Job Ndugai: Sijamisi Uspika, nina amani, haya ni mapito katika maisha

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460




Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai amezungumzia maamuzi yake ya kutogomea Ubunge katika uchaguzi ujao akisema kuna watu wanapotosha kwa kuwa wanaona kuna jina lake.

Mbali nah apo ameulizwa kuhusu kama amemisi kiti cha Uspika ambacho alikuwa akikikalia kwa miaka kadhaa kabla ya kujiuzulu mwaka huu, amesema hajamisi kiti hicho.

“Hapana, ile ni huduma (Uspika), unafanya inapokuwa ni wajibu wako, Mtanzania mwingine anafanya inapokuwa wakati wake, nina amani nipo salama.”

Kuhusu kauli yake ya kutogomea uchaguzi ujao kutafsiriwa tofauti na baadhi ya watu, anasema:

“Ni kawaida yao wakiona kitu cha Ndugai lazima wapotoshe, jimboni kwangu wanaelewa hilo, nilichofanya niliwakumbusha tu kuhusu uamuzi wangu kuhusu kutogombea 2025, hilo jambo lilikuwepo na siyo jambo baya.

“Nikimaliza Ubunge tarudi kwenye asili yangu, nalima kidogo, nafuga kiasi, siyo kila jambo kuna nia mbaya, wito wangu tuwe na upendo, siyo kila jambo kupotosha, unafiki na kuchonganisha.”

Kuhusu kupotea kwake kipindi cha hapo kati baada ya kutangazwa kujiuzulu Uspika, Ndugai anasema:

“Ni maisha tu, ni sehemu ya mapito katika maisha, Mungu atajalia, ni vitu vya kawaida, tuendeleze umoja wetu lakini kubwa zaidi tuboreshe hali ya uchumi wetu, uchumi ya familia mojamoja… nawapenda sana Watanzania, viongozi wangu wa kitaifa mimi nawapenda sana na niwahakikishie hakuna sintofahamu yoyote kati yangu na Chama changu, ni mambo ya mitandao tu.”


CHANZO: JAHAZI – CLOUDS FM
 
1652422727494.png
 
Wabongo MNA Nongwa sana,yaani wakikaa madarakani mnalalamika,wakitoka mnalalamikaakibadilisha staili ya maisha mnalalamika...Nchi ya kushangaza sana hii.
 
Mshaurini bora awe anakaa kimya deep state wanamchora tu
Nani amshauri,alivyokuwa anaharibu bunge letu alisikiliza ushauri?
Halafu leo anahubiri UPENDO.Jikumbushe ile katuni akiwa amevaa joho na toilet paper pembeni utajifunza kitu kuwa alikuwa amechokwa kila kona.
 
It's all in perceptive..., lakini ukiangalia katika Hierarchy of needs , Ndugai is better off than most..., Wakati majority ya Watanzania hata wengine eti wanaomuonea huruma Ndugai wame-stuck kwenye Physiological Needs.., Huenda Ndugai amekosa Love and Belonging; and will not get Esteem and Self-actualization needs

1652423659502.png
 
It's all in perceptive..., lakini ukiangalia katika Hierarchy of needs , Ndugai is better off than most..., Wakati majority ya Watanzania hata wengine eti wanaomuonea huruma Ndugai wame-stuck kwenye Physiological Needs.., Huenda Ndugai amekosa Love and Belonging; and will not get Esteem and Self-actualization needs

View attachment 2222450
Viongozi wetu wanatama na rushwa hawashibi pesa huyu tayari anamiss mambo mengi hasa pesa za bure na kingine hao viongozi wetu hawana aibu kabisa hivyo vya self actualization na belongings havi wahusu kabisa their totally greedy pple.
 
Viongozi wetu wanatama na rushwa hawashibi pesa huyu tayari anamiss mambo mengi hasa pesa za bure na kingine hao viongozi wetu hawana aibu kabisa hivyo vya self actualization na belongings havi wahusu kabisa their totally greedy pple.
Kwahio in comparison na mtu ambaye ametoka asubuhi hajui kama jioni atakula, watoto hawajalipiwa karo mama yake kijijini mgonjwa ana madeni kila kona na kwa kila mtu..., kila simu ikipigwa anajua watu wanampigia kumdai, in short hata physiological needs hapati...,

Ofcourse Binadamu hatosheki akishapata this goal anataka that other goal (ila ndugai atleast anauwezo wa kutimizia wategemezi wake their needs) kuliko yule baba ambaye mtoto wake anamuangalia kwamba baba ameniangusha nafukuzwa shule na ameshindwa kutimiza majukumu yake.
 
Back
Top Bottom