JK: Vumilieni shida

watanzania wa kawaida wasiomjua wakiona hizi kashfa wanaweza kufikiri utani...lakini ndio hali halisi...nyingi hapa .....tayari zinajulikana ...

hiyo ya kina gogo inasikitisha sana....mama kilango anayo machungu makubwa rohoni...HUYU GOGO ...ni yule ndugu yake jk ...ambaye anapiga deals maskani kariakoo jirani na idrissa mosque...anaitwa HAMIS ...Yupo na jamaa wengine wa bagamoyo mmoja wao kuna wakati alikuwa cuf..?

Ni sawa kabisa Philemon..Ni huyo huyo HAMISI GOGO ambaye ndiye anachochea mambo ya kidini Tanzania kwani katumwa.
Ndio huo huyo anayetuhumiwa kuhusika na surubu hiyo aliyokumbana nayo Mama Killango.
Na ndiyo maana JK hana cha kumwambia Mama Killango!
Mama ni VICTIM na ushahidi upo...Akitaka kuchukuwa nchi hata kesho anaweza.
Na JK ndio maana hana nguvu..Cha muhimu ni huyo mama awasikilize wazalendo la sivyo atabakia kuwa VICTIM milele.
 
Huu ni ukosefu wa maadili ya siasa. Ukichaguliwa kuwa kiongozi wa nchi unategemewa kuwa na majibu au mikakati ya uhakika ya kupambana na matatizo mbalimbali.

Kauli ya mheshimiwa ni sawa na mganga hospitalini kuwaambia wagonjwa wake wavumilie tu watapona ilihali hajatoa tiba.
 
Philemon samahani nilimaanisha Hamis Gogo ambaye ni mujahidina aliyekuwa CUF akahamia ccm na alimwezesha JK kushinda na pia kumwezasha mtoto wake pamoja na Benno kupata madaraka ndani ya ccm.
Na pia Khadija kupewa cheo ambacho hakipo kwenye katiba ya chama cha mapinduzi.
Privatirization ya kihivyo ni wazi itatuletea matatizo kwani mwananchi hana lake.
 
Vumilia Mwana Kalaghabaho. Huyo ni 'babasiasa'. Ndio baba wa nchi. Ni 'Kilongola' wetu. Ndiye anayetupa mwelekeo. Njia ndio hiyo. Hakika ni nyembamba. Wanaoipitia ni wachache. Tena ni wavumilivu. Hujifunga mikanda inayobana. Na vibwebe pia. Huzunguka nchi nzima. Kutuhamasisha tusife moyo. Wala tusife njaa. Sihasa wanaijua sana. Wapo 'wamejaa tele'. Wana mbwembwe nyingi. Na Ujasiri dhalili. 'Wanapepeta mdomo' vilivyo. Mithali wamezikariri zimetulia. Eti wanasema nini? Mvumilivu hula mbivu. Mbovu daima hawazili. Zimwi likujualo halikuli. Ila likikula halikwishi. Kikulacho ki nguoni. Lakini si mwako. Wewe sio wale. Ila wavumilie wale. Vumilia Mwana Mvumilivu!

Hii mikanda ya kufunga watanzania walishaifunga toka vita ya Idi Amini Dada.
Na kama kuna watu wanasema tuendelee kuvumilia na wao wana upungufu wa akili.
Milioni mia nne na sabini kustarehe na Mke wa Kiarabu Kempiski wewe unaona huo ni Mkanda na Uvumilivu!
Hiyo ni tafsiri ya kifisadi.
CAPONE JUSTICE.
WELCOME TO THE MOB WAR!
 
Hivi huyu ni mwanasiasa au ni baba yetu?

Vumilia ni maneno niliyopata kwa baba na mama na sitegemei kuambiwa hivyo na mwanasiasa. Kama hana ufumbuzi aondoke Statehouse. MWISHO.

Usanii una kikomo.

Vumilia Mwana Kalaghabaho. Huyo ni 'babasiasa'. Mzee wa nchi. Ni 'Kilongola' wetu. Ndiye atupaye mwelekeo. Njia ndio hiyo. Hakika ni nyembamba. Wanaoipitia ni wachache. Tena ni wavumilivu. Hujifunga mikanda inayobana. Na vibwebe pia. Huzunguka nchi nzima. Kutuhamasisha tusife moyo. Wala tusife njaa. Siasa wanaijua sana. 'Wanapepeta mdomo' vilivyo. Mithali zimetulia wamezikariri. Eti wanasema nini? Mvumilivu hula mbivu. Mbovu daima hawazili. Zimwi likujualo halikuli. Ila likikula halikwishi. Kikulacho ki nguoni. Lakini si mwako. Wewe sio wale. Ila wavumilie wale. Vumilia Mwana Mvumilivu!
 
Mkuu jmushi,

Mimi nilikuwa busy sijaona hizo kashfa za JK zenye ushahidi, hizi huwa tunazipata juu juu na huwa yanakuwa ni maneno tuu ya watu. Sasa kama wao wanahusika na soo lililompata Mama Kilango ndio maana ana hasira sana na serikali hii sio? Sawa. Sasa kwanini tusianike hizi data jamvini kuharakisha mapambano mkuu? Zi-float hizo data hapa na ushahidi wake full wanachama washikwe na hasira za kutosha kuandamana hata bila nguo.

Inatia uchungu sana kama walimfanyia huyo mama Kilango mambo mengine ya ajabu nje na kumnyang'anya hizo 200M, inaonyesha serikali yetu ni ya maharamia watupu. Na kuna maneno mengi kuhusu uharamia wa huyu Nchimbi ambaye unasema anaweza kuja kuwa Katibu Mkuu wetu wa chama cha majambazi, ni haramia mwenzake na JK na aliyempa mbinu nyingi wakati wa uchaguzi wa ccm maana kuna watu walipoteza maisha kipindi cha kampeni kwa sababu mingi lakini inaonekana walikuwa wahanga wa vita dhidi ya kupata madaraka ya kuuza nchi yetu kwa starehe za ngono.

Tunaomba utumwagie dataz tupate akili mkuu, wengine tunahitaji kufanya upgrade ya system zetu tuelewe haswa nini kinaendelea na nini cha kufanya mkuu.
 
Mambo ni MBAYA Mkuu AKILI na ndio maana kuna HATARI YA DAMU KUMWAGWA!
Mama Killango ni VICTIM WA UNYAMA WA WANAMTANDAO!
Mungu amsaidie na pia cha kuelewa ni kwamba watanzania wote walioko nje ya nchi ni muda wa kufanya kitu na si kukaa tu!
Kuna wale wanaopata tabu hata ya kazi kwa kubaguliwa na mzungu ambaye kwetu ni Bosi na anamiliki nchi na watu wake!
Kama JK asipojiuzulu ama kukamata hao mafisadi...Basi vita haitaepukika.
 
Mwanzoni wananchi waliambiwa shida zao ni kwasababu ya wapinzani.
Sasa si wapinzani tena...NI VUMILIENI TUUU!

Kauli za Rais Kikwete zamkera Zitto Kabwe

na Irene Mark

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amemtaka Rais Jakaya Kikwete, kutotumia ziara zake za kiserikali kufanya kazi za kisiasa.

Zitto alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, katika mkutano wake na waandishi wa habari, kuhusu ziara ya Rais Kikwete katika Kata ya Mahembe, katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mei 26 mwaka huu. Kabwe ni Mbunge wa jimbo hilo.
Kauli iliyomfanya Kabwe aitishe mkutano huo ni ile iliyotolewa na Rais Kikwete kijijini hapo kuwa matatizo ya maji wanayoyapata yamesababishwa na wao kuchagua chama cha upinzani, hivyo aliwataka kutofanya makosa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 na kuichagua CCM.
Imeelezwa kuwa Rais Kikwete alisema hayo wakati wa ufunguzi wa Sekondari ya Mahembe, iliyopo katika Kijiji cha Mahembe, shule ambayo Zitto aliahidi kuikamilisha wakati wa kampeni za uchaguzi na kwamba alichangia ujenzi wake kwa asilimia 60.
“Namshauri Rais kuacha kabisa kufanya kazi za chama kwenye ziara za kiserikali kwa sababu fedha anazotumia ni fedha za walipa kodi wote… CCM inapokea ruzuku ya sh bilioni moja kila mwezi, atumie fedha hizo katika shughuli za kichama na si vinginevyo.
“Akiwa katika jimbo langu alitumia kauli za kibaguzi ambazo kama upinzani tukiendelea kuzinyamazia zitatuletea madhara. Lakini si hivyo tu, bali imenishtua kwa vile ni za kisaliti,” alisema na kuongeza kuwa kutokuwepo kwake kwenye ziara hiyo kulitokana na majukumu ya kitaifa aliyopewa na Rais Kikwete ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Shirikisho la Afrika Mashariki.
“Inaonekana rais amesahahu ama anapotoshwa na watendaji wake, aliniteua kukusanya maoni ya uharakishwaji wa shirikisho, hivyo nilikuwa kwenye majukumu mengine, lakini alisema sikuwepo, katika hali ya kawaida ninaonekana ni mtovu wa nidhamu.
Rais Kikwete pia alitumia hoja ya maji kuukandamiza upinzani kwa maelezo kuwa matatizo ya maji wanayoyapata yametokana na kuwachagua viongozi wa Chadema,” alisema Zitto.
Alisema kero za wananchi hazina uhusiano na siasa, hivyo maneno ya rais yana lengo ya kuyatenga kimaendeleo majimbo ya wapinzani na kusisitiza kuwa ni kauli za kibaguzi na kwamba wasaidizi wake wanampotosha.
Kuhusu tatizo la maji, Zitto alisema jimboni kwake wananchi wapo katika uchimbaji wa visima kwa ajili ya kutandaza mabomba ya maji kwa ufadhili wa shirika kutoka Hispania chini ya mradi wa maji wa mainjinia wasio na mipaka, unaotekelezwa na mradi unaofadhilia na Umoja wa Ulaya (EU).
“Nashangaa kwa nini Rais Kikwete alisema jimbo langu lina matatizo ya maji wakati ripoti ya umaskini ya Desemba mwaka 2005 inaonyesha asilimia 65 ya wakazi wa vijijini hawapati huduma ya maji safi na salama, hivyo si tatizo la Kigoma peke yake.“
Mfano, Wilaya ya Mkuranga, Igunga na Sikonge, zote zipo chini ya viongozi wa CCM lakini ndizo zinazoongoza kwa wananchi wake kutopata huduma za maji safi na salama wakati Wilaya ya Bukoba Mjini iliyokuwa chini ya upinzani inaongoza kwa kuwa na maji safi na salama.
“Si hivyo tu, wilaya nyingine ni Moshi Mjini inayoongozwa na upinzani, inaongoza kwa maji safi na salama … takwimu pia zinaonyesha asilimia 92 ya wakazi wa Mkuranga hawapati maji safi na salama wakati Moshi Mjini asilimia 97 ya wakazi wanafaidi huduma ya maji,” alisema Zitto.
Alisema ziara ya Rais Kikwete imemfanya aanze kufikiria upya kuhusu uhusiano wa kikazi kati yake na viongozi wa serikali, kwa kuwa hufanya kazi zake kwa ushirikiano bila kuwa na itikadi za kisiasa.
Zitto alisema mwaka 2010 Rais Kikwete, hataulizwa ni wanachama wangapi walijiunga na CCM, bali atahojiwa kuhusu utekelezaji wa ahadi za maendeleo alizozitoa na kuitaka Ofisi ya Rais itoe kauli kuhusu ukweli wa kauli za rais kwenye Kijiji cha Mahembe.
 
Ingekuwa heri JK uage sasa

Samson Mwigamba
Tanzania Daima~Sauti ya watu

MHESHIMIWA Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, salaam aleykum. Juma lililopita niliwasiliana na Watanzania wote kwa njia hii ya makala. Nilijaribu kuwachokonoa ili kupata mawazo yao juu yako.

Na kwa bahati nzuri nilikuwa nimeongea moja kwa moja na Watanzania wote wakiwamo wasaidizi wako muhimu. Na ili kuwahakikishia kwamba niliwalenga na wao pia niliamua kuwataja kabisa pale niliposema, “Yote kwa yote ni kwamba kila mtu anajua sasa Rais Kikwete uwezo wake wa kuliongoza taifa na chama chake umepungua.

"Ninaamini ndani ya dhamiri yangu kwamba hata wasaidizi wake, wakiwamo usalama wa taifa, mawaziri na manaibu mawaziri, wanamtandao na wapambe wake, wabunge, viongozi wenzake ndani ya chama, watendaji wake serikalini na wasaidizi wake wengineo wote wanajua hili”.

Nilifanya hivyo kwa makusudi ili kupata maoni yao juu ya hili. Nawatambua sana wasaidizi wako. Ni watu mahiri sana kwa kulinda maslahi yao na ya wakubwa wao. Nilijua watanijibu haraka haraka kwa kukanusha ukweli huo mdomoni huku mioyoni mwao wakiutambua. Lakini hawakufanya hivyo. Hii inathibitisha kwamba hata wao ukweli uliwagusa na wamefikia mahali ambapo hawawezi kupingana nao.

