JK wa VITUKO: Adanganywa daraja limekamilika, AAIBIKA!

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,529
8,614
....vituko vya rais wetu haviishi safari hii alifunga safari mzobe mzobe hadi songea kwenda kuzindua moja ya darala la kuvuka mto mkenda kwenye mpaka wetu na msumbiji....akabebana na protocal yake yote ...hadi mtoni akiwemo waziri wake membe..na makamu wa ccm..kwa mbwembwe...akitaka avuke hadi upande wa msumbiji kuashiria ufunguzi...lahaula!!!...kufika pale anakuta daraja lililogharimu bilioni 1.2..ndio kwanza ujenzi umefikia asilimia 35 %...duh....

nasema HILI NI TUSI TO PRESIDENTIAL INSTITUTIONS!!!!!!

..KWANINI advance team ya ikulu haikumshauri kuwa asiende kufungua daraja kwa kuwa halijakamilika kama anavyofikiri...

..kwanini uongozi wa mkoa wa songea na watu wa itifaki hawakuondoa ratiba ya kuzindua daraja huku wakijua kuwa halijakamilika..

..kwa nini wizara ya miuondo mbinu imemdanganya rais kuwa anaenda kuzindua daraja wazi ikjua kuwa daraja halijakamilika..kama ilivyodhaniwa..

..je rais wetu ni jeuri aliarifiwa maendeleo ya ujenzi na aliamua kwenda ..tu ili aongee ...HAKUONA KUWA HILI LINAENDELEA KUMJENGEA PICHA MBAYA KAMA RAIS WA KUDANGWANYWA DANGWANYWA NA ASICHUKUE HATUA YEYOTE?????....HAONI KUWA VITENDO KAMA HIVI VINAZIDI NA VINAMFANYA AONEKANE KAMA HAYUKO MAKINI.........

..LAZIMA TAASISI YA RAIS IHESHIMIWE ..HAIPENDEZI KUMPELEKA RAIS KWENYE SHUGHULI AMBAYO HAIJAKAMILIKA ......KAMA LENGO SI KUMDHALILISHA....NA HII INAONGEZEKA KWA KUWA MARA NYINGI RAIS BINAFSI HUSINGIZIA KUDANGWANYWA HALI HACHUKUI HATUA YEYOTE....

TUNAOPATA AIBU NI WATANZANIA KWA KUONEKANA KUWA URAIS WETU HAUKO MAKINI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna picha jamaa wameiweka kwenye Majira la leo jamaa wanaonekana wauinamisha utepe ili Mkuu aweze kupita badala ya kama ilivyo wajibu "Kutembeza Mikasi"..... Ni aibu kubwa sana kwa kweli, na kama walijua kuwa ishakuwa soo sasa kwa nini huo utepe haukuondolewa?

Haya tujitahidi tutafika tu, swali ni wapi tuendapo??
 
Hivi Ikulu yetu haina timu inayoenda kukagua sehenu kabla ya ziara za rais?
 
..RAIS ANATUTIA AIBU ...NAHISI KAMA KWA TUKIO KAMA HILI LA RUVUMA LAZIMA ATAKUWA AMEPEWA BRIEFING ..LAKINI AKALAZIMISHA KWENDA..MAANA SIONI KWANINI TUKIO KAMA LILE HATA HALIKUMUOGOPESHA MKUU WA MKOA NA WATENDAJI WAKE..KIASI CHA KUJIKOJOLEA....HUWEZI KUMDANGANYA RAIS NA UKABAKI HUNA WASIWASI KAMA RAIS HAKURIDHIA KUSHIRIKI KUDANGANYA WANANCHI......

NIMEANGALIA PICHA WATENDAJI WANAONEKANA SOOO RELAXED....NYUMA KASIMAMA MAMA JK KASHIKA SIMU....YA KUTUMA SMS..

KAMA RAIS AMESHAWAHI KUPEWA CHEKI KWENYE LILE TUKIO LA EXIM..FEKI ..MANENO NA TARAKIMU TOFAUTI..WHAT DO WE EXPECT..THEN KAMA AIDES WAKE NI HAWA WA KISHKAJI ...MTOTO WA MAKAMBA..MTOTO WA DADAKE SALMA ets ..tutegemee aibu zaidi...
 
Phil,

Is it the case kwamba amekwenda kukagua ujenzi (however awkward that is) kwani amesema ujenzi umekamilika?
 
