JK: Mgomo wa madaktari ulikuwa 'ngoma nzito'... Aeleza kilichomfanya asaini haraka haraka

Mar 1

[h=1]HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 29 FEBRUARI, 2012[/h]

Written by haki | // 0 comments


Jakaya+Kikwete+CHOGM+Concludes+Australia+UL0oeJ9oF34l.jpg

Rais Jakaya Kikwete
----
Ndugu Wananchi,
Naomba sote tumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma kwa kutuwezesha kuzungumza tena mwisho wa mwezi huu. Katika mwezi tunaoumaliza leo taifa letu lilipata msukosuko mkubwa kufuatia mgomo wa madaktari. Nashukuru mgomo huo umeisha lakini makovu yake yatabaki maisha katika kumbukumbu za historia ya taaluma ya tiba hapa nchini.



Leo, Mheshimiwa Waziri Mkuu amenipa taarifa kuwa Kamati aliyounda kushughulikia madai ya madaktari imekamilisha kazi yake na kuwasilisha taarifa yake kwake. Kuanzia kesho Serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na uwezo uliopo. Nawaomba ndugu zetu madakatari kuwa na moyo wa subira.


Napenda kutumia fursa hii kuwahakikishia ndugu zetu madaktari na watumishi wengine wote wa sekta ya afya kwamba Serikali inatambua, inajali na kuthamini kazi wazifanyazo na mchango wao katika kulinda na kudumisha afya za wananchi wa Tanzania. Aidha, narudia kutoa pole zangu za dhati kwa wananchi na hasa wagonjwa nchini kwa mateso waliyoyapata katika kipindi cha mgomo. Ni matumaini yangu kuwa hali kama ile haitajirudia tena katika nchi yetu.



Ndugu Wananchi,
Tukio lingine la kusikitisha ni mauaji ya Songea. Yapo yale yanayohusishwa na imani za ushirikina, na yapo yale ambayo yalitokea kwenye maandamano. Napenda kutumia nafasi hii kuelezea masikitiko yangu kwa vifo hivyo na kutoa pole na rambirambi zangu na za wananchi wa Tanzania kwa ndugu wa marehemu wetu hao.



Tupo pamoja nanyi katika misiba hii mikubwa na majonzi. Napenda kuwahakikishia wananchi wa Songea kwamba Serikali kupitia vyombo vyake vya usalama imekuwa inafanya na itaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji haya mpaka wahusika wote wapatikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Nimearifiwa kuwa, mpaka sasa kwa mauaji 13 yanayohusishwa na imani za ushirikina watuhumiwa 26 wamekwishakamatwa. Na kwa mauaji yaliyotokana na maandamano, askari polisi wanne wamekamatwa na upelelezi unaendelea.



Ndugu Wananchi;
Nashukuru kwamba amani na utulivu vimerejea katika Manispaa ya Songea. Nawapongeza sana viongozi wa ngazi zote na wananchi kwa ujumla kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuwezesha usalama na utulivu kupatikana. Tafadhali endeleeni na juhudi hizo mpaka mambo yatengemae kabisa.




Ndugu Wananchi;
Katika mwezi huu pia, Bunge letu Tukufu lilifanya mkutano wake wa sita na miongoni mwa maamuzi makubwa yaliyofanywa ni kupitisha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 hususan kuhusu Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba ya nchi. Nimekwishatia saini marekebisho hayo tarehe 20 Februari, 2012 na hivyo sasa yako tayari kutumika.




Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi kwa Wabunge wetu kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya ya kupitisha marekebisho hayo. Aidha, natoa pongezi maalum kwa vyama vya siasa vya CCM, CHADEMA, CUF na NCCR - Mageuzi pamoja na Baraza la Taifa la Asasi Zisizokuwa za Kiserikali kwa maoni na mapendekezo yao ambayo ndiyo yalikuwa chachu ya marekebisho yaliyofanyika. Pia, nawashukuru kwa ushirikiano wao uliowezesha mafanikio kupatikana.



Tulipotoka
Ndugu Wananchi;
Bila ya shaka mtakumbuka kuwa baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Mabadikiko ya Katiba tarehe 18 Novemba, 2011, kulikuwepo na maneno mengi na maoni mbalimbali katika jamii. Wapo baadhi ya wadau hasa baadhi ya vyama vya siasa na asasi za kiraia ambao waliniomba nisitie sahihi Muswada huo kuwa Sheria na badala yake niagize Bunge liuzungumze upya. Aidha, vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF na NCCR – Mageuzi na Baraza la Taifa la Asasi Zisizokuwa za Kiserikali waliomba kukutana nami tuzungumzie mchakato mzima wa Katiba. Sikusita kuwakubalia na kwa nyakati mbalimbali tulikutana na kuzungumza nao.