Wa kwanza kabisa kuwasiliana nami ni kiongozi wa zamani wa CCM katika mojawapo ya nafasi za uongozi ndani ya chama ngazi ya kitaifa. Yeye alinipigia simu kabisa na kujitambulisha kwa jina, nami nikamtambua kwa sauti kwamba ni yeye. Akanipongeza kwa kusema nimeandika vizuri sana na kwa kweli maneno yake na sauti yake yalionyesha dhahiri kukubaliana na ukweli niliouainisha.

Huyu ndiye akazidi kuthibitisha nilichokizungumza katika aya hiyo hapo juu. Ukweli umewasuta ndani ya dhamira zao na kwa kweli umefika wakati ambao ukweli hauwezi kufichika tena. Wengi sasa wanaogopa kukutetea hadharani wasijeonekana vituko kwa kuupinga ukweli ulio wazi (naked truth).

Mheshimiwa Rais, wasomaji walionitumia ujumbe mfupi wa simu, walionipigia simu, walionitumia barua pepe na hata waliozungumza nami uso kwa uso, wote wamenipongeza kwa ujumbe uliokuwa wazi ukieleza ukweli halisi na kila mmoja wao aliishia kusema ‘atang’oka’ 2010. Baada ya kutafakari ujumbe wa wasomaji na matukio yaliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari juma lililopita, nimeamua kukuandikia waraka huu ili nikupatie ushauri makini lakini bure.

Msomaji mmoja, kwa mfano, aliongea kwa uchungu jinsi ulivyojibu swali la mwanahabari kule Ufaransa. Ulipokuuliza kwa nini nchi yako ni maskini ukasema eti hata wewe hujui. Kwa maoni yake ilikuwa ni aibu kubwa kwa kiongozi wa nchi kujibu hivyo tena mbele ya viongozi na wanahabari wa kimataifa. Uliuonyesha ulimwengu kwamba nchi hii ni ya ajabu na watu wake ni wa ajabu. Ni kama ulikuwa unathibitisha kauli iliyopata kutolewa na mwandishi mmoja kwamba Tanzania ni nchi pekee duniani inayoweza kukaa miaka 10 bila rais na bado ikabaki na amani.

Kwa maoni yangu pia, rais wa nchi kusema hajui umaskini wa wananchi wake unatokana na nini ni sawa na kusema nchi haina kiongozi. Rais wa namna hiyo hawezi kuhangaika na mipango ya kuiondoa nchi katika umaskini, maana hajui kwa nini wananchi ni maskini. Anafikiri pengine ni “wavivu tu wa kufikiri” ama “fursa zipo ila kwa ujinga wao hawataki kuzitumia”.

Rais wa namna hiyo hawezi kujua madhara ya ufisadi wa EPA, Meremeta, Tangold, Kiwira, mikataba ya Richmond, IPTL na jinsi inavyochangia umaskini wa watu wake. Hawezi kuona ubaya wa rais na mke wake kujiingiza kwenye biashara kwa kutumia ofisi, fursa na vyeo vyao vya Ikulu kuwanyonga wananchi. Na kwa sababu hiyo hawezi kujihangaisha kuyashughulikia madudu kama hayo kama unavyofanya wewe hivi sasa.

Rais wa namna hiyo atakuwa ‘busy’ na safari za nje zisizo na kikomo, kukutana na marais wakubwa kama akina George Bush tena wanapokutana Bush atampiga piga mabegani rais kama huyo kama alivyofanya alipokuja hapa Dar es Salaam, na tungetamani kupata tafsiri ya kitendo hicho cha George Bush, ambaye wafuatiliaji wanasema hata mlipokutana Japan alikupiga piga begani tena, kutoka kwa Salva Rweyemamu yule mwandishi wa zamani aliyeisakama serikali kwa kalamu yake, lakini baadaye akawa mwanakampeni wako mahiri kwa kutumia kalamu hiyo hiyo na baadaye ukamzawadia ukurugenzi wa mawasiliano Ikulu.

Mheshimiwa, watu wanashangaa hata kitendo cha serikali yako kushindwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maji, visivyokauka tulivyonavyo hapa nchini na ardhi safi tena kubwa inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kujihakikishia chakula cha kutosha. Lakini badala yake unakwenda Italia kwa kutumia mamilioni ya shilingi kuomba chakula kwa WFP.

Mheshimiwa Rais, si siri ni aibu kubwa. Mabilioni yaliyopotea kwenye ufisadi yangetosha kuanzisha ‘scheme’ kubwa 13 za umwagiliaji kwenye mikoa 13 ya nchi hii. Na hesabu zake ni rahisi mno wala huhitaji kutumia shahada yako ya kwanza ya uchumi ambayo hata hivyo sijui kma umewahi kuitumia.

Chukua milioni 152 kwa siku kwa mwaka mmoja tu zilizolipwa kwa Richmond/Dowans ambazo kwa siku 365 za mwaka ni bilioni 55. Jumlisha bilioni 2,098 zilizolipwa kwa IPTL kwa miaka minane tu kwa kuzingatia kauli ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, bungeni Dodoma Agosti6, 2007 kwamba kwa kipindi cha Julai 2005 hadi March 2006 peke yake IPTL ililipwa jumla ya bilioni 262.3. Kwa vipindi vinane tu kama hivyo kampuni hiyo imelipwa jumla ya bilioni 2,098. Jumlisha bilioni 133 zilizoibwa kupitia EPA, kisha juu yake ongeza bilioni zisizopungua 600 zilizopotea kupitia ujenzi wa minara miwili pacha pale BoT. Halafu umalizie na mabilioni yaliyopotea kupitia viufisadi vingine vingine kama ubinafsishaji wa TTCL, NBC, Kiwira, n.k ambazo nazo si chini ya 100.

Halafu chukua hiyo jumla inayofikia bilioni 2,986 bila kuongeza bilioni ulizozitumia wewe kwa safari zako za nje tangu uchaguliwe kuwa rais. Igawanye jumla hiyo kwa gharama za mradi mzima wa kupeleka maji Shinyanga ulioshikiwa bango na best yako ili aje kuonekana anafaa kuwa waziri mkuu wa nchi hii. Utapata 13 ambazo ni scheme kubwa za umwagiliaji zenye thamani ya sh bilioni 225 kila moja.

Ina maana tungeweza kuwa na scheme kama hizo katika mikoa 13 inayoongoza kwa ardhi inayofaa kwa umwagiliaji. Njaa ingetupata wapi. Hivi sasa dunia inapolia na kupanda kwa bei za vyakula sisi tunaoita kilimo uti wa mgongo wa uchumi wetu tungekuwa matajiri kwa kuuza chakula.

Lakini hivi sasa eti serikali yako inapiga marufuku kuuza chakula nje ya nchi, mkulima anayetegemea kuuza chakula chake cha ziada ili apate matumizi yake mengine ikiwamo kusomesha watoto unamwambi nini?

Mheshimiwa Rais, watu waliodunisha maisha ya Watanzania kiasi hicho eti bado hutaki kuwachukulia hatua hadi leo. Umeunda tume juu ya tume nyingine lakini mafisadi wanaendelea kutesa. Ajabu zaidi chama unachokiongoza juma lililopita, kimetangaza eti kumpa onyo kali aliyekuwa naibu meya wa Ilala na kumzuia kugombea cheo chochote zaidi ya udiwani alionao, sababu eti ni kushiriki bomoabomoa ya Tabata Dampo na kuisababishia hasara serikali ya sh bilioni 1.8, kuwasababishia usumbufu wananchi wa Tabata Dampo na kukiaibisha chama.

Gazeti hili likaiandika habari hiyo Jumatatu wiki hii, kwa kichwa kilichosema; 'CCM yacharuka'. Naomba kupingana moja kwa moja na maneno aliyoyatumia mwandishi wa habari hiyo. Kimsingi CCM haijacharuka. Bali ina mkakati pengine unaosimamiwa na wewe mwenyewe mwenyekiti wako kukisafisha chama. Msitudanganye kiasi hicho, kwamba mna uchungu sana na pesa za serikali, mnawajali wananchi na kulinda hadhi ya chama chenu.

Fikiria hasara za mabilioni ya serikali niliyoyataja hapo juu, yote yamesababishwa na wana-CCM, fikiria Watanzania milioni 40 wanaoteseka kwa ajili ya wana CCM na ukumbuke jinsi hadhi, si tu ya chama unachokiongoza bali pia ya serikali unayoiongoza ilivyoporomoka ndani ya mwaka mmoja, kwa ajili ya wana-CCM. Lakini hamjawakaripia wala kuwafuta uanachama kama mlivyofanya kwa Naibu Meya Yakubu.

Huu ni usanii ambao umeshajulikana kwa Watanzania. Mheshimiwa Rais, juma lililopita umetoa kali nyingine ya mwaka. Umewaasa Watanzania wavumilie shida wasikate tamaa. Hii nayo ni kauli nyingine ya mzaha kwa Watanzania kama ile ya kusema hujui umaskini wao unasababishwa na nini.

Natamani ungekuwa unasoma maoni ya wasomaji. Siku hizi Tanzania Daima imeanzisha sehemu ya maoni ya wasomaji wanaosoma gazeti hili, kwenye tovuti. Msomaji mmoja aliposoma alisema hivi: “Kaka yetu usipate tabu wewe sema tu.

Sisi tumezoea shida, huna tofauti na Karume anayewaambia Wazanzibari watazoea tu. Sasa sisi tumezoea na wewe endelea kula nchi maana mafuta si kazi yako. Wewe linda mtandao wako usisambaratike, maana inabidi uutumie kurudi madarakani mwaka 2010.” Haya si maoni ya mtu anayekuambia kwa wema. Huyu ana uchungu ndani ya moyo wake na kwa ujumla maneno yake ni laana kwa serikali yako.

Mwingine akasema hivi: “...Kikwete suala la mafuta na maisha magumu havimhusu kabisa. Ndiyo, si anatuonyesha hivyo kwa kuwalinda mafisadi? Na sasa kapata kisingizio cha bei ya mafuta basi ndiyo itakuwa hadithi. Hivi wadanganyika wenzangu mnafikiri bei ya mafuta ikishuka (let's say) hadi nusu, ndiyo maisha yatakuwa bora kwa kila mdanganyika? "Dhahabu imepanda sana bei katika soko la dunia. Kwa nini vitu kama hivi vimeshindwa kufidia pengo la mafuta yaliyopanda?

Watu wengine wanafananisha Bongo na Marekani - eti na Marekani maisha yamepanda. Nyie ndugu zangu hebu acheni mzaha! Wewe unakula humburg na pizza Macdonald halafu unatuambia maisha yamepanda? "Chonde chonde jamani.

Natamani mngerudi huku mkapigika mkashindia kauzu ndiyo mngejua watu wanaongea nini…” Ukurasa huu hautatosha kukupatia maoni ya kila msomaji, lakini natamani ungejisomea mwenyewe habari hiyo kisha chini yake usome maoni ya watu.

Wasaidizi wako wanaweza kukusaidia kutembelea http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/21/habari1 Mheshimiwa Rais ningekushauri jambo moja tu. Kukubali pia ni uungwana wa aina yake na Watanzania wanapenda watu waungwana.

Baada ya ziara yako ndefu mkoani Tanga, utakaporejea Ikulu fanya jambo moja tu. Andaa hotuba yako ya mwezi bila kumshirikisha msaidizi wako yeyote. Ita waandishi wa habari kana kwamba unakuja kujibu tu maswali watakayokuuliza halafu wakisha fika toa hotuba yako kabla hujaulizwa maswali.

Waeleze wanahabari na Watanzania kwa ujumla kwamba wakati unachukua fomu za kugombea urais mwaka 2005 hukuijua vizuri sababu ya umaskini wa Watanzania. Waeleze kwamba wewe ulidhani kazi uliyokuwa nayo ni kuwaita tu wawekezaji uliokuwa umeshazoeana nao sana ukiwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na kwamba wakishakuja kuwekeza tayari maisha bora kwa kila Mtanzania yanajipa.

Sema kwamba umekuja kugundua kuwa mambo sivyo yalivyo. Umaskini wa Watanzania una uhusiano wa karibu mno na utawala wa nchi. Na kwamba utawala wa nchi kwa miaka mingi umebaki kuwa mbovu hasa kupitia ‘system’ iliyojengwa na Chama chako Cha Mapinduzi ya kulindana viongozi, bila kujali madhara yanayosababishwa na viongozi mafisadi hapa nchini na hivyo hata malaika akiwa rais wa nchi hii kupitia CCM hakuna maendeleo yatakayopatikana.

Sema wazi wazi kwamba kama rais wa nchi hata kama ungekuwa na dhamira ya kuikwamua nchi kutoka kwenye umaskini unaosababishwa na uongozi mbovu, ungeshindwa kwa kuwa kikulacho ki nguoni mwako. Maswahiba zako waliofanya juu chini upate urais ndiyo hao hao mafisadi waliokubuhu hata jina la mafisadi haliwafai tena. Nasikia wengine wameanza kuwaita ‘mafisidi’.

Na wewe huwezi kuwatupa wakati ungali ukikumbuka mchango wao mwaka 2005. Kwa sababu hiyo, ili kulinda uhusiano wako nao na wakati huo huo kulinda heshima kupita kiasi uliyopewa na watanzania, umeamua kuachia ngazi na hivyo mwaka 2010 hutagombea tena.

