JK, peleka jeshi ziwa Nyasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, peleka jeshi ziwa Nyasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nanyaro Ephata, Aug 3, 2012.

 1. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Malawi inatoa wapi kiburi cha kutangaza sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni sehemu yake? Hivi si kwamba sisi tumezembea mipaka yetu hadi jirani wameona udhaifu wetu?Hivi enzi za Mwalimu Nyerere Malawi wangethubutu?

  Kimsingi hata nchi jirani wameona udhaifu wa aina ya Uongozi tulio nao, uongozi hata kwenye mambo ya msingi unasema upepo utapita.

  Serikali ya awamu ya nne chini ya utawala dhaifu wa JK,umeshindwa hata kulinda mipaka yetu,haingii akilini kuwa sasa nchi yetu imekuwa haina ulinzi wa kutosha kwenye mipaka hadi kusababisha mamia kama sio maelfu ya wahamiaji haramu kukamatia maeneo ya Katikati ya nchi,hii inaonyesha kuwa mipaka yetu haipo salama.

  Sababu ya kuipiga Malawi tunayo,Uwezo tunao,na nia tunayo,JK peleka jeshi ziwa nyasa, angalau katika hili utakumbukwa kwalo kuwa ulisimama imara kuitetea mipaka ya Jamhuri yetu, kuendelea kukaa kimya kunawapa Malawi advantage a hivyo kuadhiri wananchi kwa ujumla kisaikolojia,ni lazima serikali yako ichukue hatua
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  Naomba jk hii vita amuachie mama salma..Rais wetu tutamshushia heshima yake akianza kubishana na yule mama wa malawi...kwanza rais wao ni wa kuteuliwa bora jk aliiba kura
   
 3. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mh napiata tuuu vita shv mhh hapana
   
 4. Blood Hurricane

  Blood Hurricane JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 1,151
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Malawi hawajapata vifo siku nyingi naona wana hamu. Na huyo Muingereza aliyewatuma shauri yake atakosa mtetezi tusilaumiane.
   
 5. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  hapo ndo jeshi linatakiwa itumike,siyo kuzuia maandamano,na wananchi wanaodai haki zao,kama wana ubavu wapelekwe huko
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Where is Shimbo when we need him?

  Mboma atolewe TANESCO na arudi akapigane.

  Muda wa MALIPO umefika. TISS nao kazi ianze na siyo kumpiga Dr. Ulimboka (Tembelea Mwanahalisi website).
   
 7. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #7
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  eti serikali ya Tanzania ndiyo inayowabembeleza hawa wamalawi kuwa tugawane,sheria za Kimataifa ambazo Tanzania na Malawi wameridhia zipo wazi kabisa,kuwa pale mpaka unapokuwa ni ziwa au bahari basi mpaka unakuwa katikati(middle),kuendelea kuwabembeleza ni hatari kwa usalama wa nchi yetu na mipaka yetu.Jk aliapa kulinda na kutetea mipaka ya Tanzania
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Jeshi liko standby in place miaka mingi tu, ondoa hofu!
   
 9. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #9
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  " the 1982 UN Convention on Law of the Sea that stipulates that in case nations are bordered by a water body (sea or lake), the border of the two nations will always be on the middle of the water body."
   
 10. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  itabidi tuingie Malawi tuikalie kwa muda ndiyo watashika adabu kidogo.
  Vita siku zote ni moja kati ya mambo yanayosaidia kurekebisha uchumi,
  Watu wanakufa heshima inarudi historia inajiandika upya.

  Si ziwa tu wanataka kipande kikubwa cha Ardhi Eneo lote la Kyela na Tukuyu wanyataka pia.
  Kwa hiyo wanyakyusa jiandaeni kuwa Wamalawi.

  Bakili Muluzi tumemuhifadhi pale upanga miaka kibao leo wamejinafasi wanataka kuongeza ukubwa wa ardhi.
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nanyaro Ephata

  Angalia hii: Malawi has rightful claim to the whole lake basing on the Heligoland Treaty signed by Germany and Britain – Malawi and Tanzania’s old colonial masters.

  The treaty defines the border between the two countries as being the edge of the waters on eastern shore of Lake Malawi.

  The position of the Heligoland treaty according to Chiume, was further reinforced and adopted by resolutions of the African Union in 2002 and 2007 and its predecessor, the Organisation of African Union (OAU) in 1963 that states that ‘member states should recognize and recognize and accept the borders that were inherited at the time of independence.’

