JK: Ukosefu wa fedha unakwamisha maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Ukosefu wa fedha unakwamisha maendeleo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dr wa ukweli, Jun 20, 2011.

 1. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  RAIS Jakaya Kikwete amesema ukuaji wa kasi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika unakwamishwa na ukosefu wa fedha za kutosha za kugharimia miradi ya maendeleo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa Kimataifa wa mwaka huu wa Taasisi ya Smart Partnership Dialogue ambao pia unajulikana Langkawi International Dialogue 2011, ulioanzishwa rasmi mwaka 1995.

  Rais Kikwete alisema kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha ili kuharakisha ukuaji kasi wa uchumi, hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo.

  Rais Kikwete alisema kutokana hali hiyo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya kugharimia maendeleo ya bara hilo na watu wake.

  "Tatizo ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi inaweza kuzitoa nchi za Afrika na watu wake katika umasikini kwa haraka zaidi," Rais Kikwete, mjini Kuala Lumpur, Malaysia.

  Shabaha kuu ya Smart Partnership ama Langkawi International Dialogue ni kufanya majadiliano ya kimataifa ya jinsi ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi duniani. Mada kuu katika mkutano wa mwaka huu ni ‘Enhancing Smart Partnership for Socio-Economic Transformation'.

  Akishiriki katika mjadala huo, Rais Kikwete aliwaambia mamia ya washiriki tatizo kubwa linalokwamisha ukuaji kasi wa uchumi na maendeleo katika Afrika ni ukosefu wa fedha za maendeleo kwenye sekta binafsi, sekta ya umma na kwa Serikali.

  Rais alisema chanzo kikuu cha fedha za maendeleo kwa nchi masikini za Afrika ni misaada ya maendeleo (ODA), lakini sasa fedha za ODA zimekuwa zikipungua na wakati mwingine hazipatikani.

  "Hata ukitofautiana na kampuni yenye asili ya nchi inayotoa misaada, basi utanyimwa misaada hata kama kampuni yenyewe ndiyo yenye makosa," alisema Rais Kikwete.

  Rais alisema wakati mwingine inakuwa vigumu kuvutia fedha za maendeleo kutoka nje.

  "Hakuna fedha za kutosha kwenye masoko ya fedha ya ndani na msingi mzima wa kifedha ni dhaifu sana. Msingi wa fedha wa ndani ni dhaifu na hata msingi wa fedha za kigeni wa nchi zetu ni masikini,"alisema Rais Kikwete.

  Rais alisema hali hiyo imezifanya nchi za Afrika kujikuta katika wakati mgumu wa kutimiza wajibu na majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  "Hivyo, sisi katika Afrika tunahitaji kutafuta na kuangalia njia nyingine za ubunifu zaidi za jinsi ya kupata fedha za maendeleo," alisema Rais Kikwete.

  Mapema mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato' Sri Mohammed Najib Tun Abdul Razak ambaye hotuba yake ilizungumza masuala mengi na matatizo mengi yanayoikabili dunia kwa sasa pamoja na umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea.
   
 2. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kaenda lini tena huko Malaysia?......duh huyu jamaa kiboko
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  RAIS Jakaya Kikwete amesema ukuaji wa kasi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika unakwamishwa na ukosefu wa fedha za kutosha za kugharimia miradi ya maendeleo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa Kimataifa wa mwaka huu wa Taasisi ya Smart Partnership Dialogue ambao pia unajulikana Langkawi International Dialogue 2011, ulioanzishwa rasmi mwaka 1995.

  Rais Kikwete alisema kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha ili kuharakisha ukuaji kasi wa uchumi, hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo.

  Rais Kikwete alisema kutokana hali hiyo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya kugharimia maendeleo ya bara hilo na watu wake.

  “Tatizo ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi inaweza kuzitoa nchi za Afrika na watu wake katika umasikini kwa haraka zaidi,” Rais Kikwete, mjini Kuala Lumpur, Malaysia.

  Shabaha kuu ya Smart Partnership ama Langkawi International Dialogue ni kufanya majadiliano ya kimataifa ya jinsi ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi duniani. Mada kuu katika mkutano wa mwaka huu ni ‘Enhancing Smart Partnership for Socio-Economic Transformation’.

  Akishiriki katika mjadala huo, Rais Kikwete aliwaambia mamia ya washiriki tatizo kubwa linalokwamisha ukuaji kasi wa uchumi na maendeleo katika Afrika ni ukosefu wa fedha za maendeleo kwenye sekta binafsi, sekta ya umma na kwa Serikali.

  Rais alisema chanzo kikuu cha fedha za maendeleo kwa nchi masikini za Afrika ni misaada ya maendeleo (ODA), lakini sasa fedha za ODA zimekuwa zikipungua na wakati mwingine hazipatikani.

  “Hata ukitofautiana na kampuni yenye asili ya nchi inayotoa misaada, basi utanyimwa misaada hata kama kampuni yenyewe ndiyo yenye makosa,” alisema Rais Kikwete.

  Rais alisema wakati mwingine inakuwa vigumu kuvutia fedha za maendeleo kutoka nje.

  “Hakuna fedha za kutosha kwenye masoko ya fedha ya ndani na msingi mzima wa kifedha ni dhaifu sana. Msingi wa fedha wa ndani ni dhaifu na hata msingi wa fedha za kigeni wa nchi zetu ni masikini,”alisema Rais Kikwete.

  Rais alisema hali hiyo imezifanya nchi za Afrika kujikuta katika wakati mgumu wa kutimiza wajibu na majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  “Hivyo, sisi katika Afrika tunahitaji kutafuta na kuangalia njia nyingine za ubunifu zaidi za jinsi ya kupata fedha za maendeleo,” alisema Rais Kikwete.

  Mapema mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato’ Sri Mohammed Najib Tun Abdul Razak ambaye hotuba yake ilizungumza masuala mengi na matatizo mengi yanayoikabili dunia kwa sasa pamoja na umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea.
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,332
  Trophy Points: 280
  Pesa wanazolipana posho
  Pesa za kununulia magari ya kifahari ya serikali na idara zake
  Pesa za safari mfurulizo ng'ambo
  Pesa za Madini
  Pesa za maliasili
  Pesa za wawekezaji hewa - ATC, TRL, IPTL etc

  Hizi si pesa? angesema tatizo ni matumizi na manunuzi ya umma mabovu ndiyo yanasababisha ubutu wa maendeleo wa nchi yetu.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kilio cha pili hiko ndani ya wiki 2 mfululizo
  last week akiwa geneva alilia akisema waafrika hawana uzalendo na nchi zao na hawataki kuamini kua afrika imeendelea......this weekenda amekuja na suala la uhaba wa pesa.....slogan ya kulalamika inaendelea as usual
   
 6. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaenda jana.
   
 7. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45

  mchiz anakula bata kishenz wanatumia posho na msafara wake ipasavyo!, juzi knye ziara ya shelisheli aliambatana na msururu wa wabunge kuhudhuria sherehe za uhuru.................. tunapiga kelele kupunguza gharama yeye anatafuta jinzi ya kuzitumia bila mpangilio!
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete

  Rais Jakaya Kikwete amesema changamoto kubwa inayokwamisha ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi ya maendeleo.

  Rais Kikwete amesema kuwa kutokana ukweli kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha za kuharakisha ukuaji wa kasi zaidi hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya ubunifu zaidi ya kugharimia maendeleo ya Bara hilo na watu wake.


   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa mtazamo wangu Rais hajataja kikwazo halisi, hapa amejaribu tu kudandia hoja mradi aeleweke.
  Hoja kubwa ni uongozi bora na viongozi kuacha ubinafsi. Ukiwauliza matajiri wakubwa hawakuanza na mtaji ama anaofikiria Rais, ila uongozi bora pamoja na ubunifu wa kutumia rasilimali zetu ni njia muafaka wa kuondoa kikwazo cha uchumi.
  Mbona rasilimali zetu zenye kutuletea utajiri zinasombwa na wageni kwenda kujitajirisha kwao? Sijajua elimu ya uchumi imeeleweka kwa rais wetu au washauri wake. Ndio maana anazunguka duniana kupitisha bakuli la kuomba mikopo?
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  aliambiwa serikali yake imeishiwa akamtuma huyo mmalawi aje akanushe sasa kilo cha nini?
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,492
  Trophy Points: 280
  nani hajui hili? huyu jamaa buyu kweli
   
 12. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Doctorate ya kupewa bila credentials in action! Yaani kama Dr. Matunge vile ....

   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,492
  Trophy Points: 280
  tumelamba garasa kweli..hapo ndio mwisho wake wa kufikiria
   
 14. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kujua maeneo ya kujiletea maendeleo ni jambo la muhimu sana. Kuwa na pesa siyo maendeleo, bali matumizi mazuri ya pesa huleta maendeleo. Sasa yakowapi angalau maendeleo kidogo kutokana na hizo pesa kidogo za miradi?
   
 15. Y

  Yetuwote Senior Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=4]Haya ni maoni ya wadau - Gazeti Mwananchi [/h]


  0#10mchukia majungu2011-06-20 17:05[​IMG] Ama kweli Tanzania hatuna raisi. Kama hujui tatizo utapataje suluhisho? Tatizo ni uchumi kukaliwa ki[NENO BAYA] na wachache wakiwemo watawala wanazidi kudaganya wananchi kuwa watawaletea maendeleo, matokeo yake watu wamechoka na hawana hamasa tena na maendelea bali wanatibu njaa na matatizo ya kila aina yanayowasonga. Viongozi/watawala acheni maneno, ni wakati wa vitendo. Muungwana akishindwa huwa anaachia siyo kungángánia, utaharibu zaidi na tutafika shimoni ulilochimba tayari, chonde chote [​IMG] .

  Quote  +1#9Sam2011-06-20 14:30Hapa ndiyo utaona tofauti ya mwenye akili na asiyenazo, tofauti kati ya JK Nyerere na Jk ******. Wakati Nyrere alissitiza kuwa Fedha si msingi wa maendeleo, ****** anataka tuamini bila fedha hatuendelei.

  Badala ya kutuambia kuwa fedha ni matokeo ya maendeleo, matokeo ya kufanya kazi kwa bidii, maarifa na uadilifu, yeye anataka sisi tuamini bila fedha hatuwezi kuendelea,

  Hili lilikuwa ni mojawapo ya somo muhimu sana la Nyerere, kuwa fedha si msingi wa maendeleo, Kweli Jk hakumwelewa Nyerere hata kidogo

  Quote  0#8m.ali2011-06-20 12:51Rais wetu apotosha fikira jwenye huwo mkutano. bara la afrika ni tajiri sana. Tanzania tuna madani tele, lakini ile mikataba michafu inatufanya wananchi wanaoishi kwenye madini kuwa masikini. Angalieni mji wa Johannesburg kule afrika ya kusini. Ulijengwa na pesaa za dhahabu. Ilikuwa inatakikana shinyanga na kahama kuwa miji ya kisasa, bahati mbaya wanaonufaika sio wananchi bali wale mabepari wa kutoka nje. Itakuwaje mpaka leo mashirika ya madini wanapewa kila kitu tax free, na hawalipi kodi, wakati bei ya dhahbu imefika dola 1500 aunsi moja. wakati walipowekeza bei ya dhahbu ilikuwa dollar 600 aunsi moja. ile faida kwa nini tusawawekee kitu kinachoitwa faida isiyo kawaida ya bei ya dhahbu na watulipe ushuru asilia mia 30. Ndugu zangu nawapiya kwa jina la mungu viongozi ndiyo wabaya. mpaka sasa hawajafanikisha kuinuwa maisha ya watanzania na tuwe watu wanaoitwa middle class ni wachache sana. Tusimameni na vyama vya upinzani na tudai haki zetu hawo investors ni wezi wakubwa na wala hawana faida na nchi. mwisho tutabakiwa na mashimo matupu ambayo madhara yake ni makubwa. hakuna hata kiongozi wa serikali kuwauliza wachimbaji wanpomaliza dhahabu zao wafukiey hayo mashimo.

  Quote  0#7fatuma2011-06-20 12:04mheshimiwa rais usijifanye unahuruma sana na maendeleo ya tanzania.Fedha mmezitia vibindoni leo unasemaje?
  Futa posho ya wabunge na mawaziri iliyopo kwenye mumzo sasa tutakuona kweli wewe mwanaume

  Quote  0#6Gabriel2011-06-20 11:01Siamini kama huyu Rahisi ana washauri na kama anao hafuati ushauri wao. Mikutano kama hiii ni low key na inatosha kumtuma mchumi akajadiliane na wenzake mbinu za kuleta maendeleo. Sasa mama Salma atatusaidiaje kwenye msafara kama huu? Pili, tatizo siyo fedha ila matumizi mbovu na ukosefu wa nguvu mali. Kwa nini tulete wawekezaji kuja kutuulia ndugu zetu Nyamongo badala ya kupeleka vijana wetu wakabobee juu ya uchimbaji madini halafu tuchukue mikopo Benki ya Maendeleo ya Afrika ay Benki ya Dunia kununulia vitendeakazi vya kuchimba madini? Uchumi siyo porojo na kama huna uchangiaji wenye kuleta tija kaa kimya!