Wapatie Watanzania nafasi ya kuanza kufikiria tangu sasa chama kitakachowafaa kuongoza nchi hii hapo 2010, kutokana na sera zake kabla hawajafikiria ni nani atawafaa kuwa rais wa nchi baada yako. Uhakika mmoja tu nakupatia kwamba hutabaki ulivyo machoni mwa Watanzania.

Najua wapambe wako watakulaumu sana, maana kwa kung’oka wewe utakuwa umewakosesha ulaji mkubwa. Lakini utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri ya kuwa shujaa mbele ya Watanzania, kwa kutoboa ukweli na utapumzika kwa amani baada ya miaka 10 ya kusaka urais na miaka mitano ya kushutumiwa na Watanzania kwa kutotoa (not delivering) kile ulichotarajiwa.

Naamini pensheni itatosha, isipotosha utaongezea kilimo cha kisasa. Fanya uamuzi sasa ama utakuja kujuta utakapostaafu. Watafanya kama walivyomfanyia Chiluba hadi utashangaa.

Uamuzi ni wako Mheshimiwa Rais.
 
Chinga na mmasai wa inverstment centre wali wakatisha tamaa wawekezaji kutoka Denmark waliotaka kujenga kiwanda cha kusindika matunda pale Lushoto. Chinga aliingia ubia na rafiki zake ambao baadaye aliingia mitini bila kuanzisha hicho kiwanda chao.... Jamaa wa denmark walikwenda Kenya wakaanzisha kiwanda huko na matunda wananunua Tanga. Wakisindika wanaturudisha matunda kwenye chupa na kwa bei mbaya pale shoprite na supermarket zingine.....sio wazo jipya mzee wa bwaga moyo hilo!!!!!!!

na ssafi, bongo, - 20.07.08 @ 21:50 | #23210

NANI AVUMILIE NA WEWE NDIE MZEMBE NAMBA MOJA MAFUTA YAKAPANDA YASIPANDE HALI YA TANZANIA NI UMASKINI, MARADHI ,MADAWA HAKUNA MATATIZO YALIOKUWA HAYANA MSAADA MPAKA ATOKE MZUNGU HUKO AJE ASEIDIE KWANI NYINYI HAMUWAONI TUTASAIDIWA NA WAGENI MPAKA LINI AU TUVUMILIE WEWE NA FAMILIA YAKO MUSTAREHE.

na BONGO FLAVA, BARA, - 21.07.08 @ 01:30 | #23213

HII HALI MBAYA YA MAISHA SIO TUU KWA WATANZANIA NILA DUNIA NZIMA. hUKU MAREKANI TUNANUNUA MAFUTA GALLON $ WAKATI ZAMANI ILIKUWA $2.99! VITA VYA IRAQI NA MAPIGANO YA MUISRAEL NA MPALESTINA VINAZUA BALAA KUBWA LA MAISHA DUNIANI. WAARABU HUPANDISHA BEI YA MAFUTA KILA MPALESTINA MMOJA AKIUWAWA NA HUKO IRAQI SUPPLY YA MAFUTA NDIO KWANZA IMENYONDA SASA KIKAAANGONI TUPO MIMI NA WEWE TUNAIPATA. RAISI WETU KASEMA KWELI KABISAA NA WALA TUSICHUKULIE HASIRA WABONGO WENZANGU. HUYU NDIYE RAISI MUWAZI KULIKO WOTE WALIOPITA . TUYFANYIE KAZI HAYA MAISHA MAGUMU KWA KUOMBA VIWANDA VINGI VIJENGWE NA KUKATAA KABISAA KABISAA KUWATUKANA WAHISANI MANENO MABAYA YA KISIASA. HAYA NI MADHALA YAMETOKEA TOKA ENZI ZA TANU 1978 MPAKA LEO HII YANAPOPOOZWA NA RAISI WETU KIKWETE.

na FERDINANDO SANCHO, MEXICO, - 21.07.08 @ 01:52 | #23214

SANCHO umefananisha vitu viwili tofauti kwani taratibu za uuzaji mafuta TZ na USA ni vitu viwili tofauti umetoa mfano wa bei ya mafuta ya marekani lakini umesahau kutoa bei za majirani zake ambazo ni za chini kabisa kwa mfano VENEZUELA bei ya mafuta huko ni senti 45 kwa galoon na pia huko Mexico uliko bei ya mafuta ni dola 2.50 kwa galooni. kupanda kwa bei ya mafuta marekani kunatokana na sera za mafuta ambazo hazimlindi mteja isipokuwa kampuni za mafuta ambazo George Bush NA **** CHENEY wako karibu nazo kimaslai na ndio maana chama cha demokrasia kimekuwa kikitaka uchunguzi wa kina kwenye kampuni za mafuta kwani zinawahujumu wananchi. tukirudi Tanzania ni kwamba anayewaumiza wananchi kwa ugumu wa maisha ni Kikwete na marafiki zake mafisadi kwani mabilioni yaliyoibiwa ndani ya nchi hii yangeweza kusaidia nchi kwa kiasi kikubwa ikiwemo ku subsidise bei ya mafuta ambayo ingesaidia sana kupunguza bei ya mafuta kwa kiwango kikubwa.

na nick, Tanzania, - 21.07.08 @ 02:58 | #23219

Jamani si afazali ya JK kawambia hali alisi kuliko yule aliekwenda Rufiji kipindi kile cha mafuliko na kuwambia wajomba zangu wafanye bidii kwenye kilimo hali kuna mafuliko.isitoshe na ile kauli ya wafunge mikanda lakini lada na ile ndege ya rais lazima vinunuliwe.....
kaja mkweli na jitihada zake zinaanza tunalalamika naomba tumpe mda

na Miembe saba, Boston USA, - 21.07.08 @ 04:24 | #23223

Nick # 23219
Umetoa uchambuzi mzuri kwa kifupi. Wakulaumiwa ni Mkapa (mlalamikiwa No 1), Kikwete nae anafuatia, hasa kuhusu mikataba ya kutunyonya ambayo serikali yake imeingia.

Hali ya maisha ni ngumu kwa wastani Dunia nzima, Venezuela bei ya mafuta ni rahisi kwakuwa wao wanayo na wanayachimba kwa manufaaa ya wananchi wa Venezuela.

Maisha magumu kwa watanzani hayasababishwi na kupanda kwa bei ya mafuta duniani pekee, haya maisha magumu yalianza kabla hata ya kupanda kwa bei ya mafuta, bei ya mafuta imeongeza ugumu wa maisha na wala sio kisababishi kikuu. Utawala mbovu, kutojali maslahi ya taifa na kutofuata miiko ya kazi kwa watendaji wa serikali ni baadhi ya vyanzo vya maisha magumu kwa watanzania na waafrika kwa ujumla.
Hii safari ni ndefu, lakini tutafika.

na Avisenia Marina, Wellington, - 21.07.08 @ 05:06 | #23226

Huyu JK anachekesha sana la mafuta anaongelea,hajui kwamba kabla bei haijapanda Chinga na washirika wake waliingia mikataba michafu,JK katajiwa wahusika anaunda tume na ***** ni mjumbe kuchunguza wezi.
milioni 150/siku kwa miaka 2[365 days] na 133 bilioni haoni kuwa ni tatizo la maisha magumu.
Kaambiwa kakaa kimya eti leo anaongela mafuta,si unafiki ni nini. Kama ni karata wa tz tuna garasha.

na leader - 21.07.08 @ 05:35 | #23230

Heeee!
jamani tusidanganyane kwa kuleta data za kila mtu anapoishi , ni kweli maisha magumu kila pahala hapa duniani hakuna hata sehemu moja iliyo kuwa rahisi , ispokuwa muhimu ni juhudi yako mwenyewe kukabiliana na hiyo hali, mimi hapa ninakazi kibao ninafanuya kazi kuanzi saa12 hadi saa nne usiku kutosheleza mahitaji yangu , saa kumbi na mbili nachinja kuku islamic butchery, saa sita naenda kazini kwangu kiwanda cha magodoro, saa 12 naenda airport kwenye kazi ya kutuma vifaranga. hebu leo tuangale kule nyumbani wanaojituma ni akina mama zetu kuanzia asubuhi hadi anaingia kitandani yeye ni kazi tu , wengi wao wapo vibarazani, na kwenye mabaaa, ni kweli tatizo la sera na uongozi lipo lakini la msingi kwanza je? watz wangapi wanaojituma kwa manufaa ya taifa au tunataka raha bila ya kupata shida?
ile nch inamambo mengi ya kuangalia tusidanganyaene kwa miaka miwil au mitano kuwa kuna mtu ataleta unafuu wa maisha, unafuu wa maisha unaletwa kwa watu wote kwa kujibana na kuwajibika kwa taifa , tuache ndoto za mchana, lazima kwanza tufe ndio tupate pepo!!!!
pale kwetu kariakoo, yupo mjomba wangu anaingi shimoni karikoo , akitoka saa tisa , utamkuta maazese kaweka pamba zake anatangaza huduma kwa marafiki zake walio kuwa mitaani , sasa hiyo nchi kweli itajengwa na nani ikiwa wengi wao ni wasanii wa maisha.

na kongera, Australia, - 21.07.08 @ 05:59 | #23234

Kiwete Kwa kweli huna jipya kwani nakukumbuka pale Paris uliulizwa kwa nini wananchi wako na nchi yako ni Maskini Ukasema Hujui!! president wa nchi hujui kwa nini nchi yako ni Maskini na wananchi ni Maskini!!! My God!!! Ila huo wimbo wa kupanda kwa bei ya mafuta naona sasa umezoeleka mno labda tafuta Gear nyingine Mzee!! Hakuna siku nyingi wadanganyika wataanza kukuzomea!!! Hillooo fisadi utapenda? Hivyo tia akili tafuta wimbo mwingine!!
Pia suala la mafuta ni suala nyeti sana ila ikumbukwe kwenye nchi yetu kodi inayotozwa kwenye mafuta ni Tsh 650 kwa kila lita moja!! ina maana kama mafuta yangetolewa uarabuni Bure Kabisa, gharama ya usafiri tu ni Tsh 200 kwa lita hivyo jumla ingekuwa Tsh 850 kwa lita!! Kwa hiyo tatizo si kupanda kwa bei uarabuni ila ni kodi zetu!! Kama kweli unaipenda Tanzania punguzeni kodi Hiyo iwe Hata angalau Tsh 200 kwa lita is reasonable!!!

na TY, Tanzania, - 21.07.08 @ 07:12 | #23237

Ni jambo la kushangaza na aibu kuwa hadi leo wastaafu wa Jumuia ya Afrika Mashariki upande wa TZ hawalipwa pesa zao. Wengine wako huko huko Tanga na wanaambiwa wavumilie shiada!!! Wazee wetu walizunguushwa sana wakati wa Mkapa na sasa naona JK anafanya yale yale...Kama zipo pesa zakupeleka kila mkoa kwa wajasirimali basi uwezo wa kuwalipa wazee wetu upo.. Naomba serikali hii ya sasa imalize kabisa kilio cha wazee wetu

na Zawadi, UK, - 21.07.08 @ 07:51 | #23239

DUH, SIJUI SISI WATZ TUNA MATATIZO GANI?

HIVI HATA UKWELI BADO PIA TUNAUKATAA?

KILA PEMBE YA DUNIA HII MALALAMIKO YA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA KUNAMGUSA KILA MTU, KIKWETE ANASEMA UKWELI, LAKINI BADO KUNA WENGINE WANATAFUTA MTAJI WA KISIASA, AHH, SASA NYIE MNATUANGUSHA KWANI SI WA KWELI.

MIMI NIPO HAPO USA KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA BEI YA MAFUTA IMEPANDA MARA DUFU NA INAENDELEA KUPANDA KULA KUKICHA.

KANA KWAMBA HAITOSHI BEI YA VYAKULA NAYO IMEPANDA VILEVILE, KWA MFANO MCHELE BEI YAKE IMEPANDA SANA KWA KIPINDI HIKI CHA MWAKA MMOJA.

KWAHIYO ANAYETUAMBIA KUWA KIKWETE ANASEMA UONGO, BASI HUYO NI WAKUOGOPA KAMA UKOMA.

