JK ni Rais au Celebrity?

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Kutokana na maruweruwe ninayo yaoni imefikia mahali ninajiuliza hivi JK alipokuwa ana bid for presidential post alijua na kudhamiria kuwatumikia watanzania au alitaka tu kuwa Celebrity ndani ya Ikulu?
Napata shida ninapoona rais anashindwa kufanya very simple decisions na kutatua mambo madogo madogo. Hv kweli huyu rais anayeelewa matarajio watanzania waliokuwa nayo kwake? Kwa nini ashindwe ku deliver kwa kiasi kikubwa namna hii?. Kukosekana kwa majibu ya maswali haya bado kunanifanya niamini JK alitafuta urais kwa sababu zake binafsi tofauti na tulivyokuwa tunatarajia. Yeye haswa alichukulia akiwa rais atakuwa Celebrity wa kupungiwa mikono, kukaribishwa kwenye ufunguzi na matukio mbalimbali n.k.

Mimi naona ana act kana kwamba siyo rais anayetakiwa kuwajibika bali watu wamfagilie tu kwa kusema mara he is presentable and handsome.Most of time uwe unaonyesha uso wa tabasamu hata kama mji mzima wa AR uko msibani.

Tabia hii ra rais ya kutaka aonekana mbele za watu kuwa ni ok wakati ndani ana maumivu ya kukosa majibu ya DOWANS, EPA, msiba Arusha, mgawanyiko ndani ya Chama, katiba mpya na kushindwa majukumu ndo yananifanya nimwone kama amekaa mkao wa Celebrity wa kuchonga zaidi

Nasikitika mno
 
Mkuu huyo ndo presdaa wako bwana. mzee wa sherehe na matamasha.
 
Jk ni sawa na kuku la kisasa lisilohimili shida wala karaha.kwa ufupi ni dizaini ya wale wenzetu wenye mtindio a.k.a yaliyomo yamo a.k.a fresh mental a.k.a mkirikiri orijino.
 
Both,a president and a celebrity!Ila u-celebrity ni zaidi ya u-president!
 
IYO NDO PRESIDENT...yani ni mu predeshee mbaya...inatupaga mahela kwa jukwaaa...ndo watu nakuita jk. akifikaga kwa kongo iko mutu mingi nashangilia yeye, asema afanana na mutu ya kongo nyeupenyeupe...tunapatia yeye ile karolite nakuwa muzuri ndo TZ mwampenda zaidi.mwapendaga viongozi HB iko navutia wananji wa bongo
 
jaman msiwe na shaka tunatafuta njia ya mkato ili tuondokane nae........kwani ni shida tukipiga uchaguzi mwingine hapa kati kati?

bila kufanya namna huyu hatoki pale na atatusumbua sana huyu......
 
Lengo lake lilikuwa ni cheo cha urais siyo majukumu ya rais. Hawezi kujipambanua ktk kufanya kazi, anapenda kuzungukwa na watu anaowafahamu ambao wanampambia kuliko kuzungukwa na watendaj wa kazi, hapendi kujulikana kwamba hawezi, hiyo inamjengea u dictator maana urais ni taasisi lakini yeye anaufanya uwe wa kifamilia na kirafiki
 
Mawzo yake toka mwanzo alitaka kuwa cellebrite wala sio majukumu mazito hayo mliyoyawaza nyie. Yeye alitaka maendeleo ya nchi yaje by the way na zaidi sana alijua sassa amepata mahali pa kuchuma mapene si unaona alivyojenga kijijini kwao pale msoga?
 
JK kashikwa pabaya na MAFISADI kiasi kwamba hana maamuzi mpaka awasiliane nao kwanza,tumhurumie tu maana kasindwa kuongoza nchi.
 
kwani kuna watu walimpigia kura kikwete?........hata wana ccm tu walimtosa!..............eti watu mil.5 kati ya zaidi ya mil.40 wamemchagua...thubutuuuuuuuu............sio cerebrity wala president ni mshamba na limbukeni fulani tu
Nani alaumiwe jk au waliompigia kura?
 
Basi kama hakuna aliempigia kura natoa rai kwa kila mmoja kutengeneza tshirt zenye picha ya dr slaa my Presdent Tuzivae kwenye matukio muhimu ya kitaifa ili aone japo aibu na nafsi imsute
 
Kutokana na maruweruwe ninayo yaoni imefikia mahali ninajiuliza hivi JK alipokuwa ana bid for presidential post alijua na kudhamiria kuwatumikia watanzania au alitaka tu kuwa Celebrity ndani ya Ikulu?
Napata shida ninapoona rais anashindwa kufanya very simple decisions na kutatua mambo madogo madogo. Hv kweli huyu rais anayeelewa matarajio watanzania waliokuwa nayo kwake? Kwa nini ashindwe ku deliver kwa kiasi kikubwa namna hii?. Kukosekana kwa majibu ya maswali haya bado kunanifanya niamini JK alitafuta urais kwa sababu zake binafsi tofauti na tulivyokuwa tunatarajia. Yeye haswa alichukulia akiwa rais atakuwa Celebrity wa kupungiwa mikono, kukaribishwa kwenye ufunguzi na matukio mbalimbali n.k.

Mimi naona ana act kana kwamba siyo rais anayetakiwa kuwajibika bali watu wamfagilie tu kwa kusema mara he is presentable and handsome.Most of time uwe unaonyesha uso wa tabasamu hata kama mji mzima wa AR uko msibani.

Tabia hii ra rais ya kutaka aonekana mbele za watu kuwa ni ok wakati ndani ana maumivu ya kukosa majibu ya DOWANS, EPA, msiba Arusha, mgawanyiko ndani ya Chama, katiba mpya na kushindwa majukumu ndo yananifanya nimwone kama amekaa mkao wa Celebrity wa kuchonga zaidi

Nasikitika mno

Great thinker umeishiwa cha kusema??????????!!!!!!!!!!
Elimu ya chekechea/nursery inatosha kujua JK ni nani??!!! Kama hapo jirani kuna dent wa std one muulize atakujuza!!!
 
Back
Top Bottom