Ndugu Wananchi;
Katika mazungumzo yangu nao niliwaeleza ugumu niliouona kuhusu kuacha kutia sahihi Muswada huo na kuurudisha tena Bungeni kujadiliwa upya. Nilichelea kuliingiza taifa letu katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kikatiba usiokuwa na lazima. Mgogoro ambao tunaweza kuuepuka kwa kutumia njia nyingine za kikatiba na kisheria kufikia malengo yale yale. Kitendo cha mimi kukataa kutia sahihi kingejenga chuki kwa upande wa Wabunge walio wengi ambao waliujadili Muswada na kuupitisha. Wengeweza kuhisi wamedharauliwa na kuonekana hawana thamani.




Katika mazingira hayo mtakapowarudishia Muswada huo kuujadili kuna hatari ya kutokupata ushirikiano wao na kushindwa kupata kile kinachotarajiwa. Wanaweza kujadili na kuamua kukataa mapendekezo yote mapya na kubakia na msimamo wao ule ule.


Ndugu Wananchi;
Kwa ajili hiyo, busara ilinielekeza kuwa tusitumie njia hii bali tutumie njia za kawaida za kufanya marekebisho ya Sheria zilizotungwa na Bunge. Hakuna Sheria iliyotungwa na Bunge ambayo haiwezi kufanyiwa marekebisho. Kinachotakiwa ni kupeleka mapendekezo ya vifungu au vipengele vya Sheria husika vinavyotakiwa kurekebishwa. Bunge litavijadili na kama hoja zinatosheleza vitafanyiwa marekebisho. Mimi nilipendelea busara na hekima hiyo. Niliwaeleza wadau sababu za kuamua kutia sahihihi Sheria na kuwasihi wakubali tufanye lililo bora zaidi ambalo ni kupeleka Bungeni mapendekezo ya sheria hiyo katika maeneo ambayo tunataka marekebisho hayo yafanywe.




Nilitahadharisha kuwa hata kufanya hivyo kunaweza kuwa na ugumu wake hasa pale dhana zisizokuwa sahihi zitakapopandikizwa kwa Wabunge. Niliwaomba tushirikiane kuhakikisha dhana potofu hazijitokezi na zinapojitokeza tuzisahihishe. Niliwahakikishia utayari wa Serikali kushirikiana nao katika hatua zote, tangu kutayarisha mpaka kuwasilisha mapendekezo hayo Bungeni iwapo watapenda Serikali ifanye hivyo. Aidha, niliwaambia kuwa hata sisi Serikalini tulikuwa na dhamira ya kupeleka marekebisho kwa baadhi ya vifungu vya Sheria hiyo kwa sababu mbalimbali.



Nafurahi kwamba, kwa pamoja licha ya tofauti zetu kuhusu uamuzi wangu wa kutia saini Muswada tulikubaliana kushirikiana kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria hiyo, ambayo tuliyawasilisha katika Bunge lililopita. Nafurahi na kufarijika kwamba, baada ya mjadala mkali, na Wabunge kufanya marekebisho kadhaa na hata kuingiza mambo mengine mapya, Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ulipitishwa na Bunge tarehe 10 Februari, 2012. Baadaye uliwasilishwa kwangu na nikatia sahihi kuwa Sheria tarehe 20 Februari, 2012. Sina budi pia kukitambua Chama cha Mapinduzi ambacho kilileta mapendekezo yake. Mapendekezo hayo yalizingatiwa kama ilivyofanywa kwa yale ya wadau wengine.



Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi maalum kwa vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF, NCCR – Mageuzi na CCM na Baraza la Taifa la Asasi Zisizokuwa za Kiserikali kwa uelewa wao na ushirikiano wao kulikotuwezesha kufikia hapa tulipo katika mchakato wa kutengeneza Katiba Mpya kwa usalama, utulivu na kwa maelewano. Kwa kweli, jinsi hali ilivyokuwa huko nyuma, hatuna budi kushukuru na kujipongeza. Ni matumaini yangu na rai yangu kuwa tutaendeleza ushirikiano na utamaduni huu wa mazungumzo tuliouanzisha na kuutumia katika hatua zingine zinazofuata.



Nchi imetulia joto na jazba kuhusu Katiba havipo. Kumbe tukiamua na hasa tukizungumza inawezekana. Naomba wadau wote tuazimie kuwa mambo yaendelee hivi hata katika hatua zijazo za mchakato huu na masuala mengine muhimu kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake.

