JK, wengi hamjamwelewa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, wengi hamjamwelewa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vision2010, May 28, 2009.

 1. V

  Vision2010 Member

  #1
  May 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KILA nchi na jamii inavyo vigezo vyake vinavyotambulisha ubora wa jamii hiyo na watu wake, ndani na nje ya nchi hiyo. Na Tanzania siyo tofauti katika ukweli huu.

  Vigezo hivyo viko vingi na kwa namna nyingi na tofauti. Moja ya vigezo vipya vilivyoibuka katika miaka ya karibuni ni teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya kompyuta na matumizi yakee.

  Mawasiliano hayo pia yako mengi na ya aina mbali mbali vile vile. Moja ya mawasiliano hayo ni matumizi ya blogo na inteneti.

  Kama kuna kitu kinathibitisha ubora wa chini kabisa wa mawazo ya baadhi ya Watanzania, na hasa wale vijana waliokimbilia nje kwenda kuzamia ana kujilipua baada ya kwa wamepasua ama kutupa pasi za kusafiria za Tanzania ni aina ya majadiliano kwenye blogo na inteneti za Kitanzania.

  Siyo tu kwamba kinachojadiliwa wakati wote ni ujinga, upuuzi, matusi na ukosefu mkubwa sana wa heshima kwa watu wengine. Lakini pia kuna uongo na upotoshaji mwingi, mwingine ukiongozwa na mwelekeo wa kisiasa, mwingine ukiongozwa na ujinga wa kutokujua mambo.

  Linganisha blogo na inteneti za Kitanzania na za Waafrika wengine nje ya Bara la Afrika. Angalia inteneti za Wakenya, Waganda, za Waghana, za Afrika Kusini. Watu wanajadili mambo ya maana ya maendeleo yao na kuchuana kikwelikweli kwa nguvu za hoja. Unapata mawazo na maoni adhimu na adimu, siyo matusi na ujinga.

  Sisi tumebakia kwenye matusi na ujinga tu. Najua kuwa moja ya matatizo yetu makubwa ni kwamba baadhi ya Watanzania waliokimbilia nje ni vijana waliokwenda kuzamia na kujilipua tu. Ni watu wasiokuwa na uwezo mkubwa wa elimu, ni watu wasiojua mambo isipokuwa uwezo wa kuvunja sheria za wanakoishi na kuwakimbia polisi. Hivyo haishangazi kuona kiwango cha chini cha mawazo katika inteneti za mawasiliano za Kitanzania.

  Iko mifano mingi. Lakini angalia ujinga ambao umekuwa unaandikwa kuhusu ziara ya karibuni ya Rais Kikwete mjini Los Angeles, Marekani, ambako miongoni mwa watu wengine alikutana na nyota watengenezaji na wachezaji sinema kama vile Steven Seagal, Billy Zane na wengine.

  Wamejitokeza watu kwa kutumia inteneti za Kitanzania kumkejeli, kumdhihaka kama vile mkutano huo na nyota hao mabilionea hauna manufaa na kama vile mabilionea hawa ni watu wasiostahili kukutana na Rais.

  Ni ajabu kwamba mtu anaweza kuishi Marekani, ama nchi yoyote ya Ulaya, na bado akashindwa kujua uwezo umuhimu mkubwa wa watengenezaji na wachezaji sinema hawa.

  Hawa siyo waosha masufuria, wanyanyua mizigo viwandani, ama waonya mabehewa ya treni kama tulivyo sisi wengi Watanzania tuliozamia nje. Hawa ni nyota. Ni matajiri wenye fedha nyingi kuweza kuwekeza katika nchi yoyote.

  Nyota hao, kwa mfano, wanataka kwenda Tanzania kufungua Tanzania Studios ambazo zitakuwa za kwanza katika sub-saharan Africa kwa sababu studio pekee za kutengenezea na kucheze sinema kwa sasa ziko katika Afrika Kusini tu katika Bara zima la Afrika.

  Ikichezwa sinema moja tu katika Tanzania kiasi cha watu 400 ama zaidi watanufaika moja kwa moja na utengenezaji wa sinema hiyo. Ukitilia maanani kuwa kila mtu ana familia ya wastani watu watano, unazungumzia watu 2,000. Hawa ni mbali na wale watakonufaika kwa namna nyingine nyingi zisizokuwa za moja kwa moja.

  Kiasi cha dola za Marekani milioni 200 zitaingia katika uchumi wa Tanzania kwa sinema moja tu kuchezwa katika Tanzania ambayo inayo mazingira mazuri ya kuchezea sinema.

  Kazi kubwa ya Rais wa nchi yoyote ni kuvutia wawekezaji wenye fedha kwenda kuwekeza katika nchi yake. Mashindano ya dunia ya leo baina ya mataifa ni uwezo wa kuvutia wawezekezaji. Uwekezaji ndiyo unainua uchumi, na uchumi ndiyo uti wa mgongo wa nchi, siyo bla bla za matusi na ujinga wa kwenye inteneti.

  Je siyo kweli kuwa kama itatengezwa sinema moja nchini na kuinufaisha nchi kwa kiasi cha dola milioni 200, basi nchi itakuwa imepata kiasi kikubwa zaidi kuliko kiasi chote kinachoingizwa nchini na Watanzania wote walioko nje?

  Sasa kejeli ya nini, ama tunajaribu, kwa mara nyingine, kuthibitisha ujinga wetu kama ambavyo tumezoea kujianika hadharani?

  Isitoshe kama kweli tunaipenda nchi yetu kama ambavyo baadhi wanaandika kwa “uchungu mwingi” kuhusu maendeleo ya Tanzania kwa nini tusirudi nchini kwenda kushirikiana na wenzetu ambao wanahangaika usiku mchana kuiendeleza Tanzania.

  Sisi tuko huko, tukicheza madisco na kunywa pombe, na tukiamka ni kuporomosha matusi kwa watu ambao wanapinda migongo katika kutafuta jinsi ya kuiendeleza Tanzania na ndugu zetu tuliowakimbia.

  Kama kweli tunaijali nchi na ndugu zetu kwa nini tusirejee na kushiriki katika harakati za kuendeleza nchi, badala ya kila siku kushikilia kuwa tupewe dual citizenship? Tunataka urais wa Marekani, ama Uingereza, ama Canada wa nini kama tuna uchungu na nchi yetu ya Tanzania?

  Baadhi yetu hatuko honest. Ni wanafiki tu. Tunapenda kufaidi pande zote tukiongozwa na hadhithi ya chako ni changu, na changu ni changu.

  Ambani Adnani Joseph

  Mtanzania
  – Los Angeles.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Vision 2010,
  Kwanza karibu sana JF. Naona hii ni post yako ya nne. Unafanya kosa kubwa sana kugeneralize au ku-stereotype kuwa wengi wetu tulio Marekani tumejilipua au ni vijana wasio na elimu. Ukiangalia sana JF utakuta kuna vichwa kweli kweli.

  Kikwete ni kiongozi wa nchi yetu, na anapovurunda tunayo haki ya kusema kuwa hapa Mheshimiwa kavurunda. Kama umezoea lugha ya kusifia tu kila anachofanya kiongozi hapa si mahali pake. Tumeulizia tija ya safari lukuki anazofanya nje ya nchi muishimiwa. Kama ipo itaje.

  Tumeulizia mikataba anayosaini na aliyosaini ikiwa pamoja na kumkaribisha Sinclair achimbe dhahabu yetu. Na sasa amesaini mkataba na Wasaudi waje kujilimia mchele kana kwamba sisi hatujui kulima mchele. Kama kuna tija itaje.

  Tunaipenda nchi yetu hata zaidi ya vile unavyodhania. Siyo kila mpenda Tanzania lazima awe Tanzania. Leo hii maadui wakubwa wa Tanzania njema wako Tanzania. Tena wana vyeo vikubwa tu serikalini. Wewe unataka tuwainamie tuwaite waheshimiwa? Hapana. Tutaendelea kuwakosoa na kuwalaumu.

  Karibu sana JF.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hata G.W Bush alidhihakiwa, na wamarekani wasomi kabisa.

  Contrary to your opinion, jamii yenye wasomi na iliyo huru ndiyo inayokuwa critical na kuwachambua viongozi (kama Marekani na Ulaya Magharibi) jamii isiyo na wasomi na/ au iliyo chini ya utawala wa kidikteta kama Korea ya Kaskazini ndiyo huwezi kusikia rais anadhihakiwa.

  Halafu haya mambo ya kukoseana heshima kwamba kila mtu mbongo kajilipua yanaonyesha hali iliyokuzunguka.Kama wewe au/na jirani zako mmejilipua si lazima kila mbongo awe hivyo, kuna wengine wanaishi legally na relatively comfortable on a fast track career wise.Kwa hiyo matusi ya reja reja si mazuri.

  Halafu umekuja kwa ku-condescend watu kuhusu usomi, msomi hawezi kuleta issue kwa generalities kama ulivyoleta wewe, unakosa credibility.Kuipa credibility issue yako onyesha trends na toa mifano inayoonyesha a significant shift in trends to raise an alarm.Huo mfano wako wa Steven Segal kwa watu wanaoelewa information theory unatakiwa kuwa-expose hawa "wapuuzi" zaidi kuliko utakavyomdhalilisha Kikwete kama kweli hauna maana, kwa hiyo watu wanaoelewa maswala ya freedom of speech wanaona waachieni tu wasio hekima waonyeshe kutokuwa na hekima kwao, sasa kama wanajiumbua kwa nini unataka kuwaondolea means yao ya kujiumbua, if that is the case at all?.Msomi yeyote worth his weight in salt anatakiwa ajue kwamba the internet age is the age of more freedom of experession, not less, waacheni watu waseme wanachotaka as long as hawavunji sheria / hawawakosei heshima watu kwa mujibu wa terms of services za mitandao hii.Hii collectivist top down thinking ina mask an inner desire to cajole and forcibly control, so Stalinistic, so Soviet!

  Si kweli kwamba JF kumejaa jokers tu, ila wewe ukiwa joker unaweza kuona kila kitu ni joke.Hapa kuna kila aina ya input, kuanzia ma inteligentsia, ma literati, ma illuminati mpaka ma dadaist wanaofanya deconstruction za deconstruction na kufikiri outside the box that is outside the box.Halafu kuna vichaka na vicheche halafu kuna watu wa milupo, kuna watu wa ma party, kuna watu wa michezo, kila aina.

  Kwa hiyo jaribu kupunguza kuona mabaya tu, kwani utatuonyesha kuwa ni wewe mwenye kuakisi upungufu huu kutokana na upungufu wako.Tuna ma Sophist na ma pre-socratic philosophy experts humu, tuna ma constitutional lawyers, tuna ma hackers, tuna ma keyboard thugs, tuna familia bora na watoto wa viungani pamoja na washua zao na vile vile watoto wa uswazi.Kwa kifupi ni full mix ambayo ukiijulia utaifurahia lakini kama unataka kuleta u uptight utakoma mwenyewe.Kwani hata jioni kisomo mwenye akili anajua kazi na dawa, mradi usizidishe dozi tu.

  Kujenga nchi si lazima kila mtu ajazane Dar, kwani siku hizi kunama global economy, mtu anaweza kusunda mshiko mzuri na kutuma remmittance bongo.Sio lazima wote turudi, uchumi wenyewe mdogo hata tukitaka kuanzisha biashara purchasing power ya kuridhisha wote haipo.

  Dual citizenship is the impending tsunami, you can delay it but you can't avoid it, it is as simple as a modern day version of comparative advantage in Smithsonian economics.Sasa ni bora tulijue hili mapema na kuanza kulifanyia kazi kuliko kuacha wenzetu watupite kama mara zote halafu tunakuja kushtuka 2050 tunakuwa "Johnie come lately" wakati wenzetu wanakumbatia the next best thing.