  The treaty in part, on article one states that: “German sphere of influence…to the South by a line which, starting on coast at the Northern limit of Mozambique follows the course of the river Rovoma to the point of confluence of the Nsinje; hence it runs westwards along the parallel of that point till it reaches Lake Nyasa [Lake Malawi]; hence striking Northward, it follows the eastern, Northern and Western shores of the lake to the northern bank of the mouth of the river Songwe.”

  The Foreign Affairs Minister said that while they acknowledged Tanzania’s claim to half of the Lake basing on common law,
  “It is Malawi’s position that the principle which Tanzania depends upon applies only where there is no treaty.”

  Chiume also assured the nation that there should be no cause for anxiety or alarm as the two countries were engaged in discussions ‘so that an amicable solution is found on this long outstanding issue.’ Source hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/302633-rais-joyce-banda-wa-malawi-kutangaza-vita-na-tz-leo-au-laa.html

  Katika mazingira haya tutatumia mkataba wa mwanzo/ mipaka ya wakoloni au tutatumia hii sheria ya 1982 uliyoitaja katika kufikia uamuzi wa kutatua utata wa mpaka?

  Isieleweke kuwa naegemea upande fulani hapa. Vita si lele mama. Ni vyema kujiridhisha kwanza kwamba tutakapoamua kuingia vitani basi tumesimama kwenye ukweli na hivyo damu ya watanzania watakaokufa katika vita hiyo wafe kishujaa.
   
 12. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni wakati muafaka wa kuing'oa CCM madarakani! Vita ya ndani na nje! Natamani huyo Joyce Banda afanye haraka ili vijana tumpe support. Ni bora tupoteze ziwa Nyasa lakini tukaokoa raslimali nyingine zinazoendelea kuangukia mikononi mwa mafisadi wachache!!
   
 13. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Shimbo anaonyesha makali wakati wa uchaguzi tu. Hizo pesa walizoficha Uswis sasa wazitumie kulinda mipaka yetu!!
   
 14. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,168
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Haya yaliwahi kuibuka awamu zilizopita?
   
 15. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jeshi la JK ni la kupeleka madaktari wetu Mabwepambe. Ukiona usalama wa nchi umafikia hapo jua kuwa hata kuku wa Somalia atahamia Tanzania. Hii nchi inanuka kabisa. Hatuna kiongozi na kila mmoja wetu anajua hilo. Polisi wako mipakani na barabarani wakilinda hongo zao. Kwamba mipaka inadhulumiwa hiyo haiwahusu hata kidogo. Ni bora wakimbie kuwakamata kina mama ambao hawana makosa kabisa kwa garama za walipa kodi wa nchi hii kwa uhamiaji haramu na sio viongozi wanaohusika na makosa haya. Hawa jamaa wanakuja polepole na hatimaye watachukua Tanzania yote wachimbe mafuta na gasi kwa faida ya uchumi wao. Joyce anajua kuwa Salma muda wake ikulu ni wa kwenda kubembea hivyo acha atuchue wote na mikia yetu.
  Tuna shida kubwa sana ya uongozi Tanzania. Hatuna haki kabisa. Udhalimu umetawala nchi yetu na wanaoteseka ni wanyonge wasio na kosa. Kikwete anacheka, lakini hadi watoto wa primary wamedhihirisha hilo.
   
 16. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hili la Malawi kudai ziwa Nyasa lilishawahi kuibuka mwaka 1979 wakati ule Rais alikuwa Nyerere tena ilikuwa ni baada tu ya kumng'oa Iddi amin.
  Alichofanya Nyerere ni kupeleka majeshi mpakani mwa Tz na Malawi cha ajabu Wamalawi hawakuendeleza chkochoko mpaka leo ndio wameamua kulianzisha tena.
   
 17. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  if you give a mouse a cookie he is gonna want a glass of milk!they say they won't stop at the lake,they also demand a portion of the indian ocean!ccm existence is tested,but until then i will show high patriotism for my country either we are right or wrong
   
 18. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tunacho kikosi imara pale Kyela tangia enzi za Nyerere. Huwa nawaona wanafyeka majani baadae wanacheza draft wakisubiri mtu akatishe uwanja wa jeshi wamsulubishe. Ukienda Itungi port utakuta kuna kaboat ka zamani sana ambako hurusiwi kukapiga picha eti ni kifaa cha kivita. Sina uhakika kama hata mafuta ya patrol yanatolewa na serikali maana sijawahi kuiona katikati ya ziwa.

  Nafikiri huyu mama wa Malawi atatuamsha usingizini sasa.

  JK kama utahitaji askari wa akiba, naomba unihesabu mimi, maana tangu nimetoka JKT sikamua triga wala kuosha mtutu kwa mdeki.
   
 19. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natumia kamchina ningegonga like
   
 20. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I won't get killed to protect mafisadi interest
   
Loading...