JK na CCM yake wanalipotosha taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK na CCM yake wanalipotosha taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Nov 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,485
  Likes Received: 418,984
  Trophy Points: 280
  maeneo matano ambayo jk na ccm yake wanalipotosha taifa ni pamoja na:-

  1) kulinganisha utaratibu wa kupata katiba mpya na marekebisho ya katiba iliyopo. jukumu la kurekebisha katiba iliyopo ni la bunge wakati jukumu la kuandika katiba mpya ni la watanzania wote.

  2) kudai yapo maeneo ambayo hayajadiliwi.....................ni nani aliyetuamulia kuwa yawepo maeneo ambayo yapo nje ya mjadala wa kuandika katiba mpya..........................kama nafasi ya muungano, mihimili ya serikali n.k

  3) kusahau ya kuwa Jk na wabunge wake wa ccm waliapa kuilinda katiba iliyopo sasa wanatoka wapi kuwa waasisi wa kuinyambulisha hiyo katiba kama siyo kuvunja katiba iliyopo ambayo hata wao wanakiri kwa vinywa vyao kuwa wanaipenda hii iliyopo?

  4) Kutupotosha ya kuwa katiba ya Kenya ilifuata mchakato wa kwetu hapa.....................huu ni uongo usio na kifani Kenya tume yao ilitangazwa kwenye magazeti na wenye sifa waliomba na kuchujwa na kamati maalumu ya bunge kabla ya bunge lote kuwapigia kura...............raisi Kibaki kazi yake ilikuwa kuthibitisha uteuzi huo baada ya mchakato wa wazi kutumika na ambao ulitoa fursa sawa kwa wote....................kwetu Jk ana majina ya wajumbe wa tume kibindoni kwake..................tukihoji sisi tunaonekana tunaleta chokochoko!!!!!!!1

  5) Jk anatetea michakato ya zamani ya kufanyia marekebisho katiba iliyopo..................anachoshindwa kujifunza ni kuwa kama utaratibu ule ulikuwa sahihi mbona bado tunahitaji katiba mpya? ukweli ni kuwa michakato ile haikuwa shirikishi na ndiyo maana tulikwama................


  hitimisho:-

  mchakato huu utazaa katiba ya viongozi na wala siyo ya wataliwa na matokeo yake vuguvugu la kudai katiba mpya litaendelea hadi hapo mwafaka wa kitaifa utakapopatikana..........
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kamanda unatisha Uchambuzi umetulia...
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,485
  Likes Received: 418,984
  Trophy Points: 280
  ni mazingira waliyotufikisha hawa wanamagamba yanatisha na ndiyo maana yabidi tuwape vidonge vyao wakishindwa kuvimeza shauri lao...............
   
 4. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ahsante Ruta kwa uchanganuzi yakinifu kama huu!
  Suala la katiba kwa kweli linaniumiza sana moyo na fikra zangu.
  Kwanza, jinsi uongo huo unavyoshamiri na kuelekea kuaminika mbele ya watz wengi ambao maisha yao ni ya kusaka tonge tu!
  Kweli hapa tuendelee tu harakati hizi za kuwasha taa mchana kweupe japo watz wengi kwa sasa watatuita wakorofi na tuna maslahi binafsi kwenye katiba tunayoililia,
  Ila ukweli utajisimamia kuwa tunataka kATIBA YA WATU.
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Very constructive criticism hasa hiyo ya kenya..
   
 6. B

  Bambwene Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Asante sana kwa uchambuzi yakinifu najua wengi watanufaika na kujia kweli nayo kweli itawaweka huru
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Si kweli Mkuu,

  JK na CCM wako sahihi kabisa! Nimefuatilia maneno yake kwenye magazeti karibu yote ya leo na nukuu kwenye TV/Radio (sorry sikuwa tayari kuisikiliza hotuba yote kwa sababu sikutaka kujipa matatizo) na kuuona huo ukweli. Wanachokiongea wao ni sahihi kabisa na huu mswada wao uko sahihi pia.

  Wanataka kubadli katiba.....Hilo ndilo wanalotaka kufanya!!

