JK azidi kupasua anga Ulaya

Mtoa mada umenichekesha, huko juu umeanza kiushabiki flani hivi kama vile Kikwete anakihere here cha kusafiri,

Huku chini umejizodoa mwenyewe kua kumbe anasafiri kikazi (kutatua migogoro na kwa mialiko maalumu)

Nilijua anasafiri kwa matanuzi kumbe kikazi,

Sasa hao wanaompa mialiko maalumu kwani hawajui kua kuna rais?
Ni wazi wanautambua mchango wake au wamekubaliana na rais wa sasa awe anamuwakilisha.

Tupunguze wivu wa kike.
 
Huyu JK anaiwakilisha vyema TZ. Kwa nchi yetu ni yeye na Daimond Platnumz ndio wanaoipeperusha bendera ya taifa tulitaraji na Membe kams angebaki pale Wizarani basi kinachoendelea kati yetu na Kenya kingemalizwa ndani ya masaa 24,huku mzozo wa Burundi tungelikuwa tumeuzika siku 3 tangia kuapishwa kwake Wizara ya mambo ya ndani,Suala la bomba la Mafuta kuelekea UG pindi M7 anatua tu Entebe na bomba ndio linafika wakati huo Zanzibar imepata suluhisho lenye tija kwa Wazanzibar.
sawa Membe
 
Mtoa mada umenichekesha, huko juu umeanza kiushabiki flani hivi kama vile Kikwete anakihere here cha kusafiri,

Huku chini umejizodoa mwenyewe kua kumbe anasafiri kikazi (kutatua migogoro na kwa mialiko maalumu)

Nilijua anasafiri kwa matanuzi kumbe kikazi,

Sasa hao wanaompa mialiko maalumu kwani hawajui kua kuna rais?
Ni wazi wanautambua mchango wake au wamekubaliana na rais wa sasa awe anamuwakilisha.

Tupunguze wivu wa kike.
Mkuu Huyu team Magu ana matatizo ya akili,
 
wanawezaje kusuluhisha migogoro ya mbali wakshindwa ule wa zanzibar tu
Mchungaji Kiongozi Nabii Muheshimiwa Dr.Getrude Lwakatare anatoa Semina za Ndoa na kusuluhisha Migogoro ya Ndoa japo ya kwake ilivunjika.
Mwl Julius Kambarage Nyerere alishindwa kuelewana na wenzie kwenye EAC 1977 ikavunjika lakin alikuwa Mstari wa Mbele kupigania Africa iungane.
 
sawa mkuu
 
,at your iigya,f ioa
Wakati Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiendelea kusafiri kwenda mataifa mbalimbali kwa shughuli za kikazi na kufikisha nchi 10 alizokwisha tembelea, Rais John Magufuli leo ametimiza siku ya 143 tangu aapishwe kuingia Ikulu bila kukwea ndege kwenda ughaibuni.

Hiyo inaweza kuwa rekodi ya aina yake kwa kuwa haijawahi kutokea tangu Uhuru kwa Rais mstaafu kusafiri safari nyingi za nje ya nchi kushinda Rais aliyeko madarakani.

Hadi sasa, Rais John Magufuli ametumia siku zote za kuwa kwake madarakani kusimamia kampeni yake ya kuongeza mapato ya serikali na kukomesha vitendo vya ufisadi kupitia kile anachokiita ‘kutumbua majipu’.

Mbali na mataifa mbalimbali aliyokwishatembelea, rekodi zinaonyesha kuwa Machi 21 mwaka huu, Kikwete alikwenda nchini Tunisia kwenye mkutano wa nane wa nchi majirani na Libya ambapo yeye ni mwakilishi maalum wa Afrika wa usuluhishi wa mgogoro wa taifa hilo.

Kabla ya kwenda Tunisia, Kikwete alikuwa katika mji wa Salalah nchini Oman alikoshiriki Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya na alishindwa kuhudhuria kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Shein kutokana na kuwa nje ya nchi.

Katika mkutano wake na viongozi wa Libya, Kikwete alisisitiza kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.Juzi Rais huyo mstaafu aliwasili Dubai akitokea Tunisia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa shughuli hizo hizo za upatanishi wa mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Libya.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa tayari JK ameshakwea ‘pipa’ na kufika nchi za Ethiopia, Uingereza, Visiwa vya Comoro, Afrika Kusini, Ujerumani, Marekani, Oman, Libya, Tunisia na UAE huku baadhi ya safari hizo zikitokana na mialiko maalum anayopata.

Wakati Kikwete akiendelea kusafiri kutokana na majukumu mbalimbali yanayomkabili akiwa Rais mstaafu, Rais Magufuli ameendeleza rekodi yake ya kutosafiri.

Chanzo: Gazeti la Nipashe
27 March. 2016
,as a lot. Aaa[IM&G]
[/IMG]
 
Ni kweli kabisa. Nitamshangaa sana Rais Magufuli ikiwa atasafiri nje ya nchi katika kipindi hiki ambacho wananchi wanamhitaji zaidi
Unajua sometimes nafikiriaga labda kuna watu waliumbwa bila ubongo ili tu kuongeza idadi ya wakazi wa dunia. Umeisha jiuliza hayo matatizo yalisababishwa na nani?
 
