JK: Mgomo wa madaktari ulikuwa 'ngoma nzito'... Aeleza kilichomfanya asaini haraka haraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Mgomo wa madaktari ulikuwa 'ngoma nzito'... Aeleza kilichomfanya asaini haraka haraka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 1, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]01 MARCH 2012[/h][h=3][/h]

  *Akiri sakata la muswada wa katiba kumtikisa
  *Aeleza kilichomfanya asaini haraka haraka

  Peter Mwenda na Willbroad Mathias

  RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa mgomo wa madaktari ulitikisa taifa na makovu yake yatabaki katika kumbukumbu za historia ya taaluma ya tiba hapa nchini.

  Rais Kikwete aliyasema hayo jana katika hotuba yake kwa taifa na kukiri kuwa tayari amekabidhiwa na Waziri Mkuu, Bw.Mizengo Pinda, taarifa ya Kamati aliyounda kushughulikia madai ya madaktari.

  "Kuanzia kesho Serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na uwezo uliopo," alisema Rais Kikwete na kuongeza;

  "Nawaomba madaktari kuwa na moyo wa subira. Napenda kutumia fursa hii kuwahakikishia ndugu zetu madaktari na watumishi wengine wote wa sekta ya afya kwamba Serikali inatambua, inajali na kuthamini kazi wazifanyazo na mchango wao katika kulinda na kudumisha afya za wananchi wa Tanzania."

  Katika hotuba hiyo Rais Kikwete alitoa pole kwa wananchi na hasa wagonjwa nchini kwa mateso waliyoyapata katika kipindi cha mgomo.

  "Ni matumaini yangu kuwa hali kama ile haitajirudia tena katika nchi yetu," alisema Rais Kikwete.

  . Mauaji ya Songea

  Mbali na mgomo wa madaktari alielezea kusikitishwa na mauaji ya Songea yale yanayohusishwa na imani za ushirikina na yale ambayo yalitokea kwenye maandamano.

  "Napenda kutumia nafasi hii kuelezea masikitiko yangu kwa vifo hivyo na kutoa pole na rambirambi zangu na za wananchi wa Tanzania kwa ndugu wa marehemu wetu hao.

  Tupo pamoja nanyi katika misiba hii mikubwa na majonzi. Napenda kuwahakikishia wananchi wa Songea kwamba Serikali kupitia vyombo vyake vya usalama imekuwa inafanya na itaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji haya mpaka wahusika wote wapatikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria," alisema Rais Kikwete.

  Mabadiliko ya Katiba

  Akizungumzia hatua yake ya kusaini muswada wa mabadiliko ya katina, Rais Kikwete alisema katika mazungumzo yake na viongozi wa vyama vya siasa waliokwenda kumuona Ikulu, aliwaeleza ugumu aliouona kuhusu kuacha kutia sahihi muswada huo na kuurudisha tena Bungeni kujadiliwa upya.

  "Nilichelea kuliingiza taifa letu katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kikatiba usiokuwa wa lazima. Mgogoro ambao tunaweza kuuepuka kwa kutumia njia nyingine za kikatiba na kisheria kufikia malengo yale yale," alisema Rais Kikwete na kuongeza;

  "Kitendo cha mimi kukataa kutia sahihi kingejenga chuki kwa upande wa wabunge walio wengi ambao waliujadili muswada na kuupitisha.... wengeweza kuhisi wamedharauliwa na kuonekana hawana thamani."

  Alipongeza vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na CCM na Baraza la Taifa la Asasi Zisizokuwa za Kiserikali kwa uelewa wao na ushirikiano.

  "Kwa kweli, jinsi hali ilivyokuwa huko nyuma, hatuna budi kushukuru na kujipongeza. Ni matumaini yangu na rai yangu kuwa tutaendeleza ushirikiano na utamaduni huu wa mazungumzo tuliouanzisha na kuutumia katika hatua zingine zinazofuata," alisema na kuongeza;   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sasa kama ilikua ngoma nzito kwanini Amiri Jeshi Mwenyewe asisimame kuhesabiwa???, kwanini ajifiche kwenye vivuli ya wasaidizi wake???