Mkuu Pundit, ratiba ya Mhe. rais ilikuwa ni kufungua daraja (siyo kukagua ujenzi). Baada ya kufungua alipaswa kuvuka ili aende 4 Km ahead apako alikuwa anasubiriwa na viongozi wa Msumbiji kwa ajili ya sherehe za FRELIMO. Baada ya soo hilo Wizara ya miundombinu iliandaa boti ndogo ili imvushe Mhe. Rais hata hivyo aligoma na kumtuma Mhe. Membe.

tena ona Rais alivyozungumzia suala hilo ``Nikakatazama kale kaboti kaupepo nikasema Mmh, mimi Mkwere sijui kuogelea afadhali ya Membe, maana mwenzangu kaoa huko Mbambabay ataogelea,`` alisema.

you can see this saga is like comedy acted by Bi. Kiroboto.
 
Rais ashindwa kuhudhuria sherehe nchini Msumbiji

2008-07-27 14:24:02
Na Juma Nyumayo, PST Msumbiji

Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya FRELIMO nchini Msumbiji baada ya kushindwa kukamilika kwa daraja la Mkenda mto Ruvuma alilopangiwa kulifungua.

Kitendo cha Rais Kikwete kudanganywa kuwa daraja hilo limekamilika kimewakera wananchi wa eneo la mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ambaye angelifungua daraja hilo na baadaye kuhudhuria maadhimisho hayo muhimu kwa mwaliko wa Rais Armando Gwebuza wa Msumbiji.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Monica Mbega, aliwaaambia waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni kuwa Rais Kikwete angefungua daraja hilo lenye urefu wa mita 77, linalounganisha nchi za Tanzania na Msumbiji ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya Sh. bilioni 1.2.

Alisema mbali na kufungua daraja hilo, Rais angehudhuria sherehe za kutimiza miaka 40 za chama cha FRELIMO ambazo zingefanyika eneo la Macheje, nchini Msumbiji ambapo ni Kilometa tatu toka mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, mahali palipojengwa daraja hilo.

Kabla ya ziara ya Rais Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mbega, alisema Rais Kikwete angevuka daraja hilo la kihistoria ili kukamilisha uhusiano uliopo wa kisiasa na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa kiuchumi.

``Ufunguzi wa daraja hilo utasaidia kuimarisha uchumi wa Mkoa wa Ruvuma na nchi yetu kwa ujumla kwa maana kutakuwa na mawasiliano ya karibu zaidi hususani katika Sekta ya Biashara,`` alisema Bi. Mbega na kwamba daraja hilo ni mkombozi mkubwa kwa wana Ruvuma kwa kufungua biashara zao na kurahisisha usafiri.

Katika Ziara hiyo Rais Kikwete alimtanguliza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bara, Bw. Pius Msekwa na maofisa kadhaa wa serikali juzi kuhudhuria sherehe hizo ambapo walivuka kwa mitumbwi ya magome na boti dogo la upepo.

Rais Kikwete hakuweza kuvumilia, alimuuliza Mhandisi wa TANROAD mkoani Ruvuma kama kungekuwa na uwezekano wa kuvuka daraja hilo lililokamilika kwa kuwekwa kitanda mita 35 tu na eneo jingine kuwa wazi na haliwezi kukamilika kwa muda mfupi kwa visingizio vya kitaalamu ambavyo rais alifichwa hadi alipofika eneo hilo, akajibiwa haiwezekani.

``Mheshimiwa hakuna uwezekano,`` alisema Meneja wa Tanroad Mkoa wa Ruvuma aliyejulikana kwa jina la Kisimbo.

Pamoja na kufunga utepe wa rangi ya maji ya bahari na maua ili aukate, tayari katikati ya daraja hilo ulifungwa utepe wa njano uliokuwa ukionyesha kazi haijakamilika na haiwezekani kuvuka isipokuwa kwa mtumbwi wa upepo uliokuwa ukiendeshwa na askari wa Msumbiji uliotumiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, alipotumwa kumwakilisha Rais ambaye alikataa kuvuka na boti hiyo.

Rais Kikwete alisema katika mkutano wa hadhara mjini Songea, kuwa asingevuka mto Ruvuma kwa kutumia kijimtumbwi cha upepo ni kuweka rehani maisha yake na kulisababishia hasara taifa.

``Nikakatazama kale kaboti kaupepo nikasema Mmh, mimi Mkwere sijui kuogelea afadhali ya Membe, maana mwenzangu kaoa huko Mbambabay ataogelea,`` alisema.

* SOURCE: Nipashe
 
Rais Kikwete alisema katika mkutano wa hadhara mjini Songea, kuwa asingevuka mto Ruvuma kwa kutumia kijimtumbwi cha upepo ni kuweka rehani maisha yake na kulisababishia hasara taifa.[/SIZE]

Hasara kwa taifa how? Aaaaaaahhhhhhggggggrrrrrr!!!!!!!!
 
