Jk kukutana na chadema

Jk kukutana na chadema

Kweli watanzania tuna uelewa finyu, hivi inawezekana mtu kuchochewa kufanya vurugu bila sababu !!!!!!!
Tuache kuzungumza kwa unazi wa chama. Inatupasa tuelewe wazi kwamba vurugu za Arusha chanzo chake ni mabavu na ukatili wa serikali ya CCM kwa kutumia vyombo vya dola yani jeshi la polisi kukandamiza na kuibaka demokrasia ya watanzania wengi wanaoishi maisha ya chini na katika umaskini uliokithiri.Maandamano ni haki ya kila raia wa Tanzania, kazi ya jeshi la polisi ni kutoa ulinzi tu na kuhakikisha kwamba waandamanji hawafanyi fujo na sio kuzuia watu kuandamana. Kama jeshi la polisi lingetoa kibali cha kuandamana hayo yote yasingetokea. Hapa wa kulaumiwa ni serikali na siyo CHADEMA.
 
Dos santos una roho ngumu. Hivi kweli wewe huoni matatizo ya wananchi? Nimeona unabeza maandamano. Unadai kuna agenda ya siri. Na kweli ipo, nayo ni hii, kutaka wananchi wajue kinaga naga chango na msingi wa matatizo walio nayo. Kwa bahati mbaya serikali fisadi ikiongozwa na genge dogo la watu wachache, walafi, wachoyo na wanafiki, sitaki kusema wako kama wewe, maana huenda wewe ni kuadi tu wala hupati chochote. Likini kikubwa ni kwamba watu hawa hawataki kabisa watu watambue haki zao. Hivi sasa ni sisi hatukubali, lazima awareness iwe ya nguvu, watu wajue haki zao na wawe na ujasiri wa kuzidai. Watawala wanalalamika kwa sababu wanaogopa hili. Wanajua fika watu wakijua ndiyo mwisho wa utawala wao. Ndiyo maana wanapiga kelele wakiongea uongo kabisa kusema cdm wana agenda ya siri. Naomba usiwahadae watu. Kama maandamano hayana tiji, kama mnavyowadanganya watu, basi acheni cdm waandamane kisha watachoka wenyewe. Lakini, thubutu yenu, mmeshashikwa pabaya. Ndiyo maana mnalalamika. Bahati nzuri mlishashindwa. Hamuwezi tena kuzima moto huu. Pole kwa hoja zako zilizokufa.
 
CHADEMA kukutana na JK ili iweje?...hoja hapa ni maisha magumu kwa mtanzania, ufisadi, uzembe &kutowajibika n.k; so wanachokifanya CHADEMA mikoani ni kuzidi kuwariji wananchi na kuwaelezea sababu ya umaskini wao na maisha magumu, hakuna haja ya kukutana na JK....kwani wakikutana wataamua maisha kuwa matamu?ufisadi kuisha n.k?
<br />
<br />
POINT
 
JK Kama Rais, nina hakika anayajua matatizo yote haya. Hivyo basi kwa usalama wa nchi yake na Chama chake sidhani kama amekaa tu ametulia. No! He is doing something, let us give him time after the elections and see what will happen. We learn through misktakes. Give him a second chance. Mpaka amefika hapo alipo (Rais) sidhani kama anaweza kukaa bila kutafuta suluhu ya kero zilizopo. Hiyo Ari ZAIDI, nguvu ZAIDI na kasi ZAIDI ni tofauti na Ari MPYA ....... ipeni muda kidogo hiyo ZAIDI, inaweza ikaleta matunda. Yeyote afanyaye kosa, akishaligundua hulirekebisha. Ukimsakama wakati yuko katika process ya kulirekebisha, unamvunja nguvu na ku-disturb process zake. Mnapowapump wananchi na maneno ya kuichukia Serikali, Je hao watendaji wanapowatembelea kwa ajili ya kufuatilia maendeleo si mnataka wazomewe? Hiyo itawapa nguvu kweli? Mi kwa upande wangu namsupport sana Rais wetu, namwombea afya njema na mafanikio katika jitihada zake. Namhurumia anavyosakamwa. kuongoza nchi sio mchezo jamani.

