Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,815
- 71,262
Jana umesimama na kugeuka kuwa Spika wa Kweli kwa kumtolea uvivu Waziri Mwijage na Serikali kwa ujumla juu ya majibu yake kuhusu sukari na mengineyo.
Umeiambia serikali iache tabia ya kusema uongo bungeni, kuleta blabla na mipasho katika masuala muhimu ya wananchi kwani wanakuweka pabaya (nadhani katika kuwa support) na hivyo waache kabisa.
Hii ni wazi kuwa baada ya kipindi kirefu cha kutumika wewe na chombo chako Bunge na huu utawala hatimae umeujua ukweli na sasa hutaki tena.
Nadhani tutegemee kumuona CJ Pro. Juma naye akionya hadharani kuhusu kuingiliwa anga zake na Executive. Hakika ikifika hapo na kama hautarudi nyuma ni wazi Bunge na Mahakama vitarudi kuwa vyombo vya kuheshimika na nchi itashuhudia utawala bora.
Kwani ukiwa na msimamo huo nanihii atakufanya nini? Kama ya Lisu hawezi kurudia tena!