  Last but not least I would like to point out the irony of your chagrin with the Tanzanian people in Diaspora, vehemently disposed by your strong "back to Tanzania" stand, grandly communicated from the comfort of Los Angeles California.

  You are like that old clergyman who kept insisting "Do as I say, not as I do". How exemplary.  Ni hayo tu.
   
  Last edited: May 29, 2009
 4. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #4
  May 28, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sawa. Sisi tuibiane, madini tugawe, gesi tugawe, samaki tugawe, elimu tuibake ... tuendelee kufisadiana tu ...

  Halafu tusubiri jamaa "mabilionea", wakiridhia na ombi letu, wacheze sinema mambo yetu yawe safi.
   
 5. L

  LeoKweli JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee Karibu Jamvini.

  Sifa nyingi ulizoziongelea pengine zinakugusa wewe moja kwa moja Lakini hapa JF kuna two types of Groups.

  Moja ni watu ambao ni very patriotic ambao wana nia ya kuona Tanzania bora , when they see anything that doesnt stand for the intrest of Tanzania they speak out and nothing will ever stop them.

  Number two kuna watu ambao they are here for special intrest, Wako hapa kuwatetea wale wanaofanya madudu, kwasababu kwa njia moja au nyingine wanafaidi from hayo madudu.

  Mheshimiwa bila kukuuliza maswali mengi ninaamini ulikwepo kwenye Dina ya Mheshimiwa Rais pale LA , na pale ndipo ulipoiuzia objectivity yako, Samahani but I think umeuza objectivity yako for a very cheap price yaani kitendo tu cha kuwa na mheshimiwa kwenye chumba kimoja, si kulaumu but watanzania wengi ndio walivyo.

  Hakuna mtu mwenye akili timamu anampinga mheshimiwa Rais kutafuta wawekezaji. Tunacho kiping ni kitendo cha Rais kuchota maji na kuyaweka kwenye pipa lililo toboka. Hauwezi kujaza pipa hata siku moja kama pipa lenyewe ulalo tia maji limetoboka na ndio maana hata kule kwetu uswahilini tunatumia common sense tukishajua hilo pipa limetoboka tunaweka cement chini ya pipa kwanza , na kuzuia kutu isilitoboe tena tunapaka cement pipa zima. Kwakufanya hivi it means hata mvua ya manyunyu inaweza kulijaza hilo pipa.

  Mfano huu una maana ya kwamba mheshimiwa Rais inabidi asafishe nyumbani kwanza, leo hata akipata dola Billioni moja , wananchi masikini wataona milioni 10 tu zilizobaki zitaishia kwenye pipa lililotoboka/ufisadi , akisafisha na awafunge mafisadi wote na kuweka mazingira mazuri ya accountability ataweza kufanya any investment anayoipata na kuifanya as multiplier factor but now anapoteza mda na hata pesa kidogo tulizonazo.

  Kama wewe ni mtu wa resorning hebu angalia. Kuwafunga mafisadi na kusafisha serikali kama yuko serious it only take three month which will save us alot of money . But hizo Investment unazosema wewe za kutengeneza movie Tanzania, planning and Implimentation yake it take three to four years which means JK atakuwa anakaribia kumaliza mda wake wa kipindi cha pili. Kwahiyo watu sio wanapiga kelele it all goest to time series and what is the priority ya Mheshimiwa and we as people we see that there is many can be done fast and efficiently to improve governmenment perfomance while we are waiting for those opportunities you talking about.

  Watu wote walioko kweny Jamiiforums hawako Ulaya na Marekani there are prenty of them in Tanzania utagundua hivyo ukiangalia trend za uchangiaji, karibu sana jamvini but I think we will have more opportunity to exchange ideas and we will give you resorn on why we critical to the president and not otherwise.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Blueray,
  Umemaliza kila kitu. God bless.
   
 7. A

  August JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hivi wewe kwa akili yako ya kuzaliwa tu unafikiri kuna mtu yoyote aliye serious anaweza kuja wekeza tanzania kwenye studio ya cinema ambapo umeme wenyewe nao tumia is less than 10% of the population, barabara mbovu, reli ndio hiyo tena bandari inachukua mwezi kutoa bidha zako, iliza kwa wenzako inachukua siku ngapi kutoa mzigo au kulipia tax. juzi umeona controller and auditor general amezungumzia cost za hizo ziara, alikuwa just diplomatic kwa kutouliza upande wa pili faida zake, juzi tena wachumi kama dr haji semboja amelizungumza suala hili, lakini pia kwa kutumia busara, akaepuka kusema hazina faida kwa kujifanya "kama" zina manufaa then it is Ok, otherwise ni upotevu wa Pesa na Heshima ya Mkuu wa Nchi, sifa hazitafutwi zitakufuata kama unafanya mambo mazuri. Angalia Kenya kwanini watalii wengi wanaenda huko? kwa sababu ya miundo mbinu inayo enda na vitu wanavyo vifuata. Leo hii Kagame anafanya vitu vyake umemsikia anakutana na Seagul, Unajua Raisi ni sawa sawa na Baba Mkwe je baba Mkwe atakufuata au utamfuata. unaweza ukamkuta baba mkwe kweli hana uwezo lakini kulinda heshim,a yake kuna mambo hawezi kukwambia au kukufuata.
  wewe unaonekana hujafundwa vizuri kama mwanaume au kama ni bibi unyago inabidi upelekwe tena pale magomeni kuna akinamama hutoa mafunzo hayo, kama ni mwanaume neenda kwa wakurya au wamasai watakupa hayo mafunzo. kizuri cha jiuza kibaya cha jitembeza, kuza uchumi wako weka miundombinu vizuri kila moja atakuja. Leo hii unaweza kuona hao akina seagul wanakwenda Seychelles au Namibia kwa sababu gani.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  May 29, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280

  Pole sana Ambani Adnani Joseph Kikwete.