Elimumali upo sahihi kiasi flani, lakini kwa hiyo KASI ZAIDI ya kulazimisha malipo haramu ya DOWANS
(Ref. Waziri Ngeleja, Jaji Werema, Capt. Chiligati etc). Kama hili moja na mengine hayatoshi, wakalivuruga BUNGE ambalo ndilo lingekuwa jukwaa zuri la kuiongoza serikali (Ref. Kuanzia kupandikizwa spika, kukataa hoja za msingi kwa mabavu na tija kwa mafisadi, kuchakachua kanuni za BUNGE "hasa ile ya kubadili tafasiri ya kambi kuu ya upinzani" nk. nk.). Sasa Ndugu yangu Elimumali huoni kama tukisubiri mpaka 2015 tutakuwa tumeshaliua kabisa Taifa hili ambalo lipo ICU bila ya uangalizi. Hivyo basi, kwa CDM ambacho ni chama cha siasa chenye kutambua uwelekeo mbaya wa Taifa hili, ilikuwa ni lazima waanzishe move kwa wananchi (wenyeserikali) ili kuifumbua macho serikali (CCM) pamoja na kuwaelewesha wananchi ambao ndiyo wenye mamlaka na serikali yao KIKATIBA "ingawa kwa Tz wenye mamlaka ni CCM na dola zake"
 
maisha magumu mpaka watu waambiwe ni magumu? Kwani watu hawayaoni? Mbona Rais JK ktk hotuba yake amekiri kwamba maisha ni magumu.CDM wakiwahutubia watu maisha ni magumu ndo yanabadilika au kuwapotezea watu muda wa kuhangaikia maisha yao yawe mepesi. Maandamano hayana tija kwa mtz,ila ipo ajenda ambayo wewe huijui unafuata mkumbo. Kama hamkueleweka ktk kampeni ndo mtaeleweka sasa

Kweli kakiri kuwa maisha ni magumu. ila ni hatua gani za makusudi alizochukua kurekebisha hali hiyo mpaka sasa?
Yeye kama Rais kaacha kushughulika na matatizo ya watanzania badala yake anahangaika na watu wanaoyajadili matatizo hayo (yaani CDM) anasahau kuwa mbali na kuwa viongozi wa chadema wao pia ni watanzania na wanaguswa na matatizio hayo na kwa mujibu wa sheria wanayo haki ya kuzungumzia matatizo ya taifa lao popote bila kuvunja sheria.
Sijui hapa Viongozi wa CDM wana kosa gani?
JK na serikali yake wameshindwa kushughulikia mambo kadha ya msingi ambayo ndiyo yanaipa chadema nguvu ya kupenya kwa wananchi. wangeyashughulikia kipasavyo chadema wasingekuwa na jambo la kuueleza umma wa watanzania.

CCM wanatakiwa kusoma alama za nyakati na wasiishie kuongoza kwa mazoea na siasa za vitisho. wakati wa siasa za vitisho umepita
 
duh kazi ya kuzima moto wa wananchi sasa nadhani serikali haina uwezo cha msingi ni kutekeleza yenye manufaa kwa taifa zima
 
walikuwepo tyena CDM wamekaza uzi na kuwaambia maandamano zaidi yatafuata sasa ni zamu ya kanda ya kusini baada ya bunge la april na moja ya maazimio ya kikao hicho wameishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika URT.

Serikali ya umoja wa kitaifa ni bull-shit kabisa. Ndiyo njia inayotumika kuuwa demokrasia ya vyama vingi Afrika. Chama kilichoko madarakani kinaposhindwa hakitaki kuachia madaraka, badala yake wanatafuta vijisababu vya kuunda ujinga unaoitwa serikali ya umoja wa kitaifa, ambayo mwisho wake inaondoa kabisa ule upinzani na matunda yake. Angalia Zimbabwe, Kenya na Zanzibar kwa sasa hivi, ni kama hakuna upinzani tena. Na mbaya zaidi upinzani wanalazimishwa kufuata sera za chama kingine!!

Sijui Kama Dr. Slaa na Mbowe watakubaliana na ujinga huo wa serikali ya umoja wa kitaifa. Ni afadhali wao wanedelee kukaanga sangara mpaka kijulikane.
 
maisha magumu mpaka watu waambiwe ni magumu? Kwani watu hawayaoni? Mbona Rais JK ktk hotuba yake amekiri kwamba maisha ni magumu.CDM wakiwahutubia watu maisha ni magumu ndo yanabadilika au kuwapotezea watu muda wa kuhangaikia maisha yao yawe mepesi. Maandamano hayana tija kwa mtz,ila ipo ajenda ambayo wewe huijui unafuata mkumbo. Kama hamkueleweka ktk kampeni ndo mtaeleweka sasa

ni kweli wananchi wanaelezwa kuwa kuna ugumu wa maisha na cdm! Uzuri wake cdm wanawajulisha wananchi kuwa mchawi wa maisha kuwa magumu ni nani ili wachukue hatua stahili!
 
