Mwili ulinisisimka nilivyoona na kusikia kuwa "askari" waliomaliza mafunzo ya JKT bila kupatiwa ajira rasmi wanataka kuandamana kuelekea Ikulu. Mmmh, nikasema sasa huu ni ukurasa mpya katika historia ya majeshi yetu hapa nchini.
Askari hawa wamepata wapi ujasiri wa kuandamana kwenda Ikulu kuonana na Amiri jeshi mkuu? nani yuko nyuma yao? utamaduni huu wameupata wapi?
Kwanini wasingeazia kwa Mkuu wa majeshi kwanza kabla ya kwenda kwa Amiri jeshi mkuu?. Kama kweli vijana hawa watafanikisha malalamiko yao kwa njia hii basi iko siku "kaka zao" pia walioko kambini wanaweza kufuata njia hii hii ya kudai malalamiko yao, maana inawezekana na wao wanayo malalamiko makubwa pengine kuzidi haya ya "wajukuu zao" yaani mchezo wa ndama wanaocheza mchezo wa kupigana ndani ya zizi unaweza kuamsha hamu na hamasa ya madume nao kuanza kupigana.
Ni vema suala la vijana hawa wa JKT lichambuliwe kwa kina bila kutoa majibu ya juujuu na ya hasira. Inavyoonekana malengo ya mafuzo yao ya JKT hayakueleweka vema, au yuko mtu aliyekiuka maagano au yuko mtu nyuma yao anawashauri vibaya.
hizo ni dalili za UASI na watu kuingia MSITUNI
Mwili ulinisisimka nilivyoona na kusikia kuwa "askari" waliomaliza mafunzo ya JKT bila kupatiwa ajira rasmi wanataka kuandamana kuelekea Ikulu. Mmmh, nikasema sasa huu ni ukurasa mpya katika historia ya majeshi yetu hapa nchini.
Kama wao wameshindwa kutumia busara kuna haja gani kutumia busara kuwasikiliza hata hivyo jeshini hakuna busara kunaamri tu basi,kwahiyo hata wao lazima wapelekwe kijeshi tu.Serikali inapaswa kutumia busara sana katika kushughulika na hawa vijana, ambao tayari wameshapatiwa mafunzo ya kijeshi. Ni ajabu sana kuona ukosefu wa busara ulioonyeshwa hadi sasa katika kushughulikia tatizo lao. Nimeshangaa kusinga kiongozi wao alitekwa kwa staili ya Ulimboka! Kimsingi, suala hili halikupaswa kufikia hatua ya wao kuandamana. Kutumia nguvu kuwazima ni kosa ambalo siku moja serikali itakuja kulijutia.
Misitu gani wataingia wakati misitu yote kuna makambi na vituo vya kijeshi
Yawezekana hujitambui unafanya nini hata duniani.Nchi ikichafuka lawama zote ni kwa chama cha zamani CCM kwa kushindwa kuboresha maisha ya Watanzania.
Serikali inapaswa kutumia busara sana katika kushughulika na hawa vijana, ambao tayari wameshapatiwa mafunzo ya kijeshi. Ni ajabu sana kuona ukosefu wa busara ulioonyeshwa hadi sasa katika kushughulikia tatizo lao. Nimeshangaa kusinga kiongozi wao alitekwa kwa staili ya Ulimboka! Kimsingi, suala hili halikupaswa kufikia hatua ya wao kuandamana. Kutumia nguvu kuwazima ni kosa ambalo siku moja serikali itakuja kulijutia.
Hawa vijana ni mburukenge kabisa..hivi nani aliwaambia wakienda JKT serikali itawapa ajira?