Pole ndugu. Ila nakushauri uondoe imani hiyo kwamba hakuna fedheha kubwa duniani kama hiyo uliyoitaja. Zipo kubwa zaidi ya hiyo. Sema tu kwamba kila mtu anapopata tatizo au shida fulani ujikuta akiamini kuwa hakuna tatizo au shida nyingine kubwa zaidi ya hiyo aliyonayo. Na mtu huyo huyo baadae akija kupata shida nyingine kubwa ataona kuwa hiyo shida iliyopo muda huo ndiyo kubwa zaidi ya zote ikiwa ni pamoja na aliyowahi kupata huko nyuma.
Tukirudi kwenye hoja yako kikubwa ni kupuuza wale wanaokudharau, uweke juhudi katika kutafuta riziki yako bila kukata tamaa na pia kwa njia halali na zisizo za mkato. Pia kama wewe ni muumini wa uwepo wa Mungu usichoke kumwomba Mungu kwani kama ulivyokwisha sema mwenyewe ipo siku atakufungulia milango na wanaokudharau leo hii watabaki macho kodo.