Ndugu Wananchi;
Katika mazungumzo yetu na wadau tulikubaliana kwamba tushughulikie marekebisho ya Sheria hii kwa awamu. Kwa kuanzia tushughulikie mambo yanayohusu Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi Kuhusu Katiba ili iundwe na kuanza kazi. Baada ya hapo tuangalie mambo yahusuyo Bunge Maalum na Kura ya Maoni.




Bahati nzuri Sheria ya sasa inaelekeza kuwa Kura ya Maoni itatungiwa Sheria yake maalum, hivyo mambo yanaweza kusubiri wakati huo. Hivyo basi, baada ya muda si mrefu, Serikali na wadau tutaanza mazungumzo kuhusu mapendekezo ya marekebisho kuhusu Bunge Maalum. Kama yatakuwepo na kama kutafikiwa makubaliano, mapendekezo yatafikishwa katika Bunge letu tukufu kwa hatua zipasazo.



Ndugu Wananchi;
Bahati nzuri pia kuna kipindi kirefu kidogo wakati Tume inaendelea na kazi yake mpaka hapo Bunge Maalum litakapoanza kazi. Tume imepangiwa kukamilisha kazi yake ndani ya miezi 18 na inaweza kuongezwa miezi miwili. Wadau wanaweza kutumia sehemu ya muda huo wa Tume kushughulikia na kufanya marekebisho yahusuyo Bunge Maalum. Hata hivyo, kama mapendekezo yatakamilika mapema ni bora zaidi yafikishwe Bungeni na kushughulikiwa ipasavyo.




Wadau Kupendekeza Majina
Ndugu Wananchi;
Miongoni mwa marekebisho muhimu yaliyofanywa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika Bunge lililopita ni kuwekwa kwa utaratibu wa wadau kupendekeza kwa Rais majina ya watu wanaoona wanafaa kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni kuhusu Katiba. Nafurahi kutoa taarifa kwamba nimekwishatoa mwaliko kwa wadau husika, yaani vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, jumuiya za kidini, asasi za kiraia pamoja na jumuiya, taasisi na makundi mengine yenye malengo yanayofanana kuleta mapendekezo hayo.




Mwaliko wangu huo umeshatangazwa katika Gazeti la Serikali Namba 66 la Ijumaa tarehe 24 Februari, 2012. Kuanzia kesho itatangazwa katika magazeti ya kawaida. Katika mwaliko huo, wadau wanatakiwa kupendekeza majina yasiyozidi matatu ya watu wanaokidhi sifa zilizotamkwa katika kifungu cha 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Sifa hizo ni hizi zifuatazo:-


(a) Uzoefu katika kufanya mapitio ya katiba na sifa za kitaaluma za wajumbe kwenye mambo ya katiba, sheria, utawala, uchumi, fedha na sayansi ya jamii.

(b) Jiografia na mtawanyiko wa watu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na
(c) Umri, jinsia na uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii.




Aidha, nimeelekeza kuwa siku ya mwisho ya wadau kuwasilisha mapendekezo yao ni tarehe 16 Machi, 2012. Wadau wanatakiwa kupitishia mapendekezo yao kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Muungano au Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Nimewapa viongozi watendaji wakuu hao jukumu la kupokea mapendekezo ya majina na kuyawasilisha kwangu. Baada ya hapo nitashauriana na Rais wa Zanzibar kuteua Wajumbe wa Tume pamoja na Mwenyekiti na Makamu wake.



Ndugu Wananchi;
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba pia inatoa fursa kwa Rais kuteua Wajumbe wa Tume kutoka hata nje ya orodha ya wadau. Ilionekana ni vyema kufanya hivyo kwani wapo watu wengine wazuri ambao wanaweza kuwa hawamo katika makundi yaliyotajwa na Sheria hii. Aidha, upo uwezekanao kwa mapendekezo ya makundi kutozingatia baadhi ya mambo ya msingi kama vile jinsia, jiografia na mtawanyiko wa watu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kadhalika. Fursa hii aliyopewa Rais itasaidia katika kuzingatia matakwa haya ya Sheria.




Pamoja na hayo napenda kuwahakikishia kuwa iwapo nitaitumia fursa hiyo watu hao hawatakuwa wengi kuliko wale waliopendekezwa na makundi yaliyotajwa katika kifungu cha 6 (6) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha wadau na wananchi kwa jumla kuwa Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni Kuhusu Katiba ina Wajumbe 30 tu wanaopatikana kwa idadi sawa kutoka sehemu zotu mbili za Muungano wetu yaani 15 kutoka Tanzania Bara na 15 kutoka Zanzibar. Unapoongeza Mwenyekiti na Makamu wake kwa jumla Tume itakuwa na wajumbe 32 yaani 16 kila upande. Hivyo basi, fursa ya kila aliyeleta majina kupata nafasi katika Tume si kubwa.




