Me nadhani hii ndio serikali hopeless kuliko zote tulizowahi kuwa nazo. Yaani huyu jamaa dah tumeliwa kwa kweli tumeliwa. Matatizo ya hii nchi kwake si issue bali kutalii ndio muhimu kwake. Juzi ameenda Mbagala mikono mfukoni anaangalia wahanga wa mabomu kama vile wanyama wa Mikumi. Lakini mimi sishangai kwani ninamjua nilishangaa tu watz kumpa nchi. Alipokuwa mambo ya nje aliwahi kuweka record ya kusafiri nje consecutively kwa miezi mitatu, hii record haitavunjwa milele nadhani. Ila kama kuchemsha ndugu zangu hapa tulichemsha. Na mtoto wa mkulima naye ndio dah jamani hivi kosa gani hilo kubwa tulifanya kwa Mungu mpaka atupe viongozi fake kiasi hiki?