Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,443
- 4,386
Wakati Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiendelea kusafiri kwenda mataifa mbalimbali kwa shughuli za kikazi na kufikisha nchi 10 alizokwisha tembelea, Rais John Magufuli leo ametimiza siku ya 143 tangu aapishwe kuingia Ikulu bila kukwea ndege kwenda ughaibuni.
Hiyo inaweza kuwa rekodi ya aina yake kwa kuwa haijawahi kutokea tangu Uhuru kwa Rais mstaafu kusafiri safari nyingi za nje ya nchi kushinda Rais aliyeko madarakani.
Hadi sasa, Rais John Magufuli ametumia siku zote za kuwa kwake madarakani kusimamia kampeni yake ya kuongeza mapato ya serikali na kukomesha vitendo vya ufisadi kupitia kile anachokiita ‘kutumbua majipu’.
Mbali na mataifa mbalimbali aliyokwishatembelea, rekodi zinaonyesha kuwa Machi 21 mwaka huu, Kikwete alikwenda nchini Tunisia kwenye mkutano wa nane wa nchi majirani na Libya ambapo yeye ni mwakilishi maalum wa Afrika wa usuluhishi wa mgogoro wa taifa hilo.
Kabla ya kwenda Tunisia, Kikwete alikuwa katika mji wa Salalah nchini Oman alikoshiriki Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya na alishindwa kuhudhuria kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Shein kutokana na kuwa nje ya nchi.
Katika mkutano wake na viongozi wa Libya, Kikwete alisisitiza kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.Juzi Rais huyo mstaafu aliwasili Dubai akitokea Tunisia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa shughuli hizo hizo za upatanishi wa mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Libya.
Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa tayari JK ameshakwea ‘pipa’ na kufika nchi za Ethiopia, Uingereza, Visiwa vya Comoro, Afrika Kusini, Ujerumani, Marekani, Oman, Libya, Tunisia na UAE huku baadhi ya safari hizo zikitokana na mialiko maalum anayopata.
Wakati Kikwete akiendelea kusafiri kutokana na majukumu mbalimbali yanayomkabili akiwa Rais mstaafu, Rais Magufuli ameendeleza rekodi yake ya kutosafiri.
Chanzo: Gazeti la Nipashe
27 March. 2016