IKULU ,na all protocal officers+ Mkuu wa Mkoa na wote waliohusika bila kumsahau waziri wa Miundombinu pamoja na yeyote walipaswa saa hizi wawe wameachia ngazi.

Haiwezekani Rais kudanganywa , hii ni aibu kwa taifa kwani kama alikuwa anasubiriwa upande wa pili walijitetea kitu gani kuwa mbona rais hayupo pale?

Inatia hasira sana , haiwezekani kuendesha nchi kwa mizaha na kuigiza.

Mr. President Sir, this is insubbordination to you, take actions immediatelly, la sivyo kuna siku watakubeba mzobe mzobe kwenda kupokea wageni airport ambao hawapo.
 
Hakwenda kufungua bali alikwenda kuweka jiwe la msingi ambalo lilisubiriwa ili litakapowekwa iwe tayari daraja limeshafikia asilimia 35 na ndivyo alivyofanya yaani akutukanae hakuchagulii tusi.Na mwandishi amekurupuka tu kuandika yaani inaonyesha hajui kutofautisha sherehe.
 
uumh Mkuu Mwiba, na suala la kutaka kumvusha kwa kaboti ka upepo, ambako yeye mwenyewe Mhe. Rais alikakataa kwakuhofia maisha yake na kuamua kumtuma Mhe. Membe!

i am sure you are joking.
 
Mwiba unamwonea mwandishi kwa kusema kuwa amekurupuka, hapa tatizo lipo kwa wasaidizi wa JK na pamoja na Mkuu wa Mkoa kutokumwambia boss wake kuhusiana na daraja hilo.
 
Rais ashindwa kuhudhuria sherehe nchini Msumbiji

2008-07-27 14:24:02
Na Juma Nyumayo, PST Msumbiji

Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya FRELIMO nchini Msumbiji baada ya kushindwa kukamilika kwa daraja la Mkenda mto Ruvuma alilopangiwa kulifungua.

Kitendo cha Rais Kikwete kudanganywa kuwa daraja hilo limekamilika kimewakera wananchi wa eneo la mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ambaye angelifungua daraja hilo na baadaye kuhudhuria maadhimisho hayo muhimu kwa mwaliko wa Rais Armando Gwebuza wa Msumbiji.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Monica Mbega, aliwaaambia waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni kuwa Rais Kikwete angefungua daraja hilo lenye urefu wa mita 77, linalounganisha nchi za Tanzania na Msumbiji ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya Sh. bilioni 1.2.

Alisema mbali na kufungua daraja hilo, Rais angehudhuria sherehe za kutimiza miaka 40 za chama cha FRELIMO ambazo zingefanyika eneo la Macheje, nchini Msumbiji ambapo ni Kilometa tatu toka mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, mahali palipojengwa daraja hilo.

Kabla ya ziara ya Rais Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mbega, alisema Rais Kikwete angevuka daraja hilo la kihistoria ili kukamilisha uhusiano uliopo wa kisiasa na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa kiuchumi.

``Ufunguzi wa daraja hilo utasaidia kuimarisha uchumi wa Mkoa wa Ruvuma na nchi yetu kwa ujumla kwa maana kutakuwa na mawasiliano ya karibu zaidi hususani katika Sekta ya Biashara,`` alisema Bi. Mbega na kwamba daraja hilo ni mkombozi mkubwa kwa wana Ruvuma kwa kufungua biashara zao na kurahisisha usafiri.

Katika Ziara hiyo Rais Kikwete alimtanguliza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bara, Bw. Pius Msekwa na maofisa kadhaa wa serikali juzi kuhudhuria sherehe hizo ambapo walivuka kwa mitumbwi ya magome na boti dogo la upepo.

Rais Kikwete hakuweza kuvumilia, alimuuliza Mhandisi wa TANROAD mkoani Ruvuma kama kungekuwa na uwezekano wa kuvuka daraja hilo lililokamilika kwa kuwekwa kitanda mita 35 tu na eneo jingine kuwa wazi na haliwezi kukamilika kwa muda mfupi kwa visingizio vya kitaalamu ambavyo rais alifichwa hadi alipofika eneo hilo, akajibiwa haiwezekani.

``Mheshimiwa hakuna uwezekano,`` alisema Meneja wa Tanroad Mkoa wa Ruvuma aliyejulikana kwa jina la Kisimbo.