Nayasema haya kutahadharisha juu ya ukweli huu ili tusijipe matumaini makubwa mno na wala tusije tukashutumiana baada ya uteuzi. Hata hivyo, pamoja na ugumu wa kuchagua miongoni mwa orodha ya watu wengi wazuri, nitajitahidi tu Wajumbe wa Tume wawe watu makini, wanaowakilisha sura pana ya jamii za nchi yetu na makundi yake muhimu na utashi wa watu wa Tanzania yetu.



Tunapokwenda
Ndugu Wananchi;
Ni matarajio yangu kuwa zoezi la kuunda Tume litakamilika muda mfupi kadri inavyowezekana, baada ya kupokea mapendekezo ya makundi. Kama nilivyokwishawahi kudokeza siku za nyuma, napenda Tume ikamilike kuundwa katika robo ya pili ya mwaka huu na kuanza kazi muda mfupi baada ya hapo.




Naomba nitumie nafasi hii kutoa wito maalum kwa wananchi wenzangu kuanza kujiweka tayari kutoa maoni yao kwenye Tume. Mambo yataanza miezi michache ijayo. Najua Tume itatengeneza utaratibu wa kuelimisha wananchi kuhusu Katiba. Lakini nawaomba kila mtu binafsi yake aanze kuchukua hatua za kuifahamu Katiba iliyopo sasa ili apate ufahamu wa maudhui muhimu ya Katiba. Kufanya hivyo kutamuwezesha kuamua kwa usahihi anataka kupendekeza nini kiwemo katika Katiba mpya. Nimeagiza Mpiga Chapa wa Serikali kuhakikisha kuwa vitabu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinachapishwa kwa wingi ili wananchi waweze kuwa navyo na kuvisoma. Inawezekana, Timiza Wajibu Wako.


Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
 
Mar 1

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 29 FEBRUARI, 2012



Written by haki | // 0 comments


Jakaya+Kikwete+CHOGM+Concludes+Australia+UL0oeJ9oF34l.jpg

Rais Jakaya Kikwete
----
Ndugu Wananchi,
Naomba sote tumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma kwa kutuwezesha kuzungumza tena mwisho wa mwezi huu. Katika mwezi tunaoumaliza leo taifa letu lilipata msukosuko mkubwa kufuatia mgomo wa madaktari. Nashukuru mgomo huo umeisha lakini makovu yake yatabaki maisha katika kumbukumbu za historia ya taaluma ya tiba hapa nchini.




Aaah!!!!!!!!!!!!!!!

Kumbe bado anaendelea na utaratibu wa ke wa kuhutubia Taifa kila mwisho wa mwezi.

Yaani mimi kusikiliza ilikuwa mara ya mwisho ni mwaka 2010, kabla ya Uchaguzi mkuu. Baada ya hapo sikumsikia tena nilidhani ameacha utaratibu huu.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!​
 
01 MARCH 2012



"Nawaomba madaktari kuwa na moyo wa subira. Napenda kutumia fursa hii kuwahakikishia ndugu zetu madaktari na watumishi wengine wote wa sekta ya afya kwamba Serikali inatambua, inajali na kuthamini kazi wazifanyazo na mchango wao katika kulinda na kudumisha afya za wananchi wa Tanzania."

Katika hotuba hiyo Rais Kikwete alitoa pole kwa wananchi na hasa wagonjwa nchini kwa mateso waliyoyapata katika kipindi cha mgomo.

"Ni matumaini yangu kuwa hali kama ile haitajirudia tena katika nchi yetu," alisema Rais Kikwete.

. Mauaji ya Songea

Mbali na mgomo wa madaktari alielezea kusikitishwa na mauaji ya Songea yale yanayohusishwa na imani za ushirikina na yale ambayo yalitokea kwenye maandamano.

"Napenda kutumia nafasi hii kuelezea masikitiko yangu kwa vifo hivyo na kutoa pole na rambirambi zangu na za wananchi wa Tanzania kwa ndugu wa marehemu wetu hao.

Tupo pamoja nanyi katika misiba hii mikubwa na majonzi. Napenda kuwahakikishia wananchi wa Songea kwamba Serikali kupitia vyombo vyake vya usalama imekuwa inafanya na itaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji haya mpaka wahusika wote wapatikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria," alisema Rais Kikwete.


hiyo blue ya kwanza: wawe na subira wakati wana njaa na hawana vitendea kazi..? wawe na subira wakati wabunge wako busy kujipandishia posho na ww mheshimiwa ukiwa busy kuvinjari nje ya nchi..?

hiyo red ya pili: unawapa pole wagonjwa kwa matatizo yaliowapata kwa makosa na uzembe wa serikali yako..? na wale waliofariki kutokana na uzembe huu unawaambiaje..? wale walioachwa wajane.. yatima na wapweke unawaambiaje..?

