JK aumbuka - Mdahalo wake

Jamani niambieni, JK kajibu nin? Kweli huyu jamaa anauwezo wakuongoza nchi? Kibonde kashindilia msumali. Ndie maana kumbe alikataa debate na Slaa & Lipumba.
Nafungua mjadala

Swali Alilouliza kibonde kwa JK kama sijakosea Ukiingia Madarakani Hebu tupe taswila sahii ya Serikali yako na jinsi utakavyo mwandaaa yule utake mwachia.

Na JK alilika 50 Meters na hakujibu akaishia nijibu nini sasa hapo.

Kibonde alitaka kujua
1: Mfumo wa Baraza lake la mawaziri?
2: Serikali yake itawajibika kiasi gani kwa wananchi?
3: Nani atakuwa Mrithi wake baada ya muda wake kuisha?
 
Eti Kibonde kapigilia msumari. Unapenda ovyo.

Acha ushabiki lets talk the reality

Swali la kibonde JK alilijibu???? Kwanza utujibu kama ulikuwa unasikiliza JK alichokuwa anakijibu juu ya swali la Kibonde.

Katika Maswali yaliyo ulizwa na hao waaandichi wa habari kutoka vyombo vya habari ni Kibonde tu pekeyake swali ndio lilikuwa gumu sana kwa JK na akalikimbia.

sasa wewe tuambia ni swali gani aliloulizwa JK pale la maaana zai ya swali la Kibonde?

 
acha kupenda penda ovyo, Kibonde kauliza open-ended softball, swali ambalo unaweza kujibu vyovyote unavyotaka "Mheshimiwa, kwanza salam aleikum; Nini itakuwa sura ya serikali yako mpya"? Hilo nalo swali? originally posted by TASO

Yaani wewe ni wa ajabu sana!!! kuna swali ambalo halina jibu maalumu?swali hata kama ni open ended aliaaminishi kujibu jibu ambalo si sahihi,tofauti hapa ni namna ya kulielezea kwa kifupi au kwa kilefu,lakini umuhimu wa usahihi unabaki pale pale!!!Jamaa yako pumba tupu!!
 
acha kupenda penda ovyo, Kibonde kauliza open-ended softball, swali ambalo unaweza kujibu vyovyote unavyotaka "Mheshimiwa, kwanza salam aleikum; Nini itakuwa sura ya serikali yako mpya"? Hilo nalo swali?

Kikwete akasema nitapanga upya mawizara yawe fanisi zaidi, halafu akamuuliza Kibonde mara mbili, "unataka nijibu nini zaidi ya hapo"? Kibonde akakenua kenua meno tu, Kikwete akamwona mwepesi, akapandishia swala la serikali ijayo kukabiliana na urasimu wa makaratasi katika mfumo wa serikali ili ukiomba passport mkoani isiwe lazima uje Dar kuonana na ofisa uhamiaji. And this was arguably the better response Kikwete offered tonight. Mwishoni kina Kibonde wenyewe wakaishia kumpigia makofi Kikwete.

Kikwete ni lightweight ( na amesema hivyo leo "hata mkisema Kikwete hana akili, ovyo, mimi sijali"), lakini sio mbele ya wanahabari wa ilk ya Kibonde, wale ni vibonde wakubwa zaidi.

Una maana uandishi wa habari ni last opportunity for secondary school failures? Lakini kalamu yao inaweza kuanzisha vita!!!!!!!!
 
Nilishasema tangu siku za nyuma kuwa kibonde anajaribu kuganga njaa kwa nguvu zote ili aonewe huruma km akina salva baada ya kupiga debe ccm na kikwete.............watu km akina kibonde siamini km ni watz..............
 
