Pengine pia ni muda mwafaka kuangalia mafunzo haya yanavyoendeshwa ili kukidhi kipindi kilichopo. Kukazana tu kuwa wanafundishwa uzalendo hakutoshi, binafsi nafikiri uzalendo haufundishwi kwa miezi sita au mwaka mmoja. Gazeti la Mwananchi linaonyesha kuwa maombi ya vijana kuonana na rais yanapotoshwa. Nia kubwa si kupatiwa ajira. Pengine watueleze hasa ni nini kinataka kuwapeleka Ikulu.