Mi kudhani nilielewa vibaya kwamba ndugai hamnazo upstairs. Mbowe nilimsikia na kumwona akisema anayo hoja, tena kwa unyenyekevu sana. Nilishindwa kuelewa wapi amekosea kiasi cha kutolewa nje kwa maguvu. CCM imezoea kutumia maguvu ikiambiwa ukweli kwani daima ukweli unauma. Baadae wabunge wa ccm na Lyatonga (CCM Damu) walianza kuongelea tukio na sikumwona yeyote aliyeangelea issues. Walishangiliana kwa upuzi walioelezana kuhusu wapinzani na sio kuengelea mswada. Walijikomba sana kwa JK ati ni mvumilivu, ati wananchi wameona kwamba wapinzani hawafai, blablablaaaa. Hivi mie nawauliza wapunge wa ccm waliochoka kichwani, mnadhani Tanzania ya leo ni ileile ya 1947? Mnakosea, sisi sio wapumbavu kiasi hicho. Kibao kimegeukia ccm na wataendelea kujimaliza kwa ujinga wao wenyewe. Ni aibu kumfanyia upumbavu ule kiongozi mkuu wa upinzani bungeni ambaye kama angeruhusiwa kusema tungejua kama anaongelea takataka au tunu. Sasa CCM mnachokifanya ni kuwapa nafasi ya umaarufu wapinzani wenu maana huku nje tunachambua kila neno lisemwalo bungeni na kujua nani ni pumba na nani ni mchele. Kuweni macho ccm, ya Arusha inaelekea hayajawafunza maana sikio la kufa halisikii dawa. Mnaruhusu polisi kufanya yale mliyozoea kuwaruhusu mitaani kwa kuburuza waheshimiwa LIVE wakati dunia yote inaona, sasa mtatudanganyia wapi? Angalia baada ya wapinzani kutoka, pumba tu ziliongelewa na kulialia tu kwa mfa maji. Wapinzani ni chachu ya hioja bungeni. Nilimsikia yule bwana mdogo wa Sikonge sijui akidai CCM wanatumia hoja ya nguvu. Hakujua kwamba hata kiswahili kilimwendea kombo akashindwa kutofautisha na nguvu ya hoja na ndo matokeo ya jana.
Tanzania, CCM inatumia hila zote kuhakikisha hoja yao ya nguvu ishinde kuendeleza serikali mbili maana uhai wao umo katika serikali mbili bila Tanganyika kuwapo. Wazanzibari wenyewe wamewashitukia siku nyingi na ndo maana ccm ikaona iwakwepe kutoa maoni yake kuhusu mswada huu, maana wanaelewa kwamba Zanzibar inataka kuiona Tanganyika inakuwapo.