TUJIFUNZE KUSEMA UKWELI

TUJIFUNZE KUELEKEZA BADALA YA LAWAMA

na Mkweli, USA, - 21.07.08 @ 08:31 | #23241

KAKA YETU USIPATE TABU WEWE SEMA TU. SISI TUMEZOEA SHIDA , HUNA TOFAUTI NA KARUME ANAEWAMBIA WA ZNZ WATAZOEA TU. SASA SISI TUMEZOEA NA WEWE ENDELEA KULA NCHI MANA MAFUTA SI KAZI YAKO. WEWE LINDA MTANDAO WAKO USISAMBARATIKE MANA INABIDI UUTUMIE KURUDI MADARAKANI MWAKA 2010.

na mahsi, dsm, - 21.07.08 @ 09:07 | #23246

Huu anaotufanyia kikwete ni usanii wa maisha yetu, amesahau maneno yake wake wakati anaomba kura kuwa atahakikisha kila mtanzania anapata milo mitatu kwa siku leo anatuambia tuvumilie dhiki tuliyonayo wakati wao akina kiketwe na mafisadi wenzake ndio mnao changia hali hii. ole wenu siku ikifika ya watanzania kusema no.

na Kojak - 21.07.08 @ 09:08 | #23248

HII pesa yetu ya JUMUIYA YA AFRIKA sasa ni zaidi ya miaka 30 hivi kweli tuna Kiongozi(RAIS) anayejali watu wake ?wengi wetu wameishaaga dunia na ambao bado tupo tupo taabu tupu KWELI UFISADI HAUISHI...mara pesa zipo ngojeeni malipo..tunakaa hapo ikulu tunawaona wanapita wako saafi sisi hata mkojo wa kukojoa hakuna mwilini KIKWETE TULIPE VIJISENTI VYETU TUKANUNUE HATA NGUO ZA KUZIKIWA.

na E T LUKUBA, TANZANIA, - 21.07.08 @ 09:22 | #23251

Kula tano Mahsi dsm. Kikwete suala la mafuta na maisha magumu havimuhusu kabisaa. Ndio si anatuonyesha hivyo kwa kuwalinda mafisadi!! Na sasa kapata kisingizio cha bei ya mafuta basi ndo itakuwa hadithi. Hivi wadanganyika wenzangu mnafikiri bei ya mafuta ikishuka (lets say) hadi nusu, ndo maisha yatakuwa bora kwa kila mdanganyika?

Dhahabu imepanda sana bei katika soko la dunia. Kwa nini vitu kama hivi vimeshindwa kufidia pengo la mafuta yaliyopanda?

Watu wengine wanafananisha bongo na marekani eti na marekani maisha yamepanda. Nie ndugu zangu hebu acheni mzaha! Wewe unakula humburg na pizza Macdonald halafu unatuambia maisha yamepanda?? Chonde chonde jamani. Natamani mngerudi huku mkapigika mkashindia kauzu ndo mngejua watu wanaongea nini

Wengine wanatuita wavivu kwa kuwa wako Australia wanachinja kuku. Mbona hutuelezi unalipwa kiasi gani kwa kuchinja hizo kuku? Malipo yako kwa siku ni mshahara wa miezi miwili wa mtanzania. Halafu afadhali hizo kazi zenyewe za kuchinja kuku zingekuwepo. Ndugu yangu kama unavijikazi hebu nisaidie kamoja mwenzio niko kijiweni nimepigika. Ajira milioni tulizoahidiwa bado hazijatufikia wenzio.

na mlugaluga, danganyika, - 21.07.08 @ 09:27 | #23252

Mzee JK mbona unaanza kupingana na ahadi zako? ulisema maisha bora, sasa unasema uvumilivu, next time utasema tufe polepole.

Wakati unaahidi maisha bora ulikuwa unaropoka au kuwahadaa watanzania waliozoea kulaghaiwa kila kukicha?

Lakini hili ni fundisho kwa wapiga kura walio kama vifaranga vya kuku wanaoahidiwa kunyonya kesho hali ya kuwa wajua kabisa mama kuku hana hata chuchu moja ya kutolea maziwa.

Ha ha ha habari ndiyo hiyo.

na Cosmas Gabriel - 21.07.08 @ 09:51 | #23255

MIMI NANSHANGAA JK KILA SIKU KULALAMIKIA BEI ZA MAFUTA.TUSICHOAMBIWA NI KUWA WAKATI BEI YA MAFUTA IMEPANDA HATA BEI YA DHAHABU,TANZANITE NAMAMDINI MENGINE NAYO IMEKUWA IKIPANDA KILA KUKICHA. WAARABU WANAFAIDIKA NA MAFUTA JE SISI TUNAFAIDIKAJE NA BEI YA DHAHABU????????? HALAFU CHA KUCHEKESHA ETI NA SISI TUNALALAMIKIA KUPANDA KWA GHARAMA ZA VYAKULA BADALA YA KUSHANGILIA MAANA SISI NI NCHI YA KILIMO. ZAIDI YA WA-TZ 70% NI WAKULIMA. KAMA SERIKALI INGEKUWA NA SERA NZURI ZA KILIMO TUNGEWEZA KUFAIDI BOOM HII YA GHARAMA ZA CHAKULA LAKINI KINYUME CHAKE TUNAKAA NA KULIA. TATIZO KUBWA LA TZ NI SERA MUFILISI.

na Roman, Tanzania, - 21.07.08 @ 08:14 | #23273

Bila kutafuna maneno hali ya maisha imepanda sana[inflation] hasa baada ya bei za mafuta kupanda katika soko la dunia.
Upandaji wa mafuta unaenda sambamba na upandaji wa kila kitu [bidhaa],lakini kwa upande wa Tanzania kama rasilimali zetu zingetumika kikamilifu hali isingekuwa kama ilivyo sasa.Tanzania ina mbuga za wanyama,ardhi nzuri, maziwa, bahari na madini [dhahabu,Tanzanite,Almasi na nk].Nianze kueleza jinsi rasilimali zetu zisivyotumika kwa manufaa ya taifa.
[1] Mbuga za wanyama,Taifa limekuwa likipoteza mapoto makubwa kupitia sekta ya utali kwasababu TANAPA imeshindwa kukusanya mapato yote yanayostahili.Matumizi mabaya ya fedha kidogo inayokusanywa na TANAPA badala ya kuchangia pato la taifa inatumika au inaishia kuhudumia mafisadi.Mambo ni hivyo hivyo kwa Ngorongoro conservetion.Mahoteli yote yanayojengwa kwenye mbuga za wanyama yanamilikiwa na wageni ambao hawalipi kodi inayostahili.Kila baada ya miaka mitano wanabadilisha majina ili kukwepa kulipa corporate tax na kuendelea kupata tax holiday ya bidhaa watakazo nunua.
[2] Ardhi nzuri,Uwekezaji katika sekta ya kilimo mpaka leo ni mdogo sana,Tanzania ina nafasi kubwa sana kupiga hatua kama ingewekeza kwenye kilimo ambacho kimewaajiri asilimia kubwa ya watanzania.Serekali imekuwa hodari kuhubiri kilimo ni utii wa mgongo lakini hakipewi umuhimu hata kidogo.Ununuzi wa radar, ndege ya rais vinapewa umuhimu mkubwa lakini inapofika sekta ya kilimo tunaambiwa hakuna fedha!,kama hizi fedha za EPA, Import support,Richmond na semina elekezi Ngurdoto na nk zingepelekwa kuhudumia sekta ya kilimo tungekuwa wapi?.Wakenya leo hii wanapiga magoti wanaomba tuwauzie mahindi kama tungewekeza ipasavyo Tanzania ingeweza kuzilisha nchi zote za Afrika mashariki.
[3]Madini,dhahabu Tanzanite na nk mikataba yote tuliyoingia imejaa rushwa.
Dhahabu yetu ingeweza kutumika kupunguza makali ya bei kubwa ya mafuta.Wawekezaji hawalipi kodi,wananyanyasa wafanyakazi wa kitanzania.Kila baada ya miaka mitano wanabadilisha majina ya kampuni zao ili wasilipe kodi,mfano hapa Arusha tuna kampuni moja inayochimba Tanzanite imekuwa ikibadilisha majina kila baada ya miaka mitano,waliaza kujiita SAMAAX baada ya miaka mitano kumalizika wakajiita Tanzania one, halafu sasa wanajiita Half Gem.Ukienda kwenye machimbo ya dhahabu hadithi ni hiyo hiyo.
[4]Bahari mambo ya huko yanatisha,kwanza kuna mkataba wa TICS ambao WATZ tunaujua sina haja ya kuuelezea.Madhara yake ni makubwa sana kwa uchumi wetu,wafanyabiashara wengi siku hizi wanapitisha mizigo yao bandari ya Mombasa kwasababu ya urasimu ulioko bandari ya Dar es salaam.TICS wameongezewa mkataba na serekali ya mzee Mkapa pamoja na kuboronga kwa kiasi kikubwa.
Watanzania kama mambo yote hayo niliyojaribu kuyaeleza kwa ufupi yangefanyiwa kazi na serekali ya JK wala asingetuambia tuvumilie shida,hatukumchagua ili tuvumilie shida ambazo angeweza kuziondoa kama sio kuzipunguza.

na G KABONDE, ARUSHA,TANZANIA, - 21.07.08 @ 08:21 | #23274

'Kama Mwenyeketi wa Umoja wa Africa tunashughulikía tatizo hilo' Watanzania wanakujua kama Rais wao na si vinginevyo. Kama umeshindwa nyumbani utaweza kweli ngazi ya kimataifa. Ningekuelewa kama ungesema 'Kama member wa G8 tunashughulikia tatizo hilo' Ila umoja wa wala mihogo wapi na wapi

na TICO, Mwanza, - 21.07.08 @ 09:29 | #23294

Inaumiza sana. Sasa watanzania tujiandae kwa hali yeyote itakayotokea maana karibu robo ya waliotoa maoni mpaka sasa wanaonyesha kukata tamaa na Rais wetu Jakaya Kikwete aliyebaki yeye na makamu wake kama injini zinazojikongoja kutufikisha salama mwaka 2010.

Alituahidi watanzania mambo tuliyoamini anauwezo wa kuyashughulikia na bila hiyana tukampokea zaidi ya alivyotarajia.

Rais wetu hakuwa amejipanga kuiongoza nchi. Hii naithibitisha kwa kauli yake aliyoitoa mwishoni mwa mwaka 2004 wakati anahojiwa na kituo cha TVT wakati huo kama mgeni rasmi wa kipindi, yeye akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.

Kwa shauku ya watanzania waliokuwa na hamu ya kujua nini mustakabali wake kisiasa hasa kugombea uongozi wa juu wa nchi, yeye alijibu tena kirahisi wakati wa kulizungumzia hilo bado haujafika. Tunaamini alikuwa analinda heshima ya chama, ila nahisi katika mtandao wao waliouratubu kwa muda mrefu huenda hakukua na mtu waliyekuwa wamempata kwa ajili ya kuliwakilisha kundi lao hivyo kumuwia vigumu kuweka wazi hata kama alikuwa na dhamira ya kugombea.
Pindi walipofikia muafaka wa kuwa anafaa kuliwakilisha kundi lao tayari muda ulishapita wa kujaribu kuyatambua matatizo ya watanzania kwa undani zaidi alilazimika kuyajua kupitia kwa wanamtandao wenzake.
Hii ndiyo iliyosukuma kuwa mgombea aliyetembea sehemu nyingi wakati wa kampeni kwa sababu kila alikopita alikuwa haamini anachokiona kama watanzania ni maskini wa kutupwa namna ile hali iliyomshawishi kutamani kufikia kila sehemu.
Alilazimika kuahidi na ambayo hayakuwemo katika ilani ya chama chake kwa kulingana na sehemu aliyopita. Hakufanya hivyo kwa kuwahadaa watanzania ila ni msukumo wa kweli aliokuwa nao na hapo alijisemea nimefanya sahihi kugombea kumbe watnzania wanahitaji ukombozi wa haraka.
Haikushangaza pale alipoituliza inchi na dunia kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa bungeni siku ya kwanza iliyogusa kila sehemu kwa uwazi na uchungu. Yalikuwa ni maono yake baada ya kuyashuhudia maisha ya mtanzania kwa wakati mfupi wa kampeni aliofanya.
Ndio maana ukiangalia kwa makini hata mabilioni aliyoyatoa yalikuwa hayana tathmini aliyo ya wazi zaidi ya kukurupuka. yote hiyo ilikuwa ni haraka yake ya kuona wale aliowashuhudia wakati wa kampeni baadhi yao wajaribu kuondokana na hali waliyokuwa nayo kwa kuwezeshwa mitaji. Kwa bahati mbaya jambo lolote kubwa linapofanywa kwa kubahatisha matokeo yake yanaweza kuleta balaa kubwa kijamii. Tumeshuhudia karibuni akilalama ameibiwa pesa japokuwa hakuwataja wajanja wanaoongozwa na vinara wa mtandao.
Kutokana na hotuba yake, aliwakuna wazungu na walimdaka juu juu ili apeleke mipango ya jinsi anavyotaka kuwakomboa watanzania. Ndio maana hatukumuona akitulia inchini muda mchache baada ya kuikamata Ikulu ya Tanzania. Hakuwa na wakati wa kufuatilia kwa karibu yale aliyoyaeleza katika hotuba au aliyoyaagiza yafanywe chini ya wizara.
Mtu pekee aliyemuamini alishindwa ( Waziri mkuu aliyepita ) kufuata maelekezo yake labda kwa kuwa na nguvu katika mtandao pasipo kuangalia anayekwenda kinyume naye sasa ni Rais. Taratibu Rais wetu akaanza kutupa hofu ya utekelezaji wa aliyoyaahidi. Kwa kutumia karata ya upendo wa watanzania kwake bado aliendelea kuwa imara ndani ya mioyo ya watanzania.
Kilichotokea ni kupishana kwa utekelezaji wa masuala nyeti kati yake namtandao. Yeye alishabadilika na kujitolea kwa ajili ya wanzania, wakati mtandao bado unamalengo yake ambayo ni lazima yatimizwe kabla ya kuwahudumia wantanzania.
Wamekamatwa wakisaini KIMBUNGA CHA KWANZA KATIKA SERIKALI YAKE (BUZWAGI) nje ya maelekezo yake aliyoyatoa bungeni. kushindwa kwake kulichukulia hatua suala lile kwa kuwa lipo ndani ya mabosi wake wa mtandao ndio iliyokuwa chachu ya hata wauguzi kurejea tena kwa kasi yenye nguvu mpya kujitafutia maisha bora kwa njia za rushwa zilizokuwa zimepungua kabla.

Alikuwa nje kutafuta misaada mtandao ukabaki ndani unaitafuna inchi. Misaada aliyokuwa anaifukuzia sasa imesitishwa kwa kutokuwa na ujasili wa kuyashughulikia aliyoyasema na yametokea mengi yakiuhusisha mtandao.

Leo anarudi kwa watanzania akiwa hana aliloagiza wala aliloomba kusaidiwa la maana alilofanikiwa. Ni mpweke asiyejitambua baada ya kulihujumu kundi la mtandao waliowekeana mipaka kabla ya kumsimamisha kuwa muwakilishi wao.

Watanzania tuna kazi ya kupata mtu anayesema na hapo hapo anatekeleza kwa vitendo pasipokuangalia mke au mwanagu ataumia kwa sababu umeshaomba kuvikwa uwezo wa kuwamiliki watu wote na ukapewa.

Angeandaa utaratibu mzuri wa kuwasaidia wakulima kama alivyoongea leo tusingekuwa katika shinikizo la kupatwa na njaa. Watanzania walikuwa tayari kumsaidia Rais wao kipindi anaingia Ikulu hata kwa kujitolea kufanya kazi za harambee kuokoa nchi tofauti na aombavyo sasa. Aige marais wa Uganda na Rwanda wanaojitolea kwa hali na mali kwa ajili ya wananchi wao.

Tujipe moyo zaidi kwa watanzania kama hatutafanya kazi ya ziada, harubu azipatazo mtu wa kipato cha chini wakati njia za marekebisho ni nyingi zitageuka kuwa chachu ya machafuko ichini.

Rais wetu wafanyakazi wa viwandani wananyanyasika kwa malipo na hiana wanazofanyiwa na wahindi mliowatulia nchi.

Rais wetu waangalieni wachina wanaouangamiza uchumi wa mtanzania kwa vitu visivyo bora.

Rais wetu kama hausomi shule za Binafsi jua utaelewa zaidi somo kwa kuhudhulia masomo ya ziada.

Rais wetu ukiwa huna mtu hospitali wa kukushika mkono hata hiyo hela uliyoandaa kumpatia dr kama rushwa ili mgonjwa wako ashughulikiwe hutaipata.

Chuki imeanza wasiotupenda watatuchonganisha tumalizane. Tulia ili ujue wananchi wako wanautajiri wa kiwango gani na mpange jinsi ya kuutumia.

na Elian Gz, Tanzania, - 21.07.08 @ 10:46 | #23321

Naanza na MARINA WA vocha#23226 hivi unajua kuwa TZ kuna gas ya songosongo lakini Tanesco wananunua kwa bei mbaya mpaka wame admitt ni bora wangechimba wenye ingekuwa rahisi
Tatizo JK anawalinda sana mafisadi wake kwani most of them ni marafiki zake,watu wake wa karibu BEI ya mafuta kweli imepanda lakini kuna alternative nyingine za kuchangia ili kupunguza gharama za maisha kwa sisi masikini wa tanzania
Tuna rasili mali nyingi tulizo barikiwa na mungu lakini hazitunufaishi sisi watanzania ambazo zingeweza kutusaidia kupunguza ukali wa maisha
Zaidi ya mali zetu zetu kuwanufaisha watu wachache kwa manufaa yao nawazungu na hicho kidogo tukipatacho mafisadi wakichukua chote je kwa nn tusiumie sisi watanzania wenye kipato cha chini
JK Tusitafute mchawi bali wachawi ni sisi wenyewe na kwa mwelekeo huu maisha yatazidi kuwa magumu zaidi na zaidi wakati sisi ni matajiri wa mali za asili lakini wananufaika nazo wachache
JK Tutangazie tu kama TUFUNGE MIKANDA TUMESHAZOEA

na yakhe, pemba, - 21.07.08 @ 11:00 | #23327

hatukatai ukweli. JKN alsiema tufunge mikanda kwa miezi 18, ikawa miaka 18. Ikaendelea, AHM kukawa na nafuu ya nguvu ya soda, baadae BWM tukapata ukapa bab kubwa na kwa mbwebwe boys2men wakasema ndege inapaa kwenye MAISHA bora kwa kasi nguvu na ari mpya. Na mwenye kipaza sauti "6" kwa standard na speed, tutakuwa hatuna shida. Sasa kwa nini tunarudi kule kwa JKN kwenye yanga kwa kadi, mgao wa mafuta, foleni za sukari wakati kuna mavuno ya almasi, dhahabu, tanzanite, sangara, tumbaku, kahawa, korosho???

na plplp, lplplp, - 21.07.08 @ 11:02 | #23330

NYIE watoto wa mafisadi mlio ughaibuni acheni kushabikia msiyoyajua.kama mnafikiri sisi ni mambumbumbu basi sawa.Saa yenu itafika tutapowasimamisha vizimbani wazee wenu na kuwafilisi ndiyo na nyie mjue tunachopigia kelele kina maana gani

na DAFFA, MUHEZA /TANZANIA, - 21.07.08 @ 11:04 | #23332

IK anashangaza sana masuala anayoyaweza anayafumbia macho anarukia mambo ya mafuta,simelewi.jk shughulikia orodha ya mafisadi,orodha ya wauza madawa ya kulevya.orodha ya orodha ya watendaji wako wabovu baada ya hapo ongelea kupanda kwa bei mafuta na sio utuambie tuvumilie shida bali tuambie tuongeze bidii,ww umeanza kuongeza bidii kweny huo uvumilivu au unakaa tz wiki moja na majuu siku mbili?TUSIDANGANYANE

na jimmy, tz, - 21.07.08 @ 11:09 | #23333

navutiwa zaidi na mjadala unavyoendelea. ingawa bahati maya baadhi yetu tuaacha kuchangia mada husika.

navutiwa zaidi na watanznaia walioko tanzania, wengi wao wanauelewa mkubwa kuliko walioko nje ya nchi.

mchangiaji mmoja anayedai kuwa marekani anajitahidi kufafamua ongezeko la bei ya mafuta katika kipindi cha mwaka mmoja limesababisa maisha kuwa magumu!

nimevutiwa na maelezo ya mtanzania, aliyeko tanzania aliyejaribu kumfafanulizi kwamba bei ya mafuta kwa Mexico na Venezuela iko chini zaidi ya marekani kutokana na sera mbovu za utawala wa bush

labda niongeze kidogo kuwa, licha ya ongezeko la bei ya mafuta, ukiwa marekani unapaswa kutambua athari vita vita vinavyoendelea Iraq, Afghanistan n.k katika uchumi wa marekani

mwaka jana aliyekuwa akiitwa Iron Lady wa Tanznaia alidai kuongeza kodi ya mafuta kwa kisingizio la kujenga barabara!, lakini hakuna hata kilomita moja ( nje ya zilizoachwa na magufuli zilizojengwa), unaweza kuangalia kwmaba sera mbovu za serikali zinasababisha kupanda kwa gharama za maisha bila kusingizia ongezeko la bei ya mafuta duniani

kingine kinachofurahisha ni kuwa ukiwa marekani unafanya kazi kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne usiku!.

watanzaia wa aina yenu wanafurahisha, mkiwa kwenu hamwezi kufanya kazi kwa kujituma kwa kiwango hicho na pia mkiwa huku mnabagua kazi kama nini.

suala la msingi hapa ni kuwa sera mbovu za serikali ni sababu kubwa za kuathirika kwa maisha ya wananchi

wachangiaji wengine wameongelea kuhusu madini kwa ufasaha mkubwa na kwaba serikali hii ya kisanii imekuwa ikiwachanganywa wananchi kwa kuunda tume na tume bila kuchukua hatua.

na tunafahamu kuwa hawawezi kuchukua hatua kwani Jakaya Kikwete huyu anahusika na mchakato wa kuundwa kwa sheria ya madini na kutoa raslimali za watanznaia kwa wageni kwa bei za kutupwa, Bulyanhulu, IPTL

ukiacha hayo hivi sasa tunasikia habari za kuwepo kwa mafuta karibu kila pembe hadi kiwira, subir utaona madudu badala ya kuyatumia kutusaida sisi tunaongeza juhudi kutoa ardhi yetu ili kuzalisha nafasi za kutengeneza mafuta!

badala ya kuzalisha chakula ambacho kwa hakika sasa kina soko kubwa duniani na kuboresha kaisha ya wananchi, serikali inaagiza mashangangingi kila kukicha huku wilaya nzima hakuna trekta hata moja, Rais akifika katika wilaya hiyo akiwa na msururu wa mashangingi pengine zaidi ya 40, anawaambia mvute subira, mafuta yamepanda na kuharibu uchumi.Hii ni akili kweli!

kikwete hawezi kuboresha uchumi na hali za watanzania kwani angekuwa na nia hiyo angepunguza safari za nje ya nchi ni gharam sana

watanznaia wenzangu mliko nje kama huko USA tusaidieni kufahamu gharama za misafara ya wakubwa hawa nje ya nchi, zinaakisi kweli uchumi wa watu wanaoambiwa kuwa mafuta yamepanda, waendelea kuwa wavumilivu?

na mashilatu, ngara, - 21.07.08 @ 11:32 | #23341

haya mambo hayo !!!! tuendelee kuvumilia duu!!!! kasahau kusema tukaze mikanda? hakuna asiyejua kwamba uchumi wa nchi umeharibiwa na uongozi mbovu, tamaa na ulafi wa viongozi wa CCM. vIONGOZI HAWAJIPIMI KWA KUANGALIA WAMEWAFANYIA WATANZANIA KITU GANI BALI HUJIPIMA WENYEWE KWAMBA WAMEFAULU KUJIJENGEA MAJUMBA MANGAPI, WANAHISA KIASI GANI KWENYE MAKAMPUNI MAKUBWA, WATOTO WAO KAMA WAMEFANIKIWA KUPATA ELIMU YA JUU HUKO NG'AMBO, STAREHE ZAO BINAFSI NJE YA NCHI NAKADHALIKA.HIVYO NDIVYO VIPIMO VYA MAFANIKIO KWA VIONGOZI WETU. IKO SIKU WATATUJIBU NA SASA KAZI IMEAZA. Tumechoka kuvumilia na kuambiwa tuvumilie. Bei ya mafuta siyo sababu pekee kwa ugumu wa maisha kwa watanzania. Serikali imeweka kima chachini cha mshahara kidogo sana na kuwapa advantage hata wawekezaji wenye uwezo kulipa hivyo hivyo wakiamini MTZ Anaweza kuishi kwa kiwango hicho kisichotosha hata nauli ya mwezi kwenda kazi.

na ba - 21.07.08 @ 12:27 | #23350

JK usifikiri ni sifa kila mtu kukutaja mahala alipo kuwa we ni bomu kwa utawala bora. Angalia umeanza kutugawa wadanganyika kwa kuwatumia mafisadi na pia wana mtandao wako. Umeendeleza kutugawa wadanganyika kwa kuendeleza mfumo mbovu wa fisadi Mkapa aliyetugawa watumishi wa umma ktk viwango vya mishahara, tofauti kati ya mtumishi wa chini na wa juu imekuwa kubwa mno. Haiyumkiniki huelewi matatizo ya wanyonge kwa kuwa unakula na kulala bure. Hivi mshahara anaopewa Rais ni kwa minajili gani ilhali mtu anatunzwa na kulelewa? Au huu ndiyo chanzo cha ugonjwa wa mfumuko wa bei??

na Bodaboda, TBR-TZ, - 21.07.08 @ 12:42 | #23353

Du, jamaa kashindwa kuongoza sasa anasubiri miujiza! Ni bora aanze kutangaza kuwa kwenye uchaguzi ujao hatagombea kwakuwa hana uwezo wa kuwasaidia watanzania.Yani hali ni tete na wale waliokulwa wanakula mlo mmoja kwa siku sasa wanakula mlo nusu kwa siku. yani afadhali ya Zimbabwe kuna sababu ya hali ngumu! Yapaswa atueleze vizuri, kwanini Tanzania tuna hali hii? Aache ziara zinazozidi kuwatia machungu watanzania. Atulie ofisini aangalie ni namna gani ya kupunguza dhahama hii kwa wabongo. Ni bora basi tungegawana haya machungu kuliko kuumia watu wengi na wachache ambao wametajirika kwa dhuluma wakiendelea kufaidi matunda ya nchi hii. Yana mwisho haya!!!!

na Major, Tanzania, - 21.07.08 @ 13:12 | #23362

Maisha magumu hayajaletwa na kupanda bei ya mafuta, yanameletwa na UZEMBE wa viongozi.

Hospitali zilikuwa hazina dawa KABLA ya kupanda bei za mafuta.

Shule zilikwa hazina walimu, vitabu, majengo etc kabla ya kupanda bei ya mafuta.

Ninanaweza kuendela hapa mpaka kesho asubuhi.

Point hela zilizo ibiwa na zinazo endelea kuibiwa na viongozi - zingetumika kisahihi, shida ya mtanzania ingekuwa tofauti.

Huyo Raisi angelikuwa anashughulikia wafisadi kisahihi, speech yake ingepokelewa kitofauti.

BADO HAJAFANYA KITU!!!!

na Fimbo Kali - 21.07.08 @ 13:39 | #23365

Yaani haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana? Kuvumilia shida badala ya kula manna na asali ni ****** ya nguoni. Kama umeshindwa si uishie ndugu yangu. Tunataka maziwa na asali. Uliahidi kutupeleka Kanani siyo kwenye nchi ya kufunga mikanda bwana rais.

na Mpayukaji Msemahovyo, Siri, - 21.07.08 @ 14:08 | #23372

Mheshimiwa Rais,pamoja na kuvumilia,tilia mkazo uchmbaji mdogo mdogo wa madini,kama STAMICO itapewa nguvu ijiendeshe kama Tanesco,kisha ilete vifaa vya uchimbaji mdogomdogo wa madini,mathalani= Compressors,wet ball mill capacities 1t,2t/hr] Jaw crushers,winchi na mitarimbo na bits zake,kisha kila kanda kuwe na workshop iliyosheheni vyombo hivyo,hata kama kwa kuazia wachimbaji wtashindwa kumudu kununua,lakini kuna makota[local brokers]wanaweza kununua baadhi ya viaa kama compressor na kuwakodisha wachimbaji.Niko hapa Nyarugusu,fani yangu ni uhandisi wa migodi, najitahidi kushauri wachimbaji namna bora ya kuchimba lakini maneno matupu yanawakera maana wangependa waone vifaa,tena wengine wangeweza kupata mikopo kwenye bank iliyopo hapa hapa Nyarugusu,lakini vyombo hivyo havipo!!.Kwa hiyo STAMICO ikilielewa hili,tutaweza kuwawezesha wachimbaji wachimbe kitaalamu na vilevile ni njia bora ya kudhibiti dhahabu isiuzwe kupitia njia za panya.
Sekta hii inaweza kutoa ajira lukuki,kwa mfano:mchimbaji mwenye hati ya kuchimba,akipata vifaa ambavyo havizidi US$150,000,ANWEZA KUAJIRI WAFANYAKAZI SITINI [60],FIKIRIA KUNA HATI MILIKI ZA UCHIMBAJI ZILIZO HAI NGAPI NCHI NZIMA[KWA MADINI YA DHAHABU ZINZKADIRIW KUFIKIA 6000],INA MAANA KATIKA MIGODI YA DHAHABU PEKE YAKE KUNGEPATIKANA AJIRA 360,000[DIRECT EMPLOYMENTS]SASA JE ZILE ZITAKAZOJITOKEZA [INDIRECT],NA JE DHAHABU KIASI GANI KIGEPATIKANA?HUU UMASIKINI TUNAULEA TU KWA KUTOKUTHUBUTU,LAZIMA TUONDOKANE NA ILE DHANA YA KIZAMANI,TUFANYE YALE TULIYO NAYO,MATOKEO YAKE BEI ZA BDHAA ZA
WENGINE ZITAPAMBANISHWA NA DHAHABU YETU.Kwa mchimbaji wa kawaida aliye na mgodi unaozalisha kwa wastani ni wakia[ounce[oz]6.4/siku,lakini kuna wanaozalisha mara dufu.ina maana kwa mwezi anaweza kuzalisha wakia 160 kwa mwezi.hii ni sawa na US$ 122,880,KWA ASILIMIA 80 YA UBORA.
kAMA HUU NI WASTANI WA VIWANJA VYOTE 6000,INA MAANA KWA MWEZI DHAHABU ITAKAYOZALISHWA KWA MWEZI NI 160 X 25
4000 oz. au US$ 491,520,000.KWA MWEZI,AU
US$ 5,898,240,000 KWA MWAKA.Ikumbukwe tumechukulia wastani wa chini tu.Ukibadilisha katika shiling za kitanzania ni sawa na Sh.trilioni 6.8.Je bajeti yetu ikoje?au chukulia imepatikana asilimia 40 tu,sawa na trilioni2.72,si haba.NASISITIZA STAMICO NA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO NA VYOMBO VYA KUCHIMBIA MADHUBUTI INAWEZEKANA.

na Andrew Gadi Mrinji, Geita/Tanzania, - 21.07.08 @ 14:19 | #23378

kila siku JK ANATELEZA ULAYA HALAFU SIE TUVUMILIE TAABU NA SHIDA NA MSHAHATRA KIMA CHA CHINI KILA MWAKA WA FEDHA WANAONGEZA BUKU MBILI MBILI.
UNAWAPELEKEA UZURI WAZUNGU WE SUBIRI MATOKEO...

na wily, mby, - 21.07.08 @ 14:22 | #23379

Wazungu ndo wanaotufilisi hii nchi. Mna habari kuwa Alhamisi wiki iliyopita balozi wa Canada alienda na ujumbe Dodoma kuonana na baadhi y wabuge eti ku-loby mswada mpya na mapendekezo ya kamati ya madini usikubaliwe. Barrick ni kampuni toka Kanada wanachukua matrilioni yetu halafu wanatulete msaada wa mamilioni. Kweli wajinga ndo waliwao. Siju na hawa wabunge wanaokubali kujadili suala kama hili wanaitakia mema kweli nchi hii?

na Robert, DSM, - 21.07.08 @ 14:50 | #23385

Mheshimiwa rais nasikitika kauli yako uliyo itoa kwa wanyonge watavumilia mpaka lini?kwenye ilani ya chama chako ulisema utatoa maisha bara kwa kila mtanzania yako wapi?mfumko wa bei haujaanza leo ulianza pale tangu uliposhika madaraka. Mwaka 2006 nauli zilipanda,2007 naulizikapanda tena na 2008 nauli zimepanda pia,mbona waliokutangulia waliweza kudhibiti mfumko wa bei?.Tatizo lako mheshimiwa umekalia kuchekacheka na kuweka watu madarakani kiurafiki kwa kuangalia masilahi yako naya rafiki zako tu,kwakuwa walikusaidia kuingia ikulu kwa fedha zao hivyo hata wakianza kupandisha vitu bei huwezi kuwakemea maana wanarudisha fedha zao walizokusaidia wakati wa kampaini.Angalia richmond ilivyokula pesa za wanyonge ulipopata taarifa hukuchukua hatua zozote eti unaunda tume nayo tumeimekupa ripoti unasema eti katibu mkuu wa serikali ataangalia hatua za kuchukua sasa wewe unakazigani hapo?ni msaada gani unautoa kwa wanyonge kama rais?. Ulichaguliwa kwa kishindo lakini hakuna lolote unalofanya kazi kukumbatia mafisadi ila mungu ataipigania nchi ya tanzania.

na Joe Das, china, - 21.07.08 @ 16:00 | #23406

Hi! shida haivumiliki wakati mwenzako unamuona anamega pale patamu.Ingekuwa wote tunapata shida hapo shida ingevumilika. Je kwanini wengine wavumilie shida wakati wengine wanaishi kama peponi tena kwa wizi wa hela za walalafofo?

na MR.JOO, PWANI-KIBAHA, - 21.07.08 @ 16:38 | #23414

Kama ni ushauri basi Rais ana matatizo makubwa!! Hawa washauri wameonyesha kuwa na uwezo mdogo wa kumshauri mkuu wa nchi. Kama ni yeye mwenyewe, basi taifa lina tatizo kubwa!!

Katika hali tuliyo nayo sasa watanzania ni mtu gani mwenye akili timamu anaweza kusimama na kuwataka watu waendelee kuwa na uvumilivu? Uvumilivu maana yake ni nini? Kwa nini Rais asitamke tu kwamba wanaotaka kufa na wafe kwani serikali haijali wala haitishiki.

Waendelee kuvumilia nini? Kuvumilia kuna maana kwamba wasubiri hatua zinazochukuliwa zifanikiwe. Sasa ni hatua gani zinazochukuliwa na serikali? Kuwakingia kifua mafisadi kutatusaidia nini sii akina "kafie mbali"?

Kana kwamba hiyo haitoshi, Rais anabainisha kupanda kwa bei ya mafuta duniani kama sababu ya matatizo yetu!! Tafadhali Mheshimiwa Rais, mswalie mtume jamani!! Bei ya mafuta imepanda lini na maisha ya Watanzania yameanza kuwa magumu lini? Mwogope Mungu jamani!! Kumbuka baadhi ya viongozi wa dini wanafiki walikuita chaguo la Mungu; angalia usimkasirishe huyo Mungu maana adhabu zake ni kali kupita kiasi mnachofikiri mafisadi.

Mbona Mheshimiwa hutaji sababu yenyewe ya hali hii: ufisadi uliokithiri wa viongozi wa nchi hii? Kweli ni halali katika nchi ambayo Kiongozi Mkuu ni mmojawapo wa "the best JK eleven", kuendelea kulaumu kupanda kwa bei ya mafuta? Hata hiyo bei ingeshuka leo tutapata faida gani?

Ni jana tu TANESCO imetwambia kwamba kusitishwa kwa mkataba wa Dowans hakusaidii chochote kwani malipo yale hayakuwa na athari kwenye mapato ya shirika!! Sasa kama milioni 154 kwa siku ni vijisenti, mnataka mafuta yashuke kwa kiasi gani ili tufaidike nayo?

Acheni kutudanganya, wakati huo umepita.

na Amk, Dar, - 21.07.08 @ 17:29 | #23425

Sasa Kikwete amepata sababu ya kuwadanganya wananchi matarajio ya 'maisha bora kwa kila mtanzania' yanapoota mbawa!

na chavala, UK, - 21.07.08 @ 19:40 | #23455

Je Raisi wetu Kikwete ulidhani utarithi nchi isiyo na matatizo? Kazi ya raisi si kuzunguka nchi kukagua matatizo bali ku-solve matatizo!Ilipoingia madarakani ulilia tatizo la njaa! Ohh jamani kunaukame na tatizo la chakula hivyo msitegemea uchumi utakua kwa kasi ilele! Tukakubali! Mara ukaanza kulia Oooh ukame jamani hatuwezi kufua umeme wa kutosha kasi ya ukuaji wa uchumi itapungua, wahisana wakakukopesha fedha kwa ajili ya kufua umeme wa dharura zikaishia katika ufisadi Richmond na safari zako zisizo na mwisho! Kukaja ugonnjwa unaoathiri mifugo ukalia jamani uchumi hauwezi kukua ipasavyo tatizo la mifugo, watanzania tukala samaki Mungu akatunusuru na wala si juhudi za serikali ugonjwa ukatokomea! Haya sasa umesikia Bei ya mafuta unalia kama kawaida yako! Je Kikwete unadhani uraisi ni kulia shida au kubuni njia za kutatua matatizo. kila nchi ina matatizo: Msumbiji jirani zetu, uchumi wake unakua kwa karibu asilimia 10 licha ya miaka mingi ya vita je wao hawako kwenye dunia hihi yenye shida ya mafuta. mikakati gani sirikali yako inafanya kutumia Gesi asilia tuliyonayo kwa wingi kama nishati? Tatizo lako ni kulia tu! Mawaziri wako wakiuliywa Bungeni kuhusu mikakati ya kujikwamua utegemezi wa nishati! Majibu kila siku wizara yangu inafanya sijui inafanya upembuzi yakinifu juu ya utumia Gesia asili... mapaka lini? Tumechoka nanyi hamna ubunifu ila kulia Tu. Raisi anakwenda Hospital Muhimbili wagonjwa wanalala sakafuni yeye, waziri wake anaficha dola million moja nje! Yeye aogopa kutumia nguvu zake kmweka kiyuizini kurudisha fedha zetu! Kila mhali kucheka tu na kuahidi kutafuta wahisani Mapaka lini?

na Zamani wa Kale, Moshi, - 21.07.08 @ 21:24 | #23480

Sikilizeni ndungu zangu, mnamraum Rais bila kufikilia. Ndio nakubali wakati ni mgum! Hali hii iko dunian kote, hata huku Africa kusini mambo ni yale yale vitu vimepanda beyi sana kwa mfururizo. na Rais wetu hawezi kutatua jambo hili kwa siku moja. Hata kama tuta badirisha chama mambo yatakua yeleyale. Na Nchi yetu bado maskini. Ndoo kwanza tunaanza kupiga hatua kiuchumi kuliko huko mwanzo. Tanzania ilikua haijulikani Duniani kama inavyo julikana sasa kiuchumi na kijiografia. Watanzania tulizoea vyakunyonga bila kuangalia ushindani wa kimataifa. Leo hii tuko kwenye mfumo mpya wa kimataifa. Tafadhali tuwe na subira huku tukifanya kazi kwa bidii. Kukosoana ni jambo zuri, lakini sio vizuri kukata tamaa, tutafika tuu. Rais wetu ana mdamchache tangu kupata Urais. Kunamapengo kibao yakuyaziba ambayo viongozi wengine waliacha huko nyuma. Kumbuka Tanzania ilikuawa haina pesa kabisa serekalini banki kuu ilikua tupu na madeni kibao kutoka duniani. Licha yakwamba Nchi kibao zilitusamehe na (IMF) pia. Lakini hali yakiuchumi ilikua inatisha. Sasa hivi uchumi wa Nchi unapand kidogokidogo. Rais JK ana uchungu wa Nchi, kuliko wengine huko nyuma yake. Tuache uswazi hii ni dunia mpya. Ufisadi ni jambo gum kulishugulikia kila Nchi. It will take time not by one night, to bring all perpetrators into justice. Bila JK tusinge jua kua hera zilikua zinaibiwa, pia jambo hili hatulifikilii!!! Msidanganywe na wenye kiu na madaraka. Peace to our country TZ.

