JK azidi kupasua anga Ulaya

JK azidi kupasua anga Ulaya

Wakati Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiendelea kusafiri kwenda mataifa mbalimbali kwa shughuli za kikazi na kufikisha nchi 10 alizokwisha tembelea, Rais John Magufuli leo ametimiza siku ya 143 tangu aapishwe kuingia Ikulu bila kukwea ndege kwenda ughaibuni.

Hiyo inaweza kuwa rekodi ya aina yake kwa kuwa haijawahi kutokea tangu Uhuru kwa Rais mstaafu kusafiri safari nyingi za nje ya nchi kushinda Rais aliyeko madarakani.

Hadi sasa, Rais John Magufuli ametumia siku zote za kuwa kwake madarakani kusimamia kampeni yake ya kuongeza mapato ya serikali na kukomesha vitendo vya ufisadi kupitia kile anachokiita ‘kutumbua majipu’.

Mbali na mataifa mbalimbali aliyokwishatembelea, rekodi zinaonyesha kuwa Machi 21 mwaka huu, Kikwete alikwenda nchini Tunisia kwenye mkutano wa nane wa nchi majirani na Libya ambapo yeye ni mwakilishi maalum wa Afrika wa usuluhishi wa mgogoro wa taifa hilo.

Kabla ya kwenda Tunisia, Kikwete alikuwa katika mji wa Salalah nchini Oman alikoshiriki Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya na alishindwa kuhudhuria kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Shein kutokana na kuwa nje ya nchi.

Katika mkutano wake na viongozi wa Libya, Kikwete alisisitiza kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.Juzi Rais huyo mstaafu aliwasili Dubai akitokea Tunisia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa shughuli hizo hizo za upatanishi wa mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Libya.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa tayari JK ameshakwea ‘pipa’ na kufika nchi za Ethiopia, Uingereza, Visiwa vya Comoro, Afrika Kusini, Ujerumani, Marekani, Oman, Libya, Tunisia na UAE huku baadhi ya safari hizo zikitokana na mialiko maalum anayopata.

Wakati Kikwete akiendelea kusafiri kutokana na majukumu mbalimbali yanayomkabili akiwa Rais mstaafu, Rais Magufuli ameendeleza rekodi yake ya kutosafiri.

Chanzo: Gazeti la Nipashe
27 March. 2016
wanawezaje kusuluhisha migogoro ya mbali wakshindwa ule wa zanzibar tu
 
JPM atasafirije na keshakataza watu kusafiri hovyohovyo... Tukae wote hapa Tz tujenge nchi! Ikibidi ataenda tu,... kwa walioshindikana acha waende,
Suluhisho la Libya ni muhimu kuliko la znz
 
Huyu JK anaiwakilisha vyema TZ. Kwa nchi yetu ni yeye na Daimond Platnumz ndio wanaoipeperusha bendera ya taifa tulitaraji na Membe kams angebaki pale Wizarani basi kinachoendelea kati yetu na Kenya kingemalizwa ndani ya masaa 24,huku mzozo wa Burundi tungelikuwa tumeuzika siku 3 tangia kuapishwa kwake Wizara ya mambo ya ndani,Suala la bomba la Mafuta kuelekea UG pindi M7 anatua tu Entebe na bomba ndio linafika wakati huo Zanzibar imepata suluhisho lenye tija kwa Wazanzibar.
 
hahahaaa eti membe angebaki pale wizarani! kwan huyo alioko sasa ana mapungufu gani au ndo au una mapenzi tu na membe mkuu?
 
8235a38795feada2f7541c130b184b76.jpg

Chukua like mkuu...ila umempandisha hadhi kweli kweli...ingekuwa k....ba ingekuwa poa sana....ndo level yake hyo...na ndicho kinaongea...
 
Ni kweli kabisa. Nitamshangaa sana Rais Magufuli ikiwa atasafiri nje ya nchi katika kipindi hiki ambacho wananchi wanamhitaji zaidi
Wakati jk akiwa madarakan ulishawah kumshangaa akiwa anakwea pipa angali wananchi walimhitaji..? Yapo mambo yaliyokuwa yakitokea nchini wakati akiwa nje na alihtajika bt akaendelea kutulia huko ulishawahi kushangaa hilo...alitumia zaidi ya nusu ya mda wake nje ya nchi! Leo unashangaa Maguful kutoenda nje? Angeenda usingeacha kumsifia..unafiki bhana!!
 
Magufuli haitaji kusafir kwa sasa, mambo serikalini hayajakaa Sawa.
Mara yatakapokaa Sawa Atascadero tu.
Kikwete kwa majukumu aliyonayo ss suala la usuluhishi, kupanda ndege hakuepukiki.

Kama Magufuli anasubiri mambo yakae sawa nchi hii ndipo asafiri nje basi atasubiri sana. Itakuwa bora amkabidhi JK tenda ya safari kwa niaba yake.
 
ndio huo unafiki tulionao wabongo.....honestly unaongea kuwa zenj hakukuwa na mgogoro wa kisiasa?
Kwani mkuu wewe si umesema Zanzibar kuna mgogoro ndio mimi nakuuliza mgogoro gani maana mpaka sasa ni amani tu mimi nimezungumzia suluhisho lenye tija nikimaanisha mambo ya Muungano na sio uchaguzi
 
Huyu JK anaiwakilisha vyema TZ. Kwa nchi yetu ni yeye na Daimond Platnumz ndio wanaoipeperusha bendera ya taifa tulitaraji na Membe kams angebaki pale Wizarani basi kinachoendelea kati yetu na Kenya kingemalizwa ndani ya masaa 24,huku mzozo wa Burundi tungelikuwa tumeuzika siku 3 tangia kuapishwa kwake Wizara ya mambo ya ndani,Suala la bomba la Mafuta kuelekea UG pindi M7 anatua tu Entebe na bomba ndio linafika wakati huo Zanzibar imepata suluhisho lenye tija kwa Wazanzibar.

JK na Diamond level moja? Wadau wanaweza kufikiri unaendeleza dhihaka kwa JK kwamba naye ni msanii tu.
 
Hapana atasafir tu muda utafika. Na ninaamin na yeye ataitwa vasco dagama.
Jua na mvua kipi bora?
 
JK na Diamond level moja? Wadau wanaweza kufikiri unaendeleza dhihaka kwa JK kwamba naye ni msanii tu.
Kuwa ukawa sio kukosa akili Diamond na JK ndio wanaoipeperusha bendera ya TZ kimataifa katika nyanja tofauti JK ki dplomasia na Diamond ki sanaa au mpaka tukumulikie na tochi nyi wachaga siku hizi sijui mkoje.
 
ndio huo unafiki tulionao wabongo.....honestly unaongea kuwa zenj hakukuwa na mgogoro wa kisiasa?
Zanzibar hakuna mgogoro wowote, wananchi wamepiga kura halali na rais amechaguliwa kwa ushindi mnono na kiongozi wa upinzani alikua Dasalama kwenye hoteli yenye nyota tano akila bata...ngenge nini??
 
Hapana atasafir tu muda utafika. Na ninaamin na yeye ataitwa vasco dagama.
Jua na mvua kipi bora?
Tupo bize kushughulikia mambo ya ndani kwanza kukikaa sawa ndani ndio tunatoka nje sasa.
 
Back
Top Bottom