JK, kampeni hii ‘itakula’ kwako! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, kampeni hii ‘itakula’ kwako!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Candid Scope, Apr 6, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  TANZANIA tumeanza kushindanisha watu kwenye kugombea urais tokea mwaka 1995. Kwa lugha nyingine ni katika chaguzi kuu nne (1995, 2000, 2005 na 2010) ambapo tumeshuhudia nchini mwetu mtu akishindana na mtu ama watu katika kugombea urais. Huko nyuma tulizoea kuona mtu akishindana na kivuli ambapo mpiga kura akitaka kuchagua mtu anatia alama ya vema upande wa NDIYO na kama hamtaki huyo mtu anachagua kivuli kwa kutia alama ya vema upande wa HAPANA. Lakini napenda kusema kwamba katika chaguzi zote zilizotangulia zile za mtu na kivuli na hata zile za mtu na mtu ama watu, hakuna uchaguzi ambao mmoja alifanya faulo kama ule wa mwaka jana 2010.

  Kinachonitisha zaidi ni kwamba faulo hizo zilifanywa na mgombea wa chama tawala ambaye pia alikuwa rais hata wakati anagombea. Najua wasaidizi wa Kikwete watamdanganya kwamba nimemkosea adabu ama kosa lolote ambalo wao wataamua kunipa. Lakini naomba niseme wazi kwamba uchambuzi wangu binafsi unanituma kwamba JK katika uchaguzi wa mwaka jana alicheza faulo nyingi lakini hii moja ambayo nitaijadili kwa kina leo ni faulo mbaya kuliko zote.

  Naomba sasa nianze; Mkakati wa kwanza ulikuwa ni kumtambua adui yao mkubwa ambaye walikuja kumwona kwamba ni CHADEMA. Hilo halina tatizo kabisa kwa maana kila mshindani anapaswa kumfahamu mshindani wake mkubwa kwa jina, uwezo wake, udhaifu wake, na kadhalika ili aweze kupanga vizuri mipango ya kumshinda. Tatizo langu na JK kile anachokifanya baada ya kugundua kwamba adui wao mkubwa ni CHADEMA.

  Walianza na mkakati wa kukionyesha kwamba chama kile ni cha kikabila, wananchi wakawapuuza. Kimsingi hiyo ni faulo ambayo tumeizoea. Hata mwaka 1995 ilitumika sana wakati Lyatonga Mrema na NCCR-Mageuzi yake ilipoonekana tishio kubwa kwa chama tawala. Baadaye akasikika JK mwenyewe akidai kwamba watu wasikichague CHADEMA kwa kuwa ni chama cha msimu eti baada ya uchaguzi hawatakiona tena mpaka ufike uchaguzi mwingine. Hilo nalo likadunda maana mwenye macho haambiwi tazama. Watanzania ni mashuhuda wa dhati wa utendaji wa CHADEMA. Lugha nzuri ambayo inaweza kueleweka vema kwa watanzania wa leo ni kuwaambia kwamba CCM ni chama cha msimu, kwamba CCM wanajua sana kuongea vizuri na wananchi wakati wa uchaguzi lakini uchaguzi ukishapita wanatupa kila kitu wanasubiri uchaguzi ujao. Lakini ni chama gani kimekuwa muda wote na wananchi kikiwapigania dhidi ya dhuruma na manyanyaso wanayoyapata kila kukicha? Ni chama gani kilikuwa na wananchi bega kwa bega mwaka hadi mwaka kuwaeleza ufisadi wote unaofanywa na vigogo mafisadi wanaojijali nafsi kuliko umma? Bila shaka ni CHADEMA. Ndiyo maana wito wa JK kwa wananchi kutoichagua CHADEMA eti kwa kuwa ni chama cha musimu, ulizidi kumgeukia yeye mwenyewe.

  Wakaja na faulo ambayo wao waliiona kuwa kali zaidi na walidhani watakuwa wameimaliza CHADEMA na mgombea wake wa urais. Wakasema mgombea urais wa CHADEMA kaiba mke wa mtu. Ikavuma sana kwenye vyombo vya habari kwa mkakati maalum ulioratibiwa na makada wa CCM. Kuna taarifa kwamba zilikuwa ni juhudi maalum za Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kumtafuta kwa udi na uvumba aliyewahi kuishi na mwanamke ambaye hivi sasa ni mchumba wa mgombea wa CHADEMA. Taarifa zinazidi kueleza kwamba Makamba alikwenda mbali zaidi kwa kumpa yule bwana pesa na gari na kumwahidi kwamba wao watalipia gharama zote za wanasheria ili mradi tu yule jamaa afungue kesi ya kumshtaki mahakamani mgombea wa chadema. Lengo lilikuwa ni kumwaribia mgombea huyo siha yake mbele ya wananchi ili asichagulike. Ukitaka kulielewa hilo jiulize hiyo kesi imeishia wapi mbona haisikiki tena! Lakini hapo pia wakadunda.

