JK. Kaa la moto halifichwi mfukoni

JK. Kaa la moto halifichwi mfukoni

Miwatamu

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
1,450
Reaction score
492
Jana nilibahatika kusiliza hotuba fupi ya rais wetu wakati akiwa pale katika uwanja wa Taifa alipofungua tamasha la matumaini. Kitu alichoongea ni kuwa wote wanaoutafuta urais wasipitie kwenye mirija ya UDINI!! Je, ni kweli kuwa yeye anaweza kuepuka hili? Sio kwamba anataka kufanana na mtu anayeficha kaa la moto mfukoni mwake??!!!!


TAFAKARI
 
Kwakweli inasikitisha kiongozi wetu wa nchi kuyaangalia haya na kuyaona ni ya kawaida tu na kuyatolea kauli nyepesi bila ya kuchukua hatua. huyu mtu anayepita kwenye taasisi za dini na fedha zake ni hatari kwa afya ya tanzania.
 
Kwakweli inasikitisha kiongozi wetu wa nchi kuyaangalia haya na kuyaona ni ya kawaida tu na kuyatolea kauli nyepesi bila ya kuchukua hatua. huyu mtu anayepita kwenye taasisi za dini na fedha zake ni hatari kwa afya ya tanzania.

Ndugu,
Anakuwa na aibu na kusitasita kulisemea kwa nguvu zote suala hilo kwa sababu naye alipitia njia hizo hizo kwenye kuusaka uraisi. Hilo lilisemwa na Lipumba kwenye hotuba ambayo imo humu JF. Kimsingi, suala la wanamtandao limeharibu sana nchi, Sumaye bado analia nao hadi leo kwa sababu naye alichafuka kama walivyovhafuliwa akina Mangula, Salim, Mwandosya na wenzao. Lazima mheshimiwa awe mgumu kung'ata jongoo live kwa sababu nafsi inamsuta.
 
Kikwete ni mnafiki sana. Anashindwa kumwambia LOWASA maneno hayo kaanzia makanisani sasa yupo misikitini.
 
Unajua katika hali ya kawaida kama mzazi ni mwizi au alikuwa mwizi hawezi kumkemea mtoto aache wizi na hata akifanya hivyo atakuwa anafanya kwa woga kwani mtoto anaweza kumuuliza mbona wewe ni mwizi au ulishawahi kuwa mwizi?

Kwa mtazamo wangu Mh raisi huenda hivi vitendo vinamkera kwa sababu ameshaona athari zake lakini kwakuwa na yeye alipita katika mfereji huo huo kwa hiyo inakuwa vigumu kumkemea rafiki yake kipenzi asipite katika mfereji huo.

Cha msingi watanzania tusikubali kutawaliwa na mtu yeyote ambae ana mabaki ya kifisadi, au anapitia makanisa au misikiti ili apate kujitakasa kwa mazambi yake aliyoyafanya nyuma ili tumuanimi tumkabizi dola atuongoze kufanya hivyo ni sawa na kukubali kuendelea kuibiwa.

viongozi wa dini pia wanatakiwa kulaumiwa katika hili kama wewe ni kiongozi wa dini unajua kabisa kama mtu huyu anafanya hivi ili apate kukubalika na jamii ili kusudi 2015 atakapo gombea aonekani ni mtu mwema hili swala viongozi wa dini pia munachangia kwa kupokea fedha ambazo watanzania wote tunaojua kupambanua mambo tunajua hiyo ni kama hongo ili mumtakase mtu mwenye zambi za ufisadi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom