Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 83
- Thread starter
-
- #41
Hitimisho, Mheshimiwa Spika,
Waheshimiwa Wabunge:
nimesema Mengi. Kwa Leo Inatosha. Ninamalizia Kwa kuwahakikishieni Kuwa Nafahamu Vizuri Sasa Ukubwa Wa Heshima Na Uzito Wa Majukumu Niliyokabidhiwa Na Watanzania Wenzangu. Ninafahamu Matarajio Ya Chama Changu, Chama Cha Mapinduzi. Nitaongoza Kwa Dhati Utekelezaji Wa Ahadi Zetu Kwa Wananchi, Na Kwa Dunia. ninayajua Matarajio Ya Watanzania Wenzangu Walipoitikia Wito Wa Ari Mpya, Nguvu Mpya Na Kasi Mpya. Ninayajua Matarajio Ya Nchi Jirani, Bara La Afrika Na Dunia Kwa Awamu Ya Nne Ya Uongozi Wa Taifa Letu. Ninajua Wahisani Wetu Na Wawekezaji, Wa Ndani Na Nje, Wananisikiliza Kwa Makini, Wakitaka Kujiridhisha Iwapo Nitavijaza viatu Alivyoniachia Rais Wetu Mpendwa Wa Awamu Ya Tatu, Benjamin William Mkapa. Nitajitahidi Ingawa Ni Vikubwa Kwangu.
Kwenu Nyote, Na Kwao Wote, Naahidi Kwa Msaada Wa Mwenyezi Mungu, Na Kwa Ushirikiano Na Bunge Hili Na Wananchi Kwa Ujumla, kuwa Naweza Kutimiza Matarajio Ya Kila Mmoja. Tanzania Yenye Neema Tele Inawezekana. Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania Yanawezekana. Kila Mmoja Wetu Atimize Wajibu Wake.
Mungu Ibariki Afrika. Mungu Ibariki Tanzania.
Ahsanteni Kwa Kunisikiliza.
Naye Haroun Mlawa, mkazi wa Dar es Salaam, alisema hatua hiyo ya Rais Kikwete imewakumbusha Watanzania enzi za utawala wa Awamu ya Kwanza chini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyewataka Watanzania kufunga mikanda baada ya kumalizika kwa vita ya Uganda na Tanzania mwaka 1979.
JK: Vumilieni shida
TANZANIA DAIMA, 21ST JULY, 2008
na Anna Makange, Tanga
RAIS Jakaya Kikwete, amewataka Watanzania kuwa wavumilivu kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili kwa sasa, inayosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani.
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho Watanzania wengi, hasa wa kipato cha chini wamekuwa wakilia kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana, wilayani Muheza, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo, ikiwa ni siku ya tisa ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, mkoani Tanga.
Rais Kikwete alisema kupanda kwa bei ya mafuta, kumechangia kwa kiasi kikubwa kulipuka kwa mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali duniani kote.
Alisema hali hiyo pia imechangia kuzorotesha kasi ya ukuaji wa uchumi hasa kwenye nchi zinazoendelea na hivyo watu wenye kipato duni kukabiliwa na hali ngumu ya maisha, hususan katika upatikanaji wa mahitaji muhimu, jambo ambalo aliongeza kuwa hata yeye limekuwa likimuumiza kichwa.
Ndugu zangu Watanzania wenzangu naelewa sana jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu siku hadi siku na hali hii inasababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta hapa nchini, hivyo kila bidhaa kwa sasa gharama zake ni za juu sana, kuanzia vyakula hadi vitu vingine ambavyo ni muhimu kwa maisha ya kila siku. Linatuumiza sana hasa wale wananchi ambao ni maskini wa kipato, alisema Rais Kikwete.
Hata hivyo alisema Watanzania wasikate tamaa kwa kuona kwamba maisha yataendelea kuwa hivyo, na kusisitiza kwamba yeye kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali duniani wanalishughulikia suala hilo.
Wakati Rais Kikwete akiwataka Watanzania kutokatishwa tamaa na hali hiyo, Chama cha NCCR- Mageuzi, jana kilisema wananchi hawana sababu ya kuilaumu Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kwa kupandisha bei ya nauli na badala yake lawama hizo zielekezwe kwa serikali ya Rais Kikwete.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi, Faustine Sungura, alisema kutokana na matatizo hayo, kuna haja ya kuwepo kwa serikali mbadala, kwa madai kuwa serikali imeshindwa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi, hasa ya upandaji wa gharama za bidhaa mbalimbali.
Watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na makosa, kwani muda waliowapa viongozi wa CCM kutawala unatosha na haujaonyesha mafanikio yoyote katika maisha zaidi ya kuzidisha ugumu wa maisha, alisema.
Watu wanakosea sana wanapoilaumu Sumatra badala ya kuilaumu serikali ambayo imeshindwa kudhibiti upandaji wa bei kwenye bidhaa mbalimbali yakiwemo mafuta, alisema Sungura.
Alisema hata ziara anazofanya Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Ali Mohamed Shein ni dhihaka kwa Watanzania, kwani ahadi zao hazitekelezeki na wameshindwa kuwasaidia wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao wanashinda Ikulu.
Hivi hawa ni viongozi wa aina gani kama wameshindwa kuwasaidia wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoshinda pale Ikulu, wataweza vipi kuwasaidia watu wa huko mikoani? alihoji Sungura.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amesema serikali itahakikisha inafanya kila jitihada za kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuwekeza kwenye kiwanda cha usindikaji wa matunda wilayani Muheza, kwa lengo la kuwatafutia wakulima wa machungwa soko la uhakika.
Alisema lengo la kujenga kiwanda hicho licha ya kumtafutia soko mkulima, lakini pia itakuza kipato cha wakulima sambamba na kupunguza kiwango kikubwa cha machungwa yanayoharibika mashambani kwa kukosa wanunuzi hasa nyakati za msimu.
Serikali inaamini kwa kufanya hivi tutakuwa tumemsaidia mkulima kwa kiasi kikubwa kuwa na soko la uhakika sambamba na kukuza kipato chake ambacho hivi sasa kinapotea kutokana na kiasi kikubwa cha matunda kuharibika nawaahidi kwamba hili tutalitekeleza haraka iwezekanavyo, alisisitiza Rais Kikwete.
Miongoni mwa ahadi alizotoa rais wilayani Muheza ni pamoja na kupeleka darubini katika zahanati ya Kijiji cha Kicheba, kuchangia sh milioni mbili katika ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Mtindiro, sambamba na kutafuta magari ya wagonjwa katika wilaya zilizokosa huduma hiyo mkoani hapa.
HII SASA KALI, KAZI KWENU WADAU
Hii ni dalili mbaya sana na inaonyesha tunako elekea sio salama tunaelekea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ,nauona Uchaguzi mkuu unaokuja utakuwa na maafa mengi kuliko Uchaguzi wowote uliowahi kutokea hapa Tanzania ,Uchaguzi ambao waliopo madarakani kama hawatakubali kuendesha uchaguzi ulio huru na usio na mizengwe basi yule nyoka aliepitia kenya Zimbabwe sasa anaitambalia Tanzania.tukae mkao wa kujitayarisha.
KASHFA NZITO YA KIKWETE. !!!!!
Baada ya kusoma kwa makini kwa siku nne mfululizo, kwenye forum yetu hii tukufu, na baada ya kuona kuwa uongozi wa forum hii tukufu umeamua kuwa kila anayeona uovu wa viongozi wa kisiasa na haswa wenyeviti wa vyama vya siasa ana haki ya kuleta ujumbe wake hapa bila kubugudhiwa kitu ambacho nakiheshimu sana kwenye ujenzi wa demokrasia na pia haki ya kupata habari kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania ibara ya 18.
Na pia nimeguswa kuandika ujumbe huu kutokana na kile nilichokiona kwenye gazeti la majira la jana (front page) na pia kauli iliyotolewa na katibu mkuu wa CCM ndugu Makamba kuunga mkono hoja iliyowekwa hapa forum na wanachadema! Kama ilivyorushwa kwenye taarifa ya habari ya channel ten jana saa moja jioni .