  Maana ni faulo ambayo wameitumia mara kadhaa huko nyuma. Mwaka 1995 Lyatonga Mrema akiwa tishio kwao waliwahi kusema kwamba kampa mimba mwanamke na kumtelekeza. Yule dada akafungua hadi kesi mahakamani na hatimaye baada ya pilipilika za uchaguzi na mgombea wa CCM akatangazwa mshindi kesi imekufa. mwaka 2000 Prof. Lipumba akiwa tishio zaidi kwa Mkapa, ikavumishwa sana kwenye vyombo vya habari kwamba Lipumba hana mke ni aibu nchi kuongozwa na rais asiye na mke.

  Mke wa Lipumba akajitokeza hadharani tena mzuri wa sura kuliko wa kwao (wakati huo). Wakafunga domo na kukaa kimya. Kwa hiyo faulo hiyo nayo dhidi ya mgombea wa CHADEMA mwaka jana ikagonga mwamba. Ndipo mwisho JK akaja na silaha ya maangamizi ambayo kimsingi inamuua hata yeye lakini hakujali ili mradi afanikiwe kwanza kuingia Ikulu. Kutoka kusikojulikana tukashtukia tu JK anakuja na suala la udini. Tuliposikiliza kwa makini tukagundua kwamba eti kwa sababu Dk. Slaa aliwahi kuwa padri basi mara kanisa katoliki ndo liko nyuma yake mara Wakristo ndo wako nyuma yake, basi tu ili mradi kila aina ya upuuzi ukawa unasemwa ili mradi kutimiza lengo lao.

  Ingawa viongozi wa dini walijitahidi kueleza kwa kina kutokuhusika kwao na kampeni za kidini lakini JK hakutaka kulisikia hilo. Akasahau kwamba yeye mwenyewe ndiye amekuwa akilitegemea zaidi Kanisa Katoliki kuliko mtu mwingine yeyote. Akasahau kwamba alisoma kwenye shule ya misheni na hakuna waziri wakati wa Mkapa ambaye amekuwa karibu na kanisa hilo kuliko yeye.

  Ni yeye aliyekuwa anakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe nyingi tu za Kanisa Katoliki. Ni yeye aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe mojawapo ya kiislamu mwaka 2005 akawaponda waislam na kuwataka wajitahidi kusoma na kuendesha shule nzuri kama Wakristo akiwaambia kuacha kuwasakama Wakristo kwa kuwa bila Wakristo yeye asingepata elimu nzuri aliyonayo eti kwa kuwa tu alisoma shule ya misheni. Ni baada ya mambo yote hayo ndipo aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Methodias Kilaini, akasikika akisema Kikwete ni chaguo la Mungu. Nani sasa anayefanya kampeni za kidini.

  Haikuishia hapo, baada ya uchaguzi mkuu wa 2005 na tukiwa tunajiandaa na uchaguzi mkuu wa 2010, Kikwete akaalikwa tena kwenye mahafali ya chuo kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki. Wakiwa wameambatana tena na Askofu Kilaini na ambaye alisikika tena akisema bado kauli yake ya Kikwete ni chaguo la Mungu inasimama. Akammwagia sifa kemkemu eti kwa kuleta utaratibu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kudai eti utaratibu huo ni mzuri sana wa kuwakopesha hata wanafunzi wa vyuo vya binafsi na eti unafaa kuigwa Afrika Mashariki yote. Wakati huo niliandika makala nzima kumkosoa Askofu Kilaini. Nilimweleza kwamba mpango wa kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu ni ubunifu wa Mkapa na Waziri wake wa Elimu ya Juu wakati huo, Dk. Pius Ng’wandu. Nikamwambia hata wao waliuiga kutoka Kenya kwa mujibu wa maelezo ya Dk. Ng’wandu mwenyewe ndani ya Bunge wakati wa kupitisha muswaada huo mwaka 2005. Nikamwambia kimsingi Kikwete anastahili lawama kali kwenye suala la mikopo ya wanafunzi badala ya kumsifia.

