JKT: Sijawaelewa

JKT: Sijawaelewa

Natanguliza heshima kwa wakubwa wng. Hivi karibuni ziliyangazwa nafasi za kujiunga na Jeshi la Kujenga taifa Sasa kama kawaida nikawajulisha wadogo zangu wafanye application cha ajabu ni kwamba zile interview ni magumashi kwani vijana wenye sifa wanaachwa na wenye mikono mirefu wanapita. Inauma sana kwani dogo alikuwa na sifa za ziada tofauti na elimu ya kidato cha nne mfano ana level 1 hadi 3 ya umeme na driving lkn ndo ivo kakosa. Dah nimeumia xna.

kama unajua anasifa ungemfanyia wewe mwenyewe au fungua mashitaka na siyo kuja kulalamika huwezi kuleta ujuaji kwenye kazi za watu kwani sifa za ziada ndio nini umeambiwa na nani kuwa kule wanatengea umeme
swala la kuajili mtu mwenye ujuzi wa ziada ni suala la mwajili na inategemea mahitaji yake
 
Pole sana mkuu.
 
Kaka mbona unapanic. Heshimu mawazo yng mkuu na kama unahisi kuna kitu hakikosawa sema kwa busara na sio unakurupuka tu. Au imekutach?
 
kwani lini wanaenda kuripot me namshukuru Mungu jamaa zangu wamepata.ila cjajua siku ya kuripoti.
 
Anaweza kuwa na sifa za ziada LAKINI HUJATUAMBIA ANA DIVISION NGAP O-LEVEL?Usikute ndo division v!
 
kuna dogo moja ana 4 ya 28 wilayani wakampiga chini ila mkoani kapita,alifika mkoani kwa neema tu.
 
kweli mkuu hata mim dogo wangu wameMtoa wakati alipita usairi wote kuanzia usairi Wa kata hadi wa mkoa cha kushangaza ukarudiwa tena mara mbili sasa hivi wamemtosa kisa amemaliza zamani na amefauru vizuri sasa sijui walikua wanataka viraza tuu!
 
Naona kuna swali ambalo limeulizwa mara nyingi but wengi hawalijibu "wanareport lini?" - wanaenda depo mwezi wa Tatu but tarehe ni siri yao. So get prepared...........Dunia ya siku hizi kujuana mbele kama humjui mtu basi PESA inatakiwa kuongea japokuwa pia kuna wengine wanapata kazi bila kujuana wala kutumia pesa ila ndo 2% kati ya 100%
 
Wanaenda depo tarehe 2 mwezi March so jiandaeni vijana
...............
Na nyie mlokosa fursa ziko nyingi tuu zinakuja.so tulizeni mishono
 
Huku manyara waliambiwa waripoti tarehe 16 mwezi huu mkoani,sijui ndio kuondoka kambini au vipi!
 
vtu walivyo angalia kujibu maswali vzuri na kujiamini kwako vyeti vyako umri barua ya kuomba kujiunga kama uliandika ovyo bila muhuliwa mtendaji wala mwenyekiti hufanyi interview. kiukweli kwa asilimia kubwa wametenda haki tofauti na wilivyo kuwa wanasema mitaani.morogoro wameambiwa walipoti tar kumi na saba.
 
Dogo anaulizwa.
1.kwanini umeamua kujiunga na Jkt?

2.Uzalendo ni nini?

3.Eleza maana ya kujitegemea?
Hakuna hata swali moja alojibu kwa ufasaha sasa mtu kama huyo asaidiwe vipi.
 
Back
Top Bottom