John chiligati vs wapinzani: Vita vya maneno! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John chiligati vs wapinzani: Vita vya maneno!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KadaMpinzani, Mar 22, 2009.

 1. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Nashindwa kuelewa huyu jamaa kwa nini alisema alichosema.

  Aliyoyasema ni haya:

  (a)Aonya vyama vya upinzani kutoihusisha CCM na ufisadi, vinginevyo amani itavurugika.

  (b) Visimchafue rais Kikwete, HOW?

  (c)"Tunatoa onyo la mwisho hatutakubali kuona chama kinakashifiwa, kinatukanwa na kuchezewa vinginevyo wanachama wetu wapatao milioni nne (4) wakikasirika na kuchukua hatua ya kulipiza kisiasa AMANI ITATOWEKA!!(Damn! Yaani sheria mkononi inaungwa mkono na waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na mjumbe halmashauri kuu CCM)

  (5) Adai CCM itakufa na mtu.,

  Does this sound new to you? NO...Safari 2010 ishaaanza wazee, tusiojiweza tukaeni pembeni na kuangalia yatakayotokea!

  Je kauli za Chiligati zinafaa na zinatuma ujumbe kwa taifa lililo huru kama la Tanzania ?
   
  Last edited by a moderator: Mar 23, 2009
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Source please.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivyo ni vitisho lakini Mbowe ameshasema kuwa CCM wote ni mafisadi sasa Chilibati kamaakiamua kubakia CCM basi ajue anaingia katika mkumbo wa mafisadi ,Chama Chake kimewakumbatia mafisadi ,hadi hii leo hakijawafukuza uwana chama na wengine wamewahi kulazwa lupango.
  Jambo jingine Tanzania ina watu milioni 36 (Selasini na sita na wengine wanazaliwa kwa kasi na ari mpya) ,Chiligati kama ametamka hayo basi walikuwa na wanachama hao katika miaka hiyo ya Mwalimu Nyerere si leo ,na asijaribu kusema wanachama wake wachukue hatua mikoni mwao,kwanza ikiwa amesema hayo basi anafaa kupelekwa mahakamani haraka lakini kwanza akapimwe akili.

  Chiligati kama hajui siasa basi akae pembeni ,maana anaweza kupata maradhi ya ghafla ya gandamizo la damu na aiweze kuligandua ,halafu huyo Chiligati mapambano ya kisiasa anaonyesha hayawezi kabisa ,kijana mdogo tu kutoka Zenji anaweza kumpandisha pressure ikiwa ameingia na gea hiyi katika majukwaa basi ajitayarishe maana kuna watu wanatafuta njia ya mapambano labda kama anategemea gari la maji ya washawasha hapo itabidi kutumika mipinde kulitoboa matairi na likikaa ndio limekaa maana sidhani kama wameweka fedha za kulinunulia vipuli ,Chiligati usipige mbiu ya mapambao mtaumbuka vibaya sana Tanganyika si Zanzibar ,nguvu zenu za kivita kazionyesheni Zanzibar tu na sio Tanganyika ,nasema mtaumbuka tena vibaya sana.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  If he said what is alleged here then he should be in jail. He is calling for an uprising.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Na ndio hivyo lazima aende jela maana badala ya uprizing kuchomekewa na wapinzani anaenda kuitisha yeye alieko kwenye utawala kwa kweli ni ajabu ndio wameanza kutisha hata pale wamerapu kuhusu Nadagascar sio wameikataa serikali ya Madagascar bali wameonya hapa ndani ya nchi watu wasijaribu kuiondoa serikali eti hawatatambulika ,ndio maana yake.
   
 6. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  vitisho siku zote ni kwa wale walio wavivu wa kufikiria - Chiligati= Mvivu wa kufikiria!

  Tumwambieni Chiligati vitisho vyake vingefanya kazi lakini sio safari hii, wakati huu ni wetu (sisi watanzania) na safari ya kuinusuru nchi imeanza na kamwe hatutorudi nyuma, sasa kama anaona vitisho ndio njia sahihi basi its too late for him & his company, maana wananchi wote wanafahamu hali halisi ilivyo sasa!

  AND YES hizi habari ni za kweli na kasema hayo maneno, na pia yaliandikwa katika gazeti! Ntaleta source!

  HII KAULI YA CHILIGATI MIGHT BE A GAME CHANGER! Majibizano ya Rostam + Mwakyembe + Kauli ya Chiligati= (Who knows?)
   
 7. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Huyu mzee alitakiwa awe CCM tu, serikalini kaja kufanya nini? Waziri huyu ukiwa mpinzani utapata kiwanja kweli !!!
   
 8. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hebu cheki kaweka open quotes halafu hakuna end of quotes inayoashiria maneno ya Chiligati yameishia wapi na tafsiri na analysis za mleta habari zimeanzia wapi.

  Mleta taarifa ame pose kama anatupa maneno kutoka mdomo wa farasi halafu anaanza "aonya... adai.. asema." Tafsiri zake mwenyewe! Yani "vyanzo" vyetu vingi havijui nini ni reported speech na nini ni quoted speech.

  Posted by KadaMpinzani: Aliyoyasema ni haya:

  (a)Aonya vyama vya upinzani...

  (c)"Tunatoa onyo la mwisho hatutakubali kuona chama kinakashifiwa, kinatukanwa na kuchezewa vinginevyo wanachama wetu wapatao milioni nne (4) wakikasirika na kuchukua hatua (Yaani sheria mkononi inaungwa mkono na waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na mjumbe halmashauri kuu CCM)

  (5) Adai CCM itakufa na mtu.
   