Hakuna haja ya CHADEMA kukutana na Kiwete. Hakuna tatizo lolote la kufanya wakutane.
Kinachoonekana kama tatizo hapa ni CCM KUKATAA KUKOSOLEWA NA CHADEMA KAMA CHAMA RASMI CHA UPINZANI NDANI YA NCHI YETU.
CCM na KIWETE wao wameonyesha UDHAIFU NA MCHECHETO WA HALI YA JUU SANA kiasi kwamba wao sasa NDO WANAONEKANA KAMA CHAMA CHA UPINZANI KWA KUILALAMIKIA CHADEMA KILA KUKICHA.

Hivi ile kauli ya DHARAU ya KIWETE ya kusema kuwa vyama vya upinzani ni vyama vya MSIMU vinavyosubiri Uchaguzi tu imeishia wapi! Kwamba uchaguzi ukiisha tu navyo vinaisha! I believe Kiwete have noted something different from CDM! This time NOT for CHADEMA being a seasonal party men! CHADEMA KIMEDHAMIRIA KUONGOZA NCHI HII COME 2015, it can be even before if CCM will keep on frustrating Tanzanians economocally and politically!

ANGALIZO:Kama CCM hawatajirekebisha katika muda wa mwaka au miaka 2 inayokuja basi HALI YAO ITAKUWA MBAYA KWA NAMNA AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA NCHI YETU,HALI AMBAYO ITAPELEKEA WATANZANIA KUTAKA MAGEUZI AU MABADILIKO YA UTAWALA.
 
Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kusema serikali ya ccm ipewe mda zaidi??? Tuchukue mfano rahisi tu, wakati wamjadala wa richmond Bungeni Bunge lilitoa maazimio juu ya hatua za serikali kuchukua. Hebu tuambieni imechuka hatua gani au mnahitaji mda gani kutekeleza maazimio yale ya Bunge?!
 
CHADEMA kukutana na Kikwete ni kumpandisha chart Kikwete ambayo hanayo tena. Ajibu hoja mbali mbali za CHADEMA kuhusu uongozi wake mbovu na Serikali yake yote katika mambo mbali mbali nchini. Hivi kwa nini hawa viongozi wetu wa nchi nyingi za Bara letu hata pale kunapokuwa na ushahidi wa kutosha kwamba wameshindwa kuongoza nchi zao wanang'ang'ania kuendelea kuwepo madarakani?
 
SONGAS,IPTL,NETGROUP,kawaulize wenzio rais alikuwa nani? Tatizo mkumbo. Inaonekana hukusiliza hotuba,umehadithiwa au umeamua kupotosha kama ilivyo kawaida yenu

Sikiliza kijana unapokua hujui jambo ni bora ukae kimya ujifunze na uelimike kuliko kuleta ushabiki wa ki CCM ndani ya ishu za maana na kwa kuonyesha wewe ni pandikizi ulilotumwa ndo maana umeongea utumbo hapo kwenye red, unaongea kishabiki shabiki kama Sophia Simba, we unasema nimehadithiwa wakati nimekuwekea mpaka nukuu ya hotuba ya mmeo JK na humu JF video yake invisible ame upload. na hapo kwenye blue huyo JK alihusika moja kwa moja katika mikataba ya kishenzi na kinyonyaji, SONGAS,IPTL,NET GROUP yeye alikuwa waziri wa Mambo ya nje (Nakupa homework hebu jaribu kutafuta na kujua nini kazi kubwa ya waziri wa mambo ya nje) na hiyo RICHMOND ndio kabisa hana cha kukwepa hapo maana yeye ndiye alikuwa mwenyekiti wa baraza la mawaziri wakati baraza la mawaziri linaupitisha huo mkataba. acha kuleta u facebook, kijana you need to develop. ukitaka mpambano zaidi ni PM
 
kila kitu kinafaa kwenda kwa kufuata taratibu zake, watanzania tuna haki ya kudai mabadiliko lakini tusisahau kufuta njia muwafaka ya kutafuta mabadiliko hayo tusije tukajuta kama wenzetu wa somalia,iraq na watakavyojuta walibya, ni vizuri jk na slaa kukaa meza moja kwani mazungumzo huzaa maelewano na anaekataa mazungumzo si mtu mwema.
 