na Exodus, South Africa, - 22.07.08 @ 01:00 | #23487

We Exodus mjinga sana, ehe? Tanzania si maskini hata kidogo, bali tuna umaskini wa akili katika viongozi na wataalamu wetu. Ukitaka kujua maana ya haya ninayosema, tembelea dunia uone vinchi maskini vinavyoipatia Tanzania misaada! aibu saaaaana!

na Chengula, Musoma, - 22.07.08 @ 01:55 | #23504

Watanzania wenzangu, kawaida mti uzaao matunda mazuri ni ule wenye maandalizi mazuri tangu unapandwa. Kiwete amekabidhiwa nchi ktk wakati mgumu sana. na kazi anayoifanya kurekebisha uozo anastahili pongezi na kuungwa mkono. kilio cha mafuta na ghalama ya vitu kupanda si la tanzania tu. Sasa wewe Sungura usilete masuala ya siasa na issue muhimu kama hii. Kwani kunachama ani cha siasa kinazalisha mafuta ili tukipe nafasi ya uongozi wananchi tupone. Nilitegemea utaponda serikali na kushauri nini kifanyike ili kutatua tatizo na sio kuomba uongozi. si kwamba namtetea Kikwete na uongozi wake kuwa wako safi, la hasha, ila ponda kitu alafu sema nini kifanyike si kuomba kuongoza serikali. kwa wachambuzi tunagundua huo ni wivu wa madalaka. Fanya kitu tutakukumbuka 2010 badala ya kuponda

na kajungu mturi, Mugumu Tanzania, - 22.07.08 @ 05:39 | #23538

Tatizo kubwa walilonalo viongozi wengi duniani, ni kuelezea matatizo yaliyopo badala ya kuelezea namna ya kuyatatua.

Utakuta kiongozi anasema kwa mfano "Tuna matatizo ya njaa wakati huu, hivyo wananchi mfanye bidii katika kilimo msiwe wazembe, limeni kwa bidii ili kuepusha njaa."

Kiongozi kwa kusema hivyo anadhani kuwa kuna jambo litafanikiwa, na hivyo ndivyo viongozi wengi wanavyofanya. Hawaelezi nani afanye nini na wapi, na ni zana zipi zitatumika katika hicho wanachotaka kifanyike. Wanadhani kwa kusema hivyo tu basi wananchi watakazana kufanya kile walichoagizwa ili kujiepusha na madhara yanayowajia mbele yao. Wataanzia wapi? Kiongozi anatakiwa awe mbunifu na pia awe na uwezo wa kusimamia kile alichokibuni.

Waandishi wa habari na wengineo nao utawasikia "Kiongozi---- amewahimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii katika kuepuka madhara yatakayowapata katika maeneo yao". Kwa kufanya hivyo wengi wanadhani kuwa kiongozi kafanya jambo na kutakuwa na matokeo mazuri. Ukweli ni kwamba hakuna litakalofanyika, kila mmoja katika eneo husika atabaki kusema, kiongozi wetu amesema tufanye kazi kwa bidii.Nani afanye, aanzie wapi, hakuna.

Uongozi unaotakiwa, ni kiongozi muhusika kupanga mikakati thabiti. Pamoja na matatizo yanayokuwa yamejitokeza ili kutatua, kiongozi awapange wahusika namna ya kufanya hilo jambo analotaka lifanyike. Apange kuwa wewe utafanya moja mbili tatu, na huyu atafanya nne tano na sita. Siku ya ___ nitakuja kuangalia kilichofanyika katika hili. Hapo kweli unakuwa umefanya uongozi, kwa sababu umeeleza tatizo lililopo na namna ya kulitatua, siyo ulalamishi tu usio na ubunifu namna ya kutatua.

Ukiwaeleza watu wafanye jambo bila kufanya mikakati yoyote yakufanikisha jambo hilo lifanyike, kwamba ni nani atafanya nini na nini na kwa wakati gani, hakuna kitakachofanyika.

Viongozi wakiwa na ubunifu, mikakati na malengo na kusimamia, muda si mrefu Taifa letu litabadilika.

na Bernard Mwenda, Zanzibar, - 22.07.08 @ 10:23 | #23590
 
Huyu Raisi hazijui shida ndo maana anasema tuvumilie!Yamkini siku hizi hata hawazi alikotoka!ni kwamba tumechoka kuvumilia!
 
Mwito mzuri ungekuwa kama rais angetuambia hatua zinachokuliwa na serikali yake katika kupunguza waste kwenye katika matumizi ya uendeshaji ili kuweza kuwasaidia wananchi kukabiliana na ugumu wa maisha kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta. Baada yapo ndip angesema kuwa pamoja na hatua hizo, huenda bado maisha yataendelea kuwa mwagumu hivyo anatuomba tukaze mikanda. Ila sasa kutuambi sisi sisi kuvaa na kukaza mikanda ya vyuma huku wao viongozi wakiwa wanatembea na matumbo makubwa bila kukaza hata mkanda wowote ni kutudanganya kabisa.
attachment.php

Mwaka huu serikali ya Marekani imetoa fedha taslimu bure kwa raia wake wote ili kuwasaidia kukabiliana na ugumu wa maisha. Na sasa wabunge na serikali kuu wamekuwa wakiongelea kupunguza kodi ya mafuta na kujaribu kutafuta vyanzo vingine vya mafuta. At least unaona kuwa wanashughulika ili kusaidia raia wake. Siyo hizi lele mama za kaza mkanda, vumilia na upuuzi mweingine usio na maana kwa maisha ya raia wa kawaida kutoka kwa hawa wasanii wetu.
 
Unajua wazee wetu walitufundisha kuwa "asiyejua maana haambiwi maana." JK hajui kama uongozi wa nchi umemshinda, kwa hiyo ukimwambia hivyo hawezi kukusikia. Dawa nzuri ni kuwaandaa wananchi sawasawa kwenye kinyang'anyiro cha 2010 tu.
 
Heshima mbele wakuu.... Leo kwenye Daima naona SUMATRA wamemsaidia Mkuu kutuambia tujifunze kutembea kwa miguu.... Haya kwetu sisi tunaoishi Mbagala na kufanya kazi kawe itabidi tusitembee bali tujifunze kukimbia marathoni manake si utani kazini ninatakiwa saa mbili asubuhi na kutoka ni saa kumi na moja jioni........

Haya:
1. kazi yao kuboresha usafiri sasa wanasema mtembee kwa miguu kila mtu akitembea kwa mguu nani atapanda mabasi?? Ina maana watakuwa hawana kazi, au??
2. Huyu jamaa hajui kuwa kuna watu wamekuwa wanatembea kwa miguu kabla hata nauli haijapanda zaidi ya miaka 10 sasa. Angetembelea maeneo ya Jangwani, Morocco, Kawawa (kigogo side), Keko Mwanga nk; majira ya alfajiri kujionea ni watu kiasi gani hawahitaji kushauriwa kutembea kwa mguu kwani wamekuwa wanatembea daima dumu!

Haya mambo ndiyo hii:

Dar washauriwa kutembea kuepuka ongezeko la nauli

na Mobini Sarya

MKURUGENZI wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Israel Sekilasa, amewashauri wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kujifunza kutembea kwa miguu au kutumia usafiri wa baiskeli, ili kukabiliana na ongezeko la nauli za daladala.

Alisema hayo jana kwenye mkutano wa madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, ulioitishwa na SUMATRA kwa lengo la kuboresha huduma ya usafiri.

Alisema katika nchi ambazo zina matatizo ya usafiri kama Tanzania, wakazi wake hutafuta jinsi ya kujibana, ikiwa ni pamoja na kuongeza matumizi ya baikeli ambayo gharama zake kiuendeshaji ni ndogo.

“Wananchi wanapaswa kujenga tabia ya kutembea kwa miguu au kutumia baiskeli, ili kukabiliana na ongezeko la nauli mara itakapoanza kutumika mwezi ujao,” alisema Seikilasa.

Katika mkutano huo, madiwani walimweleza Sekilasa kuwa SUMATRA inapaswa kujenga na kuhudumia vituo vya daladala kutokana na mapato inayopata, kama ilivyokuwa ikifanya Kampuni ya UDA katika kipindi chake.

SUMATRA ilieleza kuwa suala la huduma ya usafiri limo katika manispaa na majukumu ya SUMATRA ni kutoa leseni, kwani hata mapato yanayopatikana wamekuwa wakiyagawa katika manispaa zote tatu kila moja ikipata asilimia 20.

Majibu hayo yaliwashtua madiwani wengi waliosema kuwa hawakuwa na taarifa kuwa SUMSATRA inapeleka asilimia 20 kwenye manispaa zao, kwani suala hilo halijawahi kuwekwa wazi na wakurugenzi.

Aidha, mkurugenzi huyo aliwataka madiwani wa Dar es Salaam, waende kwenye Manispaa ya Moshi wakajifunze namna ya kuboresha usafi wa mipango miji, ili wakirudi Dar es Salaam watumie maarifa hayo kusafisha jiji.

Courtesy:
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/23/habari21.php
 
Mwito mzuri ungekuwa kama rais angetuambia hatua zinachokuliwa na ........ Ila sasa kutuambi sisi sisi kuvaa na kukaza mikanda ya vyuma huku wao viongozi wakiwa wanatembea na matumbo makubwa bila kukaza hata mkanda wowote ni kutudanganya kabisa.

Mwaka huu serikali ya Marekani imetoa fedha taslimu bure kwa raia wake wote ili kuwasaidia kukabiliana na ugumu wa maisha. Na sasa wabunge na serikali kuu wamekuwa wakiongelea kupunguza kodi ya mafuta na kujaribu kutafuta vyanzo vingine vya mafuta. At least unaona kuwa wanashughulika ili kusaidia raia wake. Siyo hizi lele mama za kaza mkanda, vumilia na upuuzi mweingine usio na maana kwa maisha ya raia wa kawaida kutoka kwa hawa wasanii wetu.

Mkuu Kichug....., tayari SUMATRA wametuambia tutembee kwa mguu kukabiliana na ukali wa nauli za daladala.... Since chakula nacho kinapanda bei usishangae tukianza kuambiwa tuache kula..........

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.............
 
Ingekuwa heri JK uage sasa

Samson Mwigamba
Tanzania Daima~Sauti ya watu

MHESHIMIWA Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, salaam aleykum. Juma lililopita niliwasiliana na Watanzania wote kwa njia hii ya makala. Nilijaribu kuwachokonoa ili kupata mawazo yao juu yako.

Na kwa bahati nzuri nilikuwa nimeongea moja kwa moja na Watanzania wote wakiwamo wasaidizi wako muhimu. Na ili kuwahakikishia kwamba niliwalenga na wao pia niliamua kuwataja kabisa pale niliposema, “Yote kwa yote ni kwamba kila mtu anajua sasa Rais Kikwete uwezo wake wa kuliongoza taifa na chama chake umepungua.

"Ninaamini ndani ya dhamiri yangu kwamba hata wasaidizi wake, wakiwamo usalama wa taifa, mawaziri na manaibu mawaziri, wanamtandao na wapambe wake, wabunge, viongozi wenzake ndani ya chama, watendaji wake serikalini na wasaidizi wake wengineo wote wanajua hili”.

Nilifanya hivyo kwa makusudi ili kupata maoni yao juu ya hili. Nawatambua sana wasaidizi wako. Ni watu mahiri sana kwa kulinda maslahi yao na ya wakubwa wao. Nilijua watanijibu haraka haraka kwa kukanusha ukweli huo mdomoni huku mioyoni mwao wakiutambua. Lakini hawakufanya hivyo. Hii inathibitisha kwamba hata wao ukweli uliwagusa na wamefikia mahali ambapo hawawezi kupingana nao.

Wa kwanza kabisa kuwasiliana nami ni kiongozi wa zamani wa CCM katika mojawapo ya nafasi za uongozi ndani ya chama ngazi ya kitaifa. Yeye alinipigia simu kabisa na kujitambulisha kwa jina, nami nikamtambua kwa sauti kwamba ni yeye. Akanipongeza kwa kusema nimeandika vizuri sana na kwa kweli maneno yake na sauti yake yalionyesha dhahiri kukubaliana na ukweli niliouainisha.

Huyu ndiye akazidi kuthibitisha nilichokizungumza katika aya hiyo hapo juu. Ukweli umewasuta ndani ya dhamira zao na kwa kweli umefika wakati ambao ukweli hauwezi kufichika tena. Wengi sasa wanaogopa kukutetea hadharani wasijeonekana vituko kwa kuupinga ukweli ulio wazi (naked truth).

Mheshimiwa Rais, wasomaji walionitumia ujumbe mfupi wa simu, walionipigia simu, walionitumia barua pepe na hata waliozungumza nami uso kwa uso, wote wamenipongeza kwa ujumbe uliokuwa wazi ukieleza ukweli halisi na kila mmoja wao aliishia kusema ‘atang’oka’ 2010. Baada ya kutafakari ujumbe wa wasomaji na matukio yaliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari juma lililopita, nimeamua kukuandikia waraka huu ili nikupatie ushauri makini lakini bure.