  Najua kwako wewe na mawazo yako ya kukaa nje priority ni kutaka watanzania wawaze sinema! sio elimu kwanza, watu wajue lugha, sio washibe kwanza kilimo kipewe kipaumbele, wala sio kuwa na wataalamu wa kutengeneza video camera(sio kurepair) huwazi hayo mkuu??

  au hata mimi nina mawazo finyu kwa sababu niko nje ya nchi?

  Kipi bora tuwekeze kwenye elimu, kilimo na kuwa na viwanda vyetu wenyewe au tuangalie wamarekani, wahindi na wanigeria?? huku tukiwa watazamaji kwenye global stage of competition in almost everything???

  Ok no problem hawa jamaa wakija na kufanya watakavyo is this a big deal mpaka rais aende akaongee nao?? kwa nini JK asikutume wewe na ukamaliza kila kitu?? hatuna mawaziri??
   
 9. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2009
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ndugu Mtanzania,
  Nimeguswa mno na maelezo yako juu ya yanayoendelea nyuma ya pazia katika ziara za JK ambazo nyumbani zinapigiwa kelele nyingi mno na baadhi ya kambi zinazoona hazina umuhimu.

  Nakuunga mkono kwa hoja yako kwa sababu JK ni kinara wa aina mpya ya uongozi wa hatamu za nchi kama ambavyo Barack Obama na mkewe wanafanya... Yaani kuuvuka mipaka kwa masilahi ya nchi.... na kuwagusa watu wa kawaida.... Je tunajua kwamba Obama amemuiga JK kwenda kula Gengeni Kariakoo wakati alipoenda yeye na makamu wake Biden walipovamia Fast Food kwa ajili ya Pizza???? na wakatoa tip kwa mwuuzaji..

  Ninachowasihi wale wasio na subira au mwenye mawazo kinzani juu ya matunda ya ziara hizi wampe muda na matokeo yake tuyapime katika kipindi muafaka.

  Yapo mengi tu yanayoendelea nyuma ya pazia ..mikutano yake na watendaji wakuu wa makapuni ya kimarekani ikiwemo Microsoft na IBM juu ya uwekeaji mitambo ya kisasa ya TEHAMA kwenye chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kitapiku vyuo vikuu nchini ni jambo linalohitaji kufuatiliwa kwa hamu subira na kupewa muda kabla ya kuhukumu...
  ... JK pia anajua wakati muafaka wa kuvunja ukimya juu ya manufaa ya ziara zake..alishasema mara kadhaa na ataweka bayana wakati muafaka.... Waswahili hatutangazi jinsia ya mtoto kabla hajazaliwa.. TUSUBIRI SIKU YA KUZALIWA MTOTO TUTAJUA !!!!
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  May 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Vison2010,

  Mkuu nimeisoma hoja yako kwa makini sana na kusema kweli umeonyesha kiwango chako hafifu ktk kuelewa mambo. Huna exposure ya mambo mengi sana uloandika kwani kuwasifia watu kama Steven Segal na kumwita sijui millionea wakati umeshindwa kutueleza kukutana kwa Kikwete na huyo millionea kunaweza vipi kutusaidia sisi kama Taifa. of all movie star unamzungumzia Steven Segal ambaye hawezi hata kupata contract ya kucheza sinema ikaingia Theater..huyu ataweza vipi kutusadia sisi ikiwa maisha yake mwenyewe sasa hivi ni taaban.

  Kisha unaposema vijana wengi humu ni wakimbizi una maana gani?...Kama wakimbizi mbona wanarudi nyumbani kila mwaka uliona wapi mkimbizi akitudi kwao kila mwaka na huru kisha arudi nchi alioomba ukimbizi na akapokelewa akiwa na mhuri ktk passport yake kutoka kule alikokimbia!..Hivi unaelewa unachoandika au ******* maneno mdomoni..

  Mkuu elewa kwamba vijana wengi wanaishi nchi za nje kutokana na nchi hizo kuwa na opportunity zaidi kushinda nyumbani.. kusafiri na kkuhamia nchi nyingine ni moja ya maendeleo ya binadamu..Hiyo marekani alokwenda Kikwete imejengwa na wahamiaji. Toka waingereza, Wafaransa hadi makbila yote ya Ulaya ni wahamiaji..Na sijui Obama utamtukana vipi kama Mkenya alokataa kurudi kwao..maanake naona wewe matusi yanafungwa kama njugu ktk genge la nyanya... huchagui.
  Hiyo mitandao ya wenzetu Wakenya, waganda na wengineo umeshindwa kusioma vizuri na kuelewa inatokana na vitu gani. Kwanza blog zote za Kikenya zinazungumzia matatizo ya Kikabila..Huko ndiko utaona mgawanyiko wa Kisiasa kulingana na makabila yao na points zote huandikwa kwa kufuata kabila zao. Mjaluo hawezi kupongeza kabisa utawala wa Kibaki kwa sababu ya kabila yake..Hivyo hivyo Uganda na nchi nyinginezo utaona kwamba mijadala yao hutanguliza uzawa na kabila la mhusika..Tofauti na Tanzania ambao tunazungumzia matatizo ya safariu yetu na kama kweli Kikwete anatupeleka tunakokusudia kwenda..
  Wewe kwa mtazamo wako ni kwamba inatakiwa sisi Watanzania tumweklewe Kikwete anatupeleka wapi badala ya yeye tuliyempa dhamana kufahamu sisi tunataka kwenda wapi..Na nakuhakikishia kwamba kukaa kwako Tanzania muda wote sidhani kama unaelewa maendeleo ni kitu gani kwani hujawahi kuona zaidi ya sinema na kusoma magazeti. Lau kama ungepata hata kutoka nje ukaangaza dunia ungeelewa tunazungumza kitu gani kwani hapo ulipo huna mfano hata mmoja wa rais anayezunguka dunia kuuza nchi (kutafuita wawekezaji) huna isipokuwa Kikwete mwenyewe. Sasa nakwambia Wawekezaji hawatafutwi.. China ilipofuinuga milango yake watu walikwenda bila mtawala wao kuzunguka dunia.... Siku zote mkuu wangu Kizuri hujiuza, na kibaya ndicho kujitembeza kama wale wauza dagaa wabichi mitaani!..
  Hivi nikuulize Kikwete anapokwenda huko nje kuwavutia wawekezaji huwa anazungumzia vitu gani vya kuvutia?.. Mlima Kilimanjaro, Serengeti, madini na vitu ambavyo hao hao wazungu ndio walivitangaza na kutupa thamani ya vitu hivyo..