Hivi ktk kile kikao cha jumuia ya Ea Magufuri alipanda bajaji...
 
Kikwete ni mwanadiplomasia wa kimataifa.hiki ni kipaji alichozaliwa nacho.ataendelea kukata anga sana.ushauri wangu tuache kufuatilia safari zake kwa sasa ameshaiacha ofisi ya umma.
 
Hii story ya kiboya sana; kwa sababu haieleweki ni ujumbe gani mwandishi anataka tuupate. Anasema JK anasafiri sana lakini anamalizia kuwa safari hizi zinatokana na mialiko anayoipata. Mwandishi alitakiwa atuambie kikwete alikuwa na options gani; kukataa mialiko? ku-host mikutano hiyo Tanzania? nk. Pia angejishughulisha kufahamu safari hizi zimegharimiwa na nani, zimegharimu kiasi gani cha fedha nk na je JK kwa namna yeyote alishinikiza vikao hivyo kufanyika?...wakiitwa makanjanja wanalalamika
Mkuu bongo hii waandishi wachache.mtu mzima kaenda shule kaona hii ndio story ya kuweka kwenye public
 
Wakati Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiendelea kusafiri kwenda mataifa mbalimbali kwa shughuli za kikazi na kufikisha nchi 10 alizokwisha tembelea, Rais John Magufuli leo ametimiza siku ya 143 tangu aapishwe kuingia Ikulu bila kukwea ndege kwenda ughaibuni.

Hiyo inaweza kuwa rekodi ya aina yake kwa kuwa haijawahi kutokea tangu Uhuru kwa Rais mstaafu kusafiri safari nyingi za nje ya nchi kushinda Rais aliyeko madarakani.

Hadi sasa, Rais John Magufuli ametumia siku zote za kuwa kwake madarakani kusimamia kampeni yake ya kuongeza mapato ya serikali na kukomesha vitendo vya ufisadi kupitia kile anachokiita ‘kutumbua majipu’.

Mbali na mataifa mbalimbali aliyokwishatembelea, rekodi zinaonyesha kuwa Machi 21 mwaka huu, Kikwete alikwenda nchini Tunisia kwenye mkutano wa nane wa nchi majirani na Libya ambapo yeye ni mwakilishi maalum wa Afrika wa usuluhishi wa mgogoro wa taifa hilo.

Kabla ya kwenda Tunisia, Kikwete alikuwa katika mji wa Salalah nchini Oman alikoshiriki Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya na alishindwa kuhudhuria kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Shein kutokana na kuwa nje ya nchi.

Katika mkutano wake na viongozi wa Libya, Kikwete alisisitiza kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.Juzi Rais huyo mstaafu aliwasili Dubai akitokea Tunisia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa shughuli hizo hizo za upatanishi wa mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Libya.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa tayari JK ameshakwea ‘pipa’ na kufika nchi za Ethiopia, Uingereza, Visiwa vya Comoro, Afrika Kusini, Ujerumani, Marekani, Oman, Libya, Tunisia na UAE huku baadhi ya safari hizo zikitokana na mialiko maalum anayopata.

Wakati Kikwete akiendelea kusafiri kutokana na majukumu mbalimbali yanayomkabili akiwa Rais mstaafu, Rais Magufuli ameendeleza rekodi yake ya kutosafiri.

Chanzo: Gazeti la Nipashe
27 March. 2016
Huyu mwandishi ni jipu.
 
Hii story ya kiboya sana; kwa sababu haieleweki ni ujumbe gani mwandishi anataka tuupate. Anasema JK anasafiri sana lakini anamalizia kuwa safari hizi zinatokana na mialiko anayoipata. Mwandishi alitakiwa atuambie kikwete alikuwa na options gani; kukataa mialiko? ku-host mikutano hiyo Tanzania? nk. Pia angejishughulisha kufahamu safari hizi zimegharimiwa na nani, zimegharimu kiasi gani cha fedha nk na je JK kwa namna yeyote alishinikiza vikao hivyo kufanyika?...wakiitwa makanjanja wanalalamika
Umemaliza Mkuu, kichwa cha habari na jinsi habari ilivyogeuka geuka, Ukanjanja
 
Labda hujaelewa, jk ni kikwazo kwa kundi fulani hasa baada ya kukatwa, wameandaa tim maalum ya kutaka kumzimisha asisikike,na wanajua kabisa kama jk akisusa na akiacha kutoa ushirikiano kwenye chama na serkali ni lahisi wao kupata nafasi ya kuisumbua serkali. kumbuka walishajalibu kumgombanisha na jpm wameshindwa, nk . Sasa mbaya zaidi wanajitahidi kumzima nyumbani mwenzao anazidi kung 'ara dunia nzima, ni shiida kwelikweli.
 
Back
Top Bottom