JK ni msikivu sana ila Utekelezaji...

Mfunyukuzi nisaidie tofauti ya maneno 'usikivu' na 'utekelezaji'. Kwa uelewa wangu mdogo, haiwezekani ukawa msikivu halafu usitekeleze. Ukiwa msikivu utatekeleza, usipotekeleza wewe siyo msikivu.
 
8E9U1092+-+Copy.jpg
Jamani msimchukie JK kwa ajili hiyo tu.Kitendo cha kujishusha kwa kiongozi amiri mkuu wa majeshi ni nadra sana kwa viongozi wengi.
Mpeni hongera na moyo pale mtu anapoonyesha moyo wa kibinadamu.
Tunaona hapa Dar hata omba omba watu wanafunga vioo vya magari yao kwa kutopenda kuwa karibu na omba omba.Mioyo mibaya itawahukumu.
Huyo kilema nina uhakika alila raha mustarehe siku hiyo hata kama hakupata kitu-hongera JK.
 
NI MTU WAWATU NA MPENDA AMANI. HIZO NI CHUKI BINAFSI :eyeroll2:KUBALINI MSIKUBALI NDIO RAIS 2010 SLAA AMEISHAJIHARIBIA MWENEWE KWA KUKOSA SERA
 
Unaweza kuta JK ukimuuliza baada ya hapo hata hakumbuki uyo mama aliongea nini.
Lengo ilikuwa kupata picha
 
Anatekeleza au kuthibitisha msemo huu "linaingilia kulia na kutokea kushoto". Pia ukisikia usanii ndio huo, kwani hakuna chama cha walemavu ambako angepata mahitaji yao ya kimsingi? Mpaka akimaliza kampeni atamkumbuka kweli huyo!!!
 
du jamani na hizo picha zenu!!!.....mbona mnamwandama sana kikwete wetu na hizo picha zenu?....mara kikwete kampa pipi mtoto eti ooohhh watoto hawana madaftari yeye anagawa pipi..................mara kikwete kalala kidogo kwenye bembea watu ooooh kikwete anakimbilia kubembea jamaica...jamani yaaani miwivu tuuu wmacheni raisi wetu atuletee maisha bora kwani miaka mitano aliyopewa alikuwa anaisoma nchi sasa amejua nini cha kufanya
 
badili kauli yako ya kwamba tunamwonea wivu.nchi ni yetu sisi tumemwajiri anatumia mali zetu vibaya tunalalamika wewe unasema ni wivu.
 
kuna picha moja ya kampeni ya JK kapiga make ups halafu imefanyiwa photo shop kawa kama mtoto wa miaka 25 mwenye hiyo picha hebu atuwekee
 
Back
Top Bottom