  Mkuu wangu hakuna sababu wala haja ya kutembelea dunia kujitangaza.. MTANDAO ni sokoni, TV programs ni soko, Advertisements sasa hivi sii kupiga la mgambo, adhana wala kengele au kumfuata mtu nyumbani kwake..isipokuwa media ndicho chombo kikubwa kuliko vyombo vyote kuweza kuitangaza nchi kwa mazuri yote unayoyafanya..Sasa kama kweli Kikwete bila kuizunguka dunia haiwezekani kitu basi nambie hizo balozi zetu zinafanya kazi gani huko nje ikiwa kila balozi ina idara ya biashara. hawa kazi waliyopelekwa huko nje ni ipi ikiwa kila kazi inatakiwa Kikwete afike mwenyewe..Kuna maonyesho mengi tu dunaini ambayo hawa vijana unaowatukana humu wangeweza kabisa kuwakilisha nchi yetu, hakuna haja ya mtu kutoka Serengeti au Zanzibar na mabango ya kuitangaza nchi wakati tuna vijana wanaishi nchi hizo.. kwanza lugha zao hamzifahamu kuongea nao kwa ufasaha.. mnatisha, kisha gharama zote za nini kwa nchi maskini kama Tanzania...Kila mwaka kuna maonyesho ya Utalii kila nchi kubwa Ulaya, wewe na wenzako hamyajui hayo isipokuwa EXPO 70! - Ga damn!..

  Matusi hata sisi hatupendi matusi na tunalaani vitendo ama hoja zinazoambatana na matusi lakini isiwe sababu kubwa ya kutozungumzia mstakabali wa nchi kwa sababu anayezungumzwa hapa ni kipenzi chako..na kwa mapenzi gani basi?..We all love our President na ndio maana tunajaribu kumwonyesha njia bora za Utawala kwa sababu tunafahamu wapi tunataka nchi yetu ielekee.. hatutumii ramli wala bao la Sheikh Yahya..
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Babuk,
  Siku nzuri dalili zake huanza kuonekana alfajiri. Huyu mheshimiwa JK amekuwa mamlakani miaka minne na ushee sasa, na wewe unataka tusubiri. Mwenzake Obama amemaliza zaidi ya siku mia moja ofisini lakini tumeshatambua mwelekeo wa uongozi wake. Kama wewe una subira sisi hatuna wakati tunaangalia madini yetu yanadizi kutafunwa na wajanja, na wawekezaji walioingia nchini mpaka sasa ni fake tu, wakati tunaangalia watoto wetu wako taabani kimasomo shuleni, wakati tunaangalia shangazi zetu wakifa wakati wa kujifungua kwa sababu ya huduma duni hospitalini. Kama wewe una subira, wengi hatuna.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  Anaingia mwaka wa tano sasa tangu aingie madarakani. Ni kipi alichofanya Kikwete hadi Watanzania tumuelewe!? Alitoa ahadi chungu nzima wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2005 na wengi Watanzania wengi tukamuamini. Alikuja na ahadi za kuipitia mikataba ya uchimbaji wa madini upya ili kuhakikisha kwamba Watanzania tunanufaika na rasilimali zetu, hadi hii leo hajafanya chochote. Alikuja na ahadi ya kuleta maisha bora kwa Watanzania, hadi hii leo hatujaona maisha bora yoyote bali hali ngumu kwa Watanzania walio wengi inazidi kuongezeka kila kukicha. Alidai ameingia Ikulu na ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya tunaona USANII TU kila kukicha!!!

  Tumemuona jinsi alivyokuwa muoga katika ufisadi mbali mbali uliofanywa na wengi waliosaidia katika kampeni zake za kuwania Urais 2005. Hawa si wengine bali ni akina Rostam, Karamagi, Subhash Patel, Jeetu, Chavda na wengine wengi na wote hawa pamoja na kuwepo ushahidi wa kutosha dhidi yao lakini wote bado wanapeta uraiani na hawatafanywa lolote na serikali ya Kikwete maana wakiamua kuyaanika yaliyofanyika katika kampeni za 2005 na wana mtandao na waliounga mkono basi Tanzania patakuwa hapatoshi!!!!!

  Tumeona jinsi alivyofanya uzembe wa hali ya juu wa kutotuma watu kumuhoji Balalli au kuhakikisha anarudishwa nchini ili kuhojiwa katika ufisadi wa EPA. Pamoja na Marekani kutoa offer ya kusaidia kumrudisha Ballali nchini, Kikwete alikaa kimya bila kusema lolote kufuatia offer hiyo mpaka Ballali akafariki. Wakati Ballali ameshafariki eti ndiyo ikatangazwa kwamba makachero Watanzania wameingia Marekani kumsaka Ballali ili kumrudisha nyumbani!!!!

  Tumeona alivyokaa kimya katika issues zote zinazomuhusu swahiba wake papa fisadi Rostam. Pamoja na ushahidi mkubwa kuhusiana na ufisadi wa Kagoda, Meremeta na Deep Green hakuna hata mmoja aliyefunguliwa mashtaka hadi hii leo.

  Kiwira nayo mpaka kesho kutwa bado haijulikani hatima yake pamoja na kuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya Mkapa na Yona kwamba waliiba mgodi ule.