Msomaji mmoja, kwa mfano, aliongea kwa uchungu jinsi ulivyojibu swali la mwanahabari kule Ufaransa. Ulipokuuliza kwa nini nchi yako ni maskini ukasema eti hata wewe hujui. Kwa maoni yake ilikuwa ni aibu kubwa kwa kiongozi wa nchi kujibu hivyo tena mbele ya viongozi na wanahabari wa kimataifa. Uliuonyesha ulimwengu kwamba nchi hii ni ya ajabu na watu wake ni wa ajabu. Ni kama ulikuwa unathibitisha kauli iliyopata kutolewa na mwandishi mmoja kwamba Tanzania ni nchi pekee duniani inayoweza kukaa miaka 10 bila rais na bado ikabaki na amani.

Kwa maoni yangu pia, rais wa nchi kusema hajui umaskini wa wananchi wake unatokana na nini ni sawa na kusema nchi haina kiongozi. Rais wa namna hiyo hawezi kuhangaika na mipango ya kuiondoa nchi katika umaskini, maana hajui kwa nini wananchi ni maskini. Anafikiri pengine ni “wavivu tu wa kufikiri” ama “fursa zipo ila kwa ujinga wao hawataki kuzitumia”.

Rais wa namna hiyo hawezi kujua madhara ya ufisadi wa EPA, Meremeta, Tangold, Kiwira, mikataba ya Richmond, IPTL na jinsi inavyochangia umaskini wa watu wake. Hawezi kuona ubaya wa rais na mke wake kujiingiza kwenye biashara kwa kutumia ofisi, fursa na vyeo vyao vya Ikulu kuwanyonga wananchi. Na kwa sababu hiyo hawezi kujihangaisha kuyashughulikia madudu kama hayo kama unavyofanya wewe hivi sasa.

Rais wa namna hiyo atakuwa ‘busy’ na safari za nje zisizo na kikomo, kukutana na marais wakubwa kama akina George Bush tena wanapokutana Bush atampiga piga mabegani rais kama huyo kama alivyofanya alipokuja hapa Dar es Salaam, na tungetamani kupata tafsiri ya kitendo hicho cha George Bush, ambaye wafuatiliaji wanasema hata mlipokutana Japan alikupiga piga begani tena, kutoka kwa Salva Rweyemamu yule mwandishi wa zamani aliyeisakama serikali kwa kalamu yake, lakini baadaye akawa mwanakampeni wako mahiri kwa kutumia kalamu hiyo hiyo na baadaye ukamzawadia ukurugenzi wa mawasiliano Ikulu.

Mheshimiwa, watu wanashangaa hata kitendo cha serikali yako kushindwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maji, visivyokauka tulivyonavyo hapa nchini na ardhi safi tena kubwa inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kujihakikishia chakula cha kutosha. Lakini badala yake unakwenda Italia kwa kutumia mamilioni ya shilingi kuomba chakula kwa WFP.

Mheshimiwa Rais, si siri ni aibu kubwa. Mabilioni yaliyopotea kwenye ufisadi yangetosha kuanzisha ‘scheme’ kubwa 13 za umwagiliaji kwenye mikoa 13 ya nchi hii. Na hesabu zake ni rahisi mno wala huhitaji kutumia shahada yako ya kwanza ya uchumi ambayo hata hivyo sijui kma umewahi kuitumia.

Chukua milioni 152 kwa siku kwa mwaka mmoja tu zilizolipwa kwa Richmond/Dowans ambazo kwa siku 365 za mwaka ni bilioni 55. Jumlisha bilioni 2,098 zilizolipwa kwa IPTL kwa miaka minane tu kwa kuzingatia kauli ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, bungeni Dodoma Agosti6, 2007 kwamba kwa kipindi cha Julai 2005 hadi March 2006 peke yake IPTL ililipwa jumla ya bilioni 262.3. Kwa vipindi vinane tu kama hivyo kampuni hiyo imelipwa jumla ya bilioni 2,098. Jumlisha bilioni 133 zilizoibwa kupitia EPA, kisha juu yake ongeza bilioni zisizopungua 600 zilizopotea kupitia ujenzi wa minara miwili pacha pale BoT. Halafu umalizie na mabilioni yaliyopotea kupitia viufisadi vingine vingine kama ubinafsishaji wa TTCL, NBC, Kiwira, n.k ambazo nazo si chini ya 100.

Halafu chukua hiyo jumla inayofikia bilioni 2,986 bila kuongeza bilioni ulizozitumia wewe kwa safari zako za nje tangu uchaguliwe kuwa rais. Igawanye jumla hiyo kwa gharama za mradi mzima wa kupeleka maji Shinyanga ulioshikiwa bango na best yako ili aje kuonekana anafaa kuwa waziri mkuu wa nchi hii. Utapata 13 ambazo ni scheme kubwa za umwagiliaji zenye thamani ya sh bilioni 225 kila moja.

Ina maana tungeweza kuwa na scheme kama hizo katika mikoa 13 inayoongoza kwa ardhi inayofaa kwa umwagiliaji. Njaa ingetupata wapi. Hivi sasa dunia inapolia na kupanda kwa bei za vyakula sisi tunaoita kilimo uti wa mgongo wa uchumi wetu tungekuwa matajiri kwa kuuza chakula.

Lakini hivi sasa eti serikali yako inapiga marufuku kuuza chakula nje ya nchi, mkulima anayetegemea kuuza chakula chake cha ziada ili apate matumizi yake mengine ikiwamo kusomesha watoto unamwambi nini?

Mheshimiwa Rais, watu waliodunisha maisha ya Watanzania kiasi hicho eti bado hutaki kuwachukulia hatua hadi leo. Umeunda tume juu ya tume nyingine lakini mafisadi wanaendelea kutesa. Ajabu zaidi chama unachokiongoza juma lililopita, kimetangaza eti kumpa onyo kali aliyekuwa naibu meya wa Ilala na kumzuia kugombea cheo chochote zaidi ya udiwani alionao, sababu eti ni kushiriki bomoabomoa ya Tabata Dampo na kuisababishia hasara serikali ya sh bilioni 1.8, kuwasababishia usumbufu wananchi wa Tabata Dampo na kukiaibisha chama.

Gazeti hili likaiandika habari hiyo Jumatatu wiki hii, kwa kichwa kilichosema; 'CCM yacharuka'. Naomba kupingana moja kwa moja na maneno aliyoyatumia mwandishi wa habari hiyo. Kimsingi CCM haijacharuka. Bali ina mkakati pengine unaosimamiwa na wewe mwenyewe mwenyekiti wako kukisafisha chama. Msitudanganye kiasi hicho, kwamba mna uchungu sana na pesa za serikali, mnawajali wananchi na kulinda hadhi ya chama chenu.

Fikiria hasara za mabilioni ya serikali niliyoyataja hapo juu, yote yamesababishwa na wana-CCM, fikiria Watanzania milioni 40 wanaoteseka kwa ajili ya wana CCM na ukumbuke jinsi hadhi, si tu ya chama unachokiongoza bali pia ya serikali unayoiongoza ilivyoporomoka ndani ya mwaka mmoja, kwa ajili ya wana-CCM. Lakini hamjawakaripia wala kuwafuta uanachama kama mlivyofanya kwa Naibu Meya Yakubu.

Huu ni usanii ambao umeshajulikana kwa Watanzania. Mheshimiwa Rais, juma lililopita umetoa kali nyingine ya mwaka. Umewaasa Watanzania wavumilie shida wasikate tamaa. Hii nayo ni kauli nyingine ya mzaha kwa Watanzania kama ile ya kusema hujui umaskini wao unasababishwa na nini.

Natamani ungekuwa unasoma maoni ya wasomaji. Siku hizi Tanzania Daima imeanzisha sehemu ya maoni ya wasomaji wanaosoma gazeti hili, kwenye tovuti. Msomaji mmoja aliposoma alisema hivi: “Kaka yetu usipate tabu wewe sema tu.

Sisi tumezoea shida, huna tofauti na Karume anayewaambia Wazanzibari watazoea tu. Sasa sisi tumezoea na wewe endelea kula nchi maana mafuta si kazi yako. Wewe linda mtandao wako usisambaratike, maana inabidi uutumie kurudi madarakani mwaka 2010.” Haya si maoni ya mtu anayekuambia kwa wema. Huyu ana uchungu ndani ya moyo wake na kwa ujumla maneno yake ni laana kwa serikali yako.

Mwingine akasema hivi: “...Kikwete suala la mafuta na maisha magumu havimhusu kabisa. Ndiyo, si anatuonyesha hivyo kwa kuwalinda mafisadi? Na sasa kapata kisingizio cha bei ya mafuta basi ndiyo itakuwa hadithi. Hivi wadanganyika wenzangu mnafikiri bei ya mafuta ikishuka (let's say) hadi nusu, ndiyo maisha yatakuwa bora kwa kila mdanganyika? "Dhahabu imepanda sana bei katika soko la dunia. Kwa nini vitu kama hivi vimeshindwa kufidia pengo la mafuta yaliyopanda?

Watu wengine wanafananisha Bongo na Marekani - eti na Marekani maisha yamepanda. Nyie ndugu zangu hebu acheni mzaha! Wewe unakula humburg na pizza Macdonald halafu unatuambia maisha yamepanda? "Chonde chonde jamani.

Natamani mngerudi huku mkapigika mkashindia kauzu ndiyo mngejua watu wanaongea nini…” Ukurasa huu hautatosha kukupatia maoni ya kila msomaji, lakini natamani ungejisomea mwenyewe habari hiyo kisha chini yake usome maoni ya watu.

Wasaidizi wako wanaweza kukusaidia kutembelea http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/21/habari1 Mheshimiwa Rais ningekushauri jambo moja tu. Kukubali pia ni uungwana wa aina yake na Watanzania wanapenda watu waungwana.

Baada ya ziara yako ndefu mkoani Tanga, utakaporejea Ikulu fanya jambo moja tu. Andaa hotuba yako ya mwezi bila kumshirikisha msaidizi wako yeyote. Ita waandishi wa habari kana kwamba unakuja kujibu tu maswali watakayokuuliza halafu wakisha fika toa hotuba yako kabla hujaulizwa maswali.

Waeleze wanahabari na Watanzania kwa ujumla kwamba wakati unachukua fomu za kugombea urais mwaka 2005 hukuijua vizuri sababu ya umaskini wa Watanzania. Waeleze kwamba wewe ulidhani kazi uliyokuwa nayo ni kuwaita tu wawekezaji uliokuwa umeshazoeana nao sana ukiwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na kwamba wakishakuja kuwekeza tayari maisha bora kwa kila Mtanzania yanajipa.

Sema kwamba umekuja kugundua kuwa mambo sivyo yalivyo. Umaskini wa Watanzania una uhusiano wa karibu mno na utawala wa nchi. Na kwamba utawala wa nchi kwa miaka mingi umebaki kuwa mbovu hasa kupitia ‘system’ iliyojengwa na Chama chako Cha Mapinduzi ya kulindana viongozi, bila kujali madhara yanayosababishwa na viongozi mafisadi hapa nchini na hivyo hata malaika akiwa rais wa nchi hii kupitia CCM hakuna maendeleo yatakayopatikana.

Sema wazi wazi kwamba kama rais wa nchi hata kama ungekuwa na dhamira ya kuikwamua nchi kutoka kwenye umaskini unaosababishwa na uongozi mbovu, ungeshindwa kwa kuwa kikulacho ki nguoni mwako. Maswahiba zako waliofanya juu chini upate urais ndiyo hao hao mafisadi waliokubuhu hata jina la mafisadi haliwafai tena. Nasikia wengine wameanza kuwaita ‘mafisidi’.

Na wewe huwezi kuwatupa wakati ungali ukikumbuka mchango wao mwaka 2005. Kwa sababu hiyo, ili kulinda uhusiano wako nao na wakati huo huo kulinda heshima kupita kiasi uliyopewa na watanzania, umeamua kuachia ngazi na hivyo mwaka 2010 hutagombea tena.

Wapatie Watanzania nafasi ya kuanza kufikiria tangu sasa chama kitakachowafaa kuongoza nchi hii hapo 2010, kutokana na sera zake kabla hawajafikiria ni nani atawafaa kuwa rais wa nchi baada yako. Uhakika mmoja tu nakupatia kwamba hutabaki ulivyo machoni mwa Watanzania.

Najua wapambe wako watakulaumu sana, maana kwa kung’oka wewe utakuwa umewakosesha ulaji mkubwa. Lakini utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri ya kuwa shujaa mbele ya Watanzania, kwa kutoboa ukweli na utapumzika kwa amani baada ya miaka 10 ya kusaka urais na miaka mitano ya kushutumiwa na Watanzania kwa kutotoa (not delivering) kile ulichotarajiwa.

Naamini pensheni itatosha, isipotosha utaongezea kilimo cha kisasa. Fanya uamuzi sasa ama utakuja kujuta utakapostaafu. Watafanya kama walivyomfanyia Chiluba hadi utashangaa.

Uamuzi ni wako Mheshimiwa Rais.

Asante kwa maada nzuri yenye ukweli.
 
Back
Top Bottom