JK ateua majaji wengine 10 wa Mahakama Kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ateua majaji wengine 10 wa Mahakama Kuu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 9, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete ameteua majaji wengine wapya 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika jitihada zinazoonekana kuwa ni za kutatua upungufu wa watendaji wa idara ya mahakama ambao umesababisha kesi nyingi kuchukua muda mrefu kabla ya kutolewa uamuzi.

  Hii ni mara ya nne kwa Rais Kikwete kuteua majaji tangu aingie madarakani mwaka 2005.

  Mara ya kwanza aliteua majaji 20 mwezi Desemba, 2006 na baadaye kuteua majaji 11 wakiwemo majaji saba wanawake Mei mwaka 2008, na Julai 14 mwaka 2009 aliteua majaji kumi .

  Katika majaji walioteuliwa, wanne ni wanawake na hivyo kufanya majaji wanawake walioteuliwa tangu Rais Kikwete aingie madarakani kuwa zaidi ya 14 kati ya majaji wapatao 47 walioteuliwa na kiongozi huyo wa serikali ya awamu ya nne.

  Uteuzi huo umefanyika wakati bajeti ya mwaka wa fedha 2010/11 ikitarajiwa kutangazwa kesho na waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo na kwamba serikali imesema kuwa itaiimarisha idara ya mahakama kwa kuiwezesha kutumia vifaa vya kurekodi sauti ili kuharakisha usikilizaji wa kesi Mahakama Kuu.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu inamnukuu kaimu katibu mkuu kiongozi, George Yambesi akisema kuwa uteuzi huo ulianza rasmi tangu Juni 4 mwaka huu.

  Taarifa hiyo inawataja walioteuliwa kuwa ni Samwel Victor Karua, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa msajili wa Mahakama Kuu, Grace Kalonge Mwakipesile (msajili wa Mahakama ya Ardhi) na Agnes Enos Bukuku (msajili wa Hazina).

  Wengine ni Richard Malima Kibela (sajili wa Wilaya ya Dodoma), Ama-Isario Ataulwa Munisi (wakili mkuu wa serikali), Dk Fauz Twaib (wakili wa kujitegemea), na John Harold Utamwa (msajili wa Mahakama ya Rufani).

  Wengine waliotajwa katika taarifa hiyo ni Beatrice Rodah Mutungi (naibu mwenyekiti Bodi ya Rufani ya Kodi), Haruna Twaibu Songoro (mkurugenzi wa Huduma za Sheria) na Mwendwa Judith Malecela (wakili mkuu wa serikali)

  Katika maadhimisho ya siku ya sheria Februari mwaka huu, Jaji Mkuu Augustino Ramadhan alitoa ombi kwa Rais Kikwete kushughulikia idadi ndogo ya majaji akisema kuwa ucheleweshwaji wa kesi utaendelea iwapo mahakama haitakuwa na watendaji wa kutosha.

  Kesi nyingi, hasa za mauaji, zimekuwa zikilalamikiwa kuwa zinachukua muda mrefu kabla ya kutolewa uamuzi na kusababisha baadhi ya watuhumiwa kukaa mahabusu kwa zaidi ya miaka mitano.

  JK ateua majaji wengine 10 wa Mahakama Kuu
   
 2. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bado majaji hawatoshi kwa kweli, ukilinganisha na mihimili mingine, tuna wabunge wengi saana wasiokuwa na kazi, wakuu wa wilaya pia, haki za watu zitazidi kuchelewa na watu watazidi kuona kupeleka kesi mahakamani is a wastage of time and money, mahakama na mihimili mingine walau ilingane ktk rasilimali watu
   
Loading...