JK sasa abadilisha gia aona kheri awe "fotokopi" ya Dr. Slaa............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK sasa abadilisha gia aona kheri awe "fotokopi" ya Dr. Slaa.............

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  Pamoja na JK kuviita vyama vya upinzani ni "photocopy" ya CCM lakini nyendo zake zimenithibitishia ya kuwa yeye JK ndiyo "fotokopi" murua ya Dr. Slaa na huu ndiyo uthibitisho wake:-

  a) Kila aliposikia Dr. Slaa amefunika kwenye mikutano yake JK amejibidiisha kwenda huko ili ajipime ubavu na Raisi mtarajiwa Dr. Slaa.

  Mifano ni Mwanza, Arusha, Moshi na jana Mwembeyanga.

  JK anaona kujinusuru ni kheri azingatie usemi usemao ...."fuata nyuki ule asali..." na hapo amenithibitishia ya kuwa yeye ni fotokopi ya Dr. Slaa kwa sababu hawezi kufanya lolote mpaka Dr. Slaa kwanza awe amelifanya............yaani JK ni mwigizaji mzuri wa Dr. Slaa...

  b) CCM na hususani JK wamekuwa wakiimba ngonjera za ya kuwa elimu na afya bure haviwezekani lakini baada ya Dr. Slaa kuchanganua takwimu kwa kutumia zana nzito za upembuzi yakinifu na za kitalaamu .........JK amemwagiza Waziri wa Elimu Profesa Jumanne Maghembe kukubaliana na Dr. Slaa na Ilani ya uchaguzi ya Chadema ya kuwa elimu bwerere pia ni sera ya CCM ila Maghembe hajafafanua ni kwa nini haimo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM au hata mipango yake ya miaka kumi ijayo............Hili lathibitisha ya kuwa JK ni fotokopi ya Dr. Slaa.

  c) CCM walisema midahalo "nuksi" hawaitaki kwa sababu waliyoyafanya ni mengi na yanaonekana lakini baada ya Dr. Slaa kufanya mdahalo wake pale MOVENPICK Dar na kuwa na mafanikio makubwa kufikia hata makada wa CCM kupagawa na kudai watampigia kura kimyakimya Dr. Slaa..... JK naye akazinduka na kuja juu ya kuwa atafanya mdahalo wake kesho.............Hivi sasa ni nani kati ya JK na Dr. Slaa ni fotokopi wa mwenzie? Jibu lipo wazi JK amefilisika kisiasa na sasa hivi anasubiri rubani wetu Dr. Slaa amwonyeshe njia ya kupita........Na katika mazingira haya kumchagua kipofu JK inahitaji uwe mwehu kidogo vinginevyo huwezi kupoteza muda wako hata chembe kwa kiongozi haramu.

  Fikiria CCM imewanyima wagombea wake wa ubunge na udiwani kutojinadi kwenye midahalo lakini kwa vile JK sasa anasoteshwa na Dr. Slaa sasa ameona..... "Kheri nusu ya shari kuliko shari kamili" ......pale alipojisalimisha kwenye mdahalo wa waandishi wa habari..........

  d) Mwaka 2005 Chadema ndiyo walioanza kutumia helikopta na CCM iliwabeza kuwa wanapenda ufahari na ya kuwa Chadema watayajuaje matatizo ya wananchi wakiwa angani? JK na CCM yake mwaka 2010 imewaigiza Chadema kwa kuwa na helkopta tena siyo moja ila tatu...Hivi ni nani fotokopi wa mwenzie?

  e) Baada ya kuona umaarufu wake unapimwa na mahudhurio kwenye kadamnasi za mikutano ya Dr. Slaa, JK na CCM wakaona ni kheri wachakachue mahudhurio kwa kuhamisha watu kwa malori na mabasi kutoka maeneo yasiyohusika lili mradi waweze kujilinganisha na mikutano ya Dr. Slaa kwa idadi ya mahudhurio..............Huu ni ushahidi mwingine ya kuwa JK na CCM ni fotokopi wa Dr. Slaa....

  Upo ushahidi mwingi lakini kwa leo huu unatosha......ya kuwa JK ni fotokopi ya Dr. Slaa na aache kupotosha wananchi kuwa vyama vya upinzani ni fotokopi ya CCM wakati yeye mwenyewe amethibitika ni fotokopi ya Dr. Slaa na Chadema........
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sasa hivi wamenukuu kila sera ya upinzani, na wanaendelea kutoa ahadi kuzitekeleza, what a shame!
  Hivi 'photocopy' kwa Kiswahili inaitwaje, ndio inaitwa 'NUKUSHI' nini?
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hana jipya mkuu!tumpige chini kwa kishindo!!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Usemi wa marehemu Kolimba unajidhihirisha taratibu, hiki chama kimepoteza dira
   
 5. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni vizuri kuwa na ushabiki lakini saa zingine ni tuu mach!!

  CCM tangia mwanzo walisema elimu bure kwa shule za msingi ipo tangu 2002 (Tanzania imezawadiwa kufikia malengo ya milenia) na katika sekondari za serikali ada ilishushwa mpaka shilingi 20,000 kwa mwaka ili kupanua wigo wa wanaoweza kuchangia. Isitoshe, sekondari elimu ni ya bure kwa watoto na wazazi wasio na uwezo ambao hupitishwa na halmashauri za wilaya kila mwaka na hulipiwa ada zao kwa bajeti ya serikali kuu. Wizarani kuna maelfu ya watoto wanaolipiwa namna hii kila wilaya. Kwenye elimu ya juu, utaratibu wa mikopo umewekwa na watailipa mikopo hiyo wakianza kazi - mwanafunzi afaulu tuu mambo yatakuwa mswano! Sasa hizi ni sera kweli za CCM na sio za upinzani!

  Hivi alicho fanya Slaa pale Movenpick ni "mdahalo"? Wagombea wengine walikuwa wapi? Midahalo ni ile TBC1 na sio meet the press ya Slaa Movenpick! Kuna sehemu humu JF nilidadisi kwelu kuwa CCM's strategy may be flawed, na hapo nakubaliana na wewe kuwa wao kutokuwa kwenye midahalo TBC1 may come to bite them in the butt. Hapo naona tupo pamoja lakini haya mengine.....mhhhh!!!!

  Hivi nani alipanda au alileta helicopter kwanza ni kitu cha kufanya one candidate is better than the other? Mbona ni so trivial na haimake sense at all! Kwa hiyo watu wamchague Slaa kwa vile alianza kutumia helicopter kwanza! Say whaaat!! Kazi kweli kweli!!

  Hivyo basi, ni vizuri kuwa na upinzani, afterall hiyo ni demokrasia. Lakini nadhani tujiepushe na trivial matters that make no sense. Lets deal with the issues
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,745
  Trophy Points: 280
  JK sasa amekuwa kama baiskeli ya miti,sasa amefika kwenye kilima kazi kwake, safari ya kuondoka magogoni hiyoooooooooooooooo!!!!!!
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu kabla sijajibu hoja yako, naomba kuuliza, kama elimu bure ilikuwa ni sera ya CCM kwanini JK mwenyewe kwa kinywa chake, pia Kinana na makada wengine wa CCM walikuwa wakikanusha kwamba elimu bure kwa wote inawezekana?

  Maelezo yako hapo juu yako tofauti sana na sera ya elimu bure iliyo kwenye Ilani ya CHADEMA, naomba uisome Ilani ya CHADEMA ili uone kama inafanana na kile ulichokisema hapo juu.

  Je, umemsikia alichosema Prof. Maghembe (Waziri wa Elimu)? Je, kinafanana na kile ulichokieleza hapo juu?

  Kama kuna watoto wa masikini wanasomeshwa bure na Halmashauri za Wilaya kwa bajeti ya serikali, je ni kigezo gani kinatumika kuwajua hao watoto wa masikini? Kama bajeti hiyo ipo, Mheshimiwa Sitta angejitangaza kwamba kwa mwaka mmoja analipia ada watoto yatima 200 jimboni na ilihali kuna bajeti ya kuwalipia hao watoto? Zitto Kabwe angeanzisha mfuko wa elimu kwa ajili ya kusomesha watoto wa masikini jimboni mwake? WAMA ya Mama Kikwete ingefungua shule kusomesha watoto wa masikini na ilihali kuna bajeti ya serikali?

  Nikija kwenye swala la mikopo ya elimu ya juu, kuna watoto wa mawaziri na makatibu wakuu wanapewa mikopo 100%, wakati watoto wa masikini/wakulima wanaambiwa wachangie 60%, hicho ndio utasema kuna usawa ama consideration kwa watoto wa masikini? Kwanini wasitoe flat rate kwa wote?

  Sera ya elimu bure siyo ya CCM, bali ni ya upinzani. CCM wanachofanya ni kutoa elimu ya upendeleo kwa wachache. CHADEMA wamesema watafuta michango na ada kwa elimu ya chekechea mpaka F6.

  CUF wamesema watatoa elimu bure kuanzia chekechea mpaka elimu ya juu. Hilo swala la elimu bure siyo sera ya CCM, na kama CCM itashinda na ikaja kutekeleza itakuwa ni kwa pressure ya Ilani za CHADEMA na CUF.
   
 8. m

  monie2009 Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu nadhani nukushi ni fax au vipi?

   
 9. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  millenium goals ni mipango ya ccm?hahahaa
  ivi iyo mibango yote mtailipia ushuru lini? na pesa yetu mliotumia kununua mtaturudishia lini?
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kudesa imo jamani kama waona kizuli kwa mwenzio unarhusiwa kufanya plagiarism or sorry kucopy and paste
   
 11. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Vidunda usiwe na denials za kukufisha wewe na nchi, elewa kwamba sera ya CHADEMA siyo ya kibaguzi bali elimu bure itakuwa nai haki ya kila mtoto wa tanzania bila kujali uwezo wa mzazi, uelezacho ni ushabiki tu kwa sababu hujielewi au umeziba masikio na macho wala huoni.

  CCM WAMEFIKA MWISHO WA UBUNIFU WA MBINU MPYA ZA KUWASAIDIA WATANZANIA NA BADALA YAKE WANAIBA MCHAN KWEUPEE SERA ZA CHADEMA. BASI SI WAMWOMBE TU DK SLAA KUWA MSHAURI WAO, MBONA TU KUIBA KINYEMELA?
   
 12. LOGARITHM

  LOGARITHM JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Kwanza shukrani kwa mh. KEIL, amekupiga shule vizuri sana, na sina haja ya kurudia alichokwambia. Kwa kuwa umesema lets deal with issues umesema vema, na sasa hebu tetea pia ISSUES zifuatazo na utuambie jinsi ZILIVYOSAIDIA KUINUA UCHUMI WA TANZANIA NA USTAWI WA WATU WAKE:
  1. Richmond 2. EPA na KAGODA in particular. 3. Meremeta. 4.Deep green. 5. Kiwira Coal Mine. 6. Ukwapuaji nyumba za serikali. 7. Radar . 8.Mafisadi wenye kesi za kujibu kuitwa WATU SAFI NA WACHAPAKAZI.
   
 13. LOGARITHM

  LOGARITHM JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Kwanza shukrani kwa mh. KEIL, amekupiga shule vizuri sana, na sina haja ya kurudia alichokwambia. Kwa kuwa umesema lets deal with issues umesema vema, na sasa hebu tetea pia ISSUES zifuatazo na utuambie jinsi ZILIVYOSAIDIA KUINUA UCHUMI WA TANZANIA NA USTAWI WA WATU WAKE:
  1. Richmond 2. EPA na KAGODA in particular. 3. Meremeta. 4.Deep green. 5. Kiwira Coal Mine. 6. Ukwapuaji nyumba za serikali. 7. Radar . 8.Mafisadi wenye kesi za kujibu kuitwa WATU SAFI NA WACHAPAKAZI
   
 14. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Umesahau kuwa wameshaanza kuzungumzia kupunguza bei ya saruji na nondo
   
Loading...