Me nadhani hii ndio serikali hopeless kuliko zote tulizowahi kuwa nazo. Yaani huyu jamaa dah tumeliwa kwa kweli tumeliwa. Matatizo ya hii nchi kwake si issue bali kutalii ndio muhimu kwake. Juzi ameenda Mbagala mikono mfukoni anaangalia wahanga wa mabomu kama vile wanyama wa Mikumi. Lakini mimi sishangai kwani ninamjua nilishangaa tu watz kumpa nchi. Alipokuwa mambo ya nje aliwahi kuweka record ya kusafiri nje consecutively kwa miezi mitatu, hii record haitavunjwa milele nadhani. Ila kama kuchemsha ndugu zangu hapa tulichemsha. Na mtoto wa mkulima naye ndio dah jamani hivi kosa gani hilo kubwa tulifanya kwa Mungu mpaka atupe viongozi fake kiasi hiki?
Ukienda hapo Kenya utasikia mala chache sana Mwai Kibaki kasafiri....lakini rais wetu kwa kuzulula kha! eti anatafuta wawekezaji,wafadhili duh
Raisi wa Tanzania ni Rostam Aziz. JK ni kama Queen wa England and Wales.
Kwani Tanzania bila ya Misaada inawezekana??? Mwacheni JK azurure kutafuta misaada Jamani.....
I wish I was born in 1700* where there was no Danganyika or TZ. If my wish had happened I was not going to witness this mess. I was going to die a happy man because by then there was no Mr. President, our chiefs did not know Denmark and could not fly around like our Hon. Mr. JK. Furthermore there were no FISADIS.....................Kwani Tanzania bila ya Misaada inawezekana??? Mwacheni JK azurure kutafuta misaada Jamani. Kila kona kuna UFISADI, sasa si inabidi apunguze mawazo kwa kutembelea nchi nyingine!!!!?? Kwani Nyinyi hamjui kuwa alipata marafiki wengi nchi za nje wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje??? Sasa huu ndio wakati wake wa kwenda kuwatembelea jamani...Hii ndio Tanzania, nchi yenye amani raia wake wanabaki kulalamika kwenye vijiwe, kwenye blogs mbalimbali na ndani ya JF. Finaly tunasahau na kusahau yote yaliyofanywa na serikali ya CCM.Tusiahau kale ka wimbo ketu; TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA SANA....
The Farmer,
Ukweli ni kuwa Tanzania haihitaji kabisa hiyo misaada. Kwenye ile bajeti ya Ze Comedy (JK), ukiondoa pesa;Utaona kuwa Tanzania haihitaji msaada wowote kwa ajili ya bajeti yake, maana mahesabu yake yangebalansi vizuri kabisaa.
- Zinazoibiwa kila mwaka kulingana na mkaguzi wa mahesabu,
- Zinazopotea kwenye tenda kama za ID, Dowans, Ujenzi mbali mbali, n.k
- Zinazopotezwa na wasiolipa kodi kama Rostam n.k.,
- Ukiondoa gharama za ziara za JK,
- Ziara za Mama Salma,
- Ziara za Mawaziri nje ya nchi,
- Ziara za Mawaziri nchini,
- Ziara za Mawaziri (kuelezea bajeti),
- Gharama za kununua na kubadilisha Mashangingi kila mwaka,
- Ongezea nyinginezo hapa...........
Hivi kwa nini ziara kama hizi JK asimtume Membe??
Kwani ni lazima yeye awepo physically?
Nani ataiokoa nchi hii na upuuzi huu!!
Kwa staili hii ya kuzurura hovyo, katiba yetu inatakiwa kuwa na kipengele juu ya ziara za Rais nje. Zisizidi tano kwa mwaka!
Hivi entourage yake inakuwaga na watu wangapi kwenye safari hizi?
Nani ataiokoa nchi hii na upuuzi huu!!
... Nadhani Tungeanzia Hapa ili Kujua Damage Tunayoingia Kila Pale Mkuu Anapokwenda Kuvumbua Nchi Mpya...!