Makamba alisema kuwa viongozi wa upinzani waache kurusha mawe ile hali wao wako wakiishi kwenye nyumba za vioo!nimeshtuka na kuogopa kama huyu ndio anatakiwa kuonyesha njia ya kuweza kufikia maisha bora kwenye taifa hili , nashindwa kuamini kuwa huyu ndio dereva wa chama tawala !
Leo nimeona niweke ushahidi wangu hapa juu ya ufisadi wa ziada na au uovu uliotendwa na JK pamoja na timu yake wakati wa kuwania kuteuliwa na chama chake, na pia jinsi alivyotumia cheo chake cha waziri wa mambo ya nje kuendekeza ngono na kulisababishia taifa hili madhara makubwa ikiwa ni pamoja na mahusiano ya kidiplomasia kuwa mabaya.
Naanza kuweka hoja zangu na ushahidi wake kama ifuatavyo,
1.Kikwete wakati anagombea kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM ,aliunda timu za aina mbalimbali ila kwa hapa nazungumzia timu yake ya uharamia ambayo aliiunda, aliunda timu ya kuwafanyia maasi wagombea wenzake na mojawapo ni hii iliyokuwa inaongozwa na mtu anayeitwa Gogo kutoka kule Bagamoyo.
Huyu alinunuliwa gari aina ya Nissan patrol ,na ndio mwanzo alitumika kupita kwenye misikiti mbalimbali na kutengeneza mtandao wa kiislamu,ila huyu Gogo ndio alihusika na aliongoza kikosi kilichohusika kumpora mke wa mzee Malecela fedha taslimu zaidi ya milioni mia mbili wakati anatoka dar kwenda dodoma kwa ajili ya kampeni. ENEO LA GAIRO.
Gogo akiwa na vijana wenzake walimteka mama Kilango nje kidogo ya mji wa morogoro na kumpora fedha hizo na pia kumfanyia mambo ya ajabu ambayo kwa mtu mzima kama mimi siwezi kuyaandika hapa.(ushahidi upo na nitautoa muda wowote kama utahitajika hapa ,niandikie kwenye PM yangu.)
2.Akiwa waziri wa mambo ya nje mwaka 2004 alipokwenda nchini marekani kuiwakilisha nchi kwenye kikao cha UN alifanya ngono na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Uganda kitu kilichowafanya kutokuweza kuhudhuria mkutano kwa siku mbili mfululizo, na ndipo rais museven alimwandikia rais mkapa rasmi malalamiko yake na pia alimtimua kazi waziri huyo .
Hili linaifanya nchi yetu kutokuwa na mahusiano mazuri na serikali ya Uganda na haswa kati ya Kikwete na Museven na hili limechangia kwa kiasi kikubwa hata kutokufikiwa kwa shirikisho kwani Museven anaamini kuwa hawawezi kujadili mambo serious na JK kutokana na kutokwenda kuwakilisha nchi na badala yake ikawa ni kwenda kufanya ngono na waziri aliyetumwa na nchi nyingine bila hata aibu.
3.Kikwete akiwa na swahiba wake wa karibu anayeitwa Jack Gotham,wakiwa maeneo ya millennium towers hotel kijitonyama ,walimchukua binti wa mfanyibiashara mmoja wa jijini ambaye alikuwa anasoma shahada ya kwanza chuo kikuu cha DSM na kufanya naye ngono hapohapo hotelini na kumfanya kuchelewa kwenda kwenye ziara za kampeni kwani kipindi hiki kilikuwa ni wakati wa mchakato wa kampeni ukiwa unaendelea.
Huyu anaacha hata masuala ya maana na kwenda kumchukua binti wa rafiki yake ambaye amemchangia kiasi kikubwa cha fedha za kampeni zake na kufanya naye ngono.
4. Fedha chafu.
Kikwete aliingiza nchini kiasi kikubwa sana cha fedha chafu kutoka kwenye nchi za uarabuni na nyingine alizitoa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo (DRC)kutoka kwa Joseph Kabila na fedha hizi ziliingizwa kupitia mkoani Kigoma na nyingine ziliingilia mkoani Mwanza .
