Hakika Wakristo wa JF wanajifanya wasomi lakini ukiangalia kwa makini unaweza kujiuliza ni usomi gani walionao kiasi cha kushindwa kuangalia mambo in broader way!! Wanadanganyika na shule za Seminary (na zile chache za Kikristo zenye good track records) zinazotoa One za kutosha kila mwaka huku wakishindwa kabisa kujiuliza ni asilimia ngapi ya Wakristo wanopata hizo One, Two na Three to the total number of Christians in the country!! Ukiangalia nyingi ya hizi seminary zinakuwa na wanafunzi chini ya 50, lakini mtu anakuja hapa kwa majisifu huku akisahahu kuna malaki kwa malaki ya hao hao Wakristo wamepata Four Mbaya na Zero!! Kwa mfano matokeo yaliyopita, kati ya wanafunzi zaidi ya LAKI NNE, waliopata I, II, na III hawafiki hata 30,000!! Sasa hata tukisema wote waliopata I,III na Wakristo, Je kuna malaki mangapi waliobaki kule kwenye IV na Zero? Pitieni zile shule zingine zinazoanza na St.....muone jinsi kulivyojaa zero na Four mbaya....!!!
Hivi wakati hapa mnajinanga kwa majisifu, maua na mapambie...je, mnafahamu ni Wakristo wangapi ambao hawajui hata kusoma na kuandika? Hizi dharau na kejeli zenu zinatoka wapi sasa ikiwa wenye elimu wenyewe ni kama tone la maji tu baharini?! Au mnajifikiria wenyewe? Hivi mimi leo hii nikitembea kifua mbele kwamba Waislamu TZ ndio matajiri kv list ya matajiri wakubwa inaongozwa na waislamu; si nitaonekana mwehu?!
Wakati mnajitapa kwamba nyinyi ni wasomi, wafikirieni mamilioni kwa mamilioni ya Wakristo wenzenu wasiojua A wala Be! Mwisho ningependa kumalizia swali ambalo mara kwa mara
Ritz amekuwa akiuliza hapa lakini halijapata jibu. Nami nalirudia: Wakristo wasomi wa Tanzania mmeifanyia nini Tanzania? Mie ningependa kuongeza concern kwenye swali la
Ritz, Je umasikini wa Tanzania unatokana na Wakristo wasomi wa Tanzania ambao pamoja na kusoma kwao lakini no inputs, kwamba wamesoma lakini hawajaelimika?