Unadhani pole pekee yake itawasaidia kuwaondolea simanzi na machungu yao..? wengine wameondokewa na bread earners.. unategemea pole uliotoa itawasidia kupata fedha za kujikimu..?

kijani ya tatu: kwa nini uamini kwamba hali kama hii haitatokea wakati sababu zile zile zilizopelekea kutokea at first place bado zipo..? viongozi wa kisiasa bado wanaendelea kufanya kazi.. vitendea kazi havijaboreshwa na hata madai yao mengi ya maslahi hayatimizwa..! r u serious Mr. president..?

hiyo blue ya nne: unasikitishwa na mauaji hayo yaliotokea songea.. umechukua hatua gani..? watu wanauawa kwa imani za kishirikina.. wananchi wamelalamika mpaka wamechoka.. njia pekee wakaona ni kuandamana.. wakatokea wauaji wabaya kuliko wachawi wakawaua.. ulitoa kauli yeyote..? na pale mkuu wa operesheni na mafunzo alipowaita wale wananchi waliopigwa risasi na kuuliwa ni wahuni.. ulitoa kauli yeyote hata ya kuikemea..?

hizo aya mbili za mwisho mr president zimezidi kuleta utata.. watu wameuawa ww unatuma rambirambi..?? polisi wamewaua raia wasio na hatia wewe unatoa pole..?? raia waliokuwa wanatafuta kulindwa na polisi ndo waliokuja kuuawa na polisi hao hao.. na wewe unatoa pole tu..? no action no what..!!!! r mockin ur fellow tanzanians..? utawahakikishiaje usalama wao wakati tayari umeshawaangusha hivyo..?? wameuawa na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.. halafu unawahakikishia usalama wao..

Sure Mr President sio lazima uwe na washauri kujua kama hili si zuri.. kumbuka Alhaji Mwinyi aliwahi kujiuzulu uwaziri kwa mauaji ya polisi kama haya.. aliwajibika kwa kuwa waliouwa walikuwa chini ya wizara yake..!! umeongeza uchungu kwa wananchi...
 
01 MARCH 2012



*Akiri sakata la muswada wa katiba kumtikisa
*Aeleza kilichomfanya asaini haraka haraka

Peter Mwenda na Willbroad Mathias

RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa mgomo wa madaktari ulitikisa taifa na makovu yake yatabaki katika kumbukumbu za historia ya taaluma ya tiba hapa nchini.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana katika hotuba yake kwa taifa na kukiri kuwa tayari amekabidhiwa na Waziri Mkuu, Bw.Mizengo Pinda, taarifa ya Kamati aliyounda kushughulikia madai ya madaktari.

"Kuanzia kesho Serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na uwezo uliopo," alisema Rais Kikwete na kuongeza;

"Nawaomba madaktari kuwa na moyo wa subira. Napenda kutumia fursa hii kuwahakikishia ndugu zetu madaktari na watumishi wengine wote wa sekta ya afya kwamba Serikali inatambua, inajali na kuthamini kazi wazifanyazo na mchango wao katika kulinda na kudumisha afya za wananchi wa Tanzania."

Katika hotuba hiyo Rais Kikwete alitoa pole kwa wananchi na hasa wagonjwa nchini kwa mateso waliyoyapata katika kipindi cha mgomo.

"Ni matumaini yangu kuwa hali kama ile haitajirudia tena katika nchi yetu," alisema Rais Kikwete.

. Mauaji ya Songea

Mbali na mgomo wa madaktari alielezea kusikitishwa na mauaji ya Songea yale yanayohusishwa na imani za ushirikina na yale ambayo yalitokea kwenye maandamano.

"Napenda kutumia nafasi hii kuelezea masikitiko yangu kwa vifo hivyo na kutoa pole na rambirambi zangu na za wananchi wa Tanzania kwa ndugu wa marehemu wetu hao.

Tupo pamoja nanyi katika misiba hii mikubwa na majonzi. Napenda kuwahakikishia wananchi wa Songea kwamba Serikali kupitia vyombo vyake vya usalama imekuwa inafanya na itaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji haya mpaka wahusika wote wapatikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria," alisema Rais Kikwete.

Mabadiliko ya Katiba

Akizungumzia hatua yake ya kusaini muswada wa mabadiliko ya katina, Rais Kikwete alisema katika mazungumzo yake na viongozi wa vyama vya siasa waliokwenda kumuona Ikulu, aliwaeleza ugumu aliouona kuhusu kuacha kutia sahihi muswada huo na kuurudisha tena Bungeni kujadiliwa upya.

"Nilichelea kuliingiza taifa letu katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kikatiba usiokuwa wa lazima. Mgogoro ambao tunaweza kuuepuka kwa kutumia njia nyingine za kikatiba na kisheria kufikia malengo yale yale," alisema Rais Kikwete na kuongeza;

"Kitendo cha mimi kukataa kutia sahihi kingejenga chuki kwa upande wa wabunge walio wengi ambao waliujadili muswada na kuupitisha.... wengeweza kuhisi wamedharauliwa na kuonekana hawana thamani."

Alipongeza vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na CCM na Baraza la Taifa la Asasi Zisizokuwa za Kiserikali kwa uelewa wao na ushirikiano.

"Kwa kweli, jinsi hali ilivyokuwa huko nyuma, hatuna budi kushukuru na kujipongeza. Ni matumaini yangu na rai yangu kuwa tutaendeleza ushirikiano na utamaduni huu wa mazungumzo tuliouanzisha na kuutumia katika hatua zingine zinazofuata," alisema na kuongeza;



Hapo kwenye "RED" ukisoma vizuri utaelewa kuwa hii ni mbinu ya serikali kuepusha mgomo mwingine wa madakitari kwani tarehe 3 Machi ipo karibu. I can not comprehend as to why Mr. President will come forward to speak to the nation this month after so many months have passed without doing so. It is merely a strategic plan to cool down the doctors. Dear fellow Doctors, remember that the president used the word "if" in his promise and therefore, what you asked may or may not be solved. Just thinking aloud. :A S-confused1:
 
kikwete%20maoni.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete​
Raymond Kaminyoge
RAIS Jakaya Kikwete amesema alisaini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kukwepa hasira za wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Rais Kikwete alitoboa siri hiyo katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari aliyoitoa juzi kupitia vyombo vya habari.Uamuzi huo wa Rais kutia saini muswada huo ambao tayari ulikuwa umepingwa kila kona ya nchi licha ya kupitishwa na Bunge, ulizidi kuibua hasira za makundi mbalimbali ya kijamii.

Rais wakati akisaini muswada huo, Novemba mwaka jana, alikuwa ameanza mazungumzo na makundi ya kijamii ukiwamo ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Lakini, mwenyewe akifafanua ni kwa nini alisaini muswada huo wakati ulikua ukipingwa na wananchi na huku akiwa katika mazungumzo na wadau, ndipo alisema, “Kitendo cha mimi kukataa kutia sahihi kingejenga chuki kwa upande wa wabunge walio wengi.

... ambao waliujadili muswada huo na kuupitisha. Wangeweza kuhisi wamedharauliwa na kuonekana hawana thamani.”

Rais Kikwete alisema vyama vya siasa na asasi za kiraia waliomba asitie saini na badala yake aliagize Bunge liujadili tena muswada huo.

“Sikutaka kuliingiza taifa letu katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kikatiba usiokuwa wa lazima unaoweza kuepukwa kwa kutumia njia nyingine za kisheria na kikatiba,” alisema Kikwete.

Alisema, alipofanya mazungumzo na vikundi hivyo vya kiraia, aliwaeleza kuhusu ugumu huo wa kuacha kutia saini na kuurudisha bungeni kujadiliwa upya.

Kikwete alisema kama muswada huo ungerudishwa kujadiliwa bungeni, kuna hatari asingeweza kupata ushirikiano wao na kushindwa kupata kile kilichotarajiwa.“Wangeweza kujadili na kuamua kuyakataa mapendekezo yote mapya na kubakia na msimamo wao ule ule,” alisema.

Mauaji ya Songea
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alizungumzia mauaji ya Songea akisema, amesikitishwa na mauaji hayo, lakini akaahidi kufanyika kwa uchunguzi ili kuwashughulikia waliohusika kwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Alisema yapo mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina na yapo yaliyotokea kwenye maandamano.

“Napenda kutumia nafasi hii kuelezea masikitiko yangu kwa vifo hivyo na kutoa pole na rambirambi zangu na za wananchi wa Tanzania, kwa ndugu wa marehemu wetu hao,” alisema Kikwete.

Aliongeza;“Napenda kuwahakikishia wananchi wa Songea kwamba Serikali kupitia vyombo vyake vya usalama itaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji hayo hadi wahusika wote wapatikane,” alisema.

Kikwete alisema hadi sasa yametokea mauaji ya watu 13 yanayohusishwa na imani za ushirikina na kwamba watuhumiwa 26 wamekwishakamatwa kutokana na mauaji yao.

Kuhusu mauaji yaliyotokana na maandamano, alisema askari wanne wamekamatwa na upelelezi unaendelea.

