mgeni wenu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 3,664
- 1,730
Hasira za wabunge wa ccm ni kali kuliko za wananchi
Kiongozi huna haja ya kuchoka kazi ndo inaanza, ni jukumu letu sisi tunaoelewa hali ya mambo kuwaelimisha wale wanaozawadia viongozi kura wakati wa uchaguzi. Ni sisi ndo wakuwaambia madhara ya kuwa na wabunge wa chama kimoja zaidi bungeni. Idadi ingekuwa sawa kwa sawa haya yasingetokea. Marekani, UK na kwingineko wamefika hapa walipofika sababu wafanya maamuzi ni 50% kwa 50% so Rais hana sababu ya kuogopa kundi fulani kama hapa kwetu.Huyu ndie kiongozi wa nchi, anawaogopa wabunge wa chama chake kuliko maslahi ya nchi. Tujiulize, kama ana woga wa aina hiyo amefanya /atafanya mangapi yasiyo na maslahi kwa taifa kwa ajili ya kuwaogopa CCM. Dangerous statement!!! Sio kwamba ameacha, muelewe wapendwa wananchi anaendelea kuwaogopa!! Nimechoka
Rais ameweka bayana kuwa wabunge wa CCM ndio wanaoficha maovu ya nchi hii hali inayopelekea Rais kuwapa Respect ya uoga.Kwa kauli hiyo, wabunge wa ccm wangekuwa makini wangevunja serikali. Ni kauli ya aibu kwanza kwa Rais Mwenyewe na Chama chake na pia ni kauli ya kuwazalilisha wabunge wa ccm.
Faiza Fox yuko wapi siku hizi, au yuko kwenye ban? Ningependa kusikia ana maoni gani naye kuhusu jambo hili.
Rais ameweka bayana kuwa wabunge wa CCM ndio wanaoficha maovu ya nchi hii hali inayopelekea Rais kuwapa Respect ya uoga.
Hapo ndipo ninapoukubali undumilakuwili wa JK katika michakato kama hii. Watu wameshanuka vibaya yeye ndiyo anajisafisha sasa.
Mahali penye alama, TOO LATE to say it today! Kwanini hatukumsikia palepale, ama baada ya kutoka ughaibuni? Amrijeshi mkuu ANASIKITIKA wakati ASKARI wake WANAUA RAIA? Eti TUKO PAMOJA!01 MARCH 2012
Mbali na mgomo wa madaktari alielezea kusikitishwa na mauaji ya Songea kwenye maandamano.
"Napenda kutumia nafasi hii kuelezea masikitiko yangu kwa vifo hivyo na kutoa pole na rambirambi zangu na za wananchi wa Tanzania kwa ndugu wa marehemu wetu hao.
Tupo pamoja nanyi katika misiba hii mikubwa na majonzi.