JK azua mtafaruku kwenye daladala

Mimi nafikiri ni heri ya wanyama huko porini wanaheshimiana maana hakuna awezaye kuzichezea ndevu za Simba lakini hapa Tanzania mpaka muuza petrol anaitisha serikali na inatishika,wezi wa UDA wanashindana kusema huku hakuna anayekamatwa,yaaani..jioni hii watu tukusanyike jangwani walau tushike tu mabango yanayosema JK ONDOKA MADARAKANI,JK STEP DOWN ili walau dunia ijue kuwa tumechoka na mhuni huyu,tapeli wa kikwere.

hivi ana elimu gani? maana kwa situation ilivyo na anavyoongoza nchi ingekuwa amesoma hata std II angeshajiuzulu

Nasikia ana degree ya uchumi aliyoipata UDSM enzi hizo na Udokta wa kupewa

What next do we want?

Mgao wa Umeme, tumeukubali tukanunua magenerator.

sasa mafuta hakuna magenerator yapo Ndani.

Kwa hali hii utasikia m2 atakuja akwambie 2011 Tanzanian Econmy had a positive growth.

Si wote wenye vichwa wana ubongo wa kufikiri, mmoja wapo ni raisi wetu kazi yake kuchekacheka na kuleta hadithi za kisenge za mbayuwayu, watu wanaumia yeye yupo tu

Asubuhi ya leo nilikuwa kwenye daladala nikitokea Kinondon nikielekea Ilala,ndani ya daladala ile dereva alifungulia TBC Fm mjadala uliokuwepo ni wa watu kupiga simu na kuchangia suala la uhaba wa mafuta, wengi walitoa ushauri kuwa wauzaji wafungiwe leseni,,,,,,kwa kuwa kipindi kilikuwa ukingon kikaisha, mara mtangazaj akacheza hotuba ya Nyerere ambapo nyerere alikuwa akikemea juu ya masuala ya rushwa na jinsi wafanyabiashara wanavyokwepa kodi na the way wanavyoiweka serikal viganjani.

Abiria wote walinyamaza,,,,,punde mtangazaj akacheza hotuba ya RAIS KIKWETE, ntajitahid kumnukuu"Tangu mwaka 2001 mpaka sasa Tanzania ni miongon mwa nchi 20 ambazo uchumi wake unakua kwa Kasi", miguno ikaanza na vicheko, akatokea jamaa mmoja ambae alikaa na mwanajesh aliyekuwa akitabasamu tu,"HUYU ANATUZINGUA".

Yule jamaa aliongea huku amekunja sura, mara hotuba ya JK ikaendelea namnukuu"Watu huwa hawataki kujikubali, sasa kama hujikubali itakuwaje??"

Kilichofuata hapo tena si kuisikiliza hotuba bali ni zogo kwenye daladala, kila mtu akiibeza ile hotuba, yule mwanajesh nilimsikia akisema"HUYO NDIO KIKWETE BWANA".

Nikabaki najiuliza mbona hotuba ya Nyerere hawakuikejeli? Maana Nyerere alisema "SERIKALI CORRUPT HUWA INAWAOGOPA WAFANYABIASHARA, SERIKALI CORRUPT HUWA HAIKUSANYI KODI BALI HUWAONEA WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO, WALE WAKUBWA INAWAACHA NA HATA IKIWAAMBIA WANASEMA AH ATATUFANYA NINI HUYU?"

Haya alosema mzee Nyerere ndio yanayotokea leo kuhusu mafuta yanaendana na hiki kipande cha hotuba.
Hatuna RAIS.............

Raisi anachekacheka kijingajinga huku anadai uchumi wa Tz unakua kwa kasi zaidi ya kasi ya ukuaji wa uchumi wa Marekani halafu sisi bado maskini,dah!huyu mtu anaipeleka wapi hii nchi

Sasa hivi watanzania tunangoja nini? Hv hatuoni mifano ya nchi za Africa ambao wameamua kujitoa kwa ajili ya vizazi vyao vya baadae? Huyu jamaa (JK) si tulimweka wenyewe?

Sasa unadhani wa kumtoa? Ni sisi wenyewe....tuingieni mtaani jamani, tunaweka kambi pale magogoni siku 2 tu anaachia ngazi. Au mnataka mpaka mambo yawe mazito zaidi ndo mshtuke? Huyu mkwele amesha shndwa kuendesha hii nch tusingoje hyo miaka 4 ijayo ni mingi sana wakuu.

Kama kweli tunataka mabadiliko basi tunabid tudai na sio kuchekeana wana jamii....mi nashaur kuwa tuendelee kupeana habari ya maandamano kupinga utawala wa huyu jamaa ili j3 wiki ijayo tuingie barabarani. Au mnadhani kwa kupiga domo tv hapa jf ndo matatizo yetu yatakwisha? We need to fight....lets rise up people.

I wish ungesikia ngoma moja ametoa mtoto wa Arusha kuhusu rising!!
Anyway, utaisikia tu na itakupa mzuka sana tu..... Let's rise up people, this is our fight!!

rushwapiga.jpg

Mi nasikitikia kura yangu kiukweli roho inaniuma kumpa kura raisi wa aina ya kikwete. Hivi hajui nchi anavyoingiza nchi porini?

Kumbe wewe ni mmoja wa waliochangia kuliangamiza hili Taifa, Halafu unajuta wakati Baba wa Taifa alishatuonya, Kwenye Magazeti pia tulionywa kuhusu huyu Fisadi na Mwaka Jana Dr.Slaa alishatuonya bado hamkusoma alama za nyakati halafu unasikitika nini wakati wewe ndio uliyechangia haya Matatizo yaliopo

hana elimu ya maana... digrii yake almost adisco... na docrorial ya kuzawadiwa alipewa na chuo gani sijui..

PALE KWA MAPETE MWEMBECHAI NDO HIYO NYNGNE ALIIPATI,AGHRRRRRRR NIKIKUMBUKA NLIVYOTEMBEA KWA MIGUU LEO NAPATA JAZBA AF NIMEFKA HM NO POWER!!!

poleni sana watz mnakaribishwa Juba tuijenge jamani nchi yetu changa...

PALE KWA MAPETE MWEMBECHAI NDO HIYO NYNGNE ALIIPATI,AGHRRRRRRR NIKIKUMBUKA NLIVYOTEMBEA KWA MIGUU LEO NAPATA JAZBA AF NIMEFKA HM NO POWER!!!

pole,umepiga shato pori!!!!!!!

Mi nangojea mseme hiyo siku tutakapo ikomboa Tanzani yetu jamani,its too much aisee

Similar Discussions

Back
Top Bottom