John Cena na mkewe wasema hawataki watoto, watawaharibia mapozi

John Cena na mkewe wasema hawataki watoto, watawaharibia mapozi

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
22,323
Reaction score
56,062
John Cena na mkewe wametangaza hawataki na hawatazaa kwa sababu watoto watawavuruga katika kufurahia maisha yao.

“Mimi na mke wangu tumeamua kwamba hatutakuwa na watoto wowote, Tunataka kufurahia maisha yetu, na kuwa na watoto kutatuvuruga.”

“Ni sawa kabisa kwa watu kutaka watoto, lakini mimi na mke wangu hatuko tayari kuchukua jukumu hilo, Nataka kufurahia maisha yangu na kuwa na furaha bila mahitaji ya kulea watoto.”

“Tulifanya uamuzi huo kabla ya ndoa yetu, na tunashukuru sana tulifanya hivyo kwa sababu maisha yetu yamekuwa yenye kuridhisha sana kwa zaidi ya miaka minne.”

“Hatujali kuhusu kuacha shule, kuandaa kifungua kinywa kwa watoto, au kukaa nyumbani kwa mzazi wakati wetu wa kufurahia maisha. Kila mtu ana haki ya kuchagua anachotaka maishani, na kwangu mimi ni ndoa yenye furaha bila watoto.”
 
"Wazazi wao wangeamua kutokuzaa leo wao wangekuwepo? Waache kumkufuru Mungu aliyeagiza tuujaze ulimwengu".

Alisikika mlevi mmoja wa kimanyema kutoka Kazuramimba mwenye watoto 12 wasiojua hata usiku huu wanakula nini, akimlaani Cena na mkewe akiwa kabwia fundo la ndimasi mdomoni.
 
Maamuzi yao yaheshimiwe, na hawajavunja sheria yoyote.
Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom