JK: Safari za Nje Sasa Basi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Safari za Nje Sasa Basi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sekenke, Dec 13, 2009.

 1. Sekenke

  Sekenke Senior Member

  #1
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ilishawahi kusikika: 'Kelele za mlango hazitunyimi usingizi'

  ---

  Wiki moja iliyopita:
  'Pamoja na watu kulalamikia safari zangu, ukweli ni kuwa nalazimika kusafiri kwa kuwa safari zangu hazina mbadala'... na kwamba atasafiri kwenda Copenhagen kuhudhuria mkutano siku chache zijazo.

  Sasa:
  ... Ameamua kubadili uamuzi wa kwenda Copenhagen... badala yake amemtuma Makamu wa Rais, Dk Mohamed Shein... anayeondoka leo, kwa mujibu wa taarifa ya ikulu ya jana... Dk Shein ataambatana na Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk Batilda Buriani na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira wa Zanzibar Burhani Saadat.

  ...Kwa mujibu wa blog ya Ikulu Rais keshafikisha safari 20 nje ya nchi... anasafiri takriban mara mbili kila mwezi.

  Chanzo: Safari za Nje Zamuelemea JK, Mwananchi Jumapili, Desemba 13, 2009
   
 2. Companero

  Companero Platinum Member

  #2
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sasa zinaanza safari za kampeni ndani ya nchi!
   
 3. pius-ndiefi

  pius-ndiefi Member

  #3
  Dec 13, 2009
  Joined: Dec 11, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kikwete is not that good upstairs. Walikuwa sahihi kumpima akili
   
 4. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama rais, ana mambo mengi ya kufanya, pia ni vyema mambo mengine akaonyesha kwamba ana imani na watendaji wengine. Sio lazima kila kitu afanye yeye itakuwa haina maana ya yeye kuwa na wasaidizi binafsi napongeza kama ameona kuna haja ya kutuma wawakilishi na hasa kilio cha wananchi kwamba rais wao anasafiri sana, na hivyo ana ji expose kwenye danger.

  Kijijini kwetu tunasafiri inapokuwa lazima sana, kwani magari hupinduka!!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Hata Vasco Da Gama alijaribu wakati fulani kutulia nyumbani.. guess what.. alishindwa.
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huu mkutano wa mazingira hakuna value yoyote kwa nchi yetu afadhali amemwachia mzee shein

  Usimlinganishe rais wetu na na hilo li-reno tafadhali
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kama wanalingana au kufanana basi watalinganishwa na kufananishwa... wote wana sifa kuu na kutotulia nyumbani

  mimi kutoka ofisini wiki tu nakosa usingizi lakini mkulu anatoka wiki tatu!!! hii mbado mimi ona...
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Kamuachia kwa ajili ya kelele zetu, I am sure usiku halali kwa ajili ya kumiss hiyo safari kwa vile alishajipanga. Nani alisema kelele za mpangaji azimnyinmi suingizi mwenye nyumba?? Kamuulize JK kwa nini kamuachia makamu??? Lakini kwa JK kuachia hii wakati tulishaambiwa ankwenda nafikiri kuna safari nyingine njiani hivi karibuni!!
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Madhara ya kula Miguu ya Kuku alipokuwa mtoto, hawezi acha kusafiri huyo!
   
 10. kalikumtima

  kalikumtima Member

  #10
  Dec 14, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kusikia kipindi cha nyuma, serikali iliwataka watumishi wa serikali kutokuwa nje ya kituo cha kazi (kuhudhuria warisha, kongamano, nguvu kazi nk) kwa muda usiyozidi siku kadhaa kwa mwaka. Mwenye kumbukumbu sahihi atanisaidia. Lengo hasa ilikuwa kwamba ukiwa nje ya kituo cha kazi lazma kazi nyingi hazitalala ofsini kwako. Na huyo unayemwachia ofsi kwa kipindi icho chote ndiye anayestahili kuichukua nafasi yako, kwani inakuwazi kuwa ndiye anayefanyakazi zote pale ofsini hivyo wewe hustahili kuwepo pale? Je huu utaratibu ulifutwa au kama upo mkuu wa kaya huu utaratibu yeye haumgusi?
   
 11. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Rais haendeshwi na kelele za nje

  Ameamua kumwachia VP kwa ridhaa yake na kwa faida ya nchi!

  Yuko pale kuhudumia wananchi...na safari zake ni kwa manufaa ya nchi na watu wake..
   
 12. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi JK akikaa nchini kwa angalau miezi miwili akaomba ushauri wa wataalam wa uchumi, kilimo, elimu n.k.,
  1. Wakajadiliana juu ya nini nchi ifanye,
  2. Akaanza kutekeleza maoni yao,
  3. Akafuatilia utekelezaji wa waliyoafikiana na
  4. Kupima utendaji wake kila siku
  Hivi haya ni magumu sana kwake au miuu inamuwasha?
   
 13. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Majibu
  1. wajadiliane nini wakati kila kiongozi na wizara zinajua ifanye nini na tayari wanafanya..mbona unauliza kama vile hakuna kinachofanyika au ni uvivu wako kuona na kupima?
  2. Maoni ya nini wakati kuna election manifesto inatekelezwa hatua kwa hatua na ndio direction, maoni yanafanyika wakati wa uchaguzi sasa hivi ni utekelezaje? uchaguzi umeisha watu wana chapa kazi nchi haendeshwi kwa maoni..unafikiri ni family business hii..election manifesto imetekelezwa for almost 70% fungua ukurasa wa manifesto uone
  3. Unafikiri rais kufuatilia ni mpaka afike eneo la tukio kama daktari wa upasuaji ebbo! kuna utaratibu wa kufanya wala si lazima awepo nchini ndio utekelezaji ufanyike...
  5. Kupima utendaji wake wa kila -nani kakwambia hafanyi ulifikiri lazima atangaze hilo kwako..performance review inafanyika kila wakati kwa mujibu president office regulations...

  Tatizo lenu mnafikiri nchi ni habari moja tu ufisadi ufisadi basi...kuna shule zinajengwa, dispensary zinajengwa, barabara zinajengwa, vyuo vikuu vinajengwa, mikopo inatolewa, sheria zinatungwa..everything is in order...

  hizo kelele za wafuasi wa lowassa na wanaojiita wapiganaji ni upupu na kukosa uzalendo kwa kiwango cha hali ya juu na uki-connect DOTS unaona kabisa wote wametokea sehemu fulani (root), wengine na opportunists wengine ni wivu wengi wao ni failures
   
 14. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2009
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  JK hawezi kukaa nyumbani sababu hajui maana ya kuwa Rais wa jamhuri!! Kuna mambo mengi mno ya kufanya kuhusu Kilimo, afya, elimu, infrastructure ambayo kama angeyavalia njuga basi taifa lingepiga hatua kubwa sana.

  Huwezi kusema eti kuna mawaziri inatosha, sasa kwa mwendo huo si tunaweza kwenda mbele zaidi na kusema hakuna haja ya mawaziri sababu kuna makatibu wakuu, wakurugenzi nk????

  Rais kaa ofisini uinusuru nchi mkuu.
   
 15. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Na wewe siku yeyote ukija enda Cuba wakakupime akili zako kama zipo sawa hasa kwa kushindwa kutuambia wana JF faida anayotuletea JK akisafiri nje ya nchi mara kwa mara!

  Maneno yako na nadharia zako za "Makambalism"tunaomba ukawaambie Lumumba,JF for a great thinkers na usituletee propaganda za akina Tambwe!
   
 16. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Tumain
  Join Date: Sat Jun 2009
  Posts: 1,921
  Thanks: 553
  Thanked 446 Times in 310 Posts
  Rep Power: 24

  Otherwise kama ulibadili jina lako la zamani,mwaka huu JF tutaona mengi sana na sijui kama tutavumilia!

  Great thinker aliyekuja JF miezi 4 iiliyopita na mbwembwe za kumsifia JK kama safari zake zina maslahi kwa babu zangu waliopo kijijini Lufilyo-Kyela!

  Hopeful this dude is kidding!
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280

  HAYUPO PEKE YAKE, homeboy wako wa Kyela na yeye yumo.

   
 18. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  ehuuuuuu...angalau hatimaye amefuata ushauri...ahueni sana hii jamani..

  sasa mheshimiwa raisi apige kambi kabisa pale ikulu, aende na kule vijijini kwenyewe kabisa ambako hata baiskeli haifiki akajionee tanzania halisi anayoiongoza, labda itasaidia kumuongezea uzalendo kwa nchi yake.
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Dec 14, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  "Wamefikia hatua ya kumlinganisha Rais na Vasco da Gama, hii ni heshima kubwa, jina la Vasco da Gama ni kubwa, kuna majengo na mitaa vinaitwa jina lake, bila yeye leo Ureno isingekuwa hii tunayoijua. Mimi ningeitwa Vasco da Gama ningefurahi" - Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kama alivyonukuliwa na Gazeti la Mtanzania la Jumamosi, Januari 19, 2008 Ukurasa wa 1: 'Membe atetea safari za Kikwete'
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Imagine kiongozi mkubwa kabisa anakosekana nchini kwa muda wote huo! Hivi hatujajifunza kwamba muda ni mali? Kuna mtu anaweza kuonyesha faida ambayo mpaka sasa hizi safari zimetuletea sisi kama nchi?Vinginevyo ni upotezaji muda tu
   
Loading...