  Sasa ni lipi hasa ambalo amelifanya Kikwete unataka tumuelewe!? Wakati wa kumuelewa umeshayoyoma na wengi hatuna haja ya kumuelewa. Kama ana mapenzi kweli na Watanzania na Tanzania ni bora tu atangaze kwamba 2010 hagombei tena ili kuinusuru nchi yetu badala ya kutaka tumuelewe baada ya kuwa Ikulu kwa more than 4 years.
   
 13. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #13
  May 29, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,854
  Likes Received: 2,426
  Trophy Points: 280
  ambani ..karibu but umeongelea movie as if ndio immediate needs ya kuifanya nchi isonge...i think you are just so excited kukaa chumba kimoja na rais ...humu ndani watu wanakula naye meza moja na bado wanakuja hapa kumpa ngumi za usoni..hatumchukii bali tunamsaidia kwa faida ya wote..and with your mind you think that ....cinema industry inaweza ku boom uchumi wetu kwa haraka ....kwanini hukumpeleka kule kwenye mashamba ya divai califonia ....ili aongee na wale wakulima wakubwa waje wajenge mashamba makubwa dodoma na kwingine....tuuze mvinyo duniani...huoni kuwa hizo sinema zenu..pamoja na umuhimu wake haziwezi kuajiri mamilioni .....zaidi ya kuajiri wauza sura wachache tu....

  As a nation ..we must have the agenda[priorities] and we expect our president to carry our agenda wherever he goes...do you think that rank top ten in our agendas....umeshasoma ilani yetu ya uchaguzi,...that is the voluntary contaract between voters and the gorvernment...and we expect our president to carry that along with his holly qouran or bible...and hata akikutana na mtu anataka kusaidia anajuwa kuwa kwenye ilani ni kitu gani bado!!!...........mwaka 2010 hatutamuuliza kwanini hajajenga HOLLWOOD hapa ..;;Tutataka kujuwa yake tuliyomtuma kwanza.....na hayo ya ziada kama yatafanyika ni kama bonus..tu!!!

  unakubaliana na mimi kuwa rais habebi ajenda zake vema !!??? [nashukuru alipokutana na obama aliingia na nondoz.....angalau ameweza kuongea yaliyo kwenye ajenda .....]....ukikaa na rais kikwete ni muongeaji mzuri ....anaweza kuongea usiku kucha ....na kwa wewe uliye hapo ukimsikiliza utafikiri kesho tu tanzania inakuwa newyork na .....lami itakuwapo hadi kijijini kwako....he talks dreams ..nadhani kama umepata wakati wa kukaa naye ..utashangaa hata kwanini watu wana m challange..!!...utekelezaji ndio tatizo....tunaye rais ambaye anajuwa vema matatizo ya watanzania .....ana nia ya dhati ya kuyatatua ...lakini hawezi na hana uwezo...he is idealist!! and neither practical nor capable!!!

  nadhani kauli kama yako ...hata tukikaa na wenzetu wakenya na majirani kwa ujumla ...wanasema tunaye rais mzuri..kaama sisi tulivyomuona mwaka 2005!!!...tatizo kutekeleza[if wishes were horses beggers could ride on...]

  hakuna shaka kuwa kwenye sera za nje rais kikwete aanafanya vema ...tena sana tu,tatizo ni ndani..watu bado wanasubiri!!

  anyway karibu .... with time utatuelewa ....naomba take time kusoma kwanza kabla ya kulaumu ....kwani kwa miaka mingi hapa tumefanya kazi ya kuweka serikali sawa...sidhani kama ni busara kuilinganisha JF na blogs nyingine....!!..kote huko napita blogs za wakenya ,waganda, etc zimejaa matusi na chuki...hapa watu wapo analytical and constructive !!....sio sawa ukija na hukumu tu kwa sababu labda mazungumzo yaliyotawala pale oakland au florida waakati mnapewa chakula cha usiku kilichogharamiwa na pesa za walipa kodi maskini wa tanzania yalikuwa ya kuilaani JF.....ulitegemea nini hasa!!
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  May 29, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,854
  Likes Received: 2,426
  Trophy Points: 280

  siku hizi kwenye vikao vya chama ukitaka uporwe microphone....sema kile kibwagizo cha kikwete kwenye kampeni!!!......CCM oyeee!!! Maisha bora kwa kila mtanzaniaaa!![kiitikio:yanawezekanaaaaa!!} Tanzania yenye neemaaa[.....]...kwa ARI MPYA ,NGUVU MPYA na KASI MPYA!!!

  SASA shangaa yeye mwenyewe na kukiogopa kibwagizo kilichompa ushindi mwaka 2005!!....ni kama Obama akimbie kibwagizo chake cha YES WE CAN!![SIDHANI] eeh ..THE CHANGE WE CAN beleave IN!!

  mtu anayekimbia IMANI na sera yake mwenyewe ni mtu ambaye haamini kwa kile anachokisema ,rais kikwete ni mmoja wao...ningekuwa miimi ndio yeye ningeendela kuhubiri kibwagizo changu haata dakika ya mwisho!!!
   
 15. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #15
  May 29, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280

  Hii inauma mkuu we acha tu! nasikia matumbo yanachezacheza!
   
 16. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Naomba nitoe tamko rasmi la JF kama Premium Member nijibu hii hoja ya huyu ndugu Ambani.

  Sijui ndugu yangu umekaa Marekani hii kwa muda gani au unaona nini cha maana na kipaumbele, lakini kwa kauli zako na jinsi ulivyoshupalia kian Billy Zane na Steven Seagal, inaelekea ama umeshuka kutoka Amistad majuzi au huku uliko, weye ndiye unayekimbia hata ukiona mgambo ukiogopa kukamatwa na kurudishwa nyumbani!

  Nikujibu kwa kuanzia suala la hao Movie Stelingi na hayo mapato unayoyasifia. Kwa taarifa yake, Steven Seagal na Bill Zane si wachezaji sinema ambao wanaweza hata kulipwa Dola milioni moja kwa sinema moja sasa hivi.
  Pili hata wakichezea sinema, sana sana bajeti ya sinema wanazocheza si zaidi ya Dola milioni 10 na hiyo ni risk kubwa sana kwa kutegemea hawa jamaa wawili unaowasifia.