  Wakati kina Mkapa wanaanzisha mfumo huo walilenga kumkopesha kila mwanafunzi kwa asilimia mia ya gharama zake za kusoma chuo kikuu ama chuo chochote cha elimu ya juu, kuanzia ada ya masomo, ada nyinginezo zote zinazotozwa na chuo, gharama za kuishi mwanafunzi (malazi na chakula) pamoja na gharama nyinginezo zinazomhusu mwanafunzi kwa mfano vitabu, mafunzo kwa vitendo na utafiti.
  Kikwete akadai akiingia yeye ataboresha lakini alipoingia akaleta madaraja kwamba kuna wanaostahili kwa A kwa maana ya kukopeshwa asilimia 100, B ni asilimia 80, C ni asilimia 60 na kadhalika.

  Ni katika kipindi cha Kikwete sasa migomo ya elimu ya juu imeongezeka mara 5. Lakini kwa kuwa wakati huo askofu alikuwa upande wa Kikwete haikuwa nongwa.
  Kasheshe ikaanzia pale Baraza la Maaskofu lilipotoa waraka kwa waumini wake juu sifa za kiongozi bora ambaye waumini wake wanatakiwa kumchagua. Niliupitia waraka ule pote na sikuona dini ikiwa mojawapo ya sifa za mtu ambaye baraza la maaskofu lilimpendekeza kwa waumini. Wala sikuona jina la mtu kiasi kwamba tunaweza kusema hawakusema lakini walimtaja mtu wao kuwa ndiye anafaa. Lakini kuna siri moja katika waraka ule. Maaskofu walisisitiza kwamba umefika wakati ili tulikomboe taifa tuchague viongozi wasio mafisadi. Huo ni ujumbe ambao hata Kikwete mwenyewe ameutamka kinafiki mara nyingi sana kwa wananchi wake. Maneno hayo hayo yalipotamkwa na viongozi wa dini ambao kimsingi si, na hawatakiwi kuwa wanafiki, Kikwete akashtuka.

  Akaona waumini watawaelewa na kimsingi watafanyia kazi na wakifanyia kazi waraka ule inakula kwa CCM maana ndiyo iliyojaza mafisadi. Ndipo faulo ya udini ikaanza kuandaliwa. Ikasemwa kwamba kuna mgombea anafanya kampeni za udini. Eti maaskofu wamewaelekeza waumini wao kumchagua mgombea wa CHADEMA.

  Wengi walidhani na hata waasisi wa faulo hiyo walifikiri kwamba baada ya kampeni na uchaguzi kwisha, hiyo faulo itaijiishia yenyewe wala haitakumbukwa. Hawakujua ubaguzi huo Mwalimu alishasema ni sawa na kula nyama ya mtu, ukishaanza utaendelea tu. JK akajikuta baada ya uchaguzi anafanya kazi ya kuwalilia waandishi wa habari eti wasaidie kuondoa makovu ya udini yaliyojitokeza wakati wa kampeni.
  Ni sawa na kwamba alikuwa akisema kuwa wakati wa kampeni alianzisha propaganda ya udini ambayo ilibebewa bango sana na vyombo vya habari vilivyokuwa vimejitoa mhanga kuhakikisha anashinda tena urais kwa njia zozote zile.

  Sasa ameshinda anawaomba waandishi wa habari wale wale waliokuza propaganda ya udini wasaidie kuiondoa. Kazi ambayo hakujua kwamba hawaiwezi katu! Kwa ujumla, waumini wa faulo hiyo wamebaki wakiwa na kutu hiyo vichwani mwao na ni vigumu kuiondoa kabisa. Hivi sasa mkakati umeanza kufanywa na viongozi wachache wenye maslahi binafsi katika dini fulani.

  Wameanza kutaja kwa majina tena wazi wazi chama fulani na kukihusisha na dini fulani tena wakitoa wito wazi wazi kwa waumini wao na kuwataka eti wasishiriki maandamano ya chama hicho kwa kuwa chama hicho hakitetei maslahi ya dini yao. Haya ninayoyasema ni yale niliyoyasikia mimi mwenyewe kwenye redio moja ya dini hiyo ambayo hurusha matangazo yake kutokea Morogoro.