Taarifa kutoka katika Mkoa wa Ruvuma zilisema watu wanne waliuawa na Polisi wakiwa kwenye maandamano hayo.“Nashukuru kwamba amani na utulivu vimerejea katika Manispaa ya Songea, nawapongeza viongozi wa ngazi zote na wananchi kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuwezesha amani kupatikana,” alisema Kikwete.
chanzo.
JK: Nilisaini Sheria ya Katiba kuepuka hasira za wabunge
 
He acted so cleverly I may say. When making such high decisions, it is crucially important to take into account the resulting outcome of those decisions. He thus opted not to please Magwand.a minority at the expense of losing support of the CCM majority and in that regard he deserves enormous eclats.
 
He acted so cleverly I may say. When making such high decisions, it is crucially important to take into account the resulting outcome of those decisions. He thus opted not to please Magwand.a minority at the expense of losing support of the CCM majority and in that regard he deserves enormous eclats.
JK has acted so silly, President should not be making decisions based on fear of retaliation that is the stupidest thing i have never heard. President should make decision for the fact IT IS THE RIGHT TO DO and not otherwise.
For your info. the chadema stands reflect the will of majority of Tanzanians which is The president has no business in making the constitution that task should be left to wananchi alone.
 
Kimsingi suala la kuandaa Katiba sio la Rais, ni la wananchi kupitia Bunge la Katiba linaloundwa kwa uwakilishi wa kijamii. Bunge, Serikali na Mahakama ni matokeo ya Katiba. Kauli ya JK ni tata kwa kuwa ni yeye ndiye aliyeandaa muswada kwa hiyo hakuwa na sababu ya kuwasingizia wabunge wa CCM ambao kazi yao ni NDIYOO ! kama asemavyo Masaburi.
 
...napata ukakasi kumweelewa JK,inamaana alisaini huo mswada pamoja na kuuona kuwa haufai ili wabunge wa ccm wasiudhike!?...ama kweli watanzania tuna "RAHISI",kwa hiyo watanzania tuamini kwamba hao wabunge wako wakikwambia kula k.i.n.y.e.s.i utakula ili usiwakasilishe and then utajitia kidole mdomoni utapike uchafu wote utoke maisha yaendelee!!!???...
 
He acted so cleverly I may say. When making such high decisions, it is crucially important to take into account the resulting outcome of those decisions. He thus opted not to please Magwand.a minority at the expense of losing support of the CCM majority and in that regard he deserves enormous eclats.

.....cleverly? nipe breki kidogo. Hivi kweli Kikwete sku hizi anawaogopa wabunge kiasi hicho? mbona nchi hhii ingeshaendelea kitambo! Kwa kusaini kwake sheria hiyo ya katiba alifahamu kasa kuwa alikuwa anaiangamiza nchi, isingekuwa presha kubwa kutoka upinzani na asasi zingine. Kikwete angekuwa mnyonge namna hiyo mbele ya bunge, na wabunge wa ccm wangekuwa wanakomalia mambo ya Msingi tungekuwa mbali sana.......Msinichoshe mie..:yawn:
 
He acted so cleverly I may say. When making such high decisions, it is crucially important to take into account the resulting outcome of those decisions. He thus opted not to please Magwand.a minority at the expense of losing support of the CCM majority and in that regard he deserves enormous eclats.

Only the likes of you will see this as a clever decision, but for those who are rational, unbiased and are not ready to boot-lick will call it COWARDICE and rightly so.

Btw: Kwa wale mnaouliza alipo Faiza Fox ndio huyu anaejiita sasa Radhia Sweety. Whatever that means!
 
The president! I feel so sad for decisions he made. Had that been the reason (what he is trying to explain now was true), should hearrange for such a big ceremony? The wholy issue is questionable. I think he is trying to manipulate the Tanzanians.
 
wht evr...the prezdei has made a clevely decisions..hpo nampigia makofi....:lol:
 
Considering the pressure... He did what was right. Though to my opinion he has to be smart. He should not allow his people to drive him...
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema alisaini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kukwepa hasira za wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Rais Kikwete alitoboa siri hiyo katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari aliyoitoa juzi kupitia vyombo vya habari.Uamuzi huo wa Rais kutia saini muswada huo ambao tayari ulikuwa umepingwa kila kona ya nchi licha ya kupitishwa na Bunge, ulizidi kuibua hasira za makundi mbalimbali ya kijamii.