 9. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hiyo hapo 100_3793.JPG (image)
  Kuhani, mimi sio editor wa magazeti! Ukiitazama hii habari na mtiririko wake unashindwa kuelewa kilichoandikwa au ndo mashauzi tena kuhani ??
   
 10. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #10
  Mar 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Karibu tena kada ulikimbilia wapi au wewe ndio umechukuwa ngoma mwafrika wa kike nini - tuelezane
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chochote alichosema hii saa ni mbaya hivyo akae chonjo na maneno ya uchochezi.
   
 12. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  nipo mzee, MWK hata sijui kakimbilia wapi !LOL....kile kifaa kisingenifaa mm kwanza! am out for the day!
   
 13. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  It is not uncommonly unfair
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,443
  Likes Received: 81,492
  Trophy Points: 280
  Hiki ni kichekesho cha hali ya juu. Hivi kusema ukweli ambao unajulikana na kila Mtanzania anayefuatilia mambo ya siasa nchini kwamba CCM ni chama cha mafisafi ni kashfa!!!? :confused:

  Mbona mafisadi waliojaa ndani ya chama hicho akina Mkapa, Lowassa, Msabaha, Mkono, Karamagi, Mramba, Rostam Azizi, Chenge na wengineo chungu nzima hawajachukuliwa hatua yeyote kuhusiana na ufisadi wao dhidi ya nchi yetu!? Safisheni chama ambacho mmeruhusu kichafuke kwa kukumbatia mafisadi vinginevyo ukweli ndiyo huo kwamba CCM si chama cha wakulima na wafanyakazi kama kilivyo miaka ya nyuma bali ni chama cha mafisadi.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mafisadi siku zote wana vitisho ujapata kuona.
  Hivi hawa wanachama 4m wanadhani wao wanaweza kutunyamazisha watanzania 40m?
  Mara nyingine hawa fisadis wanachekesha kwa kweli.
  Kama wanadhani wao ndio wao wajaribu kuivunja hiyo amani waone. Binafsi nitaendelea kuwachukia na kuwasema.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,443
  Likes Received: 81,492
  Trophy Points: 280
  Halafu hawa CCM kila wakiona hawana hoja zenye nguvu dhidi ya tuhuma nzito dhidi ya mafisadi mbali mbali ndani ya chama hicho basi huja na hili tishio la amani kupotea na kumwaga damu. Kama wanataka kuanzisha vurugu za kumwaga damu kila la heri maana vyombo vyote vya dola viko chini yao kwa hiyo haitakuwa na ugumu wowote kuanzisha umwagaji damu kwa visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu.
   
 17. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  This is really getting out of hand!! naona kila mmoja anajaribu kutoa onyo tu siku hizi, na wanaoonywa ni watz. Ana uhakika gani kama watu milioni 4 wapo tayari kutetea CCM na UFISADI, nina uhakika wanamtandao wanaweza, lakini sina uhakika na uprising ya watu milioni ambao wametumiwa kwa miaka takribani 40 na zaidi kwa manufaa yake Chiligati na wenzake! Huku ni kulewa madaraka, na kudhani wao ni watz kuliko wengine, this is quite unfair. Hii ni nchi yetu sote bana, kuwa CCM wasijione kuwa wao wanastahili zaidi. Nina uhakika hakuna mtu anayeweza kwa hiari yake kwenda kuitetea CCM labda kama wataamua kuwanunua watu wakafanye fujo badala yao, kama wanavyojitahidi siku zote!!
   
 18. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2009
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ippmedia.com
   
 19. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  e bwana we sasa kweli, chiligati anaona mbali tena kuna hatari anajua kuwa Mafisadi wanatoka katika chama chake,akatae kama hakuna makada wa chama chake walioshakiwa kwa ufisadi, akatae kama mawaziri wa chama chake hawakuachia ngazi kwa tuhuma za ufisadi, yote haya yanawahusu chama gani kama si CCM? chiligati aseme kuwa hawana la kuwaambia wa tanz kuhusu uadilifu wa chama chake ifikapo 2010, katika kulinda utajiri wa nchi hii unaoliwa na mafisad wachache.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Naanza kuumwa na kichwa. Tunashindwa kujua nani mwenye akili timamu kati ya wapinzani na watawala waliotulia. Bora ukichaa uwe kwa wapinzani kwani ni debe tupu lakini ukihamia kwa watawala na wao ndio wanaowamiliki maaskari tunaweza kuashuhudia yale ya Pemba kwa Large Scale.
  Nategemea Muungwana atakuwa bado hajapatwa na hiki kagonjwa na kuwadhibiti watu wake. CCM kuwakumbatia mafisadi kosa la kwanza,kuukana ukweli kosa la pili, kuogopa kivuli cha matendo yake kosa la tatu na sasa hili la kutishioa amani ni kosa la nne.
  Chonde Chonde CCM gombaneni wenyewe kwani mnakijua mnachogombania lakini tuwachilieni amani yetu Watu millioni 4 isiwafanye kuhisi kuwa mnaimiliki nchi.

  Rais wetu kwa hili Chiligati ameenda mbali kwani tumeshashuhudia CCM ikichafua hadhi ya vyama vyengine lakini haijawahi kuwa nongwa.
   
Loading...