  Huyo Billy Zane mshiko mkubwa liowahi kupata ni Milioni 2 mwaka 1999 alipokuwa kwenye show ya Televisheni na ni mshiko wa series nzima na si episode.
  Steven Seagal, anajitahidi kutoa movie, lakini zinakwenda kwenye video kama si Television za kawaida na si Cable. Ndio ana project yake ya philanthropy kuusu Humanitarian focusing in AIDS, lakini si mvuto wa kutengeneza fedha hivyo hizo dola zako Millioni 200 unazoziringia sijui umezitoa wapi huku inajulikana wazi kuwa Barrick Gold wanaochimba dhahabu yetu na kujipatia karibu Dola Bilioni moja kwa mwaka, huipa Serikali ya Tanzania Dola milioni moja (By the way, ni huyo huyo Kikwete aliyetuletea Barrick ambayo imeajiri Watanzania kibao ambao mpaka keshi ni masikini!).

  Nikija kwenye uhalisi wa kuvutia watu waje kutengeneza Sinema Tanzania, jiulize kwa nini Sinema zote ambazo zina kittu kuhusu Afrika watengeneza filamu wengi huishia kwenda Afrika Kusini, Namibia na Botswana na si Tanzania? NI kitu gani ambacho na urahisi wa maisha na kima cha chini cha mishahara ambacho kinawazuia Wamarekani au Watengenezaji Sinema wakubwa kuvuna kwa kuja kutumia soko la bei poa kama Tanzania? Jibu lake ni Maji, Umeme, Afya, Elimu, Miundombinu na Uduanzi wa Hujuma, Rushwa, Ukiritimba na Uvivu!

  Sasa nikija kwa upande mwingine wa kudai Rais Kikwte anakutana na wenye pesa, nikuulize, si tuliwalipa Wamarekani weusi waje pale Arusha na Sullivan yao, je ni wangapi iwe ni Chris Tucker, Shaq, Tyson, Denzel, Maxine Walter, Michael Steel na wengine ambao wamerudi na kuwekeza na kutoa hizo ajira unazosema?

  Je mwenzetu ulisoma makala ya Economist ambayo watu humu wanadai Mkenya kaandika na kukasirikia Mwandishi na si maudhui ya makala?

  Sasa kama unataka kuongelea watu wenye pesa au kuleta maendeleo, nikuulize, alipokuja Bob Geldorf kwa nini alimtukana kiutuuzima Rais Kikwete kuwakingia vifua wahujumu na wala rushwa halafu wewe lwo unakuja unasema wanaolalamika wapande mchuma warudi kujenga Taifa?

  Kwa taarifa yako basi kwa kuwa wewe ni msomi au mpembuzi mwenye uchungu nakuahsa hivi. Kila safari ya Rais Kikwete kuja Marekani hugharimu si chini ya Dola Milioni moja za kimarekani.

  Tangu awe Rais wa Tanzania, amekuja Marekani karibu mara 10, hiyo ina maana Dola Milioni 10 ya kusafiri kuja Marekani pekee, bado hajaenda Ulaya, Asia na sehemu nyingine za Afrika.

  Jiulize, ikiwa kila safari zinatumika fedha nyingi namna hiyo, halafu hakuna anayerudisha mabaki au kutoa tathmini halisi ya fedha zilizotumika na faida au matunda ya mtaji huo, huoni kuwa basi hao wabeba maboksi walioko Omaha, Cardiff na hata Seoul wana haki kulalamika kwa sababu Wazazi wao wanateseka kwa kukosa hata Panadol kisa Serikali inasema hakuna pesa, lakini Rais keshatumia si chini ya Dola Milioni 20 tangu awe Rais kwa ajili ya kusafiri nje ya nchi?

  Unazungumzia wenye pesa, nitakupa Upembuzi mwingine uutfakari. Nakuuliza hivi, kwa nini nchi yetu ilipokuwa ikikabiliwa na hali mbaya ya hewa ya kukosa mvua na kujulikana wazi tutakosa umeme, Rais Kikwete alipokuja Marekani miezi kadhaa kabla ya Tanzania kuingia mkataba na Richmond, kwa nini hakuomba Ikulu au Wizara ya mambo ya nje ya Marekani impigie krosi akutane na jamaa wa GE ambao wanatengeneza mitambo ya kuzalisha umeme na vifaa vya umeme?

  Je si inafahamika wazi kuwa Tanzania tuna uhaba wa vifaa vya hospitali, mbona hajaomba kukaa chini na kina GE, Siemens, Phillips na wenginewe aingie mkataba wa bei nafuu tuuziwe kwa riba ndogo au bei poa vifaa vya kisasa vya hospitali ili kuachana na gharma za kupeleka watu nje ya nchi kwenda kufanyiwa MRI au CAT Scan?

  Marekani hii si ina matajiri walioelimika na shule nyingi, mbona hatujasiki abaada ya kupewa shahada na St. Thomas ya kule Minnesota kusikia Rais akiomba au kuandaa mchakato wa vyuo vikuu vikubwa vya Marekani hata hiyo Stanford aliyoitembelea majuzi huko California waje Tanzania na kusaidiana na Wizara ya Elimu na kuboresha elimu ya Tanzania?

  Je katika mahusiano yake na Bush na kutembeza bakuli, amewahi kuomba basi hata Peace Corps waongezwe wanaokuja Tanzania waje kufundisha Watanzania kazi mbali mbali au kufundisha mashuleni, kama si kuja kama matabibu?

  Nitamaliza kwa kusema nilitumia muda wangu kusoma mada yako kwa kuwa nilidhani nitapata mwangaza mpya kuhusu Rais Kikwete ambao ni tofauti na ule nilioukwisha ufanyia tathmini mara nyingi mpaka nikaamua kuacha kumchambua kama mchicha.