  Kuna wimbo unasema "you say it best, when you say nothing at all"

  samahani kama nimewakwaza...
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  angesema kuanzia leo marufuku polisi kutumia risasi za moto kuzima maandamano ningemuelewa!hizo ni blaa blaa
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Yeye Mwenyewe alikuwa Nje ya Nchi - hakujua chochote kinachoendelea, labda Mwanae wa kike ambaye ni Dr. alikuwa anampa story
   
 5. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo ninapoukubali undumilakuwili wa JK katika michakato kama hii. Watu wameshanuka vibaya yeye ndiyo anajisafisha sasa.
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Du JK ana mtoto Dr?
   
 7. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Sijui kwanini kila linapokuja suala la JK huwa nakosa comment....
  Just ni kweli kuwa
  "Taifa lilitaka Rais, tukampata Kikwete"
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  maiti imefufuka na kuanza kuongea..huyu mtu namfananisha na baba ambaye majambazi walipovamia nyumbani kwake alijifanya amelala fofofo na kujiangusha chini akaliacha godoro ili wabebe kilaini bila kumdhuru,majambazi walipoondoka akajifanya kastuka"wako wapi?wako wapi nasema niue mtu"
   
 9. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndiiyo, ni mmoja kati ya watoto wake wawili wanaodaiwa ada na Bodi ya Mikopo
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,088
  Likes Received: 6,554
  Trophy Points: 280
  mkuu wetu anaanzia nyuma. lol mbele alikuwa anapumzika huko ughaibuni.
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nimekosa cha kucomment ghafla...!!! mmhh lazima nirudi tena hapa
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Kuna wale wanaomdanganya akikunja uso watu watakimbia kwa kuogopa...yeye mwenyewe amekiri ule mgomo ulikuwa mzito kwake.
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Oh yeah wa Kike, kasoma Muhimbili
   
 14. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Jk kama askari wa kwenye move baada ya tukio wao ndio wanafika kwa mbwembwe na ving'ora wanakuta game over
   
 15. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  JK kweli ndio BASATA mwenyewe, hivi ataacha lini sanaa, yaani imembidi asubiri mpaka mwisha wa mwezi ndio aongelee habari za mgomo wa madaktari!!!! duuuuuuu, changanya sisi kabisa
   
 16. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280

  hahahahahahahahah!!!!!!

  Ni ukweli kabisa. Kesha ingiza uongo wa kisiasa hapa kutubadilisha akili zetu. Hakuan cha maana hapo.

  Cha muhimu ili kunusulu Taifa na majanga yaliyotokea mfano. Mgomo wa Madakitari na Mauaji ya kinyama yaliyofanywa na Polisi kule Songea inabidi Serikali ije na uamuzi mgumu ambao ni kuwachukulia hatua wote waliohusika. Mf. Waziri Mkuu, Waziri na naibu (Afya), Waziri na naibu (Mambo ya Ndani), IGP, Mkuu wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

  Labda akifanya hivyo kidogooooooooo NITAMUELEWA!!!!

  Lakini vinginevyo tumeshawazoea viongozi wa tanzania kwa kupenda kuchanganya Siasa katika masuala ambayo siyo ya Siasa.


  RAISI FANYA MAAMUZI MAGUMU HAPA ILI UELEWEKE!!!!  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 17. Zagazaga

  Zagazaga JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 519
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  no ni dentist.
  mia
   
 18. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280

  Wajameni kwa mliosikiliza Hotuba hii, Je, alisema kuwa ndio anaanza tena kuhutubia Taifa kila mwisho wa mwezi??

  Au hii ni dharula tu, hatoonekana tena hadi kutokee mauaji mengine yatakayofanywa na Polisi na watendaji wazembe??


  Mwenzenu kwetu Umeme walikata Tanesco siku nzima ya Jana wamerudisha usiku hata sijui ilikuwa saa ngapi kwani hadi saa 7 usiku ilikuwa bado.


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 19. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  yaaani hii nchi bana, jamaa hakudhubutu fungua kinywa leo anasema madaktari ilikuwa so. mhhh
   
 20. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Mzee wa Mia umekuja kwa ID nyngne
   
Loading...