Joel Jaffer A’ita, ataka kuinunua Chelsea FC na kuiita Kongolo FC

fantastic philip

Senior Member
Oct 17, 2015
194
680
Joel Jaffer A’ita amekuwa gumzo baada ya kuwasilisha ombi la kuinunua Klabu ya Soka ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.

Mhandisi huyo wa Ujenzi ambaye ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, pia anamiliki Klabu ya Michezo ya Arua Hill ya Ligi Kuu ya Uganda.

Aliwasilisha rasmi ombi lake la kuinoa The Blues, na kuwa raia wa pili wa Uganda kutoa zabuni kwa klabu ya soka ya Uingereza baada ya jaribio la Michael Ezra Mulyoowa kwa Leeds United mwaka 2004 (Pauni Milioni 60).

"Niko tayari kutwaa Klabu ya Soka ya Chelsea " A’ita aliiambia Kawowo Sports Media Alhamisi, Machi 3, 2022. A’ita anatoa ofa ya dola bilioni 3.3 kwa Bilionea wa Urusi Roman Abramovich, mmiliki wa Klabu ya Soka ya Chelsea na anakusudia kuuita klabu hiyo Klabu ya Soka ya Kongolo (Kongolo FC)

“Kufuatia taarifa kwa umma kuhusu nia ya kuuza Chelsea FC, ningependa kueleza nia yetu ya kununua klabu. Kwa thamani ya sasa ya $ 3.2 bilioni, tunatoa $ 3.3 bilioni. Tunakusudia kubadili jina la klabu kama Kongolo FC” Aita aliandika barua kwa Abramovich.

Aita aliingia katika ulingo wa soka nchini Uganda mwaka wa 2019 alipotwaa Klabu ya Soka ya Doves All Stars.

#chanzodwswahili
#starTvupdate
FB_IMG_1646840434400.jpg
 
Inabidi wakati mwingine ukitaka kufanya kitu lazima ujue masharti na sheria kwanza

Kitu ambacho huwezi kufanya katika team za mpira wa Uingereza ni kubadili jina
Ajifunze sheria za hapa kwanza kabla hajakurupukuka kama blaza K

Hivi Dangote nae alitaka kununua team gani vile?

IMG_4567.jpg
 
Publicity ya Bure...

Leo kila mtu kamjua na Club anayomiliki inajulikana nina uhakika hata akikubaliwa ataanza kuleta story za oooh ngoja kwanza na story kibao

Au atachuku aende kuikopea mikopo ya kufanya issue zake....
 
Watu wana mpunga na hawana mawazo kabisa.

Tatizo ni mweusi mno. Halafu hiyo kongolo ameshaharibu, ameonyesha akili za kiafrika mno.
Unaelewa maana ya kongolo kikwao huko? Hata ukienda Japan kuna uwanja unaitwa Kumamoto
Belgium walikua na mchezaji anaitwa Mboo
 
Back
Top Bottom