Za masiku Barubaru....Hivi ni Mengi na Mbatia tu wachangiaje. Je waislamu wote hakuna? Kwa kujua kuwa uchumi wa waTanzania umekamatwa kwa more than 73% na wageni na more than 50% ni waislam je wapo wapi hapo?
Bakwata inabidi mjitazame na kujisahihisha? mna mengi ya kujifunza toka kwa waislam na sio hao mnaowaongoza kwa sasa ambao ni viongozi tu wa Serikali.
nafikiri watz wengi wakipata elimu, na uelewa wa mambo mengi yanayotugombanisha utakuwepo na migogoro hii inayotugawanya itapungua ili tuishi kwa amani na kuiendeleza hii nchi aliyotupatia mungu tuikalie. Sina pesa tu lakini hata mimi ningeenda kuchangia hela hapo kama ningekuwa na uwezo huo. Mungu ibariki tanzania!
Za masiku Barubaru....
Kuhusu why hakuna Waislamu, jibu ni simpo! Mchango katika elimu ni mchango bora sana....huu ni kama ibada!! Usitarajie Muislamu Safi wa Roho akachangia mbele ya Kamera....wewe unalifahamu hili!! Si ajabu hao ambao wanaonekana hawajachangia ndio wakachangia kiasi kikubwa zaidi kuliko hawa ambao wanachangia mbele ya kamera!!
Kwamba BAKWATA ni uozo usiotamanika angalau kuusikia kwa hakika ni jambo lisilohitaji shahada yoyote kulifahamu! Na kama kuna mtu awaye yote awezae kuitetea BAKWATA basi mtu huyo atakuwa ni wa ajabu asiye mfanowe! Ni bahati nzuri kwao kwamba wamekuwa wakibebwa kwa sababu zilizo dhahiri shahiri. Hata kama nafahamu ya kwamba Al Haramain inaendeshwa na BaKWATA, sikupata kabla ya hapo kufahamu ni nani hasa alijenga taasisi ile. Hata hivyo, isingeweza kupitia akilini mwangu japo punje kwamba BAKWATA wawe ndio waliojenga huku nikifahamu wazi kwamba BAKWATA hawawezi kuwa na jeuri hiyo abadani!mashukuura ya akhuy.
Lakin lazima ukweli usemwe pasi na kuficha chochote. BAKWATA huko tanzania hususan Bara imekosa mvuto kwa waislam imekuwa ni chombo cha viongozi wa Serikali tu bila kuwa na wafuasi ambao ni waumini wa kawaida. na ndio maana hata hapo katika hiyo picha hata tukio zima utaona wale waliohudhuria.
Kwa pamoja na kupewa mali za iliyokuwa EAMWL lakin mpaka leo hawana ofisi mzuri wala chochote cha kujivunia kwa waislam na hawana mikakati ya kuonyesha umma wa waislam unataka nini.
Je unakuwa Al haramain ilijengwa na nani? mpaka leo Bakwata wanajinasibu kwalo? hapa nmkumbuka Brother wangu Al marhum Burhan Mtengwa wakti huo baada kuanzisha masjid Quba na ile ya bagamoyo na kuja hapo.
Inna Lillah wainna Illaihi Rahihunna. Pole sana Bakwata