  Quote  +1#5Musa2011-06-20 07:28“Hivyo, sisi katika Afrika tunahitaji kutafuta na kuangalia njia nyingine za ubunifu zaidi za jinsi ya kupata fedha za maendeleo,” alisema Rais Kikwete.

  Katika njia nyingine za ubunifu wa kupata fedha ni kufuta posho zenu viongozi, 987 billion kwa mwaka si haba, ikawekwa kwenye shughuli za maendeleo na ikasimamiwa vizuri kwa kila mwaka miaka mitano ni 4,935 billion, kwa mawazo yangu huu ungekua mwanzo mzuri , TAFADHALI MH NJOO NYUMBANI USIMAMIE HAYA KABLA YA BAJETI KUPITA, ACHA KUENDELEA KUTUMIA PESA ZA WANANCHI KWA KUKAA NJE

  Quote  +4#4msemakweli2011-06-20 06:03I cant believe this.
  Tatizo siyo Ukosefu wa fedha tatizo ni matumizi mabaya ya fedha na hasa kwa Tanzania.
  Pili acha kuongea kana kwamba Afrika yote in matatizo. Hapo kwa watani wa jadi kenya mambo yao yanakuwa biyee kabisa,Rwanda kumekucha,Namib ia, Afrika Kusini, Ethiopia pale pananukia maendeleo,na nchi kibao zimeanza kujiweka sawa. Wewe unawaongelea kivipi. Ongeleamatatizo yako pekee.
  Mimi nashangaa kama kweli Mheshimiwa ana washauri..!
  Nchi ina watu milioni 42++ ina vitega uchumi kibao, inakusanya kodi kidogo na kuifyeka yote kwa anasa za viongozi, kama hiyo ziara ya umechoma dola ngapi kabla hujasema hakuna hela. Kungekuwa hakuna hela ungesafiria Economy class au usingeenda kabisa na kumtuma balozi wako awakilishe serikali,

  Ujumbe huu uwafikie wasaidizi wako wote ambao ndo wakulaumiwa kwa kuipotosha dunia

  Quote  -2#3Ludigo2011-06-20 03:28UMATONYA UMEKUWA KAMA WIMBO WA TAIFA KWA NCHI ZETU ZOTE.LAKINI TANZANIA IMEZIDI.SUBIRI KUNA WATU WATAKUJA HAPO MTAONA KAMA PESA ITATOKA WAPI.
   
 16. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  mimi simwamini kiongozi anayezungumzia sana maswala ya fedha,
  nafikiri kiongozi anatakiwa awe mbunifu na sio kulalama hamna pesa
   
 17. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Ili tuendelee tunahitaji >>watu, ardhi. siasa safi na uongozi bora.
   
 18. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  JK ni m.a.t.a.k.o tu. takataka kabisa! kwanza sitakaa nimtambue kama Rais. Na nikipata nafasi ya kumpasua kichwa, sitaipoteza. Fisi mkubwa!!!!
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hapa Rais wangu kaniacha hoi na kunichekesha kweli kweli! Hivi haya maneno yanamtoka Rais akijijua au akiwa amepigwa ganzi ya Ubongo? mbona hayaendani na hali halisi ya Tanzania na kauli zake?

  Mbona Rais alitoa ahadi lukuki za maendeleo wakati wa Uchaguzi au ndio anathibitisha yale maneno kuwa alikuwa andanganya!? na Je alipokuwa anatoa zile ahadi lukuki hakujuwa kuwa fedha hazipo?

  Na je fedha za Madini na maliasili zetu mbona hatuzi-manage vyema kujenga nchni? Mbona hatufanyi mapinduzi kwenye ardhi ambayo mtaji wake ni mdogo sana?! Kweli Rais wetu bado anaamini katika kuwa omba omba!
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hata ungempa Kikwete dola trilion kumi, bado hataweza kuifanya tanzania iendelee kwa staili hiyo ya uongozi.
   
Loading...