jk aukacha mkesha wa maombi

mpinga shetani

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
3,236
954
Rais kikwete kaukimbia mkesha wa maombi ya kuukaribisha mwaka mpya unaofanyika hivi sasa ktk uwanja wa taifa.
Alitarajiwa kuwa mgeni rasmi lakini kamtuma mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kumuwakilisha.
 
loh
unataka akumbane na aibu ya jangwani wanamaombi wachache tu wakisali huku akiongea akasikia kizunguzungu pwaaaaaaaaaa
 
anajua hakuna la maana huko zaidi ya zinaa. Safi jk. Watu wanaenda kukesha wamevaa vimini. Mtujulishe watoto wa zinaa watakaopatikana kwenye mkesha wa mwaka mpya. Ukhabith tu umewajaa.
 
Zinaa ni yupi mbona sijamwona kila nikisoma maneno yako embu nisaidie mpwa amevaa nguo gani yukoje ana shape gani mpwa
happy new yr zinaa
 
Utachezaje rumba la yesu na mke wa mwenzako tena gizani uwe salama ?-matokeo ni zinaa.
 
mwakilishi wa Chadema anaitwa kusalimia na watu wanalipuka kushangilia. Anaitwa Miriam Glory Mkumbwa naye anadai ni mhubiri
 
Hongera JK, hakuna la maana huko. Hakuna la maana zaidi ya kuambukizana ukimwi
 
loh
unataka akumbane na aibu ya jangwani wanamaombi wachache tu wakisali huku akiongea akasikia kizunguzungu pwaaaaaaaaaa
Bahasha za michango zimetembea ? Hati miliki ya hilo onyesho ni la kanisa gani ? Maana kuna mauzo ya DVD?
 
Mwaka jana Mgeni Rasmi alikuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR.Mohamed Gharib Bilali

Sasa Mwaka Huu walidhani Rais Jakaya Kikwete angekubaliana nao! Maana hawa jamaa ni tofauti na Malengo ya Heshima la Kanisa! Ndio maana Rais Kikwete kaamua kwenda kwao! Na siku zotemwenda kwao si Mtoro!

Wanakwaya wamevaa nguo Mpaka chuchu tunaziona mbaya zaidi vimini vimebana hadi Pindo la Chupi linaonekana! Achilia hilo kukatika gani kule Kama Small Jobiso au Jesca Charles hii inaonyesha kuwa Mungu kaonekana Mtu na Si Mungu!

Ole wao jana Yesu angerudi nasema asingechukua Kwaya nzima Maana hakuna adabu hata kidogo maana mimi nilikuwepo!

Sinza Christian Center wamegeuza Dili la Mwisho wa Mwaka! Namna hii ni Hatari kwenu na Kazi ya Mungu mnaitia Doa!

Mbaya zaidi Mshereheshaji a.k.a MC. Lawrence Mwantimwa anatudanganya Rais Kikwete yupo Juu ya Jukwaa wakati sisi tunamwona Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Sadick namna ni Kufanya Usanii kwenye Mamlaka ya Nchi na Taasisi ya Rais.

Kiukweli kama mtakaa vema jipangeni zaidi katika kuutafuta uso wa Kristo na si Michongo ya Kutafuta Pesa na Kuuza Sura! Mungu hataniwi hata Kidogo!

Kama hamtambuli nguvu za Mungu kwa Ulimwengu uliza wana wa Kora kilchowakuta wakati Husika walipotaka kuleta Jeuri na Dhihaka!
 
ana haki ya kwenda kokote. Hata bagamoyo anaweza kwenda akakesha kumuomba Mungu wake. Mradi ametuma mwakilishi intatosha.
 
Hata ukiwa nyumbani kwako unaweza kuliombea taifa

DUA HAINA MBWEMBWE KOKOTE IKISOMWA ITAMFIKIA SUBHANNA
 
Afadhali hakuja angetuharibia wengine mood zetu tu tena binafsi nikichanganya na ile hutuba yake ya jana network zingekata.
 
Maaskofu na wahubiri mashuhuru wamejaa kila kona ya nchi wanaacha kuwaalika katika shughuli zao za kidini, badala yake wanajipendekeza kwa mtu ambae hamkubali Yesu kuwa mwana wa Mungu kuwa mgeni wao rasmi. Kama huu sii wendawazimu ni nini. Hapa ninachoona ni mchongo wa kupanua hirizi za kunasa mshiko. Afadhali amewakatalia, mwaka huu watakula kwa Yesu wanaesema kuwa wanamwamini. Magogoni no mshiko!!
.
 
Back
Top Bottom