Pamoja na kufunga utepe wa rangi ya maji ya bahari na maua ili aukate, tayari katikati ya daraja hilo ulifungwa utepe wa njano uliokuwa ukionyesha kazi haijakamilika na haiwezekani kuvuka isipokuwa kwa mtumbwi wa upepo uliokuwa ukiendeshwa na askari wa Msumbiji uliotumiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, alipotumwa kumwakilisha Rais ambaye alikataa kuvuka na boti hiyo.

Rais Kikwete alisema katika mkutano wa hadhara mjini Songea, kuwa asingevuka mto Ruvuma kwa kutumia kijimtumbwi cha upepo ni kuweka rehani maisha yake na kulisababishia hasara taifa.

``Nikakatazama kale kaboti kaupepo nikasema Mmh, mimi Mkwere sijui kuogelea afadhali ya Membe, maana mwenzangu kaoa huko Mbambabay ataogelea,`` alisema.

SOURCE: Nipashe

Mwiba huyu naye kakurupuka?
 
Unajua hapa ndo utajua sisi wadanganyika ni kalaga bhao yaani mpaka leo hatujamjua raisi wetu ni mtu gani? Hivi unafikiri mkuu wa mkoa, waizara walikuwa wajinga kiasi hicho? na hawa jamaa usalama wa taifa? kwanza ki protocol hawa jamaa wa usalam wa taifa wana ratiba za viongozi in advance ya miezi hivyo walikuwa wamempa taarifa yote na allikuwa anajua na wala hili lakusema mtumbwi alikuwa anajua kuwa anaenda kupanda mtumbwi. JK asingeivunja hii safari anajaribu kujiweka mbali na huu mjadala wa muungano, habari za ndani wanasema CCM bara wameshtushwa na kauri ya serikali ya mapinduzi.
 
Mkuu Pundit, ratiba ya Mhe. rais ilikuwa ni kufungua daraja (siyo kukagua ujenzi). Baada ya kufungua alipaswa kuvuka ili aende 4 Km ahead apako alikuwa anasubiriwa na viongozi wa Msumbiji kwa ajili ya sherehe za FRELIMO. Baada ya soo hilo Wizara ya miundombinu iliandaa boti ndogo ili imvushe Mhe. Rais hata hivyo aligoma na kumtuma Mhe. Membe.

tena ona Rais alivyozungumzia suala hilo ``Nikakatazama kale kaboti kaupepo nikasema Mmh, mimi Mkwere sijui kuogelea afadhali ya Membe, maana mwenzangu kaoa huko Mbambabay ataogelea,`` alisema.

you can see this saga is like comedy acted by Bi. Kiroboto.

hata sioni tena umuhimu wa kumuita mheshimiwa ... kwa mambo yake ya ajabu ajabu
 
upande wa msumbiji kuashiria ufunguzi...lahaula!!!...kufika pale anakuta daraja lililogharimu bilioni 1.2..ndio kwanza ujenzi umefikia asilimia 35 %...duh....

Nilichosikia kwenye TBC1 ambacho kilikuja kama breaking news baada ya taarifa ya mwandishi aliyepo kule Ruvuma kumaliza ni kwamba hivyo vyuma ambavyo vilitakiwa kufungwa ili daraja lipitike vilikuwa vimekamilika jioni ya jana, yaani baada ya Rais kuwa ameshaondoka!!! Haya mengine mimi sijui...

Lazima tukubaliane kwamba huenda ratiba ilikuwa tayari imepangwa in advance na rais hakuona sababu za kuivunja ratiba ati kwa sababu daraja halijakamilika...
 
IKULU ,na all protocal officers+ Mkuu wa Mkoa na wote waliohusika bila kumsahau waziri wa Miundombinu pamoja na yeyote walipaswa saa hizi wawe wameachia ngazi.
Haiwezekani Rais kudanganywa , hii ni aibu kwa taifa kwani kama alikuwa anasubiriwa upande wa pili walijitetea kitu gani kuwa mbona rais hayupo pale?

Inatia hasira sana , haiwezekani kuendesha nchi kwa mizaha na kuigiza.

Mr. President Sir, this is insubbordination to you, take actions immediatelly, la sivyo kuna siku watakubeba mzobe mzobe kwenda kupokea wageni airport ambao hawapo.

Sio JK, wala maofisa wengine wa serikali wanaoona umuhimu wa kuwajibishana. Hii ni serikali ya kishikaji na mambo yanakwenda kishikaji.
 
.

``Nikakatazama kale kaboti kaupepo nikasema Mmh, mimi Mkwere sijui kuogelea afadhali ya Membe, maana mwenzangu kaoa huko Mbambabay ataogelea,`` alisema.

...ooohoo kwa hiyo membe kaoa MALAWI nini...!!

benard membe ..presidential hopeful.........
 
Back
Top Bottom