JK: Safari za Nje Sasa Basi!

Majibu
1. wajadiliane nini wakati kila kiongozi na wizara zinajua ifanye nini na tayari wanafanya..mbona unauliza kama vile hakuna kinachofanyika au ni uvivu wako kuona na kupima?
2. Maoni ya nini wakati kuna election manifesto inatekelezwa hatua kwa hatua na ndio direction, maoni yanafanyika wakati wa uchaguzi sasa hivi ni utekelezaje? uchaguzi umeisha watu wana chapa kazi nchi haendeshwi kwa maoni..unafikiri ni family business hii..election manifesto imetekelezwa for almost 70% fungua ukurasa wa manifesto uone
3. Unafikiri rais kufuatilia ni mpaka afike eneo la tukio kama daktari wa upasuaji ebbo! kuna utaratibu wa kufanya wala si lazima awepo nchini ndio utekelezaji ufanyike...
5. Kupima utendaji wake wa kila -nani kakwambia hafanyi ulifikiri lazima atangaze hilo kwako..performance review inafanyika kila wakati kwa mujibu president office regulations...

Tatizo lenu mnafikiri nchi ni habari moja tu ufisadi ufisadi basi...kuna shule zinajengwa, dispensary zinajengwa, barabara zinajengwa, vyuo vikuu vinajengwa, mikopo inatolewa, sheria zinatungwa..everything is in order...

hizo kelele za wafuasi wa lowassa na wanaojiita wapiganaji ni upupu na kukosa uzalendo kwa kiwango cha hali ya juu na uki-connect DOTS unaona kabisa wote wametokea sehemu fulani (root), wengine na opportunists wengine ni wivu wengi wao ni failures

Hata kama ni uchama lakini lazima tuseme ukweli kwamba rais kikwete anatumia pesa nyingi za walipa kodi kusafiri tu na safari zenyewe hazina tija. Mfano suala la kuondoa magari yote ya kifahari serikalini ili kupunguza matumizi ni nini kimeshindikana??

Suala la TRL ni nini kinaishinda serikali yake kuuvunja mkataba huo?

Tumeshuudia rais mzima anansema anawajua wala rushwa pale bandarini, hii si kauli ya kuwaambia wananchi, wananchi wanataka waone ni nini umefanya ktk sekta mbali mbali na siyo porojo.
 
Hiyo safari kamwachia Shein kwa vile ni ya Copenhagen, Ingekuwa US au UAE thubutu!
 
Niliwahi kusikia kipindi cha nyuma, serikali iliwataka watumishi wa serikali kutokuwa nje ya kituo cha kazi (kuhudhuria warisha, kongamano, nguvu kazi nk) kwa muda usiyozidi siku kadhaa kwa mwaka. Mwenye kumbukumbu sahihi atanisaidia. Lengo hasa ilikuwa kwamba ukiwa nje ya kituo cha kazi lazma kazi nyingi hazitalala ofsini kwako. Na huyo unayemwachia ofsi kwa kipindi icho chote ndiye anayestahili kuichukua nafasi yako, kwani inakuwazi kuwa ndiye anayefanyakazi zote pale ofsini hivyo wewe hustahili kuwepo pale? Je huu utaratibu ulifutwa au kama upo mkuu wa kaya huu utaratibu yeye haumgusi?

On paper, our government has the best policies and guidelines!!! Sasa tuje kwenye matendo....
 
ehuuuuuu...angalau hatimaye amefuata ushauri...ahueni sana hii jamani..

sasa mheshimiwa raisi apige kambi kabisa pale ikulu, aende na kule vijijini kwenyewe kabisa ambako hata baiskeli haifiki akajionee tanzania halisi anayoiongoza, labda itasaidia kumuongezea uzalendo kwa nchi yake.

Kwa vile kaachia hiyo safari, sasa tusikilizie safari za mikoani!!!!!
 
Afadhali na Dr Shein naye akatembee kidogo, maana siku nyingi kazi zake zimekuwa kuzindua miradidi ya CCM na mashule ya JK.
 
Hivi JK akikaa nchini kwa angalau miezi miwili akaomba ushauri wa wataalam wa uchumi, kilimo, elimu n.k.,
  1. akajadiliana juu ya nini nchi ifanye,
  2. Akaanza kutekeleza maoni yao,
  3. Akafuatilia utekelezaji wa waliyoafikiana na
  4. Kupima utendaji wake kila siku
Hivi haya ni magumu sana kwake au miuu inamuwasha?

Unfortunately, he does not have the capacity to neither understand nor concentrate for long on important issues!! NDIO MAANA LOWASSA NA GENGE LAKE WANAMYIMA USINGIZI.
 
Hata Vasco Da Gama alijaribu wakati fulani kutulia nyumbani.. guess what.. alishindwa.
kwaahiyo Vasco da Gama mweusi amechoka kidogo, anapumzika .
mimi naamini anataka kusimamia finishing kwenye msululu wa majumba yake pale CHALINZE, maana anaviwango vyake nasikia anaremba yale majendo yafanane yale ya dubai kwa nakshi...JK bwana.
 
Kama wanalingana au kufanana basi watalinganishwa na kufananishwa... wote wana sifa kuu na kutotulia nyumbani

mimi kutoka ofisini wiki tu nakosa usingizi lakini mkulu anatoka wiki tatu!!! hii mbado mimi ona...

ndo madhara ya kukulia jkwa bibi ukiwa mtoto.maana mkichinja kuku basi unapewa miguu ule sasa madhara yake ndo haya ukubwani..we mtu hatuliii kutwa anatangatanga tu kwenda kubembea mara kupiga picha na waigiza sinema...mweee
 
hahaaaa

umenikumbusha mbali sana, lakini tujiulize kwa kweli kabisa safari za namna hii na continuity ya quality service kwa wananchi vinaendana??

Kwa wale wataalam hebu usaidieni kucheki katika east african federation kila rais amesafiri mara ngapi (ndani na nje ya nchi) in the past 12 months?
 
Tumain
Join Date: Sat Jun 2009
Posts: 1,921
Thanks: 553
Thanked 446 Times in 310 Posts
Rep Power: 24

Otherwise kama ulibadili jina lako la zamani,mwaka huu JF tutaona mengi sana na sijui kama tutavumilia!

Great thinker aliyekuja JF miezi 4 iiliyopita na mbwembwe za kumsifia JK kama safari zake zina maslahi kwa babu zangu waliopo kijijini Lufilyo-Kyela!

Hopeful this dude is kidding!

Kujiunga zamani JF hakumaanishi chochote kwa jamii hiyo ni hoja dhaifu sana kuitumia kama wewe ni thinker lol...usinilazimishe niwatetee unaofikiri kwamba ni wema kwa mawazo yako..

Ni demokrasia kumsifia mtu yeyote kwa vigezo sasa unayemkandia JK hujatoa vigezo naona kama unalalamika tu bila hoja ndugu

Safari zina maslahi kwa taifa kama vile utalii, (pato la taifa), mahusiano ya kibiashara (business opportunity) nk

Waliopo kijijini wanafaidikaje inabidi urudi shule kusoma uchumi mpana
 
Tumain,
Naomba unitajie vitu vitatu tu kuanzia 2005-2009 ambavyo Tanzania imefaidika navyo kutokana na safari za JK. That's all.
 
Tumain,
Naomba unitajie vitu vitatu tu kuanzia 2005-2009 ambavyo Tanzania imefaidika navyo kutokana na safari za JK. That's all.
Kwanza ufahamu rais wa nchi anaposafiri mambo mengi mengine yanafanyika mfano business opportunities, utalii na hivi vinafanywa na maofisa katika foreign office...sasa wewe kama siyo katika kundi hilo upo na kazi zako za kuajiriwa tu huwezi kujua faida za safari za rais hata kidogo unajua kudai mshahara wako na bonus finito!
 
Ndio maana nimeomba unitajie vitu vitatu tu ambavyo tunaweza kusema ni tangible results of safari za JK nje. Mathanal amesaidia kuongeza watalii, amesaidia kuongeza ajira ya Watanzania kwa kuleta wawekezaji wa viwanda na manufacturing, ni vitu kama hivyo ningependa unitajia siyo longo longo za business opportunities.
 
Kwanza ufahamu rais wa nchi anaposafiri mambo mengi mengine yanafanyika mfano business opportunities, utalii na hivi vinafanywa na maofisa katika foreign office...sasa wewe kama siyo katika kundi hilo upo na kazi zako za kuajiriwa tu huwezi kujua faida za safari za rais hata kidogo unajua kudai mshahara wako na bonus finito!

Kwa Jk labda ye ndo anaenda kutalii ila si kufanya jitihada za kukuza utalii wa Tanzania mifano kama tulivyoona akibembea Jamaica.JK kama prezda safari zake zinatugarimu sana na kulazimika kutumia hazina ya vijisenti vya kigeni tulivyokuwa navyo kumsafirisha yeye wakati hatujaona manufaa ya safari zake.Mbona hatuoni maraisi wa nchi kama U.S wakisafiri kila leo kama JK?
 
Nilikua najiuliza kila siku hasara za raisi kuzurula, hatimae jana nikapata moja.
sasa hivi kumekua na lundo la wawekezaji kuja tz kucheki sehem za kuwekeza, na mara nyingi wale watu wako na timetable fixed

sasa jana kaja tajiri namba 50 duniani ni wa rusia, kaja kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya construction, kama uchimbaji wa mafuta, ujenzi wa mahoteli makubwa, ujenzi wa vinu vya kuzalishia umeme wa gesi, biogas na wind power.

hao watu wako smart sana, imagine watacreate ajira kiasi gani kwa watanzania....?

lakini wamesema walishatuma deligates wao several times bila mafanikio, kwani hawakuweza kukutana na mkuu...wakati wanaongea hivyo walikua wametoka kenya, huko kenya wameshasaini contracts nao, unaambiwa wakenya wanavalue sana projects ambazo zinatija na nchi yao, hawana ukiritimba usio na maana, na mara nyingi ofisi za wakuu wao wa nchi hua haziwi empty.

yani maranyingi kutokuwepo kwa mkuu nyumbani kumbe kunalikosesha taifa faida kubwa sana mbali na kuchezea hela za walalahoi kwenye misafara yao huko ulaya. imagine mtu kaja kwa dhumuni la kufanya hizo investments then anawakosa watu muhimu wa kuongea nao...

Jana alionana na ma-economist wa tz wakuu wala hawakuwepo...wenyewe wanafikiria jinsi ya kuspend hela zilizopo instead of thinking on how to increase them.
 
Back
Top Bottom