Hadithi za paukwa pakawa na zile za enzi zileee za "...nina mjomba wangu Ulaya ataniletea gari na kutujengea nyumba" si ndio anachoamini kua mabaamedi ni ajira na vibarua katika makampuni ya wawekezaji ndo ajira nzuri.... hafai kua hata kiongozi wa familia yake
 
Ilikuwa ni aibu kubwa mkulu wa nchi amekaa mbele na waandishi/ watangazaji wachache walioruhusiwa kuuliza/ kusoma maswali waliyopewa. imethibitisha kauli ya Makamba kuwa hataki midahalo kwa sababu ataulizwa maswali na watu wa Kariakoo ambao watakuwa na njaa kweli alitafuta waloshiba akina Sussan Mungy, Masako, Kibonde, Mallya, David Ramadhani etc nao wamejiabisha kwani hawajui shida za watz wanauliza porijo za sisiem tu. AIBUUUU !!!!!!!!!!!!!!!!
 
anahitaji kupumzika kwa sasa, asing'ang'anie atakuja umbuka zaidi kama akitaka kutafuta ushindi wa mezani.
 
Baada ya kurusha huo waliouita 'mdahalo', na namna alivyojibu maswali yaliyokuwa yameandaliwa, tena yakiulizwa na watu wanaosomwa majina yao, Kikwete akichaguliwa kwa halali bila kuiba kura, ni wazi Watanzania ni wavivu wa kweli wa kufikiri. Nitakubaliana na Mkapa.:nono:
 
Hivi wale walokuwa wanamuhoji kikwete ni Waandishi Waandamizi au waandishi Wandaazimu?
maana JF ilituambia kuwa wameandaliwa maswali na majibu anayo mzee mkwerte ktk daftari lake maalum. Teh teh teh teh :evil:
 
Nimemsikia Hassan Mhelela wa BBC asubuhi kuwa alialikwa kwenye kikao hicho; amesema alitamani sana kumuuliza Rasi swali lakini hakupewa nafasi ya kuuliza!

Kilichonishangaza zaidi jana ni jinsi hao Wahandisi wa Habari waalikwa walivokuwa wakimpigia makofi anapomaliza kujibu maswala (maswali?) yaani kweli hao ni waandishi wa kulipwa.

Wadau mnaweza kutbandikia majina na Wahandisi walioalikwa na kuhudhuria kikao cha jana. Nilikuwa safarini na nilikuwa nafuatailia kikao hicho kupitia RFA
 
Jamani niambieni, JK kajibu nin? Kweli huyu jamaa anauwezo wakuongoza nchi? Kibonde kashindilia msumali. Ndie maana kumbe alikataa debate na Slaa & Lipumba.
Nafungua mjadala

Mkuu Nadhani Kibonde anajuta kumuuliza mku wa kaya lile Swali, Kibonde ni Kibaraka wa Jk na alitegemea amemuuliza Mshkaji wake Swali ambalo lingemjenga kumbe ndio likamharibia matokeo yake akajiumauma
 
Nini itakuwa sura ya serikali yako mpya"?


Nionavyo mimi swali halikuwa baya. Pengine alitaka kujua baraza lake la mawaziri litapangiliwaje. La 2005 lilikuwa na mawaziri 60. Dr. Slaa ametupa indication namna atakavyoweka wizara zake na anategemea maximum ya 20 cabinet ministers.

Kwahiyo ilikuwa busara kujua na CCM itakuwaje. Lakini mheshimiwa akashindwa kulijibu hilo swali ambalo kwangu mimi lilikuwa straight forward. Akishinda ni vile watu wanaogopa mabadiliko lakini vyovyote mtakavyoita iwe mdahalo, mahujiano au hotuba ana kazi ya ziada hakuwa amejiandaa kabisa. Kuna maswali kama mkuu wa nchi alitakiwa ayajibu lakini hakuweza amepoteza muda mrefu kuongea without substance.
 
Katika the so called mdahalo, nilipenda uulizaji wa susan mungi . Hakuonesha kuchekacheka(she was serious and straight foward) . Vile vile kikwete alivyojibu nonsense ilinifurahisha sana sababu anampa ushindi asilimia nyingi sana slaa .
 
Back
Top Bottom