Elections 2010 Jk na kukua kwa uchumi tanzania..... Aibu kubwa

MartinDavid

JF-Expert Member
May 22, 2009
874
144
WAKATI TAARIFA YA IMF INASEMA KUWA UCHUMI UMEKUWA KWA 2.7%

JK ANASEMA UMEKUWA KWA 5.5% SASA NANI MKWELI???

SOMA REPOTI YA IMF.. CHINI...

Katika mkutano wa leo kati ya Bw. Olivier Blanchard, ambaye ni mchumi Mshauri na Mkurugenzi wa Idara ya utafiti katika shirika la Fedha la Kimataifa, alifafanua kwa umakini juu ya ripoti inayoelezea hali ya uchumi ilivyo kwa sasa.

Bw. Blanchard katika mkutano huo aliambatana na Jörg Decressin, ambaye ni Mkurugenzi msaidizi katika idara ya utafiti wa uchumi, Petya Koeva Brooks, ambaye ni Mkuu katika kitengo cha mafunzo ya uchumi Duniani, Rupa Duttagupta, ambaye ni msaidizi wa Bw. Petya katika kitengo cha mafunzo ya uchumi Duniani pamoja na William Murray, ambaye ni Mkuu wa kitengo uhusiano na waandishi wa habari.

" Hali ya uchumi wa Dunia inaendelea kuwa katika hali yake ya kawaida. Lakini ninaweza kusema kuwa si sana kama inavyotakiwa. Nchi zilizoendelea zimeathirika sana kuliko hata zile nchi ambazo zinaendelea na zile za kati." Hayo aliyasema Bw.Blanchard alipokuwa akiwasilisha ripoti yake ya mtazamo wa chumi Duniani kwa waandishi wa habari.

Ili muweze kuelewa zaidi mnaweza mkaangalia vigezo ambavyo vinaonyesha uimara wa uchumi. Zaidi ya mwaka sasa tumeona kuwa akiba yetu imekuwa si sawa na miaka iliyopita, na akiba ya fedha za kigeni imepungua. Kinachotakiwa sasa ni kuwa na matumizi lakini na uwekezaji nao pia uongezeke.

Katika nchi zilizoendelea , matumizi na sehemu ya uwekezaji bado ni hafifu sana na itabakia kuwa hivyo kwa kipindi Fulani. Kinyume na nchi zile ambazo zinaendelea na za kipato cha chini. Matumizi na uwekezaji umekuwa imara na unakuwa. Kwa hiyo kitu nilichokuwa na taka muelewe ni hizi pointi mbili ambazo ni matumizi na uwekezaji kisha mziweke kwenye matokeo ya kisera. alisema Bw. Blanchard.

Udhaifu wa utumiaji na uwekezaji katika nchi zilizoendelea una ashiria kusababisha msukosuko huo na ningependa mfahamu kuwa hili ni lazima lirekebishwe.

Kwa watumiaji wa Marekani ambao hawajawahi kukopa kabla ya mtikisiko sasa hivi wameweza kuweka akiba zaidi na kutumia kidogo. Hiki ni kitu kizuri kwa mwenendo wa muda mrefu lakini si kizuri kwakipindi cha muda mfupi. Uwekezaji kwenye nyumba utakuwa ni wa chini kwa kipindi kilichobakia.alisistiza Blanchard.

Udhaifu katika mifumo ya fedha inazidi kupunguza uwezekano wa kupata mikopo kama mlivyoona katika ripoti ya mambo ya fedha jana.

Ripoti hii ndiyo inayotuongoza kujua mapema kuwa kuna ukuwaji mdogo wa nchi zilizoendelea. Namba zinaonyesha kuwa itakuwa asilimia 2.7 kwa mwaka 2010 na asilimia 2.2 kwa mwaka 2011.

Kutokana na ukuaji huo mdogo , tunatazamia kuwa ukosefu wa kiwango cha ajira utakuwa juu sana. Namba zinaonyesha kuwa, kwa Amerika ni asilimia 9.6 kwa mwaka 2010 na asilimia 10 kwa ulaya kwa mwaka 2011.

Kwa ujumla nchi zilizoendelea zimekuwa zikichangia katika uwekezaji lakini kwa sasa tunaona kuwa kwa nchi hizo zilizo juu zaidi na kwa nchi zinazoendeelea kwa ujumla uchumi unakua kwa asilimia 7.1 kwa mwaka 2010 na asilimia 6.4 kwa mwaka 2011. Kama tukiangalia bara la Asia,tunaona uchumi unakuwa kwa asilimiaIf 9.4 kwa mwaka huu na asilimia 8.4 kwa mwaka ujao.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu mtikisiko kuwa umeathiri vipi bara laAfrika? Rupa alijibu kwa niaba ya Bw. Blanchard kuwa, Afrika pia ilikumbwa na huu mtikisiko lakini tunashukuru walikuwa na sera nzuri za uchumi ambazo ziliweza kuhimhili mtikisiko huo.

Nchi nyingi zilijijengea misingi imara ya kifedha ambayo iliweza kuhimili vishindo vya mtikisiko huo. Na hii ndio sababu kwanini mtikisiko huo haukuchukua muda mrefu. Alieleza Rupa.

Lakini tukienda mbele zaidi , tunaweza kuona kuwa mtikisiko huo unapunguza nguvu ya kufikia malengo ambayo nchi hizo za Afrika imejiwekea, kama vile malengo ya milenia. Kwahiyo ni muhimu sana kutumia nafasi hii sasa kujenga misingi imara ya kifedha ili kuwa na vitu muhimu kwa mahitaji ya wa Afrika kama vile kuwekeza katika sekta ya afya, elimu na katika huduma za kijamii. Alimalizia Rupa.

Mikutano hii ya mwaka bado inaendelea na inategemewa kufikia kilele chake hapo tarehe kumi mwezi huu. Hali ya hewa ni baridi na manyunyu ya hapa na pale.
 
Back
Top Bottom