  Naam umeamsha ghadhabu za Mchungaji aanze tena kumfanyia tathmini Rais Kikwete na tujue tumepata faida gani tangu awe Rais wa Tanzania!

  Rudi wewe kwanza Dar Es Salaam ukawatengenezee kina Steven Seagal na Billy Zane mikakati ya kuwapiga picha Wamasai wakiruka mori na rubega, halafu tukishapewa hiyo Cheki ya Dola Milioni 200, basi nitarudi kukuomba kazi!

  Gaademu Ninkampupiism!
   
 17. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hii kweli ni Babu Kubwa!

  Unafurahisha Baraza au ndio ukweli wa mambo unatuambia na ndio majigambo ya Muungwana mkiwa naye vijiweni?
   
 18. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tusubiri siku ya kuzaliwa mtoto hata kama vipimo vya kitaalam vinatuonyesha kuwa atakayezaliwa si mtoto bali ni chura?Busara zinapaswa kuendana na wakati.Hizi si zama za kale ambapo ilikuwa impossible kufahamu jinsia ya mtoto kabla jajazaliwa.Teknolojia imepiga hatua,ndugu yangu!

  Tukiachana na mifano ya "jinsia ya mtoto",ni dhahiri kuwa hatuhitaji kusubiri siku JK atueleze namna gani amekuwa akiwakumbatia mafisadi kama Rostam Aziz na genge lake.Ni ubabaishaji wa hali ya juu kusikia JK akiwaomba wahandisi wampatie orodha ya mafisadi kwenye sekta ya ujenzi wakati alipokuwa Bandarini Dar alitangaza anawafahamu mafisadi wa mahala hapo na hadi leo hajawachuluia hatua.Hivi wewe mwenye akili timamu huwezi kujiuliza kuwa huyu mtu ni m-babaishaji aliyekubuhu?Kipi rahisi,kusubiri upatiwe orodha ya mafgisadi ili uchukue hatua au kuchukua hatua kwenye listi ambayo tayari anayo?

  Na kwanini aombe makandarasi wafanye kazi hiyo wakati kuna vyombo vyenye wajibu huo,na wanalipwa kufanya kazi hiyo?Na hata tukiliweka hilo kando,kuna uhakika gani kama atachukua hatua ilhali tunakumbuka hotuba yake ya 2006 kuwa anawajua wala rushwa (mafisadi) na anawapa muda wajirekebishe?

  Tatizo lako wewe na huyo Vision2010 (hili jina linaweza kueleza bayana kuwa huyu anajipendekeza akumbukwe 2010 not knowing kuwa zama hizi za ufisadi kujikomba kwake,ashakum si matusi,kutiashia kuwa mithili ya condom:used and disposed of) ni KUJIKOMBA,Period!
   
 19. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  thanks kishoka!!

  Unazungumzia wenye pesa, nitakupa Upembuzi mwingine uutfakari. Nakuuliza hivi, kwa nini nchi yetu ilipokuwa ikikabiliwa na hali mbaya ya hewa ya kukosa mvua na kujulikana wazi tutakosa umeme, Rais Kikwete alipokuja Marekani miezi kadhaa kabla ya Tanzania kuingia mkataba na Richmond, kwa nini hakuomba Ikulu au Wizara ya mambo ya nje ya Marekani impigie krosi akutane na jamaa wa GE ambao wanatengeneza mitambo ya kuzalisha umeme na vifaa vya umeme?

  Je si inafahamika wazi kuwa Tanzania tuna uhaba wa vifaa vya hospitali, mbona hajaomba kukaa chini na kina GE, Siemens, Phillips na wenginewe aingie mkataba wa bei nafuu tuuziwe kwa riba ndogo au bei poa vifaa vya kisasa vya hospitali ili kuachana na gharma za kupeleka watu nje ya nchi kwenda kufanyiwa MRI au CAT Scan?  Gaademu Ninkampupiism!
   
 20. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2009
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nyota hao, kwa mfano, wanataka kwenda Tanzania kufungua Tanzania Studios ambazo zitakuwa za kwanza katika sub-saharan Africa kwa sababu studio pekee za kutengenezea na kucheze sinema kwa sasa ziko katika Afrika Kusini tu katika Bara zima la Afrika.

  Ikichezwa sinema moja tu katika Tanzania kiasi cha watu 400 ama zaidi watanufaika moja kwa moja na utengenezaji wa sinema hiyo. Ukitilia maanani kuwa kila mtu ana familia ya wastani watu watano, unazungumzia watu 2,000. Hawa ni mbali na wale watakonufaika kwa namna nyingine nyingi zisizokuwa za moja kwa moja.


  What a waste Ambani! Mimi naona urudi hapa Tanzania ili upate elimu zaidi kwa vile umepoteza muda wako kwenda kusoma U.S. na kuandika crap kama hiyo hapo juu. Nahisi nyie ndio wale mnaopata fursa kusoma nje na mkirudi hutundika shahada zenu ukutani na kujisifia. God forbid tusije kuwa na viongozi kama nyie! Ungeliandika hivi,....... Nyota hao kwa mfano, wanataka kwenda Tanzania kuanzisha Irrigation schemes kwa kujenga dams kwenye kila mkoa ili tuachane na kilimo cha kutegemea mvua. Irrigation project hiyo itakuwa ya kwanza katika East and Central Africa, kwa sababu serious irrigation schemes ziko Southern and Northern African countries kama South Africa, Zimbabwe, Egypt n.k.

  Tanzania ina bahati ya kuwa na mabonde mengi tena karibu kila mkoa na mobonde hayo hepeleka maji yote ya mvua baharini kila msimu wa mvua. Kama viongozi wetu huko nyuma na mpaka leo wangekuwa na vision na kufanya plans za kwa mfano, kujenga Dam moja kila baada ya miaka mitano hivi, wewe unafikiri ni wa-Tanzania wangapi wangenufaika tena mijini na na hasa vijijini? Bado unafikiria usanii na cinema?
   
Loading...