Mfahamu Job Yustino Ndugai

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Job Yustino Ndugai (amezaliwa 21 Januari 1960) ni mbunge wa jimbo la Kongwa katika bunge la kitaifa nchini Tanzania. Anatokea katika chama cha CCM.

Tangu tarehe 17 Novemba 2015 hadi 6 Januari 2022 alikuwa Spika wa Bunge la Tanzania. Baada ya kuingia katika ugomvi na rais Samia Suluhu Hassan alipaswa kujiuzulu uspika

Job Yustino Ndugai ni mwanasiasa kutoka Tanzania ambaye anahudumu kama Spika wa Bunge tangu mwaka 2015. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Maisha na Historia yake
Alizaliwa Januari 21, 1960 alipata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1971-1977. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa mbunge wa Kongwa kwa miaka 21 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa spika wa bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
 
... kumbe ni agemate wa mtukufu? Naona nyota zimezinguana mambo ya ulimwengu wa roho hayo! Tunachokiona katika ulimwengu wa kimwili ni matokeo tu; vita halisi vinapiganwa huko kwenye "anga za mbali".
 
Hilo jina la mkewe nahisi limesadiki kubatua akili za jamaa. Kichwa cha jamaa kimebatuka kile, hakipo sawa.
 
... kumbe ni agemate wa mtukufu? Naona nyota zimezinguana mambo ya ulimwengu wa roho hayo! Tunachokiona katika ulimwengu wa kimwili ni matokeo tu; vita halisi vinapiganwa huko kwenye "anga za mbali".
Kabisa mkuu kiage ni mate wa mtangulizi wa mama.
Mengine ngoja tusikilizie.
 
...
Maisha na Historia yake
Alizaliwa Januari 21, 1960 alipata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.
...
... rekebisha hapo red.
 
Job Yustino Ndugai (amezaliwa 21 Januari 1960) ni mbunge wa jimbo la Kongwa katika bunge la kitaifa nchini Tanzania. Anatokea katika chama cha CCM.

Tangu tarehe 17 Novemba 2015 hadi 6 Januari 2022 alikuwa Spika wa Bunge la Tanzania. Baada ya kuingia katika ugomvi na rais Samia Suluhu Hassan alipaswa kujiuzulu uspika

Job Yustino Ndugai ni mwanasiasa kutoka Tanzania ambaye anahudumu kama Spika wa Bunge tangu mwaka 2015. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Maisha na Historia yake
Alizaliwa Januari 21, 1960 alipata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1971-1977. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa mbunge wa Kongwa kwa miaka 21 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa spika wa bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Ndio mana tunasema wasomi kutoka bara it is good for nothing wanafanya mambo ya hovyo sana, pesa kwao ni bora kuliko taaluma zao
 
Back
Top Bottom