  Sie wengine tunataka kuandika katiba mpya (tena mpya kabisa), isiyokuwa na kivuli wala mwangwi wa katiba ya sasa!

  Hivi vitu ni tofauti kabisa.....Na hapa tunaongea lugha tofauti...

  Bahati mbaya haya tuliyaona toka day zero, pale walipoanza huu mchakato wao wa kutuzuga!!
   
 8. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Niko doria
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Yafaa Jk atumie busara kuachia uongozi wakakae na ccm yake wajipange wajue walipokosea wafanye marekebisho waje tena labda labda labda tunaweza kuwajaribu tana
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,485
  Likes Received: 418,984
  Trophy Points: 280
  hizo busara huwezi kuwa nazo kama ni mtumwa wa dhambi hususani kuwapora watanzania haki zao za kimsingi..............
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,485
  Likes Received: 418,984
  Trophy Points: 280
  tatizo ni kuwa wao tunawapima kwa kauli zao......................muswada wanauita marekebisho ya katiba lakini kauli zao wanadai ni katiba mpya.........................waache unafiki waseme ukweli ya kuwa haya ni marekebisho ya 15 ya katiba iliyopo hapo watakuwa sahihi..............
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,485
  Likes Received: 418,984
  Trophy Points: 280
  jk na ccm yake wamezidisha kipimo siyo cha kuongopa tu hata cha unafiki wakati umefika wa kuwakemea..........
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,485
  Likes Received: 418,984
  Trophy Points: 280
  ni kweli penye ukweli uongo hujitenga...........
   
 14. U

  UNIQUE Senior Member

  #14
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KWA KWELI RAISI WETU HUYU NA CCM YAKE WANASUMBULIWA NA WOGA! NIMEANGALIA WALE VIKONGWE ALIOKUWA ANAONGEA NAO ASILMIA 75 (75%) WALIKUWA WAMELALA KABISA. MIMI NI CCM LAKINI KWELI WE HAVE A WEAK PRESIDENT ANAOGOBA MIJADALA.
  Atelemke hapo chini RWANDA AAJIFUNZE KWA KAGAME; KILA MWEZI ANA PRESS CONFERENCE NA WAADISHI WA HABARI WOTE WANAALIKWA NA WANAULIZA MASWALI YA PAPO KWA PAPO NA JAMAA ANAPANGUA HOJA ZOTE. PILI KILA ANAPOKWENDA LAZIMA WANANCHI WAULIZE MASWALI. NDIYO MAANA WATUMISHI WA SERIKALI WAKICHAKACHUA WANAUMBULIWA HAPO HAPO!
  KWA KWELI WALE WAZEE ALIWASUMBUA NA KUWALETEA MAUMIVU TU. KWA NINI ASIITE HATA WA VYAMA VYA UPINZANI NA WATU BAKI! ANAOGOPA NINI. WENGI WALIKUWA NA VAZI LA ARUSI KIJANI TUPU. HUYU NI RAIS WETU SOTE HATA KAMA ALITUCHAKACHUA NA HAO ANAODAI ANA HAKI YA KUTEUA. HAYA MZEE KIPINDI HIKI TUTAONA KAMA HIYO KATIBA ALIYOPINDA ITATUVUSHA
   
 15. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja!
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,485
  Likes Received: 418,984
  Trophy Points: 280
  angeenda kuwahutubia wanafunzi wa UDOM na kuwapa nafasi ya kuuliza maswali hapo angeliona cha moto.............
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mkuu ruta, naunga mkono mawazo yako yote hapo juu..
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hujatuweka wazi usawa wao uko wapi
   
 19. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kumbe wakati mwingine huwa unaandika vitu vyenye akili!! Nimependa umeongelea mfano mzuri ni Kenya. Alichoongea JK ni uwongo wa makusudi maana siamini mtu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na baadaye Rais wakati mchakato unaendelea hajui ukweli. Kama hajui ni nini kilifanyika Kenya basi hakustahili kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Rais,maana uwezo wake utakua ni mdogo sana.
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,578
  Likes Received: 1,674
  Trophy Points: 280

  Duh, MKWEREE kalishwa tena SUMU? Jamaa huwa Hatafakari au?
   
Loading...