  Nilimsikia kwa masikio yangu kiongozi mmoja akisema wazi wazi kwamba ni dhambi kubwa kwa muumini wa dini yao kushiriki maandamano ya chama (akikitaja kwa jina) ilhali akijua kwamba chama hicho hakitetei haki za dini yao. Kama angesema maandamano ya chama chochote cha siasa ningemwelewa, lakini kitendo cha kukitaja chama kwa jina huku ikiwa dhahiri kabisa kwamba kuna vyama kadhaa ambavyo vimekuwa vikiitisha maandamano kwa makusudi hayo hayo ya kisiasa lakini havisemi vyama hivyo, ni dhahiri kwamba huyu anavigawa vyama vya kisiasa kidini.
  Namuuliza JK, kampeni zetu za uchaguzi zikianza kuwa za kidini itakula kwa nani? JK, kampeni hii itakula kwako!

  Acha kabisa masuala ya kutumia udini kushinda uchaguzi ama kubaki madarakani. Vita ya CHADEMA na CCM ni vita ya vyama vya siasa si vita vya ukristo na uislam. Unawakosea sana Watanzania Waislamu na Wakristo kuwaingiza katikati ya vita ya CHADEMA v/s CCM. Kuna Waislamu tena wengi ndani ya CHADEMA kama ilivyo kwenye CCM na kuna Wakristo wengi ndani ya CCM kama ilivyo ndani ya CHADEMA.
  Kuanza kuwagombanisha kwa maslahi yako na yenu ya kisiasa ni dhambi isiyosameheka.

  Kama unataka kuipumzisha CCM kutoka madarakani lakini ukaiacha nchi inamwagika damu na wewe mwenyewe umekimbilia uhamishoni Saudia, endelea na mchezo huo!

  Source: Tanzania Daima
   
 2. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ..Inafikirisha..ni maneno mazito. Tumwombe Mungu atuepushe balaa hili.
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Bravo! Somo limewekwa vizuri. Kama ana masikio atasikia; vinginevo ni kumpigia mbuzi gitaa.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu kuna makubwa na bado kwani ilmu ya uraia inazidi kusambaa
   
 5. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mungu atuhurumie kwani hatujui tulitendalo. Nimekugongea thanks mkuu.
   
 6. D

  Donell Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Kweli imeanza kula kwake maana Mwalimu Nyerere alisema na nakuuu " mkishaanza kujitenga na mambo ya udini,hamtaishia hapo tu maana mtaenda kwenye ukabila na n.k ",mwisho wa kunuku.

  Angalia sasa UVCCM wanaongelea kwamba watu wa kaskazini hawataki kuwaona watu wa pwani wakiongoza na hii itaendelea kwamba watu pwani hawataki watu wa kusini kuongoza na hii dhambi itaendelea hivyo hivyo.

  Ahsante.
   
 7. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  ..of course mgawanyiko anaouacha JK kwa nchi na chama chake ni mkuwab kuliko ule ambao aliukuta wwakati anapokea nchi kwa Mkapa. Kwa sasa hii migawanyiko ni visible sana, kikanda, kikabila, kidini n.k. Anakotupeleka siko kabisa. The situation is beyond his control
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nilichoshtuka na kushangaa kipindi cha kampini mwaka jana hoja ilizuka ghafla tu kutoka kwake Kikwete, na hatukuona dalili zo zote toka kwa wananchi au chama kingine cha Siasa. Na hata ndani ya CCM hatukusikia au kuona dadali za kampeni za kidini, ila kikwete ndio aliitungia wimbo pamoja na mke wake Mama Salma Kikwete.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa sasa amekuja na mpya nyingine ya kusema Maandamano ya Chadema yanashinikiza kumpindua Rais madarakani.

  :A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
   
 10. N

  Nanu JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli hii dhambi aliyoanzisha Kikwete itaipeleka Tanzania kusikotarajiwa!!!!
  Maneno huumba na JK kwa maneno yake ametuumbia udini na kwa sasa tunaona mikinzano ya wazi wazi ya kidini yameanza kuibuka na yeye kwa sasa kakaa kimya wala hakemei.
  Inatakiwa hata akemee UVCCM (yeye ni baba) hatakiwi kuwaacha watoto wakiendelea kueneza maneno ya chuki na ukabila na ukanda nchini. Kwa hili kwa kutolisemea amechelewa sana na hili nalo litaumba!!!
   
Loading...