Rais wakati akisaini muswada huo, Novemba mwaka jana, alikuwa ameanza mazungumzo na makundi ya kijamii ukiwamo ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). RAIS Jakaya Kikwete amesema alisaini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kukwepa hasira za wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Rais Kikwete alitoboa siri hiyo katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari aliyoitoa juzi kupitia vyombo vya habari.Uamuzi huo wa Rais kutia saini muswada huo ambao tayari ulikuwa umepingwa kila kona ya nchi licha ya kupitishwa na Bunge, ulizidi kuibua hasira za makundi mbalimbali ya kijamii. Rais wakati akisaini muswada huo, Novemba mwaka jana, alikuwa ameanza mazungumzo na makundi ya kijamii ukiwamo ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Source: Mwananchi 02/03/2012
Maoni yangu

Nimesikitishwa na kauli ya JK kusema kwamba alisaini sheria mbovu ya Katiba ili kukwepa hasira za wabunge wa CCM. Kauli hii nadhani ni kauli ya kwanza mbovu kutolewa hadharani na viongozi wa Taifa hili. JK amesahau kuwa yeye ni sehemu halali ya kutunga Sheria na kama hajaridhishwa na sheria ni haki yake ya kikatiba kutoipitisha. Kwa kauli yake, sitoshangaa tena tunapokuwa na sheria nying zilizotungwa kibabaishaji kwa Maslahi ya CCM na sio kwa Maslahi ya Taifa kwa ujumla. Maana halisi ya maneno ya JK ni kwamba anaogopa kutopitisha kitu kilichopendekezwa na wabunge wa CCM kwa kuwa kitaibua hasira za wabunge hao na hatimaye wataanzakuongea mengi yatayopelekea yeye kupoteza unga.


Kwanini Rais aogope hasira za wabunge wa CCM wakati ni haki yake kupitisha/kutopitisha sheria yoyote????? Kwanini Rais amejipambanua kuwa yeye ni Ruber stamp???Kwa nini Rais alipuuza maoni ya raia wake walio wengi na kuheshimu wapunge 250 wa CCM na kuamua kupitisha Sheria mbovu??Utaratibu huu wa kuogopa hasira za wabunge wa CCM na kupitisha vitu sub standard umeanza lini, Ni utaratibu wa Kikatiba??????Kwa hiyo Rais anataka kusema wabunge wa CCM ndiyo wanaolinda maovu nchini mwetu????

JK anamaanisha kuwa masuala kama ya Mikataba mibovu ya Migodi, Wizi wa fedha katika Taasisi zetu mbalimbali, Ufisadi mbalimbali, Matatizo ya umeme na maufisadi ndani yake yanalindwa na Wabunge wa CCM???? Mana kama wabunge wa CCM wasingekuwa wanayalinda, kwa uoga huu wa Rais naimani tungekuwa tumeshabadilisha mambo mengi sana yanayoenda mrama hapa nchini. Naomba niwashkuru wabunge wa CCM kwa kutusaliti na kutetea uovu humu nchini kiasi kinachopelekea Rais kupitisha vitu vya hovyo ili kulipa fadhira ya wema mnaomtendea kwa kutokutimiza wajibu wenu kama wasimamizi wa serikali au kwa kutokemea maovu yanayofanywa na Serikali.

Vyama vya upinzani ni wajibu wenu kulifikisha hili kwa wananchi na kulifanyia kazi ili 2015 wafanye maamuzi sahihi kwani uwingi wa wabunge wa CCM bungeni ndio chanzo cha hali hii mbaya inayotukabili, kwani tuliowatuma kuisimamia Serikali, wamekuwa walinzi wa maovu, kiasi cha kupelekea kulipana fadhira kwa kupitisha vitu vya hovyo hovyo ili kuwafurahisha wabunge kwa gharama ya Taifa. WanaJF wenzangu nyie kauli hii mnaitazama kwa mtazamo gani??

Aidha, katika katiba ijayo inafaa tulingalie suala zima la kupitisha sheria upya kwani utaratibu huu wa kupitisha sheria ili kuzuia hasira za wabunge wa chama tawala tuondokane. Nchi imejaa matatizo kibao ambayo source yake kuu ni sheria mbovu, angalia mikataba tunayoisaini. Sisi kama wananchi hatukujua kuwa source ya ubovu huu ni uoga wa kutoibua hasira. Aidha, huko mbeleni inabidi tuwe na kiongozi aliye msafi ili hata kama hizo hasira zitaibuliwa, basi wabunge wasipate sifa na vigezo za kumlipua.

JK kadhihirisha kuwa si msafi na hivyo anaomba msaada wa wabunge kumlinda ili amalize muda wake salama. Tena tusishangae kwa kauli kama hizi ndio Mana Spika na Pinda wanajitangazia Posho bila hata Rais kuzipitisha kwani wanajua Rais ni Ruber Stamp tu, wao kama viongozi wa bunge wakitaka kitu, kinakuwa.Sasa nimemwelewa Pinda na Makinda pia.Hawa wamemkalia Rais Kichwani kwani ndo walioshika mpini.
 
Back
Top Bottom