John heche afunguka wanafunzi wa chuo kufukuzwa

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
62,204
128,020
[h=6]
John Heche


[/h][h=6] TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUFUKUZWA .
UTANGULIZI:

Kwa miaka ya hivi karibuni Vyuo mbalimbali vimekua na tabia ya kuwafukuza ama kuwasimamisha masomo wanafunzi wanaoendelea na masomo kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini mwetu kutokana na mashinikizo mbalimbali kutoka kwa viongozi wa kiserikali kwa kisingizio kuwa wanafunzi hawa wanafanya siasa vyuoni.
Itakumbukuwa kuwa migomo na maandamano ya wanafunzi kwa vyuo vikuu hapa nchini haijaanza pale mfumo wa vyama vingi uliporuhusiwa kuanza mwaka 1992 ,bali migomo na maandamano haya yamekuwepo tangu kuanzishwa kwa vyuo hivyo.
Mathalani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa na historia ya migomo na maandamano ya mara kwa mara tangu kuanzishwa kwake , na hivyo dhana ya kuwa wanafunzi wanagoma kutokana na misukumo ya kisiasa sio sahihi hata kidogo bali ni mbinu ya watawala kujaribu kuficha madhaifu yao .
Wanafunzi hawa wamekuwa wakigoma kutokana na serikali ya CCM kuendesha mambo yake kibabe na kwa dharahu ya hali ya juu ambapo imefanya elimu kuwa Privilage na si haki kwa watanzania.
Kwa mantiki hiyo basi, kutokutendewa haki kwa wanafunzi hawa na serikali yao, kukosekana kwa miundombinu bora ya kusoma na kujifunzia, wanafunzi hawa kunyanyaswa na watawala wa vyuo hivyo, kukosekana kwa mikopo kwa wakati muafaka, serikali kuingilia uendeshaji wa vyuo ,serikali kuvunja serikali za wanafunzi bila kutoa sababu za kimsingi na sababu nyingine mbalimbali ndio chanzo cha vurugu na migomo vyuoni.
Hivyo basi , kutokana na sababu tajwa hapo juu Baraza la Vijana na CHADEMA (BAVICHA) tunatamka wazi kuwa kitendo cha Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam, Dodoma na Muhimbili kuwafukuza wanafunzi kwa ujumla wake zaidi ya 100 ni kitendo cha uonevu kwa wanafunzi hawa na kamwe hakivumiliki hata kidogo na haswa ikizingatiwa kuwa ni watoto wa watu masikini na ambao kimsingi wanajilipia ada wenyewe kwani wanakopa na baada ya muda watapaswa kulipa fedha hizo.
Kwa nini tunapinga uamuzi huu wa kuwafukuza wanafunzi vyuoni;
1. Ni kinyume na Tamko la Ulimwengu la mwaka 1990 la uhuru wa kitaaluma (Academic Freedom) ambalo tulisaini mnamo mwezi April tarehe 29 hapa Dar Es Salaam , linasema wazi kuwa ni lazima Vyuo vijiendeshe kwa uhuru kamili bila kuingiliwa na serikali .

2. Kufukuzwa kwa wanafunzi hawa ni utekelezaji wa Maazimio ya vikao vya CCM vilivyofanyika na haswa vile vya Halimashauri Kuu ambavyo vimetoa maelekezo mbalimbali kwa Serikali juu ya kuwachukulia hatua wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakiikosoa serikali waziwazi , na hata wahadhiri ambao wamekuwa wakitumia taaluma zao kwa uwazi na kusema juu ya mapungufu ya serikali wachukuliwe hatua ya ama kufukuzwa kazi na au ajira zao kusitishwa. Hivyo hii ni muendelezo wa utekelezaji wa maamuzi hayo.