Majadiliano!! Mazungumzo!! Wakutane cdm na ccm!!! What for? Sisi watanzania hatutakikuskia such nosense. Cdm endeleen kutoa elimu kw wa tz,msikubal kuchakachuliwa kama cuf.
 
Katika vugu vugu la chadema kuendelea na maandamano nchi zima ambayo yameleta hofu kubwa kwa ccm na serikali yake, na pia kusababisha vyama vya siasa jana kukutana kwa dharura kutatua mzozo huo ila wamependekeza rais Jakaya Mrisho Kikwete kukutana na chadema na kuzungumza ili pawe na maelewano na chadema.
My take:
Sidhani kama Chadema na JK kutakuwa na maelewano kwani JK ameshindwa kujibu hoja za chadema na maisha yanaendelea kuwa magumu na uchumi unaendelea kudorora. Kama jana vyama vya siasa vilipokutana vilishindwa kuelewana je JK ATAWEZA?


Kabla ya mazungumzo kutokana na sheria za nchi na utawala bora awachukulie hatua RA, EL, Chenge, Mkapa, Manji et al kwa kutumia sheria ya uhujumu uchumi then CDM wanaweza kuanza kunsikiliza na ngonjera zake mpya.
 
Kikwete ni chumvi iliyoharibika.Sasa chumvi ikiharibika iwekwe nini hadi ikolee?Nothing can be done.Ni ya kutupa tu. tu.
Katika vugu vugu la chadema kuendelea na maandamano nchi zima ambayo yameleta hofu kubwa kwa ccm na serikali yake, na pia kusababisha vyama vya siasa jana kukutana kwa dharura kutatua mzozo huo ila wamependekeza rais Jakaya Mrisho Kikwete kukutana na chadema na kuzungumza ili pawe na maelewano na chadema.
My take:
Sidhani kama Chadema na JK kutakuwa na maelewano kwani JK ameshindwa kujibu hoja za chadema na maisha yanaendelea kuwa magumu na uchumi unaendelea kudorora. Kama jana vyama vya siasa vilipokutana vilishindwa kuelewana je JK ATAWEZA?
 
Ila ndivyo walivyopendekeza ili kuwe na maelewano na chadema . Ila John Tendwa uwezo wake wa kufikiri umefika tamati kwa kuendeshwa kama gurudumu bovu kwani anafikiria ndio litakuwa sululisho badala ya Raisi kusikiliza hoja za chadema na kutatua matatizo yanayowakuta watazania na hali ngumu ya maisha.

Hilo litendwa sifuli MUNGU alichukue tu halina issue hapa duniani
 
Katika vugu vugu la chadema kuendelea na maandamano nchi zima ambayo yameleta hofu kubwa kwa ccm na serikali yake, na pia kusababisha vyama vya siasa jana kukutana kwa dharura kutatua mzozo huo ila wamependekeza rais Jakaya Mrisho Kikwete kukutana na chadema na kuzungumza ili pawe na maelewano na chadema.
My take:
Sidhani kama Chadema na JK kutakuwa na maelewano kwani JK ameshindwa kujibu hoja za chadema na maisha yanaendelea kuwa magumu na uchumi unaendelea kudorora. Kama jana vyama vya siasa vilipokutana vilishindwa kuelewana je JK ATAWEZA?

Hapo kwenye red, CHADEMA haina mzozo na JK pamoja na serikali yake isipokuwa inamtaka JK aache ufisadi na kuwakumbatia mafisadi wenzake (e.g, Rostam Aziz na Edward Lowassa) ili awatumikie wananchi kwa maslahi ya watanzania wote. CHADEMA ni wasemaji tu wa walalahoi na wanapigania haki za wananchi wote wa Tanzania. Hapo kwenye kijani ni kweli JK na Wassira wanalia lia tu kwenye vyombo vya habari badala ya kujibu hoja na madai ya za msingi. Hakuna haja ya Mkwere kukutana na CHADEMA lakini kama atataka tu ushauri wa kuongoza nchi maana washauri wake wameshindwa kabisa kama yeye mwenyewe.
 
Kama kuna kitu kinati kichefu chefu nchi hii ni mambo ya kipuuzi kama haya. Labda kama hii honja ingeletwa na watoto wa darasa la sita katika mijadala ya somo la Uraia.

Hivi JK akikutana na CHADEMA watakuwa na agenda gani?

Huo mkutano utakuwa wa hovyo na hauna tija (sorry,...it will be..CRAP)!!
 
Back
Top Bottom