Ujumbe wa watu wa kongo uliongozwa na Luten Jenerali Peter Gessimba Gabonne akiwa na wasaidizi wake watatu ambao walikuwa ni viongozi wa jeshi tiifu kwa Kabila.
Fedha hizi zilitolewa kwa masharti kuwa endapo angeshinda ni lazima ahakikishe kuwa Kabila naye anashinda kule Congo kitu ambacho alikifanya na hata kutumia pesa za taifa hili kwa ajili ya uchaguzi wa congo kwa wale mnaokumbuka Asha Rose Migiro alisema kiasi cha pesa zilizotolewa na misaada mingine ..
5. Ngono.
JK akiwa na maswahiba wa mwanae wa karibu waitwao Benno (huyu kwa sasa anagombea ujumbe wa NEC ndani ya chama chetu),Said (huyu ni msaidizi maalumu wa kumsaidia mzee Makamba) ,Mussa (huyu alikuwa ni kiongozi mwandamizi wa mbio za mwenge mwaka huu), na Sisko (huyu ni chief protocol wa ikulu)wakiwa kwenye club mojawapo jijini dar,(ipo mkabala na red cross-barabara ya Alhassan mwinyi) kabla ya mchakato wa kampeni kuanza rasmi walimchukua binti anayeitwa Hadija aliyekuwa anasoma UDSM (Third year Sociology) na pia ni mfanyibiashara wa mjini Arusha, ila alikuwa pia ni mke wa aliyekuwa meneja msaidizi wa kituo kimoja cha kimataifa nchini , na kufanya naye ngono .
Kitendo hiki kilimfanya Hadija kuachika /kuachwa na mumewe na kumnyanganya magari pamoja na mtaji kitu kilichopelekea binti huyu kuishi kwa taabu hadi JK alipoweza kushinda urais wa nchi na kumpangishia nyumba maeneo ya Kijitonyama ambako anaishi hadi sasa.
Pia JK alimwamuru Benno ambaye ni afisa mwajiri wa jumuiya ya UVCCM kumwajiri bint huyu makao makuu na kwa sasa ameajiriwa kama katibu wa uhamasishaji wa taifa cheo ambacho hakipo hata kwenye katiba ya umoja huo, kwa toleo la 2003 ambalo ninalo hapa.
6. Ngono ,
Alifanya ngono iliyoligharimu taifa hili zaidi ya shilingi milioni mia nne Na themanini, (480 milioni) akiwa kule Zanzibar Hotel Kempinski pale alipokuja na mkewe mpya kutoka uarabuni na kukaa naye kwenye mapumziko hayo ambayo yaliliingizia taifa hasara hiyo kwa muda wa siku 9 tuu.
Mkuu wetu wa nchi anatumia rasilimali zetu kwa ajili ya kujistarehesha yeye binafsi na wanawake zake kutoka huko uarabuni.
7.Ubadhirifu.
Aliweza kujichukulia eneo ndani ya mbuga za wanyama kule Serengeti na sasa anajenga hotel ya kisasa nah ii anaijenga yeye kwa ubia na mke wake huyo wa uarabuni akishirikiana na mashemeji zake hao , swali la kujiuliza ni je?huu mkataba hautaishia kwenye kuliuza taifa hili?
Mke anaenda kupewa mahari ya rasilimali zetu? Kama kila rais akioa ni sharti atoe sehemu ya mbuga zetu je? Mpaka lini tutakuwa tunachezea taifa kwa faida za kuoa ama kupata ngono!
Huyu ndio mwenyekiti wa chama chetu na bado tunamwona kama malaika aliyetoka mbinguni kama sio kuzimu!
Nitakuja na taarifa pia za kina juu ya ndugu Nchimbi ambaye naambiwa kuwa anaweza kuwa ndio katibu mkuu wa chama chetu, jambo ambalo mimi nalipinga kwa nguvu zote kwani huyu naye anaendelea kufanya mambo ya aibu na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya umma nchini.
Ni mimi mwanachama mtiifu na mpenda maendeleo ya chama chetu kitukufu.