEMA waahidi kujenga chuo kumuenzi hayati Edwin Mtei

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Makamu Mwenyekiti wake Taifa, Mheshimiwa John Heche, kimezungumza na waandishi wa habari pamoja na wanachama wa chama hicho, na kueleza masikitiko makubwa kufuatia kifo cha Hayati Edwin Mtei, Mwasisi wa CHADEMA.

Akizungumza katika mkutano huo, Heche amesema chama kimeguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huo mzito, na kueleza kuwa Hayati Mtei alikuwa nguzo muhimu katika harakati za demokrasia nchini.

Katika kumuenzi na kudumisha kumbukumbu ya mchango wa Hayati Mtei, Heche ameeleza kuwa CHADEMA kimepitisha azimio la kujenga chuo maalum kitakachotumika kama kumbukumbu na heshima ya kudumu kwa Mwasisi huyo wa chama.

 
Kuna tetesi kuwa kipindi Cha mwl Nyerere kuliwahi kutokea janga la moto pale Benki kuu na kuteketeza KILA KITU na gavana kukimbilia nje ya nchi. Ndicho kipindi Cha Mtei akiwa gavana?mwenye ufahamu tafadhali
 
Badilsha hapo isomeke CHOO
Wajenge chuo na tonetone au wanaota kushika nchi?
 
Back
Top Bottom