3. Kuvunjwa kwa taasisi za wanafunzi na haswa serikali za wanafunzi , hii ni kutokana na tangazo la serikali kuhusiana na kanuni za serikali za wanafunzi lililochapishwa tarehe 12/06/2009 ambalo ni tangazo namba 178 lilivunja rasmi nguvu za serikali za wanafunzi kuanzia na muundo wake, majukumu yake na hata jina la vyeo husika kwa kufuta rasmi cheo cha urais kwenye serikali za wanafunzi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa mara baada ya taasisi hizi kuvunjwa wanafunzi wamekosa chombo cha kuwasilisha matatizo yao kwa menejimenti za vyuo husika.

4. Wanafunzi waliofukuzwa vyuoni hawajatendewa haki kwani hawajapata fursa hata ya kusikilizwa na kujitetea mbele ya vyombo husika vya vyuo hivyo, na wakati huo huo walikuwa wanamadai ya kimsingi kabisa .Hivyo hii ni kinyume kabisa haki za kimsingi (Natural Justice).

5. Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Dr Shukuru Kawambwa amekuwa na tabia ya kuingilia taasisi za elimu ya juu , kwa mfano mnamo tarehe 22/06/2011 aliandika dokezo sabili kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo akitoa maelekezo kwa Bodi ya mikopo kusimamisha mikopo kwa Wanafunzi kwa ajili ya Mafunzo kwa vitendo hadi hapo uongozi wa UDOM utakapoamua nani alipwe na nani asilipwe. Pamoja na ukweli kuwa wanafunzi wana mikataba na bodi ya mikopo bado waziri anaweza kuagiza mikataba hiyo kuvunjwa na bodi husika. Na hata kitendo cha kuwafukuza wanafunzi hawa ni muendelezo wa serikali kuingilia vyuo hivi na utendaji wake.

6. BAVICHA , tunapinga na kulaani tamko lililotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuwa vijana hawa wasipate fursa yeyote ya kudahiliwa na vyuo vingine hapa nchini , hii ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa kila mtu ana haki ya kujiendeleza kwa kadiri ya uwezo wake. Hivyo kitendo hiki kamwe hakivumiliki kwa mtu mmoja kuwa na mamlaka ya kuwanyima wengine fursa ya kupata elimu kwa sababu ambazo hazielezeki na ni vitisho visivyovumilika hata kidogo.
Hivyo basi BAVICHA tunaitaka serikali na management zake za vyuo ziache tabia ya kutibu matokeo au matawi ya matatizo vyuoni humo kwa kukimbilia kufukuza wanafunzi bali kutatua kiini cha matatizo.
Pia tunawahimiza vijana wote wanaosoma katika vyuo , Sekondari ,taasisi mbalimbali za kitaaluma, wanaharakati na wadau wa elimu na maendeleo ya kweli hapa nchini kuungana pamoja ili kuupinga utamaduni huu mpya wa kuwanyanyasa wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
Jambo hili likiachwa ili liendelee bila kuchukua hatua litaathiri sana taifa kwani watawala wanataka kutengeneza taifa la watu waoga na wasiokuwa na uwezo wa kuhoji masuala mbalimbali.
Sambamba na haya, kuna wanafunzi wengi waliopaswa kuanza mwaka wa kwanza wa masomo mwaka huu lakini wameshindwa kufany hivyo kwa kile kinachoelezwa na bodi ya mikopo kutokua na bajeti ya kuwakopesha. Wanafunzi hawa wamesharudi makwao.
Majibu haya ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi hawa ni kielelezo cha serikali ya CCM kutokujali wala kuthamini elimu na kwamba anasa na kutapanya mali za umma ndio kipaumbele chake. Serikali haina fedha za kusomesha wanafunzi lakini ina fedha za kulipa posho kwa viongozi wake wachache. Katika hili, BAVICHA tunaitaka serikali itafakari upya swala la elimu na hata sera ya elimu ya juu hapa nchini
Tamko hili limetolewa na;

…………….
John Heche
Mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA.
[/h]
 
Back
Top Bottom